Mke anadai mimi nimemuibia pesa zake, amani imetoweka

Mke anadai mimi nimemuibia pesa zake, amani imetoweka

sikufichi nipo kwa ajili ya watoto na kuchukua haki yao sio kwa mapenzi kwa hali alioniweka simuamini hata kidogo,ilobaki basi tuu na anajua nimebadilika,ule ucheshi wa mwanzo kwake sina tena na i know inamla roho lakini let it be...
Samehe saba mara sabini
 
Ndio ni mchaga

ndio madhara ya kuoa wachaga mkuu usilaumu sana..wengi wanathamini pesa kuliko kitu chochote..

sasa kama angepata mume kama wa kwangu angefanyaje, huyu wa kwangu alichukua pesa ambazo niliziweka kwa ajili ya ujenzi km 5m na akakiri kuwa amechukua lkn wala hatujagombana kiviiiiiiiile mi nilinyamaza tu nikaamua kuweka pesa kimya kimya bila kumshirikisha asijue mana akijua tu anabeba..hata kama si zote atapunguza tu..sasa huyu angeweza kuishi na mtu wa hivi kweli?
 
Wallah Ndoa haina RAHA tupu kuna na mitihani kama hiyo ni wajibu wetu tukiwa kama binadamu kuthibiti,sisemi kua ni rahisi lakini jitahidi sana kua mvumilivu na muelewa Mkuu,kwanza fikiria familia yako pili usi fanye maamuzi ukiwa na hasiri..
Mimi yalinikuta hayo niliambiwa nimeiba mil 12 za shemeji yangu wakati hata chumbani kwa shemeji siingi,wakunitetea alitakiwa awe mumewangu nnae lalanae na kuamka nae na yeye pia alijiunga na ndugu zake sikutegemea kama angeweza kunubadilikia,lakini niliepusha shari pesa niliwapa na Sorry nikaomba nikawa nanuka wizi kwenye ukoo mzima, baada ya siku 20 nikiwa naimba mungu sanaaa kwa vilio,kumbe mtoto wa yule shemeji ndio alie chukua hela akaenda South Africa kipindi kile cha kuzamia wakakamatwa njiani hela zikaibiwa na kupigwa juu,akaletwa nyumbani hoi kuulizwa ilikuwaje ndio akasema mwanzo mpaka mwisho,ebu vuta picha kama ungekua wewe ungefanyaje?
Kama kuna mtu alie simama na mimi kua siwezi kuiba ni Mkwe wangu mamake mume wangu ukweli ulipo julikana tuu,nilifungasha wanangu kwetu nikasema hiyo pesa mkinipa sawa na msiponipa pia nimesamehe Talaka yangu mr utaileta
nyumbani kwetu.....nisikuchoshe mkuu.... chamsingi vuta subra familia yako ni muhimu sanaaaaa..
Hongera kwa kuvuka hilo mummy!

Kuna kipindi inafika unakua kwenye mtihani mzito kiasi kwamba kama ni mwepesi wa kuachia uliposhikilia mambo yanavurugika...

Nimependa hapo uliposimamia maombi na hatimae Mungu kwa wakati wake akafunua ukweli uliokua umefichwa.
 
ninachokiamin ni kwamba uongo haukai na ukweli na ipo siku ama unataka ima hautak lazima utajulikana tu ukweli ni upi na uongo ni upi. namjua dada mmoja alitalikiwa mumewe kisa kaiba pesa za mumewe. mke akaenda kwao kwa kilio sana huku akisema sijaiba wala sinaga hii tabia. mume akasema ni ewe mama chumban hakuna anaeingia zaid yako pekee.

Kumbe chumban kwao kulikua na dari na shemej yake (mdogo wa mwanaume) ndo aliakuwaga anapanda kwenye daari na kusaula kchumba kwa kaka yake. mwisho wa siku ikaja kujulikana baada ya kaka mtu kukuta hela mil 1 na mkewe hayupo yuko kwao mkoa mwingine. kuulizia kitaa amaambiwa mbona mdogo wako anachezaga kamari hadi za mamilion ya pesa?? yaani ilikuwa tabu kumfwata mke kwenda kuomba msamaha.

bidada adi leo anabembelezwa na hajarudi na wala hatak kurudi anadai mie mwiz siwez kuish na watu wema kama nyie.
Inauma shosti simuombei hata ADUI wangu limkute balaa hili khasa yule unaemtegemea aku bail out ndio anaekushindilia
mie my hubby alinambia wewe hutosheki hiyo pesa ulochukua si pesa ya watoto yakuchezea holiday unamuibia maskini wawatu hutosheki unashida gani nini nisokupa mpaka unaniaibisha namna hii? unaumasikini gani kwenu,nililia mpaka nikamshika miguu mume wangu umenioa hatuna kitu mimi ndio nnae fanya kazi leo hii nimekua mwizi? alinambia za mwizi 40 na leo imetimia hapo ndio mwanzo wa mimi kupata BP,hizi Ndoa we acha tuu mtu akikuona nje umependeza na unacheka anaona unashida gani? unaweza kuka kwenye gorofa uka wish ukae nyumba ya chumba kimoja lakini Happy...
 
amekwambia hajachukua amlipe vipi sasa
Huyo mwanamke hawezi kumsingizia coz kasema alirudi na hiyo pesa usiku na mwanaume alirudi usku amelewa means walikuwa wawili chumbani!..asa we unahisi ni nani kaichukua?...Ni mtazamo wangu lakini mkuu.
 
Hongera kwa kuvuka hilo mummy!

Kuna kipindi inafika unakua kwenye mtihani mzito kiasi kwamba kama ni mwepesi wa kuachia uliposhikilia mambo yanavurugika...

Nimependa hapo uliposimamia maombi na hatimae Mungu kwa wakati wake akafunua ukweli uliokua umefichwa.
Asante lakini yataka moyo sanaaaaaaaaa...
 
Pole sana mkuu ,nafikiri hakurudi nyumbani na huo mpunga
 
https://m.facebook.com/groups/1583482838575673?mess age_id=1693509107573045
fungua hapo yupo muzee huko kenya ni balaa / hiyo pesa itamgandia mkononi fasta.
 
Ndoa zinachangamoto saaana nilijua ni mimi tu ninayepitia shida. Mungu atusaidie
 
Mke anaanzia wapi kumshutumu mumewe kama sio kuwa na Jambo lake pembeni?
Mwangalie vizur kabla ya kutoa final conclusion.
 
Ki ukweli kama hujachukua ww bhas alikuwa anakutafutia sababu either anataka mil 6 nyingine or analengo lake na ndio maana amebadilika ghafla
"..Mwanamke hatumii Busara ila ajaribu kumchunguza je ana Tabia za kusingizia?"
 
Ni kweli yataka moyo tena moyo mkuu mummy na sikuzote wenye moyo mkuu ndio wanaoshinda[emoji1]
MMMM shosti mie nasubiri na naomba mwenyezi mungu awakuze wanangu na anipe umri mrefu lakini nimeshaanza kuwapeleka nje kusoma nimebaki na hawa wadogo nao pia hawatokua namda ntawapeleka baada ntaomba tumalizane tuu
kiroho safi...
 
Back
Top Bottom