Mkuu Ogah,
Heshima mbele, umesahau kuwa nitawa-suprise Wa-Tanzania kwa kuwapatia rais anayefaa na wasiyemfikiria, unakumbuka ilikuwa ni kauli ya nani hiyo mkuuu?
Baada ya uchaguzi akaenda kukaa chini na Wakuu wa Dini, ili wahalalishe suprise yake, umesahau ya nabiii?
Au hujui aliyewashinikiza hao hao wakuu wa dini ni nani?
Mkuu Ogah, ninajua kuwa una upeo mzito wa kuona ishus, Biblia inasema mkuu shetani ni sungura sana katika kujigeuza geuza, maana akija kwetu wana-adam kama alivyo wote tutamkimbia, kwa hiyo hujifanya malaika, au sometimes intellectual kama Mkapa, halafu hujifanya mtiifu kwa Baba Wa Taifa na kuwa ni mwanafunzi wake hodari sana, halafu hutengeneza uchumi wa nchi na baadaye kupigia kelele sana rushwa, halafu pia hutoa hotuba nzuri sana huko majuu kuhusu matatizo yetu,
ni mpaka akishaondoka madarakani ndio wananchi mnakuja kugundua kuwa yeye na famili a yake, walikusanya kila kitu, lakini hakuna ushahidi na hata ukiwepo aliowaweka madarakani wanamkingia kifua, Mkuu wangu yanayotukuta sasa hivi as a nation ukweli ni kwamba yanaanzia kwake, maana ni yeye peke yake ambaye Mwalimu alikuwa akimuamini kuwa wanafanana kwa kila kitu, wewe leo kiongozi mtuhumiwa wa mauaji aliyeko nje kwa dhamana, anawekwa kwenye safari za mawaziri kuhutubia wananchi hao hao ambao mmoja wao alimpiga kwa bastola bila sababu,
Nasikia kuwa Mungu, aliwaadhibu Sodoma na Gomora kwa kuwa a lawless nation, sasa kama anatuachia sisi Tanzania bila kutuadhibu, basi anahitaji kwenda kuwaomba radhi wale wakuu wa Sodoma na Gomora, au?