Mke anadai mimi nimemuibia pesa zake, amani imetoweka

Mke anadai mimi nimemuibia pesa zake, amani imetoweka

Pastor kimeo mkuu, ndio aliekusababishia yote haya! Poor pasta
 
Mchungaji mwenyewe ukimuona ni full magumashi na usanii hela ambazo wife ameshapeleka huko kanisani kama zaka na sadaka sasa hivi angekua na migahawa miwili
Lakini wanachangishwa hela kama Hawana akili nzuri

Mm huyo pastor nilimgomea kusali kwenye kanisa lao niliwaambia siwezi kuhama kanisa langu la asili tangu hapo huyo pastor hanipendi sana
Hivyo pastor akaanzisha kampeni maalum wanamletea akina mama wa maombi wanamweleza wife kuwa imani yake haikui sababu yangu

Hivyo Kuna historia flan ya mgogoro kati yangu na huyo mchungaji

Bahati mbaya na wife amemwani huyu pastor na kanisa Lake
Siku nikahama R.C naenda kuabudu ng'ombe
 
Hiyo ndoa imeshapata jeraha au tayari Ina majeraha mengi.

Je ukiacha kumpa mtaji wa kuanzia uliendelea kumsapoti mkeo kwenye hiyo biashara?

Maana huenda akaamini umechukua ili kumkwamisha maana hutaki aendelee na shughuli hiyo.
Mkuu nimetoa msaada mara kadhaa biashara hiyo inapoyumba sio mara moja wala mbili ni mara nyingi tu
Shida ni huyu pastor aliemlisha sumu
 
Mkwe wangu tunaelewana SANA na anajua katika wakwe zake 13 basi mie ndio kipenzi chake manake simchukui kama mkwe
ni Mama kwangu nirafiki yangu na nimtu ambae sifanyi langu bila kumwambia kwahiyo anajua na sijui mumewangu alishikwa na nini mpaka akafanya vile lakini haya ndio mitihani ya ndoa..
Pole na hongera Mungu akubariki sana na huyo mama mkwe wako.
 
nakubaliana na wewe...na aende tu kwa kweli ila kuna kitu...kwamba wakiona maisha ya jamaa yameanza kuimarika watakuja na hadithi....'mnaona ni zile hela alizomuibia mkewe'
na yakiwa kawaida utasikia wakisema "kapoteza mke na hela alizomuibia hata hazijamsaidia chochote ni heri angemrudishia wakabaki wote tu"
yakienda vibaya utawasikia
"ona maisha yake yanavyoenda kombo, ni laana za kumuibia mke wake hela"
 
Mchungaji mwenyewe ukimuona ni full magumashi na usanii hela ambazo wife ameshapeleka huko kanisani kama zaka na sadaka sasa hivi angekua na migahawa miwili
Lakini wanachangishwa hela kama Hawana akili nzuri

Mm huyo pastor nilimgomea kusali kwenye kanisa lao niliwaambia siwezi kuhama kanisa langu la asili tangu hapo huyo pastor hanipendi sana
Hivyo pastor akaanzisha kampeni maalum wanamletea akina mama wa maombi wanamweleza wife kuwa imani yake haikui sababu yangu

Hivyo Kuna historia flan ya mgogoro kati yangu na huyo mchungaji

Bahati mbaya na wife amemwani huyu pastor na kanisa Lake
kutokana na maelezo haya kuna chance ya 75% kuwa hizo hela ameibiwa na huyo mchungaji
 
I can imagine! mtu unayetegemea asimame upande wako anapokuwa on your contrary!me ndoa ingeisha tu kwa kweli...
Hapo ndio ustahamilivu unapokuja na sikufikiria mimi nafsi yangu ila watoto wangu walikua wadogo just 4months nimetoka na sikupenda watoto wangu wakue bila mzazi wao...na vile vile binadamu tuwe na moyo wa kusamehe ikiwa mwenyezi mungu anasamehe why not sisi...
 
rudisha hela ya mkeo acha mambo ya zamani,hata mimi naona wewe ndiye suspect namba moja,
Hakuna kama unasema huyo bibie aende polisi ili mbivu na mbichi zijulikane lkn kama ushahidi wake pekee ni maono ya mchungaji basi polisi lazima watamnywaaa alafu baadae wanamtoa baro manake hakuna kesi hapo.
 
ha haha basi we tulia tu mda ufike afanye maamuzi ila umpe neno moja tu kuwa maamuzi yake asije jutia milele...... haya makanisa wanaharibu kabisa huyo mchungaji hana hekima .. kuna gape kubwa kati ya mkeo na wewe ambapo huyo mchungaji ameshaambia kila kitu yeye anachofanya ni kugongelea msumari tu
Tafuta kanisa la huyo jamaa ulipige kiberiti hana maana hata kidogo
 
Kama kweli hujachukua kwanza, chunguza kama kweli kuna mkopo alichukua popote, ukipata uhakika mwambie mke wangu sijachukua pesa yako ila nitakurudishia, tafuta hiyo hela umpe ingekuwa mtu baki sawa lakin kama ni mke wako fanya tu na weka nia kuwa unafanya kwa ajili ya kulinda ndoa na watoto wako, akipata mke wako ndo wamepata watoto n.k., Ila lazima kutakuwa na tatizo unajua ni ngumu mtu kukuwazia vitu kama hivyo kama hukuwahi kuonyesha kitu kibaya (yaani kukosa uaminifu), siko upande wa mwanamke lakin kuna katabia unako ambacho kinamshawishi kuwaza ni wewe ndo umechukua, pengine hiyo tabia ya ulevi.

Kiufupi kama unawezo mlipe hata nusu nusu 6m ni ndogo sana juu ya ndoa yako na watoto wako, msiwaathiri watot kwa 6m, pole sana, na pia Mungu amekuonyesha unaishi na mwanamke wa aina gani, hiyo ndio moja ya changamoto za ndoa, na usije ukathubutu kutafuta mwanamke kipindi hiki una matatizo, utaongeza matatizo Zaidi na Zaidi baada uje umsingizie shetani, sahau kwa sasa kutoka nje ya ndoa, tatua tatizo kutoka nje ya ndoa ni kulikimbia tatizo, fikiria watoto wako na uache pombe plz au punguza lol.
 
pole sana
Mimi ni binadamu na nna Moyo pia,sababau ya kutoondoka pale mwanzo nikutaka kujua wapi hela imekwenda,ningeondoka maneno yangezidi ilifikia mpaka mumewangu chakula nnachopika akawa hali anakula kwa ndugu zake,nilisema ntabakia hapa mpaka nijue ukweli,nilipotapa ukweli ndio siku nilochukua wanangu nikaondoka,nilikua na mawazo mengi sanaa,khasa mumewangu ndugu zake kuniamini au kutokuniamini is the list of my concern lakini yeye ndio aliekua ananiumiza kichwa siamini masikio yangu wala macho yangu nikimuangalia nalia kama nimepigwa nasikia uchungu machozi yamotooooo
yani roho inaniuma hata sijui nielezee vp..mmmm it was BAD...
 
Aisee hapo nikifikia kuoa nafikilia mengi imagine MTU umempa mtaji mwenyewe Leo anakopa alafu akwambii vuta picha hiyo Leo anakuja na gea kuwa we ndo mwizi aisee kweli duniani kuna mambo sasa fikilia hpo kuna ndoa kweli
 
Wallah Ndoa haina RAHA tupu kuna na mitihani kama hiyo ni wajibu wetu tukiwa kama binadamu kuthibiti,sisemi kua ni rahisi lakini jitahidi sana kua mvumilivu na muelewa Mkuu,kwanza fikiria familia yako pili usi fanye maamuzi ukiwa na hasiri..
Mimi yalinikuta hayo niliambiwa nimeiba mil 12 za shemeji yangu wakati hata chumbani kwa shemeji siingi,wakunitetea alitakiwa awe mumewangu nnae lalanae na kuamka nae na yeye pia alijiunga na ndugu zake sikutegemea kama angeweza kunubadilikia,lakini niliepusha shari pesa niliwapa na Sorry nikaomba nikawa nanuka wizi kwenye ukoo mzima, baada ya siku 20 nikiwa naimba mungu sanaaa kwa vilio,kumbe mtoto wa yule shemeji ndio alie chukua hela akaenda South Africa kipindi kile cha kuzamia wakakamatwa njiani hela zikaibiwa na kupigwa juu,akaletwa nyumbani hoi kuulizwa ilikuwaje ndio akasema mwanzo mpaka mwisho,ebu vuta picha kama ungekua wewe ungefanyaje?
Kama kuna mtu alie simama na mimi kua siwezi kuiba ni Mkwe wangu mamake mume wangu ukweli ulipo julikana tuu,nilifungasha wanangu kwetu nikasema hiyo pesa mkinipa sawa na msiponipa pia nimesamehe Talaka yangu mr utaileta
nyumbani kwetu.....nisikuchoshe mkuu.... chamsingi vuta subra familia yako ni muhimu sanaaaaa..

Duu pole sana . nimesoma hapa mpaka nimesikia roho inauma , heri Mungu alifunua ukweli hapo hapo
 
Back
Top Bottom