Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Urgent; Nani anaweza kutuambia exactly tarehe aliyotoa hotuba hii mzee Luhigo... kuna watu wamenipigia wanataka kuitumia kuwakumbusha Watanzania wenzetu ambao hawapati wasaa wa kusoma JF...
 
Wakuu hebu acheni siasa na shule kwenye wizi wa makapa, kama Chenge amechota hela zote zile kwenye deal ya Radar, makapa alipewa ngapi? Makapa ameiba hela nyingi sana za taifa letu kupitia Miundo Mbinu, in fact kuna menngi ambayo hayajasemwa bado ya uchafu wake, kama ni msafi kwa nini asiombe kuondolewa immunity akajisafishe mahakamani?

Hivi ni lini bingwa wa kujenga hoja Mwalimu, aliwahi kujificha nyuma ya political immunity?
 
Wasiwasi wangu bwana ni pale Mkapa atakapoongea. kwa kadri tunavyomjua Mkapa, ni muongeaji mzuri mwenye kupenda sana kutumia nguvu ya ushahidi kuliko hisia. Sasa wasiwasi so far sasa hivi madai mengi ya ufisadi wa Mkapa yanaelea sana. Sijasoma vizuri sheria ya maadili, lakini sijaona hasa mtu akijenga hojahoja sawasawa katika mantiki ya ushahidi wa kisheria wa kumtia hatiani Mkapa. Isije ikawa tunapambana na Mkapa badala ya mfumo wa kisheria za kifisadi ambazo zinalinda ufisadi. Isije ikawa kila kitu alichofanya Mkapa kuhusu uwekezaji wa kifisadi ANBEM, Kiwira, etc akawa alifanya ndani ya sheria.

Sasa kama sheria mbovu ndizo zilizomlinda Mkapa akafanya yote anayodaiwa sasa hivi siku akiongea atatuumbua sana na atakuwa amewasafisha mafisadi wengi mno na kuonyesha kwamba wengi wetu tunaongeaga kwa hisia zaidi. Kwa kifupi, wasiwasi wangu ni huu: isije ikawa tunapambana na individuals tukifikiri walifanya makosa nje ya sheria kumbe walifanya makosa yanayolindwa kikamilifu kabisa na mfumo wa kisheria. I hope am wrong and one day Mkapa and the company will be brought to the law before their days on this earth expire as it happened to Dito!

Sasa kwa kuanzia ili tumuwahi Mkapa kabla hajaanza kushuka mawe yake, hebu wale wanaoujua hizi sheria alizovunja Mkapa vizuri, tuwekee hapa kipengele baada ya kipengele na jinsi Mkapa na hayo mauwekezaji yake alivyozivunja ili tumkome nyani gladi sawasawa!

Mkuu Kitila,

Lakini si ni mfumo huo huo ambao ulikuwepo na bado akina Nyerere, Kawawa, Warioba bado hawakujirundikia mali?

Nafikiri kosa la Mkapa sio lazima liwe la kisheria na badala yake ni moral issue. Kutoka kuitwa clean mpaka kuitwa fisadi ni hatua kubwa sana.

Mimi sioni hata sababu ya kumshitaki Mkapa, amejiangusha yeye mwenyewe pamoja na watu ambao walimwamini miaka na miaka.

Sisi ambao tulipata scholarships pale wizarani miaka hiyo, tunajua kwamba Mkapa na Mahalu walikuwa wanachukua visenti. Hata nilipoona Mkapa anaanza kukwangua kila kitu, binafsi sikushangaa.

Mkapa ni looser kwenye hili maana hata asingeiba bado kwa mfumo wa Tanzania alikuwa na uhakika wa kutanua anavyotaka. Lakini sasa anaogopa hata kuonana na Watanzania wenzake. Kuna faida gani hapo?

Adhabu kubwa kwa Mkapa ni kwa wananchi kumdharau na kumpuza. Sioni kama kuna haja ya kumbuluza mahakamani, kwa sheria zetu za sasa inaweza kuwa ni kupoteza tu pesa za walipa kodi. Adhabu anayopata Mkapa sasa ni kubwa kuliko hata kumfunga jela mwaka mmoja. Kinachotokea TZ ni fundisho kubwa sana kwa viongozi hata wa baadaye.

Labda muhimu ni kutengua tu baadhi ya contracts alizoingia kama vile mgodi wa Kiwira na nyumba walizojipatia bure yeye na mkewe.
 
Mkuu FMES,

Usitie shaka kabisa kuhusu chuki yangu kwa mafisadi. Tena mimi ni mojawapo ambaye nina chuki kabisa na Mkapa sio kwa wizi wake tu lakini pia kwa kuturudisha nyuma sana kwenye demokrasia ya vyama vingi. Mkapa kwangu ni ovyo kwa viwango vyote vya neno ovyo. To me he is so far the worst and the most immoral president our country has had. Tukianza kuorodhesha uchafu na makosa ya Mkapa hii forum haitatosha!

Hoja yangu ni kwamba hatutafanikiwa sana kwenye haya mapambano kwa kuwaua tunaodhani ni mashetani bila kuua mazalio ya ushetani! Hapa ndipo hoja yangu kuhusu sheria inapokuja. Ok, Lowasa kajiuzulu, Chenge naye kaenda na maji, n.k. Lakini je, kwa hatua hizi ndio tuseme tunaanza kuushinda ufisadi? Mimi nasema hapana kwa sababu so far hatujagusa mazalio ya huu ufisadi ambao ni kwenye mfumo wa utawala na sheria. Numeshasema mara nyingi hapa kwamba kwa hulka ya binadamu, kila mtu anaweza kubadilika kuwa chochote. Kwa hiyo wataalamu wanasema ili uweze kuzuia ubinafsi wa viongozi wa kisiasa ni lazima uweke misingi imara ya kitaasisi ya kuzuia watu kufanya maovu hayo na pale watakapopatikana wamefanya maovu basi kuwe na misingi imara ya kuwashugulikia. Ndio maana wenzetu wanakazana sana kuweka taasisi imara. Hii imewasaidia kwamba hata mtu kama Bush ameweza kuwa Rais wa America kwa miaka nane bila America kuyumba. Nakwambia kwetu kwa mfumo tulio nao siku tukipata Rais wa aina ya Bush ndio nchi itakuwa imekwenda hivyo!

Sasa angalia, utasemaje kwamba tunapambana na ufisadi wakati mfumo wa PCCB ni huohuo, nguvu za Rais wetu ni hizohizo. Utasemaje tunapambana na ufisadi wakati waziri mkuu anasema kwamba serikali haiwezi kuwakamata baadhi ya majambazi kwa kuwa wana nguvu sana na wanaweza kuiyumbisha serikali? Are you there mkuu FMES? kama majambazi waliotuibia wanaweza kuitisha serikali yetu wewe huoni kwamba hapo tunashida kubwa sana na mfumo wetu wa utawala?

So, there you are. Simtetei kabisa Mkapa. Ila nina wasiwasi sana kama tutaweza kumfikisha Mkapa mahakamani. Wasiwasi wangu ni mkubwa zaidi kama akifika mahakamani tutaweza kumshinda maana ni yeye aliyeweka hizo sheria kuhakikisha kwamba zinamlinda katika wizi wake huo. na je, hujiuliza Chenge anatoa wapi kiburi chote hicho? Bila shaka, yeye kwa kuwa alikuwa mwanasheria mkuu, anajua fika kabisa kuwa hakuna cha kufanya.

Kwa hiyo mzee hebu tukazanie yote. Wakati tukiwapiga mawe hawa akina Mkapa, tuwe tunarudi nyuma na kuangalia mifumo iliyowafanya wawe walivyo ili nayo tuishambulie! Na kikubwa zaidi ni muhimu kabisa tufike mahala tubadilishe chama kinachotawala, najua hili tutatofautiana, but think about it!
 
..duuh, Mtanzania bwana........ nawe umedumu kweli mshirika, eti "mwaka 1995 niliwahi kuandika"....... enzi hizo mimi nd'o najifunza a e i o u na ba be bi bo bu,..... kumbe mwenzetu ulishaanza 'kumkoma nyani giladi' tayari!! loooooh, kweli jf ina magwiji 🙂

have a nice wkend buddy,

kunradhi wana jf kwa kuwa out of topic.

SteveD,

Inabidi uwe unatoa shikamooh! kwi kwi kwi kwi!!!

Wengine tulipata bahati ya kuijua Internet mapema mno, asante magwiji wa
Tanzanet kama akina Dr. Ali, Twakyondo, Mwikalo na wengine. Wakati huo nilikuwa Europe lakini hata huku majuu watu walikuwa hawajui internet ni nini au email ni nini? Mimi nilikuwa darasa la Computer Science lakini mpaka mwaka wa pili ndio nikajua hata kutumia emails kuwasiliana na wengine nje ya nchi. Kupitia Tanzanet nikajifunza kumkoma Nyani Giladi, lakini kikubwa zaidi nikaipenda IT mpaka leo. Ndio maana hivi vijiwe siwezi kuvihama hata niwe nani!
 
Mkuu Kitila,

Mimi sioni hata sababu ya kumshitaki Mkapa, amejiangusha yeye mwenyewe pamoja na watu ambao walimwamini miaka na miaka.Sisi ambao tulipata scholarships pale wizarani miaka hiyo, tunajua kwamba Mkapa na Mahalu walikuwa wanachukua visenti. Hata nilipoona Mkapa anaanza kukwangua kila kitu, binafsi sikushangaa.

Adhabu kubwa kwa Mkapa ni kwa wananchi kumdharau na kumpuza. Sioni kama kuna haja ya kumbuluza mahakamani, kwa sheria zetu za sasa inaweza kuwa ni kupoteza tu pesa za walipa kodi. Adhabu anayopata Mkapa sasa ni kubwa kuliko hata kumfunga jela mwaka mmoja. Kinachotokea TZ ni fundisho kubwa sana kwa viongozi hata wa baadaye.
Labda muhimu ni kutengua tu baadhi ya contracts alizoingia kama vile mgodi wa Kiwira na nyumba walizojipatia bure yeye na mkewe.

Kama kweli tunataka hili la Mkapa liwe fundisho kwa vizazi vya sasa na vijavyo, inabidi Mkapa achukuliwe hatua kali mno. Moja afilisiwe mali zake zote ambazo amazipata baada ya yeye kuwa Rais ikiwa pamoja na makampuni yote anayoyamiliki na pia anyanywe shares pale ambapo yeye ni shareolder. Pili afungwe kifungo cha maisha. Afungwe mwaka mmoja? no way!

Ukisema kwamba tumdharau tu itasaidia nini kwa wananchi wa kawaida ambao Mkapa amewaweka katika Ukapa usioelezeka? Hiyo haitakuwa adhabu, mtu mwenyewe jeuri, hata mkimneglect yeye haitamsumbua na ninahakika hata sasa hakuna kilichomkuna zaidi ya kusema 'this country bwana, is very stupid and poor'
 
Mtanzania:

Sio kweli kwamba akina Nyerere na akina Kawawa hawakufanya ufisadi kwa utashi tu. Ndio pamoja na utashi na moral standing yao, usisahau hawa bwana walijiwekea vizingiti vizito sana chini ya Azimio la Arusha ambalo hawa jamaa wa CCM mpya wakaja kuisambaratisha. So, there you are; there was a very elaborate and effective system to prevent leaders from falling into the devil's immoral track ambayo sasa hivi hatuna!

Hiyo ya kumdharau nakubaliana na wewe kabisa. Naogopa sana ya kumfikisha mahakamani Mkapa kunaweza kukamsafisha kuliko kumtia hatiani and the consequences will be far reaching maana hata mafisadi wengine watakuwa wamesafishwa kwa njia moja au nyingine. Hii adhabu wanayopata sasa hivi hawa jamaa ya kuzomewa na kudharauliwa na wananchi ni ya maana zaidi kuliko ya kupelekwa mahakamani.
 
Kitila ,

Mwanzoni uliuliza kama kuna sheria zinazoweza kumbana Mkapa katika hili , nimekupatia source lakini baada ya wewe kuquestion validility ya hizo sheria katika hii issue wewe umeamua kuleta siasa. Kitila umeamua kwa makusudi kutumia kifungu hiko kimoja kwa sababu unajua ya kuwa kina loop holes lakini kama ungesoma vizuri ungeona ya kuwa , kipengele hiki kina deal na hizo loop holes.

Apart from improper use of, and benefit from, information obtained in the course of carrying out official duties and which is not generally available to the public, Section 12 (1) of the Public Leadership Code of Ethics Act also states other ways in which a public leader will be considered to have breached the law .

Hili suala halina siasa hata kidogo na sheria zetu za sasa hivi kama zitatumiwa vizuri zinatosha kabisa kummmaliza huyu bwana.Mimi nataka nichambue hivyo vipengele na jinsi gani huyu muungwana alivyhusika na huu wizi

And section 14 (1) requires that ’’where a public leader has an interest in a contract that is made, or is supposed to be made by the government, and has not made a sufficient declaration under subsection (4) in relation to the contract, the public leader shall as soon as practicable make a declaration of his interest in relation to the contract, specifying the nature and extent of his interest.’’

Jee Mkapa alifanya hivi katika Mkataba wa Kiwira ? Wewe unafikiri ni kwa nini kwa mara ya kwanza Karamagi anatangaza sasa hivi kwamba ana own 35% ya share za TICTS , sio kwamba amependa bali anajua nini kinakuja .

section 13 (1) of the same legislation also states that ’’a public leader shall not speak in the Cabinet, National Assembly, in a local government council or a committee thereof, or in or at any other official forum or part of it, on any matter in which he has a direct pecuniary (financial) interest unless he has disclosed the nature of that interest to the Cabinet, the Assembly, the council, committee or such other forum or part of it.’’

Jee Mkapa alifanya hivi kabla ya kuzungumza kwenye hivyo vikao . Vipi kuhusu Yona alideclare interest zake kabla ya kuzungumza kwenye vikao mbali mbali vya bunge wakati alipokuwa waziri ?

Section 14 (3) states that ’’the interest of the spouse or spouses, or of the children of a public leader in relation to the government contract, shall be deemed to be the interest of the public leader.’’

Huu ndio msumari kwenye coffin, hapa Mkapa hawezi kukimbilia kusema ya kuwa ilikuwa kampuni ya mama. Kwani kampuni ya mama according to hii sheria ni ya kwake pia.Mimi nadhani ni muhimu kuangalia hivi vipengele kabla ya kuzilaumu sheria zetu.
 
And section 14 (1) requires that ''where a public leader has an interest in a contract that is made, or is supposed to be made by the government, and has not made a sufficient declaration under subsection (4) in relation to the contract, the public leader shall as soon as practicable make a declaration of his interest in relation to the contract, specifying the nature and extent of his interest.''

Jee Mkapa alifanya hivi katika Mkataba wa Kiwira ? Wewe unafikiri ni kwa nini kwa mara ya kwanza Karamagi anatangaza sasa hivi kwamba ana own 35% ya share za TICTS , sio kwamba amependa bali anajua nini kinakuja .

section 13 (1) of the same legislation also states that ''a public leader shall not speak in the Cabinet, National Assembly, in a local government council or a committee thereof, or in or at any other official forum or part of it, on any matter in which he has a direct pecuniary (financial) interest unless he has disclosed the nature of that interest to the Cabinet, the Assembly, the council, committee or such other forum or part of it.''

Jee Mkapa alifanya hivi kabla ya kuzungumza kwenye hivyo vikao . Vipi kuhusu Yona alideclare interest zake kabla ya kuzungumza kwenye vikao mbali mbali vya bunge wakati alipokuwa waziri ?

Section 14 (3) states that ''the interest of the spouse or spouses, or of the children of a public leader in relation to the government contract, shall be deemed to be the interest of the public leader.''

Huu ndio msumari kwenye coffin, hapa Mkapa hawezi kukimbilia kusema ya kuwa ilikuwa kampuni ya mama. Kwani kampuni ya mama according to hii sheria ni ya kwake pia.Mimi nadhani ni muhimu kuangalia hivi vipengele kabla ya kuzilaumu sheria zetu.

Rufiji: very good and many thanks for the trouble to bring along all those useful legal clauses.

Hakuna neno kabisa kuweka siasa kwenye hili maana thread yenyewe hii inahusu siasa!

Ok, vipi ikiwa jibu kwa maswali yako yote hapo juu ni ndiyo, what is next?

Katika sera ya ubinafishaji, kuna ubaya gani kama kungekuwa na sheria inayowakataza viongozi wa serikali kununua share katika mashrika ya umma yanayobinafisishwa? Huoni kwamba kama sheria kama hii ingekuwepo hili swala la Kiwira ingekuwa a non-issue kwa sababu hata hao akina Mkapa isingewezekana wanunue huo mgodi. Piga hatua mbele zaidi, ni nani waliomuuzia Mkapa huo mgodi kama kweli sheria inakataza kufanya hivyo? Sasa mbona hao waliomuuzia hatuwataji ina maana wao hawajavunja hiyo sheria?

Kwa maneno mengine, kama hawa jamaa wasingelibaka Azimio la Arusha pale Zanzibar huu utitiri wa ufisadi tusingeuona. Kwa hiyo tunarudi kulekule, kwa kiasi kikubwa ufisadi wa akina Mkapa ulifanikishwa na udhaifu wa mfumo wetu wa kiutawala na kisheria na ni mfumo huohuo unaoendelea kuwalinda na wawe na kiburi. Na hii itathibitika siku Mkapa akiamua kunyanyau mdomo. Atatusambaratisha kwa sheria hizohizo ambazo yeye alizi-architect na wabunge wetu wakizipitisha pale Dodoma kwa kishindo na mbwembwe chini ya kiburi cha Chama cha Mapinduzi. ndugu yangu tupende tusipende, bila kuweka sawa mifumo yetu ya utawala na sheria, mafisadi wataiamliza nchi yetu!
 
Kitila ,

Mwanzoni uliuliza kama kuna sheria zinazoweza kumbana Mkapa katika hili , nimekupatia source lakini baada ya wewe kuquestion validility ya hizo sheria katika hii issue wewe umeamua kuleta siasa. Kitila umeamua kwa makusudi kutumia kifungu hiko kimoja kwa sababu unajua ya kuwa kina loop holes lakini kama ungesoma vizuri ungeona ya kuwa , kipengele hiki kina deal na hizo loop holes.

Apart from improper use of, and benefit from, information obtained in the course of carrying out official duties and which is not generally available to the public, Section 12 (1) of the Public Leadership Code of Ethics Act also states other ways in which a public leader will be considered to have breached the law .

Hili suala halina siasa hata kidogo na sheria zetu za sasa hivi kama zitatumiwa vizuri zinatosha kabisa kummmaliza huyu bwana.Mimi nataka nichambue hivyo vipengele na jinsi gani huyu muungwana alivyhusika na huu wizi

And section 14 (1) requires that ’’where a public leader has an interest in a contract that is made, or is supposed to be made by the government, and has not made a sufficient declaration under subsection (4) in relation to the contract, the public leader shall as soon as practicable make a declaration of his interest in relation to the contract, specifying the nature and extent of his interest.’’

Jee Mkapa alifanya hivi katika Mkataba wa Kiwira ? Wewe unafikiri ni kwa nini kwa mara ya kwanza Karamagi anatangaza sasa hivi kwamba ana own 35% ya share za TICTS , sio kwamba amependa bali anajua nini kinakuja .

section 13 (1) of the same legislation also states that ’’a public leader shall not speak in the Cabinet, National Assembly, in a local government council or a committee thereof, or in or at any other official forum or part of it, on any matter in which he has a direct pecuniary (financial) interest unless he has disclosed the nature of that interest to the Cabinet, the Assembly, the council, committee or such other forum or part of it.’’

Jee Mkapa alifanya hivi kabla ya kuzungumza kwenye hivyo vikao . Vipi kuhusu Yona alideclare interest zake kabla ya kuzungumza kwenye vikao mbali mbali vya bunge wakati alipokuwa waziri ?

Section 14 (3) states that ’’the interest of the spouse or spouses, or of the children of a public leader in relation to the government contract, shall be deemed to be the interest of the public leader.’’

Huu ndio msumari kwenye coffin, hapa Mkapa hawezi kukimbilia kusema ya kuwa ilikuwa kampuni ya mama. Kwani kampuni ya mama according to hii sheria ni ya kwake pia.Mimi nadhani ni muhimu kuangalia hivi vipengele kabla ya kuzilaumu sheria zetu.

Kitila

Ulipo uliza mwanzoni nilijua unatafuta msaada wa kisheria kujua kama kweli Mkapa ana kesi ya kujibu.

waziweka data za kisheria ambazo kwa sisi ambao pamoja na kwamba hatujasomea sheria lakini tukaona kila kitu kiko wazi.

Lakini baadaye ukaonekana kugeuka na kuona tayari hizo sheria zote haziwezi kumuweka Mkapa Matatani kwa sababu mojawapo anajua kujieleza na sheria zetu ni mbovu.

Hivi ningependa ufafanuzi kibovu ni mahakama zetu?, Sheria zetu au nini?

Mimi sioni haja na sitaona huruma kwa Mtanzania yeyote aliyepewa madaraka na kuyachezea kwa manufaa yake.

Vinginevyo haina haja ya kuwa na viongozi. Mimi pendekezo potelea mbali akashinda mahakamani(kama yuko sawa atakuwa amejisafisha)Mkapa ni Lazima aende akajisafishe mahakamani. Hili litakuwa fundisho kwa viongozi wa sasa na viongozi wa vizazi vijavyo.

Pia ukiona mkapa amekanyaga mahakamani ndio utakuwa mwanzo wa kuhakikisha kila aliyefanya uhujumu uchumi anafikishwa ktk vyombo vinavyohusika.

Hakuna cha uhuruma katika masirahi ya taifa. Huwa wanasema ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni. Hakuna haja ya kuangalia usoni FISADI yeyote.
 
...mimi naamini mkapa anayo makosa yake lakini kamwe hii haitaharibu historia yake iliyotukuka ya kujenga uchumi..hapa siongelei ushabiki economic indicators alizotuachia ni ushahidi....

mimi naamini njia bora ya kumdhalilisha mkapa ni kwa rais aliyemadarakani kum outsamart kiutendaji na wataalam wa uchumi watuambie hivyo...zaidi ya hayo tutabakia kumlaumu mkapa wakati kazi haifanyiki...

watanzania tuliowengi tunaendelea kumuheshimu mzee mkapa kutokana na rekodi yake ..... kama kuna ufidadi thats another case kwa kuwa serikali hii leo ufisadi upo na kazi hakuna...saasa si bora mkapa!!!!

kama mkapa kuna alichochukua mnakitaka mwambieni arudishe ....msimwaribie rekodi yake!!!!!!
 
Kakindomaster,

Kwanza nikushukuru kwa analysisi nzuri . Ni kweli mwanzoni Kitila aliuliza kama kuna sheria ambazo zinaweza kumbana Mkapa katika hili sasa naona premise ya swali lake imeshift ghafla ! Kuanza kuzungumzia kwa nini Azimio la Arusha lilivunjwa haitasaidia katika kutatua tatizo , suala la kuangalia ni jee Mkapa alivunja sheria za nchi wakati ule ?

Kwa nini tuumize vichwa kuhusu Sheria ambazo hatuna wakati sheria tulizonazo zinatosha kumtia huyu bwana hatiani .

Kitila pia ameuliza Piga hatua mbele zaidi, ni nani waliomuuzia Mkapa huo mgodi kama kweli sheria inakataza kufanya hivyo?

Hakuna mtu aliyemuuzia huyu mtu mgodi bali amejiuzia yeye mwenyewe kwa kutumia nafasi yake.
 
...hiyo familia ya nyerere inataka sisi tukubali kuwa nchi yao au? ikiwa mkapa ni familia, dilini nae kifamilia......kwanini mseme nje...pia mkapa kutoswa na familia nyie sioni kutamuathiri vipi

Gaijin, heshima mbele Mkuu.

Tatizo nadhani si hii familia bali ni jarida la THISDAY. Ndio wamechora picha ya 'the small but influential Zanaki tribe.' Natanguliza taadhima zote kwa Wazanaki, lakini katika masuala ya Kitaifa na Siasa wana influence nini wao - au kabila lingine lolote - cha kumtisha Mkapa? Yani Media ya Bongo inatia aibu!

Tunaingia katika mjadala wa Kitaifa na kupata mategemeo ya suluhisho la ishu kwa sababu mja fulani wa THISDAY ametoa ma assumption yake ya ajabu kuhusu uzito wa kikundi fulani.

Mzito kuliko wote katika hii familia ni Mzee Butiku, ambae nae hakuweza kumfanya Mkapa abadili msimamo. Watoto watoto wengine wa familia Mkapa anawaona cha mtoto tu. Msimamo wa Mkapa ni kuto ongelea hili jambo. Sasa nini kitamfanya ghafla akubali kufungua mdomo eti kuogopa kutoswa na familia ya 'influential Zanaki tribe'? Ni kuto kumuelewa Mkapa.

Tanzania hakuna Media. Kuna uhuru wa vyombo vya habari wanasema, lakini ni sawa na Mtwana aliye mruhusu Mtumwa asiye jua kusoma asome, katika mfumo ambao Mtumwa alikuwa haruhusiwi kusoma. Hakuwahi kujifunza kusoma, kwa hiyo sio hatari kwa Mtwana kumruhusu asome!
 
Kuhani Mkuu

Wewe unahisi nini kinapswa kifanyike ili Mkapa azungumze ? cause we would like to hear his side of story also.
 
Kitila Mkumbo,
Mkuu nakubaliana na hoja zako na kweli sheria zilizotungwa na chama kimoja cha CCM kupitia Azimio huko Zanzibar ni sheria ambazo zinahitaji mabadiliko haraka iwezekanavyo.
Kama utakumbuka kuna siku nimeuliza swali moja zito na sikupata jibu kabisa. Swali lenyewe lilikuwa msimamo wa vyama vya Upinzani kuhusiana na Azimio la Arusha!.. Je, wao wanapinga Azimio hilo na kama kweli wanalipinga inakuwaje wameshindwa kulisimamisha Bungeni! - Are they Opportunist? wakitegemea nao siku ya kuvuta zao! na wanashindwa nini kufanya maandamano yanayohusiana na Azimio hilo la Kishetani, wakaendelea kugombea uchaguzi ktk mfumo wa shetani?..Inatisha..

Mkapa alijua anafanya nini pamoja na yote hayo nadhani FMES kesha tuonyesha sehemu alizoteleza kisheria kama ununuzi wa Rada. Pia sehemu zote ambazo zimekutwa na Ufisadi na viongozi wake wa chini kujiuzuru leo ni sehemu kubwa ya ushahidi unaomhusisha yeye kama rais wa nchi. Bado kuna ushahidi kibao ameushikilia leo hii wa majumba ya serikali ambayo familia yake na hasa mkewe anayashikilia. Kisha tukiangalia Kiwira ambayo thamani yake ilikuwa millioni 700 na imeuzwa kwake kwa millioni 70 ni sababu tosha ya kufungua mashtaka kisha hata kama Mahakama itashindwa kumfunga basi nina hakika ushahidi mdogo mdogo uliopo uta.maliza...
Kumbuka tu watakao msimamisha Mahakamani ni wananchi na sheria mkuu ni msumeno kama alivyohukumiwa Saadam Hussein - Sababu ndogo sana ilimwondoa na zile kubwa hazikufikishwa mahakamani.
Hakuna Mtanzania anayetaka Mkapa afungwe jela ama kunyongwa isipokuwa asilisiwe mali zake na pengine mafisadi wengine wote waliojificha nyuma ya jina lake na madeal yake watajitokeza... trust me kwa miaka mitano ya mwisho wa Utawala wake pamoja na miaka miwili ya JK tunaweza kuwavuta kokoro limejaa samaki wakubwa kina Kamongo na Sangara. Hii inaweza kusanya fedha ambazo zitakata tegemeo la misaada kwa kiasi kikubwa sana....
Jamani hii ni fedha yetu haya maswala ya kumwachia Mungu hali tumeibiwa ni ishara tosha za mtu maskini.
 
Hawa jamaa wa Nyerere ni lazima wafikishane na Mkapa mahakamani, wana uchungu na mali aliyoiacha baba wa Taifa
 
Kuhani Mkuu

Wewe unahisi nini kinapswa kifanyike ili Mkapa azungumze ? cause we would like to hear his side of story also.

Mkapa anamuogopa mtu mmoja tu Tanzania. Amesha kufa!

Tumshtaki mahakamani.

Kumuomba azungumze ni ndoto, kwa sababu Mkapa analindwa na 'tafsiri' fulani ya sheria. Sasa akianza kuzungumza anatibua maji yaliyo tulia na atazidi kuwaudhi watu. Kukaa kimya ni mbinu kali sana ya Mkapa.

Butiku alianza kumchokonoa, eti njoo ujieleze, tutakuelewa tu. Mkapa akashtukia hiki ki mtego. Akakaa kimya. Siku ya pili Butiku akasisitiza Mkapa msafi, ajieleze tu. Mkapa sio mjinga hata kidogo, akatulia. Siku ya tatu Butiku akacharuka, Mkapa fisadi! Mkapa nadhani alicheka sana: Well, nilidhani ulisema nijitokeze nijieleze mtanielewa!

Kuna tafsiri ya hiyo kinga ya Rais inayo ruhusu ashitakiwe akifanya madhambi nje ya wadhifa wake wa Urais. Tumshtaki. Ahsante
 
1. mimi naamini mkapa anayo makosa yake lakini kamwe hii haitaharibu historia yake iliyotukuka ya kujenga uchumi..

2. ...zaidi ya hayo tutabakia kumlaumu mkapa wakati kazi haifanyiki...

3. watanzania tuliowengi tunaendelea kumuheshimu mzee mkapa kutokana na rekodi yake .....

4. kama kuna ufidadi thats another case kwa kuwa serikali hii leo ufisadi upo na kazi hakuna...

5. saasa si bora mkapa!!!!

6. kama mkapa kuna alichochukua mnakitaka mwambieni arudishe ....msimwaribie rekodi yake!!!!!!

Mkuu wangu Philemon,

Kama huu msimamo ndio msimamo wa Chadema, basi wa-Tanzania tutegemee miaka mingi sana ya upinzani kabla ya kuingia Ikulu, kwa sababu kama wabunge wa CCM tayari wamemshitukia makapa, sasa for you kuwa na huu msimamo inasikitisha sana kama haitii huzuni kwa mwananchi yoyote anayeheshimu na kutaka respect kwa the rule of law,

Among all the people bongo kweli wewe unaweza kuwa na huu msimamo? Hivi unawalaumuje mtandao bila ya kumalumu aliyewaweka? Unasema record? Wale wanaomiliki ile zawadi ya MO hawakuziona hizo record za makapa? Kweli mkuu is this a serious message unayowatumia wabunge wa CCM kina Kimaro, wanaolala macho kumfikisha makapa kwenye sheria? Hebu niambie makosa ya Chenge ni nini? Kama sio Radar? nani hasa ni mzee wa Radar kama sio makapa? Hebu niambie mkuu toka tuipate ile Radar exactly kilichotubadilikia as a nation as opposed na tulipokuwa hatuna hiyo Radar ni nini? hivi unajua mkuu ma-exepert wa vita duniani walisema kuwa Israel ndio hasa wenye kuiihitaji ile Radar na sio sisi Tanzania, na kuna habari kuwa haijawahi hata kufanya kazi toka tuiinunue?

Eti makapa anaweza kuwa na kosa linalozidi kutupa hawa mafisadi na mtandao for the next 10 years? Jamani labda kuna something I am missing on this ishu!
 
Mkuu wangu Philemon,

Eti makapa anaweza kuwa na kosa linalozidi kutupa hawa mafisadi na mtandao for the next 10 years? Jamani labda kuna something I am missing on this ishu!

I agree with you, kuwalaumu hawa wana mtandao wa leo bila kumlaumu Mkapa ni uhuni, na kuwalaumu hawa washikaji katika serikali ya Kikwete bila kumlaumu Mkapa ni uzembe. Ukweli ni kwamba kama ni madudu wanayoyafanya hawa ndugu zetu akina JK ni muendelezo wa madudu ya Mkapa na serikali yake. Lakini lazima tukubali hawa washikaji akina JK na wenzake wamekwama mno maana hata yale mafanikio kiduchu ya Mkapa wameshindwa kuyalinda achilia mbali kuyaendeleza.

Niseme pia kwamba nchi yetu ni nzuri na ya ajabu sana kisiasa. Tukumbuke wakati tunamchagua Kikwete tulimchagua kwa yeye mwenyewe kutuambia kwamba wanaotegemea mabadiliko katika utawala wake wanajidanganya. Akaenda mbele akasema wazi kabisa kwamba angeendeleza yote aliyokuwa anafanya Mkapa (including ufisadi I suppose). Hapa kimantiki ni kwamba tuliridhika sana na mafanikio ya Mkapa kiasi kwamba tukamchagua Kikwete kwa ahadi hiyo ya kuyaendeleza. Ingekuwa nchi zingine ukatoa ahadi kama hiyo ujue umeliwa. Niambie leo hii kama MacCain akasema ataendeleza ya Bush au Gordon Brown angeingia kwa gia ya kuendeleza ya Blair au Mwanawasa angeingia kwa gia ya kuendeleza ya Chiluba au Zuma angesema ataendeleza ya Mbeki ingekuwaje kwa wapiga kura?

Narudia kauli zangu nyuma kuwa moja ya weakness yetu kubwa sana kama raia wa nchi ni kwamba huwa tunaona makosa ya viongozi wetu wakishatoka madarakani. Sijui hii ni bahati mbaya au ni ile ile kasumba yetu ya woga na unafiki! Kwa sababu kama tungeyaona haya ya Mkapa kama tunavyoyaona leo hata kampeni za ugombea urais ndani ya CCM zingekuwa tofauti sana. Lakini wagombea wote wa CCM walijinadi kwa minajili ya kuendeleza yote ya Mkapa, halafu tunashangaa kwamba wanaendeleza ufisadi, we are screwed as a people and a country!
 
Back
Top Bottom