FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,520
Kuna Mwanamke anatafutwa, tunaomba utusaidie kutuonesha alipojificha.

Kama mnavyojua, safari ya kumtafuta mwenza wa maisha ina njia nyingi, na hakuna njia maalumu ndio maana nchi zilizoendelea wana mpaka dating sites zinazowaunganisha wenza.

Kijana wetu anatafuta mwenza ama mke kwa njia tofauti tofauti ila bado hatujafanikiwa. Tunawaomba msaada wenu wanajamiiforums kutusaidia katika njia hii ya mtandao.

Msaada wenu uwe kwa ushauri na kupoint mwanamke mwenye sifa zinazotafutwa alipojificha. Maana huwezi jua kwa kuota ndoto kwamba Mbagala Chamazi kwa Mzee Mkojani kuna binti wa fulani ana sifa mnazozitafuta ila hajui, hivyo karibuni kwenye mtaa wetu mumuone. Ama huwezi kujua kama Kigamboni kwa Urassa yupo huyo mwanamke na yeye anatafuta mume njooni mumuone.

Kijana wetu anaetafuta mwenza amenyooka kitabia na kimaisha, kwao amefunzwa vizuri na yuko tayari kuweka uwazi kwenye mambo yake yotee ambayo binti atahitaji kuyajua kwa ushahidi ulionyooka ili binti wa watu asiuziwe mbuzi kwenye gunia.

Kama mnavyojua ndoa ni jambo kubwa sana na ni kumuongeza mtu kwenye ukoo wenu, mzazi kupata mtoto mpya, sidhani kama kuna mtu anapenda kumuongeza kwenye ukoo wao mtu mwenye tabia mbovu ama sifa mbovu, kwa hiyo tunaomba sana msaada wenu kutuonesha huyo binti mwenye tabia na sifa nzuri alipojificha maana tunamsaka sana ila hatumuoni.

Sifa za kijana anayetafuta mwenza
1. Dini ni Mkristo na umri ni miaka 34

2. Kazi ni muajiriwa wa private sector na mfanyabiashara wa real estate, kipato chake ni cha kati yaani kipo kati kati ila kwa ufupi sio chini ya milioni moja na sio zaidi ya milioni 3 kwa mwezi

3. Elimu yake ni ya Chuo Kikuu.

4. Muonekano ni mrefu kwa makadirio ni zaidi ya futi 5 na nusu, na rangi maji ya kunde

5. Asili yake anatoka kabila mojawapo kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

6. Afya ni mzima na yupo tayari kupima magonjwa yote kabla ya ndoa kama ataonekana huyo binti anayemtafuta.

7. Mwisho kabisa kijana ni decent man na anatoka kwenye decent family pia.

Sifa za binti/mwanamke ambaye anatafutwa alipojificha

1. Binti awe na umri wowote usiopungua miaka 24 na usiozidi miaka 34.

2. Binti awe na sifa nzuri, decent background, tabia zake za nyuma zisilete maswali mengi kwa yeyote.

3. Binti awe na elimu isiyopungua kidato cha nne, na college education level yoyote iwe cheti, diploma ama degree ni sawa tu. Akiwa amesoma mchepuo wa sayansi itapendeza zaidi kuongea lugha moja maana taaluma ya mume ipo ndani ya STEM.

4. Binti awe na heshima, mwonekano na haiba za kike akiwa mrefu itapendeza zaidi.

5. Nyumbani ama sehemu alipokulia binti pasiwe mbali na mkoa wa Dar es salaam ili iwe rahisi kumtafuta na hata kujiridhisha kwa uchunguzi kabla ya taratibu zingine hazijafanyika.

Natambua humu JamiiForums tupo watu tunaoishi sehemu tofauti tofauti na tunajuana na watu tofauti tofauti, ombi langu kwenu kwa wale ambao maeneo wanapoishi, wanapofanya kazi ama wanaposali ibada zao wanamuona huyu binti anayetafutwa amejificha huku hajui kama anatafutwa.

Mfikishieni ujumbe wake. Na pia mniambie humu tuje wapi kumuona.

Wanajamiiforums wa madale tunaomba mtuambie kama kajificha madale, ama wale wa mbagala mbande mtuambie kama binti tunaemsaka kajificha mbande, wale wa gongo la mboto, pugu, chanika, kimara tunaomba mseme kama binti kaonekana huko kwenu na wale wa tegeta, bunju,ubungo, magomeni na wengineo wote tunaomba ushirikiano wenu katika kumtafuta mke wetu

Huwezi jua ya Mungu mengi ukawa msaada mkubwa kwenye kufanikisha hitaji la kijana

Kwa yoyote mwenye pendekezo pm ipo wazi.
 
Wake wapo wengi punguza masharti

Hakuna vigezo vigumu . Anatafutwa binti ambaye amelelewa vizuri kwa ajili ya ku raise familia yake mpya itakayokuja mbeleni vizuri.

Tambua kwamba Your partner is a representation of you. And most importantly she is the future mother of your children.

Kwa hiyo huwezi kumchukua yeyote tu.

Hata wanawake wana vigezo vyao pia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom