Mke anadai mimi nimemuibia pesa zake, amani imetoweka

Mke anadai mimi nimemuibia pesa zake, amani imetoweka

Yeah nimerudi nilikua nyumbani kwetu miezi 6 na yeye kasema talaka hatoi baadae nimlani shetani,lakini nishamjua nani mzuri na nani mbaya nimejifunza mengi sana shosti...

Wamekurudishia hela zako ?
 
Hakuna kama unasema huyo bibie aende polisi ili mbivu na mbichi zijulikane lkn kama ushahidi wake pekee ni maono ya mchungaji basi polisi lazima watamnywaaa alafu baadae wanamtoa baro manake hakuna kesi hapo.
chumbani si mnakaa wawili lakini?
 
Kama kweli hujachukua kwanza, chunguza kama kweli kuna mkopo alichukua popote, ukipata uhakika mwambie mke wangu sijachukua pesa yako ila nitakurudishia, tafuta hiyo hela umpe ingekuwa mtu baki sawa lakin kama ni mke wako fanya tu na weka nia kuwa unafanya kwa ajili ya kulinda ndoa na watoto wako, akipata mke wako ndo wamepata watoto n.k., Ila lazima kutakuwa na tatizo unajua ni ngumu mtu kukuwazia vitu kama hivyo kama hukuwahi kuonyesha kitu kibaya (yaani kukosa uaminifu), siko upande wa mwanamke lakin kuna katabia unako ambacho kinamshawishi kuwaza ni wewe ndo umechukua, pengine hiyo tabia ya ulevi.

Kiufupi kama unawezo mlipe hata nusu nusu 6m ni ndogo sana juu ya ndoa yako na watoto wako, msiwaathiri watot kwa 6m, pole sana, na pia Mungu amekuonyesha unaishi na mwanamke wa aina gani, hiyo ndio moja ya changamoto za ndoa, na usije ukathubutu kutafuta mwanamke kipindi hiki una matatizo, utaongeza matatizo Zaidi na Zaidi baada uje umsingizie shetani, sahau kwa sasa kutoka nje ya ndoa, tatua tatizo kutoka nje ya ndoa ni kulikimbia tatizo, fikiria watoto wako na uache pombe plz au punguza lol.
Unaposema amenihisi kwa kuwa huenda nina ka tabia flani unakusudia nn hasa? Mama yangu ninapokwambia ushahidi wake ni maono ya mchungaji huniamini?
Hana ushahidi mwingine wowote ule zaidi ya maono ya mchungaji,, mchungaji ambae ni msanii ni full magumashi
Mm binafsi nilipomuona huyu pastor for first time nilikataa kabisa kuingia kwenye Hilo kanisa

Sina tatizo la ukosefu wa uaminifu in anyway
Mtaji wa biashara hiyo nimeutoa mm hata biashara ikiyumba huwa ni mm ndio nasaidia hadi sasa biashara hiyo imekua kubwa kiasi cha kuhitaji expansion

Siwezi kulipa hiyo pesa kutokana na utovu wa nidhamu aliouonesha na maneno ambayo yameshasambaa
Nikilipa pesa hiyo atajisifu na kutangaza ukoo mzima kwamba ni mm nilichukua hiyo pesa na kwamba nimebanwa hadi nimerudisha hivyo itaniachia picha mbaya mbele ya jamii

Najua wanawake mnaweza kufanya vitu vingi hata vya kudhalilisha ili kuokoa ndoa lakini sio kwa sisi wanaume Kuna ukomo

Siwezi kukubali kuonekana mwizi kisa nataka kulinda ndoa hiyo mnaweza kufanya nyinyi wanawake

Ushauri pekee nilioupokea kutoka kwako na ambao naahidi kuufanyia kazi ni kuacha pombe
 
Mwezi mmoja uliopita wife alipata mkopo kutoka mahala fulani wa shilingi 6 million, lengo la mkopo huo ilikua ni kuimarisha biashara yake ya restaurant na kuipanua zaidi, mm ndie nilitoa mtaji wa hiyo restaurant wakati inaanza

Siku ya tukio alichukua pesa hizo benki na kuziweka kwenye pochi kubwa na kuanza kuzunguka nazo tangu asu ubuhi hadi jioni aliporudi, mm nilirudi usiku mwingi kutoka kwenye pombe na nilimkuta ameshalala nilihudumiwa na hg chakula nikaenda kulala, asubuhi ndipo hakuziona pesa zake kwenye pochi
Mm sikua najua hata kaja na hela hadi aliposema haoni pesa zake na kuangua kilio kizito sana

Jioni akaenda kwa mchungaji wa kanisa lao na kufanya maombi kuhusu jambo hilo, eti katika maombi hayo mchungaji akaoneshwa kuwa ni mm ndio nimechukua hizo pesa, usiku hatukulala aliongea usiku kucha tena sebuleni akipayuka kuwa nimrudishie hela zake la sivyo ndoa itaishia hapo na atanifungulia kesi, ni mwezi sasa tangu tukio hilo hatuongeleshani, hakuna tendo, usiku anakwenda kulala kwa watoto, ametoa ultimatum kuwa kama sijamrudishia pesa zake nisije nikamlaumu, nikamjibu sawa naisubiri hiyo ultimatum tuone,

Nimekataa vikao vyote vya usuluhishi kwa sababu ya maneno yake machafu, na nimeona ni udhalilishaji kwenda kujadili kuwa nimechukua hela pesa za mke wangu, kama hataki abebe vitu vyake aondoke, nimejiepusha kumpiga tangu mwanzo kwa kuzuia hasira zangu, lakini sasa inaenda kushindikana

Kuna yoyote kati yenu mwenye wazo jipya juu ya ufumbuzi wa mgogoro huu?

Maana nimeathirika kisaikolojia, watoto pia hawaelewi kwa nn mama analala room kwao, wameathirika pia, lakini zaidi ya yote nina mwezi mzima sijapata haki yangu ya msingi (matrimonial right) na sasa nimeanza kufikiria njia mbadala iwapo mgogoro huu utaendelea

Nahitaji mawazo yenu
Mfuate huyo Mchungaji aliye mwambia kwamba wewe ndio uliochukua hizo fedha.....
(hawa wachungaji yuko mmoja nitakula maini yake soon)
 
Unaposema amenihisi kwa kuwa huenda nina ka tabia flani unakusudia nn hasa? Mama yangu ninapokwambia ushahidi wake ni maono ya mchungaji huniamini?
Hana ushahidi mwingine wowote ule zaidi ya maono ya mchungaji,, mchungaji ambae ni msanii ni full magumashi
Mm binafsi nilipomuona huyu pastor for first time nilikataa kabisa kuingia kwenye Hilo kanisa

Sina tatizo la ukosefu wa uaminifu in anyway
Mtaji wa biashara hiyo nimeutoa mm hata biashara ikiyumba huwa ni mm ndio nasaidia hadi sasa biashara hiyo imekua kubwa kiasi cha kuhitaji expansion

Siwezi kulipa hiyo pesa kutokana na utovu wa nidhamu aliouonesha na maneno ambayo yameshasambaa
Nikilipa pesa hiyo atajisifu na kutangaza ukoo mzima kwamba ni mm nilichukua hiyo pesa na kwamba nimebanwa hadi nimerudisha hivyo itaniachia picha mbaya mbele ya jamii

Najua wanawake mnaweza kufanya vitu vingi hata vya kudhalilisha ili kuokoa ndoa lakini sio kwa sisi wanaume Kuna ukomo

Siwezi kukubali kuonekana mwizi kisa nataka kulinda ndoa hiyo mnaweza kufanya nyinyi wanawake

Ushauri pekee nilioupokea kutoka kwako na ambao naahidi kuufanyia kazi ni kuacha pombe
Mie sikusema moja kwa moja sabab sikujui na yeye mke wako ndo anakufahamu Zaidi, alichofanya mke sawa ni utovu wa nidham lakini kwa nilisikiliza upande mmoja tu wako, ili kweka sawa upande wa pili lazima kuwepo akiba ya maneno kama vile, Kama kweli huna katabia chochote cha kumfanya akuhisi hivyo, basi chunguza iko namna, aidha anatafuta sabab tu, aidha kwa kukuchomoa pesa nyengien kijanja au yapo mengi nyuma ya pazia, cha msingi kuwa mpole na kama umeamua kutolipa hiyo pesa, basi simamia ndoa yako irudi kama zamani, mana hata mkiachana doa litabaki pale pale kuwa ulimuibia pesa kama alivyoeneza, pamoja nakuwa amefanya kitu cha ajabu kukuzushia kitu kama hicho cha aibu, mana wanawake wengi tunaamini aibu ya mume ndo aibu ya mke au ya familia sijuia aliwezaje kwenda kuongea huo utumbo nje...pole sana.
 
Kama ndoa yenu haina kuaminiana, una tatizo kubwa sana.

Hapo ndoa yenu inaonekana haizidi thamani ya sh milioni sita.

Kama anaamini kweli umemuibia hela, sioni maana ya kuendelea kuwa pamoja. Kwa sababu kitakachotokea kingine chochote mshukiwa ni wewe.
 
Wallah Ndoa haina RAHA tupu kuna na mitihani kama hiyo ni wajibu wetu tukiwa kama binadamu kuthibiti,sisemi kua ni rahisi lakini jitahidi sana kua mvumilivu na muelewa Mkuu,kwanza fikiria familia yako pili usi fanye maamuzi ukiwa na hasiri..
Mimi yalinikuta hayo niliambiwa nimeiba mil 12 za shemeji yangu wakati hata chumbani kwa shemeji siingi,wakunitetea alitakiwa awe mumewangu nnae lalanae na kuamka nae na yeye pia alijiunga na ndugu zake sikutegemea kama angeweza kunubadilikia,lakini niliepusha shari pesa niliwapa na Sorry nikaomba nikawa nanuka wizi kwenye ukoo mzima, baada ya siku 20 nikiwa naimba mungu sanaaa kwa vilio,kumbe mtoto wa yule shemeji ndio alie chukua hela akaenda South Africa kipindi kile cha kuzamia wakakamatwa njiani hela zikaibiwa na kupigwa juu,akaletwa nyumbani hoi kuulizwa ilikuwaje ndio akasema mwanzo mpaka mwisho,ebu vuta picha kama ungekua wewe ungefanyaje?
Kama kuna mtu alie simama na mimi kua siwezi kuiba ni Mkwe wangu mamake mume wangu ukweli ulipo julikana tuu,nilifungasha wanangu kwetu nikasema hiyo pesa mkinipa sawa na msiponipa pia nimesamehe Talaka yangu mr utaileta
nyumbani kwetu.....nisikuchoshe mkuu.... chamsingi vuta subra familia yako ni muhimu sanaaaaa..
I'd yako inaonesha bado upoupo tu hupendi tena
 
Duu pole sana . nimesoma hapa mpaka nimesikia roho inauma , heri Mungu alifunua ukweli hapo hapo
Wallah nilishukuru lakini hizo siku niliziona kama miaka100 nilikua natafuta dawa yakukonda lakini dawa ilikua hiyo
nilikonda kila sehemu ya mwili wangu nilikua naisikia chungu moyo ndio usiseme unaniuma vibaya,na sio sababu ya inlaws sababau mume wangu yani nasema hata wewe pia? nimlilie nani mie hili umeweza kua na ndugu zako jee ingekua jirani au mtu wa nje sindio ningekufia jela mie? zamani nilikua namuamini nikinunua kitu hata kama nimenunua peke yangu naandika jina langu na lake,baada ya hapo nimebadilisha majina yote ni ya watoto wangu na mimi mwenyewe yeye asahau....
 
it depends na uhusiano wenu ulivo,

katika hali ya kawaida asingeweza kukopa bila kukuambia, acha kukusingizia angeishia kupata kichapo cha kwa nn kakopa bila taarifa then ifuatie kwann anakusingizia!

Lastly kama kero zinaongezeka ndo ingefuata talaka halafu hizo hela ndo zingemfuata kwao!

hahahaa aaa unifanya nicheke kwa sauti ofcn..
 
I'd yako inaonesha bado upoupo tu hupendi tena
sikufichi nipo kwa ajili ya watoto na kuchukua haki yao sio kwa mapenzi kwa hali alioniweka simuamini hata kidogo,ilobaki basi tuu na anajua nimebadilika,ule ucheshi wa mwanzo kwake sina tena na i know inamla roho lakini let it be...
 
Wallah Ndoa haina RAHA tupu kuna na mitihani kama hiyo ni wajibu wetu tukiwa kama binadamu kuthibiti,sisemi kua ni rahisi lakini jitahidi sana kua mvumilivu na muelewa Mkuu,kwanza fikiria familia yako pili usi fanye maamuzi ukiwa na hasiri..
Mimi yalinikuta hayo niliambiwa nimeiba mil 12 za shemeji yangu wakati hata chumbani kwa shemeji siingi,wakunitetea alitakiwa awe mumewangu nnae lalanae na kuamka nae na yeye pia alijiunga na ndugu zake sikutegemea kama angeweza kunubadilikia,lakini niliepusha shari pesa niliwapa na Sorry nikaomba nikawa nanuka wizi kwenye ukoo mzima, baada ya siku 20 nikiwa naimba mungu sanaaa kwa vilio,kumbe mtoto wa yule shemeji ndio alie chukua hela akaenda South Africa kipindi kile cha kuzamia wakakamatwa njiani hela zikaibiwa na kupigwa juu,akaletwa nyumbani hoi kuulizwa ilikuwaje ndio akasema mwanzo mpaka mwisho,ebu vuta picha kama ungekua wewe ungefanyaje?
Kama kuna mtu alie simama na mimi kua siwezi kuiba ni Mkwe wangu mamake mume wangu ukweli ulipo julikana tuu,nilifungasha wanangu kwetu nikasema hiyo pesa mkinipa sawa na msiponipa pia nimesamehe Talaka yangu mr utaileta
nyumbani kwetu.....nisikuchoshe mkuu.... chamsingi vuta subra familia yako ni muhimu sanaaaaa..
ninachokiamin ni kwamba uongo haukai na ukweli na ipo siku ama unataka ima hautak lazima utajulikana tu ukweli ni upi na uongo ni upi. namjua dada mmoja alitalikiwa mumewe kisa kaiba pesa za mumewe. mke akaenda kwao kwa kilio sana huku akisema sijaiba wala sinaga hii tabia. mume akasema ni ewe mama chumban hakuna anaeingia zaid yako pekee.

Kumbe chumban kwao kulikua na dari na shemej yake (mdogo wa mwanaume) ndo aliakuwaga anapanda kwenye daari na kusaula kchumba kwa kaka yake. mwisho wa siku ikaja kujulikana baada ya kaka mtu kukuta hela mil 1 na mkewe hayupo yuko kwao mkoa mwingine. kuulizia kitaa amaambiwa mbona mdogo wako anachezaga kamari hadi za mamilion ya pesa?? yaani ilikuwa tabu kumfwata mke kwenda kuomba msamaha.

bidada adi leo anabembelezwa na hajarudi na wala hatak kurudi anadai mie mwiz siwez kuish na watu wema kama nyie.
 
Back
Top Bottom