Shilingi Milioni 251 zatengwa kulipana posho kuondoa machinga Jiji la Mwanza,wanaolipwa CD, DC na wenzao

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Milioni 251 zatengwa kulipana posho kuondoa machinga Jiji la Mwanza.

Wanaolipwa CD, DC na wenzao

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida jiji la Mwanza limetenga Sh. milioni 251 kwa ajili ya kulipana posho watumishi wake kwa siku 10 ili kusimamia zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu Machinga katikati ya jiji na kwenda maeneo waliyotengewa.

Kadhalika, jiji hilo limetenga Sh. milioni 10 kwa ajili ya kuchimba mtaro wenye urefu wa wa mita 100 katika uwanja wa Mchafukuoga uliokuwa ukitumiwa na shule nane zikiwamo za msingi na sekondari kwa ajili ya michezo ili kuuweka sawa kwa ajili kuhamishia machinga 2500 wa mtaa wa Makoroboi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mmoja wa Diwani aliyeshiriki kupitisha bajeti hiyo ya jiji iliyopitishwa Oktoba 5 mwaka huu, alisema fedha hizo ni nyingi, lakini cha kushangaza madiwani asilimia 99 walikubali kuipitisha.

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake, diwani huyo alifunguka kwamba huo ni ufisadi wa kutisha kwa sababu kuhamisha machinga hakuhitaji fedha nyingi kiasi hicho.

Alifafanua kwamba machinga walio wengi wamekubali wenyewe kuhama na huko wanapopelekwa hawajengewi vibanda wala hawalipwi gharama za kuhamisha biashara zao.

"Hizi fedha ni nyingi sana ndugu mwandishi na cha kushangaza hawa madiwani wote walikubali kupitisha bajeti hii ambayo waandishi wa habari walitolewa nje ya kikao cha baraza la madiwani,'' alisema.

Aliongeza kuwa katika bajeti hiyo waandishi wa habari nao wametengewa posho zao ili kuandika mambo mazuri pekee katika zoezi la kuhamisha machinga hao.

Alifafanua kuwa jiji lina magari yenye vipaza sauti ambayo yanapita kila kona walipo machinga na kuwataka wahame na kuwaelekeza sehemu za kwenda, lakini anashangaa kuona fedha hizo zinatengwa kwa ajili ya kuratibu zoezi hilo.

Kuhusu uwanja huo wa michezo, diwani huyo alisema, Serikali ilielekeza maeneo ambayo hayapaswi kupelekwa machinga kuwa ni pamoja na kuvamia viwanja vya shule.

Alisema shule hizo zilizopo kata ya Igogo watoto wake kwa sasa hawatakuwa na sehemu za kuchezea na kwamba kutakuwa na mwingiliano wa watu wengi hatua ambayo inaweza kuharibu masomo ya watoto hao.

Kuhusu kutengwa Sh. milioni 10 kwa ajili kuchimba mtaro na kusambaza udongo katika uwanja huo, alisema kiasi hicho pia ni kikubwa kwa kuwa jiji lina magari na magreda yake ambayo kama yangetumiwa wangeweza kuokoa fedha nyingi.

Akizungumzia kupitishwa kwa bajeti hiyo ya mamilioni, Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Sekiete Yahaya alisema suala hilo siyo kweli na kushindwa kueleza ukweli.

Alipoulizwa kikao cha Oktoba 5 mwaka huu cha baraza la madiwani ambacho kiliitishwa kwa dharura kilikuwa na ajenda gani alikata simu na alipopigiwa hakupokea tena.

Aidha, alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno kutaka ufafanuzi, Mkurugenzi huyo hakujibu kitu siku nzima ya jana.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi, alipotafutwa kuzungumza tuhuma hizo, alidai yeye sio anayepanga bajeti ya Jiji la Mwanza ambapo awali Mkurugenzi wa Jiji hilo Yahaya alidai zoezi hilo linaratibiwa na Mkuu huyo wa wilaya.

Zoezi la kuhamisha machinga na kuwapeleka maeneo waliyopangiwa linaendelea jijini Mwanza na linatarajia kukamilika Oktoba 14 mwaka huu.
 
Wache walipane ili hela ziingia mtaani zitaongeza atleast mzunguko wa hela katika biashara wachane upimbi kwani hiyo yote hela itakwenda kwa wafanya biashara.
 
Hii ndio gharama mwendazake hakujua baada ya kuruhusu na kuleta tatizo la machinga kila kona mpaka vyooni kwa watu.
 
Acha wale Rais si anajifanya mpole na mwenye huruma, sasa 2025 wabunge wa chama cha majambazi hakuna kurudi bungeni
 
Hii taarifa siwez ishangaa...HAKUNA JIPYA CHINI YA CCM YOTE NI YALEYALE YOTE NI UBATILI
 
Wache walipane ili hela ziingia mtaani zitaongeza atleast mzunguko wa hela katika biashara wachane upimbi kwani hiyo yote hela itakwenda kwa wafanya biashara .
Nchi haiwezi kujengwa kwa watu kuiibia serikali, sanasana wizi ukizidi serikali huanguka kabisa. Hivy hiyo sio suluhu ya pesa kuingia mtaani. Pesa kuingia mtaani ni nchi kuzalisha sana na kuuza
 
Nchi haiwezi kujengwa kwa watu kuiibia serikali, sanasana wizi ukizidi serikali huanguka kabisa. Hivy hiyo sio suluhu ya pesa kuingia mtaani. Pesa kuingia mtaani ni nchi kuzalisha sana na kuuza
Ule sio wizi ni taaratibu za serikali DUNIA nzima kulipana posho za vikao kwahiyo sio wezi ni Matumizi hali za halimashauri husika hakuna shida wache wapate posho zao ili maisha yaendelee wachane fikra za wivu na rohombaya.
 
Ule sio wizi ni taaratibu za serikali DUNIA nzima kulipana posho za vikao kwahiyo sio wezi ni Matumizi hali za halimashauri husika hakuna shida wache wapate posho zao ili maisha yaendelee wachane fikra za wivu na rohombaya.
Unajua shida sio kulipana, Bali je hayo malipo ni sahihi?

Kumbuka huu sio wivu Wala roho mbaya kwa maana matumizi haya ya namna hii ndio yanayozidi kuleta maisha magumu kwa watu wengi.

Fikiria Leo hii kuna sehemu nyingi wagonjwa wanabebwa kwa machela za miti

Wanafunzi wanaendeshe mtumbwi wenyewe kwenda shuleni
 
Naona watu wanawaka tu na kuripuka bila kujiuliza. Source ya hiyo habari ni nini?!! Katika akili ya kawaida (common sense), hivi hilo linaingia akilini?!!! M251 kulipana posh tu?!! Mwanza tu?!!! Halafu dar, bilioni ngapi?!!! Msiwe vilaza namna nyie magreat thinkers aisee!!
 
Hii ndio gharama mwendazake hakujua baada ya kuruhusu na kuleta tatizo la machinga kila kona mpaka vyooni kwa watu.
we kilaka, utaitaje riziki za watu,matatizo!!??,kwani Kuna shida gani wakifanya biashara mijini katkat ya miji!!??,watu wanatunza family zao kwa kazi ya machnga,hawaoni vibaka na majambazi walipungua mitaani,kuwaondoa kwenye soko lao ni kutaka kuwafukuza kwenye hiyo biashara,matokeo yake wengine watajikita kwenye kazi haramu Kama mbadala wa kupata kipato!!
 
Unajua shida sio kulipana, Bali je hayo malipo ni sahihi?
Kumbuka huu sio wivu Wala roho mbaya kwa maana matumizi haya ya namna hii ndio yanayozidi kuleta maisha magumu kwa watu wengi.
Fikiria Leo hii kuna sehemu nyingi wagonjwa wanabebwa kwa machela za miti
Wanafunzi wanaendeshe mtumbwi wenyewe kwenda shuleni
Ndugu yangu ngoja ni kwambia kitu DUNIA hii unayo iona haina Usawa popote uendapo kwahiyo jua hilo kwanza sio ULAYA,ASIA au kungine kokote ukujuapo hii ndio formula ya DUNIA.

Fanya jitihada ktk maisha yako kama ukipata uwezo fanya safari sn kwenda NCHI zingine utajifunza mambo mengi sn ktk maisha haya ya ulimwengu wa FUJO then utajua kuappreciate mambo mengi sn ktk maisha.
 
Wanatumia pesa kuhamisha tatizo na kuliendeleza na kulikuza, sio kuondoa mzizi wa Tatizo....

 
Back
Top Bottom