Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kwanini hutaki kuwalipa watumishi pesa yao ya likizo June 2023?

danfodio

Member
Dec 2, 2018
80
58
Amani ya bwana Mungu Mwenyezi iwe nanyi enyi ndugu zangu wa jf.

Naomba niingie moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.

Mkurugenzi wa jiji la Mwanza kwa nini hutaki kulipa pesa ya likizo kwa watumishi ambao walitakiwa kulipwa toka Juni 2023?

Watumishi woote waliotakiwa kwenda likizo mwezi Juni 2023 mpaka leo hii hujalipa stahiki zao haliyakuwa sheria inataka watumishi wapewe pesa zao za likizo kabla ya kuanza kwa likizo hiyo.

Na jambo la kushangaza wilaya na majiji mengine nchini watumishi washapewa pesa hizi za likizo ya Juni 2023. Kwa nini wewe Mkurugenzi wa jiji la Mwanza hujawalipa watumishi wako wa jiji?

Kwa mfano walimu wote ambao wanatakiwa kulipwa likizo zao kwa mwezi june 2023 hawajalipwa achilia mbali baadhi ya wauguzi wa afya.

Hivi ingekuwa ni wewe unafanyiwa haya ungefurahia? Mkurugenzi hebu tenda haki kwa kulipa stahiki za watumishi gawa kwa wakati.

Ndugu waziri mwenye dhamana Tamisemi lishughulikieni hili ili kuleta haki kwa hawa watumishi wenu.

Naomba kuwasilisha.
 
Kwa upande wa jiji la Mwanza. Kikweli wapo slow sana kwenye kulipa stahiki za watumishi wa umma.
 
Mkuu nyie huko mpo vizuri,mimi nadai ya june 2022 na kwa utaratibu wa huku kwetu ulivyo natarajia kulipwa mwakani nitakapokuwa na likizo nyingine isiyo ya malipo.
 
Hawa Wakurugenzi wanashangaza sana, Utafikiri hizo hela zinatoka mifukoni kwao

Wizi, Tamaa na Ushamba tu

Kilichobaki ni kuwataja kwa majina
 
Mkuu nyie huko mpo vizuri,mimi nadai ya june 2022 na kwa utaratibu wa huku kwetu ulivyo natarajia kulipwa mwakani nitakapokuwa na likizo nyingine isiyo ya malipo.
Ndg yngu sheria na utaratibu wa utumishi ni kwamba kila mtumishi anapokuwa anatakiwa kwenda likizo anatakiwa kulipwa pesa ya likizo kabla ya kwenda hio likizo na si hivi hawa wakurugenzi wanachokifanya. Kiuhalisia kila mtumishi anajulikana likizo yake ni mwaka na mwez gn.
 
Hizo hela wanawabania watumishi kiaha wanaenda kuhonga kamati za bunge,wakaguzi wa cag na kujilipa miposho mikubwa mikubwa,inasikitisha sana.
 
Bora nyie TAMISEMI, mimi kwenye wizara yetu sijawahi kulipwa hela ya likizo tangu nianze kazi na maombi ya pesa za nauli nimeomba sana tu.2019.
 
Hawa Wakurugenzi wanashangaza sana, Utafikiri hizo hela zinatoka mifukoni kwao

Wizi, Tamaa na Ushamba tu

Kilichobaki ni kuwataja kwa majina
Kwa upande wa jiji la Mwanza leo kumbe kuna walimu wanadai pesa ya kusimamia mtihani wa darasa la nne toka mwaka 2016. Leo hii ndio walimu hao wanaodai pesa hizo za kusimamia mtihani wa darasa la iv mwaka 2016 wameitwa kwenda kujaza vendor form ili sasa waanze kulipwa.
Mkurugenzi kweli hujalipa walimu toka mwaka 2016 mpka leo hii??? Oneni aibu basi haki za watu mnazichelewesha bure palipokuwa na sababu zozote za msingi.
 
Watu wanakuwa wezi matumbo makubwa mpaka midomo inatoa harufu kwa wizi ...Inakuwaje unapanga kudhumulu mtu haku yake basi mtu ni haki yake ila utasikia mpaka wafanye uhakiki
 
Kwa upande wa jiji la Mwanza leo kumbe kuna walimu wanadai pesa ya kusimamia mtihani wa darasa la nne toka mwaka 2016. Leo hii ndio walimu hao wanaodai pesa hizo za kusimamia mtihani wa darasa la iv mwaka 2016 wameitwa kwenda kujaza vendor form ili sasa waanze kulipwa.
Mkurugenzi kweli hujalipa walimu toka mwaka 2016 mpka leo hii??? Oneni aibu basi haki za watu mnazichelewesha bure palipokuwa na sababu zozote za msingi.

Inasikitisha sana,wao hawawezi kwenda pepote bila posho.
 
Back
Top Bottom