Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mwaka huu kuna kazi. Mimi niliwahi andika mwaka 1995 kwamba Mkapa hakuwa clean, alikuwa hajapata nafasi ya kuchota zaidi ya vile visenti vya waomba scholarship pale wizara ya elimu ya juu.

Nakumbuka wakati huo kuna watu wengi sana walinishambulia na kusema naleta uzushi. Mungu mkubwa, karibu wote sasa wanaelewa kwamba haikuwa majungu.

Wasiwasi wangu bwana ni pale Mkapa atakapoongea. kwa kadri tunavyomjua Mkapa, ni muongeaji mzuri mwenye kupenda sana kutumia nguvu ya ushahidi kuliko hisia. Sasa wasiwasi so far sasa hivi madai mengi ya ufisadi wa Mkapa yanaelea sana. Sijasoma vizuri sheria ya maadili, lakini sijaona hasa mtu akijenga hojahoja sawasawa katika mantiki ya ushahidi wa kisheria wa kumtia hatiani Mkapa. Isije ikawa tunapambana na Mkapa badala ya mfumo wa kisheria za kifisadi ambazo zinalinda ufisadi. Isije ikawa kila kitu alichofanya Mkapa kuhusu uwekezaji wa kifisadi ANBEM, Kiwira, etc akawa alifanya ndani ya sheria.

Sasa kama sheria mbovu ndizo zilizomlinda Mkapa akafanya yote anayodaiwa sasa hivi siku akiongea atatuumbua sana na atakuwa amewasafisha mafisadi wengi mno na kuonyesha kwamba wengi wetu tunaongeaga kwa hisia zaidi. Kwa kifupi, wasiwasi wangu ni huu: isije ikawa tunapambana na individuals tukifikiri walifanya makosa nje ya sheria kumbe walifanya makosa yanayolindwa kikamilifu kabisa na mfumo wa kisheria. I hope am wrong and one day Mkapa and the company will be brought to the law before their days on this earth expire as it happened to Dito!

Sasa kwa kuanzia ili tumuwahi Mkapa kabla hajaanza kushuka mawe yake, hebu wale wanaoujua hizi sheria alizovunja Mkapa vizuri, tuwekee hapa kipengele baada ya kipengele na jinsi Mkapa na hayo mauwekezaji yake alivyozivunja ili tumkome nyani gladi sawasawa!
 
Mkuu vipi tena?..
Hata kufungua kampuni ikitumia address ya Ikulu bado unaona hakuna ushahidi..
Upatikanaji wa Kiwira, Rada, Majengo ya Msajiri, Gharama za ujenzi wa benki kuu na kadhalika bado unauliza ushahidi mkuu?
 
Nisome tena! Ninachotaka kujua kuna sheria inakataza hili? Nauliza hili kwa sababu hawa jamaa walipokaa pale Zanzibar walijihalalishia karibu kila kitu; sasa isije ikawa hili nalo lilihalalishwa halafu Mkapa atakapofungua mdomo tukabaki kushika matama! Mimi nimeanza kuwa mwoga sana maana isije ikawa tunapambana na hawa jamaa moja moja na kuacha mfumo uliowalinda kufanya yote haya. Sijasikia kabisa kule bungeni wabunge wetu waki-cite specifically vipengele vya sheria ambavyo Mkapa na wenzake walivunja. Nilichosikia ni wao wabunge wetu kulia kama vile sisi tunavyolia hapa JF na wananchi wa kawaida, sasa sidhani kama kulia pekee kutamfikisha Mkapa kwenye witness box. Kitakachomfikisha Mkapa mahakamani ni criminal offence na sio moral offence, ndio maana hapa tulipofikia sasa inabidi tuwe makini sana hasa tukizingatia uimara wa Mkapa wa kujibu hoja!
 
Alikula yamini ...kama unaelewa maana ya Yamini

Mkandara:

Hapo ndugu wa Nyerere walichemsha BIG TIME. Pamoja na kumlaumu Nyerere kwa siasa zake, lakini Mzee hakutaka influence yake itumike kwa watoto wake, mke wake au familia yake. Hawa ndugu zake walitaka kujichanganya kwa kutumia jina la Nyerere na sasa wanaona wamekaribisha wevi.
 
Posted Date::4/26/2008
Serikali ya Rais Kikwete yawasha moto kumchunguza Rais Mstaafu Mkapa
Na Mwandishi wetu

SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete imeamua kutofautiana na zile za marais waliomtangulia kwa kutamka uamuzi mzito ambao haukuwahi kufanyika tangu Tanzania ipate uhuru, kwa serikali yake kuamua kuchunguza kashfa ya Rais Mstaafu , Benjamin Mkapa.

Uamuzi huo umetoa mwelekeo mpya wa serikali ya Kikwete kwamba sasa ameamua kufumba macho na kuwatosa watu muhimu kwake wanaotuhumiwa kwa ufisadi bila ya kujali wana nyadhifa gani.

Kitendo cha kuachia ngazi mawaziri wanne katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na kashfa za ufisadi na kuanza kumchunguza Mkapa kinaonyesha wazi kuwa sasa shikizo la wananchi na nchi wahisani kuhusu vitendo vya ufisadi limemfanya Kikwete abadili mwelekeo wa utendaji wake wa kazi.

Hata hivyo, mtihani mkubwa ulioko mbele yake ni namna atakavyoendesha uchunguzi dhidi ya Mkapa na endapo atabainika amehusika kutumia madaraka vibaya na kukiuka maadili ya uongozi akiwa Ikulu, je ataweza kumfikisha mahakamani?

Mtihani utakuwa mgumu kwa Kikwete kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka vipengele vinavyomlinda mno rais aliyepo madarakani au ambaye amestaafu.

Kwa mujibu wa katiba ibara ya 46 (3) wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilotenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya urais, ila tu kama angalau siku 30 kabla shauri kufunguliwa mahakamani, rais atapewa au ametumiwa kwanza taarifa ya madai kwa maandishi kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge na taarifa hiyo ikiwa na maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina la mdai na anwani ya mahali anapoishi na anapaswa aliainishe jambo analodai.

"Isipokuwa kama ataacha kushika maradaka ya urais kutokana na masharti ya ibara ya 46 (A) (10), itakuwa ni marufuku kushitaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo alilofanya yeye kama rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya rais."

Hata hivyo, Bunge linaweza kumshitaki rais kama ametenda makosa ambayo yanavunja katiba au sheria ya maadili ya viongozi wa umma.

Kwa mujibu wa katiba hiyo, kabla ya Bunge kumshitaki, taarifa ya maandishi iliyotiwa saini na kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku 30 kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa bungeni, ikifafanua makosa aliyotenda na ikipendekeza kuwa kamati maalum ya uchunguzi iundwe ili ichunguze mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya rais.

Iwapo uchunguzi wa serikali utabaini kuwa Mkapa anahusika katika kashfa ya kutumia vibaya ofisi ya umma alipokuwa madarakani, kuanzisha kampuni binafsi kinyume cha sheria ni wazi kwamba itabidi katiba ya nchi ifanyiwe marekebisho ili iwe rahisi kwa rais mstaafu kushtakiwa kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani.

Hata hivyo, kama wabunge wakiamua kufuata taratibu hizo na kama serikali haitaweka vikwazo, Mkapa anaweza kushtakiwa na kuhukumiwa kutokana na matendo ambayo yatabainika kayafanya wakati akiwa rais na ambayo ni kinyume na maadili ya uongozi.

Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa tayari baadhi ya wabunge wamejipanga sawa kuhakikisha wanaendelea kutoa hoja binafsi za kuwabana vigogo wote waliohusika katika ufisadi.

Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanaona hatua hiyo ya Kikwete ni ya kijasiri na inapaswa kufanyika wakati huu ambao nchi imekumbwa na ufisadi wa kutisha.

Hata hivyo, baadhi ya watu wanaona kwamba hatua ya kumchunguza na kisha kumchukulia hatua Rais aliyeondoka madarakani ni nzuri lakini pia Rais aliyepo madarakani naye anapaswa kuwa msafi ili anayekuja asije kumwigiza naye katika matatizo.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wiki hii aliliambia Bunge mjini Dodoma kuwa serikali ina taarifa za tuhuma hizo, ambazo alisema zimeibuka kwa nguvu katika siku za hivi karibuni.

Kutokana na hali hiyo, alisema serikali inazichunguza ili kufahamu ukweli wa kilichotokea na kwamba ukipatikana ushahidi wa kutosha, hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya taifa.

Kauli hiyo ya Pinda ambayo ni ya kwanza kutolewa na serikali tangu kuibuliwa kwa tuhuma hizo dhidi ya Mkapa na aliyekuwa Waziri wake wa Nishati na Madini, Daniel Yona, inafuatia maswali yaliyoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed.

Katika swali lake la msingi, Hamad ambaye pia ni Mbunge wa Wawi (CUF), alisema Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 1995, inamzuia mtumishi yeyote wa serikali kutumia ofisi ya umma (serikali) kufanya shughuli binafsi.

“Sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuna taarifa kwamba, Mheshimiwa Rais Mstaafu Mkapa na kiongozi mwingine wa serikali ya awamu ya tatu, walitumia ofisi zao kuanzisha kampuni binafsi je, serikali inasema nini juu ya hilo?” aliuliza.

Baada ya Pinda kujibu swali hilo, Hamad aliuliza swali la nyongeza akisema: "Kwa kuwa tuhuma dhidi ya watu hao, ni za muda mrefu, BRELA (Kitengo cha serikali cha Kusajili Makampuni), inalifahamu suala hilo na kuna watu wengine waliobainika kutenda kosa kama hilo walichukuliwa hatua. Kwa nini serikali imekuwa na kigugumizi kuwafikisha mahakamani watu hao?"

Waziri Mkuu alisisitiza kuwa kinachofanywa na serikali hivi sasa ni kuangalia iwapo kuna jinai katika tuhuma zinazowakabili watu hao na kwamba, itakapojiridhisha itachukua hatua zinazotahili kwa maslahi ya nchi.

Februari mwaka huu, mawaziri watatu akiwamo waziri mkuu, Edward Lowassa walijiuzulu kutokana na kukumbwa na kashfa ya mkataba wa kampuni kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond na hivi karibuni, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge amejiuzulu baada ya kutuhumiwa kuwa na dola za Marekani milioni moja ambazo zimewekwa katika Kisiwa cha Jersey ambazo zinahusishwa na ununuzi tata wa rada.

Tuma maoni kwa Mhariri
 
Nisome tena! Ninachotaka kujua kuna sheria inakataza hili? Nauliza hili kwa sababu hawa jamaa walipokaa pale Zanzibar walijihalalishia karibu kila kitu; sasa isije ikawa hili nalo lilihalalishwa halafu Mkapa atakapofungua mdomo tukabaki kushika matama! Mimi nimeanza kuwa mwoga sana maana isije ikawa tunapambana na hawa jamaa moja moja na kuacha mfumo uliowalinda kufanya yote haya. Sijasikia kabisa kule bungeni wabunge wetu waki-cite specifically vipengele vya sheria ambavyo Mkapa na wenzake walivunja. Nilichosikia ni wao wabunge wetu kulia kama vile sisi tunavyolia hapa JF na wananchi wa kawaida, sasa sidhani kama kulia pekee kutamfikisha Mkapa kwenye witness box. Kitakachomfikisha Mkapa mahakamani ni criminal offence na sio moral offence, ndio maana hapa tulipofikia sasa inabidi tuwe makini sana hasa tukizingatia uimara wa Mkapa wa kujibu hoja!

Mkapa kachemsha. Mkapa hana uimara wowote wa kujibu hoja. Uimara wake uliuona kwa kujibu hoja ambazo yeye hakuwa mharifu. Na hajawahi kujibu hoja yoyote wakati yeye akiwa ni mtuhumiwa na kukiwepo na vithibitisho vinavyohamasisha umma kuwa yeye ni mharifu.
 
Mimi naona kuanza kuchokonoa mambo ya Mkapa ni kazi bure ilhali kuna watu ambao ushahidi dhahiri dhidi yao upo wazi na umeshatumika hata kuwatoa kwenye madaraka, lakini bado wanatesa mitaani na pesa walizotuibia: Lowassa, Karamagi, Msabaha, Chenge (angalao hawa ushahidi umeshawekwa mezani na wameshindwa kuupinga ndio maana imewabidi kujiuzulu).

Sasa kuanza kuchokonoa wengine wakati hawa waliokwishapatikana dhahiri kabisa hawajachukuliwa hatua za kisheria mimi naona ni kupoteza muda. Ni kupoteza nguvu tu sawa na kujisumbua kulima eneo kubwa bila kupanda chochote, kule tulikotifua sasa magugu yanaoteana kabla hatujapanda chochote, bado tunajisumbua kutifua tu, ni dalili ya wehu! Wapelekwe mahakamani kwanza hawa waliokwisha kupatikana, huyo Mkapa kama anahusika atajikuta tu na yeye anaingia humohumo. Au hata yeye Mkapa akiona maswahiba wake wanaburuzwa kortini atajua kweli arobaini yake iko karibu na watu hawana utani. Kwa mwendo ninaouona hapa sitashangaa kusikia kuwa Mkapa huko Lushoto anakofyonza whisky anaangalia matukio yote haya na kuchekelea maana ameshawafananisha na lile kundi la ze Comedy la kina Masanja Mkandamizaji!
 
Hata hivyo, kama wabunge wakiamua kufuata taratibu hizo na kama serikali haitaweka vikwazo, Mkapa anaweza kushtakiwa na kuhukumiwa kutokana na matendo ambayo yatabainika kayafanya wakati akiwa rais na ambayo ni kinyume na maadili ya uongozi.

Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa tayari baadhi ya wabunge wamejipanga sawa kuhakikisha wanaendelea kutoa hoja binafsi za kuwabana vigogo wote waliohusika katika ufisadi.

Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanaona hatua hiyo ya Kikwete ni ya kijasiri na inapaswa kufanyika wakati huu ambao nchi imekumbwa na ufisadi wa kutisha.

Hata hivyo, baadhi ya watu wanaona kwamba hatua ya kumchunguza na kisha kumchukulia hatua Rais aliyeondoka madarakani ni nzuri lakini pia Rais aliyepo madarakani naye anapaswa kuwa msafi ili anayekuja asije kumwigiza naye katika matatizo.

a81e14513982753a4afb7b4ee8f4979d.jpg
 
THISDAY REPORTER
Musoma

THE family of the late Mwalimu Julius Kambarage Nyerere intends to summon ex-president Benjamin Mkapa to Butiama Village next month to discuss widespread allegations of corruption and abuse of office now besetting the former head of state.

A member of the Nyerere family, Peter Wanzagi, has confirmed to THISDAY that Mkapa, who holds the position of honorary son of Nyerere’s Zanaki tribe, will be called to the family meeting scheduled for next month.

He will be asked to explain the allegations being made against him, Wanzagi said.

The family meeting at Nyerere’s birthplace of Butiama in Mara Region, will be chaired by the current Zanaki tribal chief Japhet Wanzagi.

Said Peter Wanzagi, who is also Butiama Village councillor: ’’Mkapa is one of us (family), so we have seen fit to call him to the family meeting, where we will discuss these allegations against him.’’

2cqmzcz.jpg
 
Wasiwasi wangu bwana ni pale Mkapa atakapoongea. kwa kadri tunavyomjua Mkapa, ni muongeaji mzuri mwenye kupenda sana kutumia nguvu ya ushahidi kuliko hisia. Sasa wasiwasi so far sasa hivi madai mengi ya ufisadi wa Mkapa yanaelea sana. Sijasoma vizuri sheria ya maadili, lakini sijaona hasa mtu akijenga hojahoja sawasawa katika mantiki ya ushahidi wa kisheria wa kumtia hatiani Mkapa. Isije ikawa tunapambana na Mkapa badala ya mfumo wa kisheria za kifisadi ambazo zinalinda ufisadi. Isije ikawa kila kitu alichofanya Mkapa kuhusu uwekezaji wa kifisadi ANBEM, Kiwira, etc akawa alifanya ndani ya sheria.

Sasa kama sheria mbovu ndizo zilizomlinda Mkapa akafanya yote anayodaiwa sasa hivi siku akiongea atatuumbua sana na atakuwa amewasafisha mafisadi wengi mno na kuonyesha kwamba wengi wetu tunaongeaga kwa hisia zaidi. Kwa kifupi, wasiwasi wangu ni huu: isije ikawa tunapambana na individuals tukifikiri walifanya makosa nje ya sheria kumbe walifanya makosa yanayolindwa kikamilifu kabisa na mfumo wa kisheria. I hope am wrong and one day Mkapa and the company will be brought to the law before their days on this earth expire as it happened to Dito!

Sasa kwa kuanzia ili tumuwahi Mkapa kabla hajaanza kushuka mawe yake, hebu wale wanaoujua hizi sheria alizovunja Mkapa vizuri, tuwekee hapa kipengele baada ya kipengele na jinsi Mkapa na hayo mauwekezaji yake alivyozivunja ili tumkome nyani gladi sawasawa!

Kitila ,

Mbona unakariri , ni kweli Mkapa anajua kuongea lakini ushahidi juu ya maovu yake haupingiki. Hivi ni sheria kuanzisha kampuni ukiwa ikulu na kutumia inside information kwa manufaa binafsi " kununua kampuni " sio kosa?

Baadhi ya vifungu vilivyovunjwa unaweza kuviona kwenye hii website :

http://watanzaniaoslo.blogspot.com/2007_08_20_archive.html
 
Kitakachomfikisha Mkapa mahakamani ni criminal offence na sio moral offence, ndio maana hapa tulipofikia sasa inabidi tuwe makini sana hasa tukizingatia uimara wa Mkapa wa kujibu hoja!

Mkuu Kitila, Heshima mbele:-

Makapa ana kesi nyingi sana za kujibu mkuu, vipi recently umekuwa ukitetea mafisadi, nakumbuka hukuwa na kauli za kimapinduzi kuhusiana na ufisadi wa Lowassa na kujiuzulu, here you are again na makapa vipi mkuu?

Chenge unafikiri kwa nini amejiuzulu kama hela zake ni za halali? chenge amepata hela zile akiwa mwanasheria mkuu wa makapa, na katika kutia dole tu kwenye deal ya Radar, sasa makapa mwenyewe alipewa ngapi? Mramba alipewa ngapi? Mgodi wa Kiwira haukutangazwa zabuni sasa yeye na Yona walijuaje kuwa unauzwa? Mgodi "uliotakiwa" kuuzwa kwa shillingi miilllioni 700, wao wakaununua kwa shillingi millioni 70 tu? Unasema kwamba ukifanyika uchunguzi wa kisheria hana makosa huyu fisadi? You must be kidding me!

Hivi unafikiri lile "Faili" mtandao walilompa hawana copy yake? Mkuu Kitila wakati mwingine kunyamaza ni busara pia na hasa kwa mtu kama wewe kichwa!
 
🙄 Imeshapikwa! 😀 Tehe he Halloooo! Haya sasa kazi hapa...wapulizaji wa moto huo...Where we dare... Au?
 
Posted Date::4/26/2008
Serikali ya Rais Kikwete yawasha moto kumchunguza Rais Mstaafu Mkapa
Na Mwandishi wetu

SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete imeamua kutofautiana na zile za marais waliomtangulia kwa kutamka uamuzi mzito ambao haukuwahi kufanyika tangu Tanzania ipate uhuru, kwa serikali yake kuamua kuchunguza kashfa ya Rais Mstaafu , Benjamin Mkapa.

Uamuzi huo umetoa mwelekeo mpya wa serikali ya Kikwete kwamba sasa ameamua kufumba macho na kuwatosa watu muhimu kwake wanaotuhumiwa kwa ufisadi bila ya kujali wana nyadhifa gani.

Kitendo cha kuachia ngazi mawaziri wanne katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na kashfa za ufisadi na kuanza kumchunguza Mkapa kinaonyesha wazi kuwa sasa shikizo la wananchi na nchi wahisani kuhusu vitendo vya ufisadi limemfanya Kikwete abadili mwelekeo wa utendaji wake wa kazi.

Hata hivyo, mtihani mkubwa ulioko mbele yake ni namna atakavyoendesha uchunguzi dhidi ya Mkapa na endapo atabainika amehusika kutumia madaraka vibaya na kukiuka maadili ya uongozi akiwa Ikulu, je ataweza kumfikisha mahakamani?

Mtihani utakuwa mgumu kwa Kikwete kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka vipengele vinavyomlinda mno rais aliyepo madarakani au ambaye amestaafu.

Kwa mujibu wa katiba ibara ya 46 (3) wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilotenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya urais, ila tu kama angalau siku 30 kabla shauri kufunguliwa mahakamani, rais atapewa au ametumiwa kwanza taarifa ya madai kwa maandishi kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge na taarifa hiyo ikiwa na maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina la mdai na anwani ya mahali anapoishi na anapaswa aliainishe jambo analodai.

"Isipokuwa kama ataacha kushika maradaka ya urais kutokana na masharti ya ibara ya 46 (A) (10), itakuwa ni marufuku kushitaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo alilofanya yeye kama rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya rais."

Hata hivyo, Bunge linaweza kumshitaki rais kama ametenda makosa ambayo yanavunja katiba au sheria ya maadili ya viongozi wa umma.

Kwa mujibu wa katiba hiyo, kabla ya Bunge kumshitaki, taarifa ya maandishi iliyotiwa saini na kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku 30 kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa bungeni, ikifafanua makosa aliyotenda na ikipendekeza kuwa kamati maalum ya uchunguzi iundwe ili ichunguze mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya rais.

Iwapo uchunguzi wa serikali utabaini kuwa Mkapa anahusika katika kashfa ya kutumia vibaya ofisi ya umma alipokuwa madarakani, kuanzisha kampuni binafsi kinyume cha sheria ni wazi kwamba itabidi katiba ya nchi ifanyiwe marekebisho ili iwe rahisi kwa rais mstaafu kushtakiwa kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani.

Hata hivyo, kama wabunge wakiamua kufuata taratibu hizo na kama serikali haitaweka vikwazo, Mkapa anaweza kushtakiwa na kuhukumiwa kutokana na matendo ambayo yatabainika kayafanya wakati akiwa rais na ambayo ni kinyume na maadili ya uongozi.

Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa tayari baadhi ya wabunge wamejipanga sawa kuhakikisha wanaendelea kutoa hoja binafsi za kuwabana vigogo wote waliohusika katika ufisadi.

Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanaona hatua hiyo ya Kikwete ni ya kijasiri na inapaswa kufanyika wakati huu ambao nchi imekumbwa na ufisadi wa kutisha.

Hata hivyo, baadhi ya watu wanaona kwamba hatua ya kumchunguza na kisha kumchukulia hatua Rais aliyeondoka madarakani ni nzuri lakini pia Rais aliyepo madarakani naye anapaswa kuwa msafi ili anayekuja asije kumwigiza naye katika matatizo.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wiki hii aliliambia Bunge mjini Dodoma kuwa serikali ina taarifa za tuhuma hizo, ambazo alisema zimeibuka kwa nguvu katika siku za hivi karibuni.

Kutokana na hali hiyo, alisema serikali inazichunguza ili kufahamu ukweli wa kilichotokea na kwamba ukipatikana ushahidi wa kutosha, hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya taifa.

Kauli hiyo ya Pinda ambayo ni ya kwanza kutolewa na serikali tangu kuibuliwa kwa tuhuma hizo dhidi ya Mkapa na aliyekuwa Waziri wake wa Nishati na Madini, Daniel Yona, inafuatia maswali yaliyoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed.

Katika swali lake la msingi, Hamad ambaye pia ni Mbunge wa Wawi (CUF), alisema Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 1995, inamzuia mtumishi yeyote wa serikali kutumia ofisi ya umma (serikali) kufanya shughuli binafsi.

“Sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuna taarifa kwamba, Mheshimiwa Rais Mstaafu Mkapa na kiongozi mwingine wa serikali ya awamu ya tatu, walitumia ofisi zao kuanzisha kampuni binafsi je, serikali inasema nini juu ya hilo?” aliuliza.

Baada ya Pinda kujibu swali hilo, Hamad aliuliza swali la nyongeza akisema: "Kwa kuwa tuhuma dhidi ya watu hao, ni za muda mrefu, BRELA (Kitengo cha serikali cha Kusajili Makampuni), inalifahamu suala hilo na kuna watu wengine waliobainika kutenda kosa kama hilo walichukuliwa hatua. Kwa nini serikali imekuwa na kigugumizi kuwafikisha mahakamani watu hao?"

Waziri Mkuu alisisitiza kuwa kinachofanywa na serikali hivi sasa ni kuangalia iwapo kuna jinai katika tuhuma zinazowakabili watu hao na kwamba, itakapojiridhisha itachukua hatua zinazotahili kwa maslahi ya nchi.

Februari mwaka huu, mawaziri watatu akiwamo waziri mkuu, Edward Lowassa walijiuzulu kutokana na kukumbwa na kashfa ya mkataba wa kampuni kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond na hivi karibuni, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge amejiuzulu baada ya kutuhumiwa kuwa na dola za Marekani milioni moja ambazo zimewekwa katika Kisiwa cha Jersey ambazo zinahusishwa na ununuzi tata wa rada.

Tuma maoni kwa Mhariri

Kwenye redi redi mhh, mie yangu macho... hii poa Kula Breki!!!
 
i dont see this helping any one in the long view.
hiyo familia ya nyerere inataka sisi tukubali kuwa nchi yao au? ikiwa mkapa ni familia, dilini nae kifamilia......kwanini mseme nje
pia mkapa kutoswa na familia nyie sioni kutamuathiri vipi
 
Kitendo cha kutamka tu kwamba rais mstaafu atachunguzwa ni hatua moja kubwa sana kwa nchi zetu za kiafrika. Ukweli ni kwamba kwa sasa Mkapa hana hadhi tena ndani na nje hata kama mambo hayatafika kule wananchi wote tunapotaka yafike.

Kwa sasa hivi yuko kama kizuizini; hawezi kuongea, kushiriki shughuli zozote za nchi na hatimaye anaanza kukimbia waandishi. Jamani huyu bwana "Clean" anaweza kujinyonga. Subirini tu mtasikia!!
 
Kitila ,

Mbona unakariri , ni kweli Mkapa anajua kuongea lakini ushahidi juu ya maovu yake haupingiki. Hivi ni sheria kuanzisha kampuni ukiwa ikulu na kutumia inside information kwa manufaa binafsi " kununua kampuni " sio kosa?

Baadhi ya vifungu vilivyovunjwa unaweza kuviona kwenye hii website :

http://watanzaniaoslo.blogspot.com/2007_08_20_archive.html
"According to the Public Leadership Code of Ethics Act of 1995, a copy of which has been availed to THISDAY, a public leader shall be considered to have breached the Act if he or she acquires any significant financial advantage, or assists another person to acquire such gain, by ''improperly using or benefiting from information which is obtained in the course of his/her official duties and which is not generally available to the public".

Mkuu mimi nilikuwa nataka wanasheria wetu watusaidie, ili tuweze kujenga hoja sawasawa, sheria hasa ambayo Mkapa kavunja. Nashukuru umenipa hiyo link. Lakini baada ya kuisoma, bado sioni hasa sehemu inayomkataza Mkapa kuanzisha biashara akiwa yeye ni Rais. Hiyo sheria hapo juu ni kosa kama ametumia taarifa vibaya ambayo haipo wazi kwa public. Sasa, swali linakuja, je, ubinafishwaji wa mgodi wa kiwira haukutangazwa? Ukweli ni kwamba ilitangazwa ndani na nje ya nchi. Hii inakuonyesha jinsi ambavyo hii kesi itakuwa ngumu na jinsi ambavyo ni rahisi sana kwa akina Mkapa kushida.

At the end of the day all I am saying is that there is something fundamentally wrong with the present legal and administrative system of our country. Mchawi wa yote haya ni kuruhusu viongozi wetu kufanya biashara na serikali huku wakiwa madarakani. Kwa maneno mengine ni kuwa mfumo tuliokuwa nao unatoa nafasi kwa kila mtu kuwa shetani. Haishangazi basi kwamba watu waliokuwa kuwa clean kama Mkapa na wengine walipopata nafasi ya kuingia kwenye mfumo wa ushetani wakageuka kuwa mashetani wa kutisha. Kosa ambao tunalifanya sasa hivi katika haya mapambano ni kujaribu kumuua shetani bila kuua mfumo unaozalisha ushetani. Nadhani unaweza kuanza kupata picha ninapotoka na ninapoenda!
 
Mkuu Kitila,

Ni kweli inabidi tuwe waangalifu katika suala la Mkapa.Ni kweli kabisa inabidi tuainishe bayana ni sheria ipi au kifungu kipi huyu bwana alikivunja na kwamba ni kipengele kipi kilimzuia kufanya vile na yeye akaendelea na mipango yake kama kawa!.Maana kama tungelikuwa bado tunalitumia azimio la arusha huyu bwana tayari angekuwa kavunja vifungu kibao ila katika mfumo huu nina wasiwasi huyu bwana anaweza kupata pa kutokea.
 
hakuna mtu serious ambaye anaamini kitu kinachotoka kwenye mdomo wa Pinda,wote tunafuatilia mambo kwa karibu tunakumbuka acceptance speech yake.Huyu mtu hana confidence ya kuenforce chochote,kitu kizuri kinachotokea sasa hivi maneno yake yanasaidia kuchochea hasira za wananchi na kuendeleza mdahalo kwa siku nyingine
 
Back
Top Bottom