Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Masatu,
Mmiliki wa Sophia houses ni mke wa Mkapa...haya yote yalikuwa majengo ya NHC ama Msajili wa majumba..
Pili umeuliza maana ya Fisadi nadhani nitakupeleka kwenyewe kwa watu wa pwani..sikiliza vizuri maneno ya nyimbo hii utaelewa.
http://www.youtube.com/watch?v=IZFuQ99fy7A
Nadhani ubishi tumeumaliza hapa.... tugange yajayo!
 
Slaa na magazeti ya mengi wako entitled kwa maoni/mitazamo yao sanjali na wewe na wa JF kwa ujumla, lakini ukweli utabaki kuwa the guy has done commendable job

Sitaki kutia neno katika majibu waliyokupa wakubwa hapo juu, lakini kwa ufupi kabisa ni kwamba, ni kweli alifanya mazuri mengi, lakini yale mazuri aliyoyafanya alitimiza wajibu wake wa URAIS na ndiyo mambo anayolindwa nayo na KATIBA, lakini baada ya kukusanya KODI nyingi, akajiingiza katika UFISADI hasa baada ya kifo cha BAba wa Taifa, MWalimu Nyerere.. Sasa hapo utasema unamsamehe kwa sababu alifanya mema miaka minne ya kwanza? Hebu angalia, mzee wa watu JAji Warioba, amefanya mema miaka yote ya uhai wake, hata sasa bado anafanya mema, lakini alipoingizwa mkenge na kina MAHALU wa Mwananchi Gold, alisemwa, alipochemsha kueatetea MAFISADI alikemewa.. na kwa kweli HISTORIA YA MEMA YA MTU HAIMPI KINGA KUFANYA UFISADI AMA UOVU WOWOTE DUNIANI KOTE NA WAKATI WOWOTE ULE
 
Mkandara,
1. Nimekutana na watu wengi wa nchi zingine hata huku majuu wanampa 5 BWM..wazungu kwa waafrika..kusini na kaskazi! "That Tz we have wonderful leadership on that seed planted by Mwal. until today..they actually seem to admire us- as a nation" Sasa sisi tumekuwa tunalaumu tuuuuu! Je hatuoni mazuri kujivunia?
2. BWM hakuwa Mungu- ni mwanadamu. Kukumbatia wala rushwa- na yeye kuwa mwizi -mimi sina ushahidi- ushahidi uliotolewa hapa ni wa kimazingira. Kwamba ana nyumba 2 au 3- Masatu ametoa maelezo.
Kamata kamata walarushwa- as a president you need social harmony ili uweze kutawala. May be ndo maana hata JK anasita kukamatakamata bila ushahidi tosha. JE wapi hiyo kamakamata in SSA imeleta matokeo haraka?

3. Ana mapungufu..BWM na sii malaika. Ila mimi kwa kifupi, I was and I am stil proud of him!

Naamini kama utakua unatenda haki kwa IMANI YAKO BINAFSI NA KIZAZI CHAKO, utakua umefuatilia tuhuma zinazoelekezwa kwa Mkapa na familia yake. Kama wewe unaona hizo tuhuma hazina ushahidi kabla sijakupa ushahidi mwingine mzito zaidi, ungeniridhisha kwamba hayo yaliyoandikwa na THISDAY na magazeti mengine ni MAJUNGU vinginevyivyo;

1-Nitaanza kuamini kwamba unaweza kuwa uko ndani ya PCCB na kwamba tayari mumeshachunguza kama mulivyochunguza Richmond na kubaini kwamba HAKUNA USHAHIDI WA RUSHWA JAPO KULIKUA NA UZEMBE, kwa hiyo MKAPA na MKEWE hawakukosea Kuanzisha ANBEM na kupata fedha kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ZAWADI, MICHANGO, MIKOPO, MISAADA, BAKSHISH, AKIBA, KUWAWEKEA WATU, na kadhalika wakati AKIWA MADARAKANI kwa hiyo PCCB IMEWASAFISHA.

2. Nitaanza kufikiria (maana hatutumii majina yetu) ama wewe ni MKapa (maana anasoma sana mtandao), ama mtu wa karibu naye ama mtu aliyenufaika naye kwa kuwa huwezi kukubaliana na ushahidi ama neno lolote litakaloweza kuathiri maslahi yako. Ndio maana mhalifu akisomewa shitaka anakana hata kama alikutwa waziwazi.

3. Naweza pia kufikiri kwamba wewe ni mtu mwenye akili nyingi sana, maana kuna mzee wangu mmoja aliniusia, "wakati wote jifanye hujui kitu ili upate kujulishwa zaidi, wakati mwingine pingana na wenzake ili wapate kujitetea na wakijitetea watatoa taarifa nyingi zaidi" kwa hiyo na wewe inawezekana kabisa unataka faida na kama hivyo ndivyo NAWAPONGEZA SANA na ndio ROHO YA FORUM YOYOTE YA WATU MAKINI.

4. Lakini naweza kufikiria pia kwamba wewe ni mtu unayetumiwa, hapo ndipo nitakapokuonea HURUMA NA KUKUOMBEA MUNGU AKUSAIDIE NA KUKUONGOZA UWEZA KUACHA MARA MOJA KUTUMIKA. SITAKI KUAMINI HILI NA NDIO MAANA NIMELIWEKA LA MWISHO.

KWA KIFUPI MKAPA NI FISADI MKUBWA. MKAPA ANASTAHILI KUSHITAKIWA, MKAPA NDIYE ANAYEUFANYA HIVI SASA TUANZA KUONA MACHUNGU MAANA KAMA HUJUI, SEHEMU KUBWA YA FEDHA AMBAZO ULIKUA UNASIKIA ZINAJENGA MIUONDOMBINU, ZIMETOKANA NA MIKOPO YA TAASISI ZA FEDHA ZA KIMATAIFA, MIKOPO AMBAYO MIMI NA WEWE NA VIZAZI VYETU VITALIPA AMA VIMEANZA KULIPA, WAKATI FEDHA HIZO BAADHI ZIMEWANUFAISHA WACHACHE. (HII NI MADA PEKEE YA WAKATI WAKE, HAPA TUSEME TU TUSIMTETEE MKAPA NI FISADI)
 
Masatu,
Mmiliki wa Sophia houses ni mke wa Mkapa...haya yote yalikuwa majengo ya NHC ama Msajili wa majumba..
Pili umeuliza maana ya Fisadi nadhani nitakupeleka kwenyewe kwa watu wa pwani..sikiliza vizuri maneno ya nyimbo hii utaelewa.
http://www.youtube.com/watch?v=IZFuQ99fy7A
Nadhani ubishi tumeumaliza hapa.... tugange yajayo!

This is really interesting now... haya tunaomba ushahidi wa nyumba za Sophia house kumilikiwa na mama Mkapa pls.

Hivi siku hizi hoja hujibiwa kwa mipasho! kwa hiyo maana ya fisadi kiwembe ya iliyotolewa na mabingwa wa kiswahili sio sahihi bali iliyo sahihi ni ile ya sijui ndio Mwanahawa au Khadijah Kopa...

Kazi kweli kweli....
 
Uzalendo ni nini? Hivi ni kweli unaishia ktk uandika makala online,magazetini TV au ?

Uko wapi Utanzania wenu,mnamwita mwizi,fisadi,jeuri na wengine mnamwita mjivuni sawa tumewasikia,what next? Who told u Mengi ni rafiki wa Mkapa? And why not Msuya? Huenda tupo hapa kuwaangalia wenzetu tu lakini vivuli vyetu vikawa vinatusumbua; Nina mashaka na uzalendo wetu huu,rudini hapa TZ muungane na hao waandishi na magazeti mkamshitaki tujue moja kuwa kweli sasa haki itatendeka kwa walio wengi.

JF iachane na mitizamo binafsi juu ya watawala,niliwahi kuyaona maoni ya binadamu mmoja humu,alishauri ni vema tukawaiga Wamarekani,When ur through with presidency, to them u become the saint na ndiyo hoja ya JK,ukiweza kupita tanuru la mamlaka pasipo kugunduliwa na kushitakiwa basi wewe ni mstaafu bora wa jumba jeupe;He is out of Magogoni house,he is the third saint from Magogoni,mwacheni akapumzike,mkubalini ni rais wenu wa tatu,ndiye mwenye nuru na wakubwa duniani hilo halina ubishi,kama tunadhani tuko sahihi kuendelea na kuwa This day na kulikoni basi ni vema tuwaulize wakubwa wa sasa kama waliweza kudhibiti media zote juu taarifa ya Slaa walishindwa vipi kudhibiti taarifa za Kulikoni na This day? Wana agenda yao ya kumzima Ben Mkapa lakini bahati mbaya hawajui madhara ya zoezi hilo,sidhani kama Ben alizuia ripoti ya Warioba kwa hofu au shinikizo la Mwalimu tu,kuna mengi yanafanyika ila hamtaki kuyasema.

The only way to delete Ben is by kuvunja rekodi zake na maaskari wake makini wa miavuli,Lowasa hatasahau kuachwa kwake ktk baraza 1995-97 licha ya kuwa Alhaj Mwinyi aliwaombea kazi mbele ya wajumbe wote Mkutano mkuu wa CCM,kumbuka kauli yake ya kwanza juu ya matatizo ya umeme -

Ikulu itaongozwa na binadamu ambaye sifa yake kuu ni udhaifu ;ikumbukeni kauli ya mheshimiwa Bill Clinton
"I did not have sexual relations with that woman." - Clinton

Todate USA inamkubali kwa uwezo wake mkubwa wa kushawishi na kuthubutu ktk harakati za maendeleo.Why not Ben William Mkapa? Kila heri waungwana
 
Mkuu hapo umehitimisha kila kitu, if read btw the line watu wanakumwa na chuki zao binafsi kwa huyu Great Man. Lakini panapo ukweli uwongo hujitenga.
 
Masatu,
Tofauti kati yangu na wewe ni kwamba wewe unatumia kitabu cook book hali mimi mwenzako ni lugha ambayo huitumia kila siku...Kwa hiyo unaweza endelea kutumia kamusi yako. Yaani hata neno Fisadi umeenda litzama ktk kamusi!.... damn.

Ushahidi wa mama Mkapa kumiliki Sophia house - SINA kama vile sina ushahidi kuwa wewe ni mwanaume....Na sielewi ushahidi kama huo nitauweka hapa kwa njia ipi?
Mjomba sasa umeishiwa hoja!
 
Masatu,
Tofauti kati yangu na wewe ni kwamba wewe unatumia kitabu cook book hali mimi mwenzako ni lugha ambayo huitumia kila siku...Kwa hiyo unaweza endelea kutumia kamusi yako. Yaani hata neno Fisadi umeenda litzama ktk kamusi!.... damn.

Ushahidi wa mama Mkapa kumiliki Sophia house - SINA kama vile sina ushahidi kuwa wewe ni mwanaume....Na sielewi ushahidi kama huo nitauweka hapa kwa njia ipi?
Mjomba sasa umeishiwa hoja!

Kaka Mkandara,

Tofauti kati yangu na wewe nin kwamba wewe unatumia mipasho ya Khadijah Kopa hali mimi mwenzio natumia Kamusi ya Kiswahili Sanifu kutafsiri maneno.. Kwa hiyo unaweza kuendelea na mipasho yako.. yaani hata neno Fisadi unaenda kulitafuta ktk mipasho!... damn

No research no right to speak, same as no evidence no right kupayuka! kwa kifupi umechemsha!
 
Sawa mkuu ebu tupe sentesi moja ya kiswahili ukitumia neno hilo! FISADI = KUTONGOZA na kama kuna mtu atakuelewa!
Pili , kisha basi Khadija Yusuph siye Khadija Kopa!...watu wawili tofauti kabisa, haya sii maji yako mjomba Masatu! Lugha ya watu hii utashinda na kamusi na kamwe hutaelewa kitu. Unazidi kujibamiza, kama hujui kitu si kubali yaishe yote haya yanatoka wapi?... kwa Mkapa na hizo hotuba zake!
This is my message...and where I'm coming from!
Ebu kaisikilize hotuba ya Mugabe alotoa UN, imepongezwa na wasomi kibao kuwa imejitosheleza, wengine wamesema hakuna hotuba iliyowa touch kama hiyo. (haya naomba usilete tena habari zako za ushahidi)...
Lakini hiyo hotuba haiwezi kumfanya Mugabe kuwa kiongozi bora kwa Wazimbabwe. Hatuwezi kutumia hotuba ama maandishi kumpa kiongozi sifa za Uongozi bali ni matendo yake!..hotuba hutungwa kama tunzi. Ni uandishi sio Uongozi!
 
Sawa mkuu ebu tupe sentesi moja ya kiswahili ukitumia neno hilo! FISADI = KUTONGOZA na kama kuna mtu atakuelewa!
Pili , kisha basi Khadija Yusuph siye Khadija Kopa!...watu wawili tofauti kabisa, haya sii maji yako mjomba Masatu! Lugha ya watu hii utashinda na kamusi na kamwe hutaelewa kitu. Unazidi kujibamiza, kama hujui kitu si kubali yaishe yote haya yanatoka wapi?... kwa Mkapa na hizo hotuba zake!
This is my message...and where I'm coming from!
Ebu kaisikilize hotuba ya Mugabe alotoa UN, imepongezwa na wasomi kibao kuwa imejitosheleza, wengine wamesema hakuna hotuba iliyowa touch kama hiyo. (haya naomba usilete tena habari zako za ushahidi)...
Lakini hiyo hotuba haiwezi kumfanya Mugabe kuwa kiongozi bora kwa Wazimbabwe. Hatuwezi kutumia hotuba ama maandishi kumpa kiongozi sifa za Uongozi bali ni matendo yake!..hotuba hutungwa kama tunzi. Ni uandishi sio Uongozi!

Mkuu mbona wajichanganya? Tafsiri ya neno fisadi kwa mujibu wa kamusi imeelezwa vizuri kabisa kama ina maana zaidi ya mmoja, sasa hili zoezi unalonipa la kutunga sentensi wewe mahala pa tongoza weka fisadi na na sentensi yako itakamilika, kama hilo haliwezekani basi mabingwa wetu wa kiswahili tuwafute kazi wote.

Habari ya Khadija Yusuph na Khadija Kopa inaonyesha kiasi gani upeo wako ulivyo mdogo ku analyse mambo nimetaja mipasho kwa ujumla wake na kutolea mfano wa Khadija Kopa, mbona hujamtaja Mwanahawa ambaye nimemtaja lakini hakushiriki wimbo huo, kumbe inabidi tuweke tuition ya kiswahili hapa sasa...

Hivi mazuri yote ya Mkapa wewe umeona hotuba tu... rejea postings zangu za awali kuona kama nimesema urais wake ulikuwa mzuri kwa sababu alikuwa anatoa hotuba nzuri, yaani una spin hata ktk hili!

Kazi unayo.....
 
Masatu,
Imekuwa hayo tena! yaani sasa hivi imefikia hata kueleza upeo wangu kuwa mdogo ktk neno moja tu FISADI! neno ambalo hata mtoto mdogo asiyejua kusoma anafahamu maana yake..
Na kwa kipimo gani hasa mjomba umeweza kujua upeo wangu wa kufikiri ikiwa hapa tu unashindwa kwa hoja na kuanza vioja vya mashambulizi ya nguoni!.mbona unaanza kutoka nje!...
Mjomba wewe mwenye upeo mkubwa, Kiswahili ni Lugha ilikuwepo kwanza kabla ya kamusi.. kamusi ni maandishi ya tafsiri kuwarahisishia lugha watu wasiojua maana na matumizi yake, haikuanza kuandikwa kabla ya maneno ya kiswahili kikavumbuliwa.... unazidi kuchemsha tu!

Kuna kitu gani hasa kilichokuuma kiasi kwamba unashindwa kubana pumzi zako kwa hoja bali umeingia ktk ile signature ya mzee wetu Njabu ngabu!..
 
1.
Uzalendo ni nini? Hivi ni kweli unaishia ktk uandika makala online,magazetini TV au ? Uko wapi Utanzania wenu,mnamwita mwizi,fisadi,jeuri na wengine mnamwita mjivuni sawa tumewasikia,what next?

What is next, ni tunamuomba kila wakati rais wa sasa aruhusu kufunguliwa mashitaka kwa mhesshimiwa mstaafu Mkapa, na hasa kuhusiana na ununuzi wa Radar, ambao hata Waingereza wenyewe waliotuuzia wanadai kuna uhuni umefanyika, it is the matter of time kabla siku moja mkulu hajatinga mahakamani, mara ya mwisho aliandikiwa Mkuu Hosea, akasema kuwa sheria hairuhusu so far, kwa hiyo ishu haijafa bado iko hai na yeye mwenyewe analijua hilo sana, uzalendo sio lazima upigie kelele maovu ukiwa nyumbani, Ayatolahh Khomein, alipiga kelele akiwa France for at least 16 years, siku moja akarudi kuiongoza Iran, ambayo mpaka leo bado inafuata nguzo za uongozi wake, if the uzalenmdo thing is an ishu, kwa sababu sihitaji kuwa mzalendo kumsifia Zitto, na Dr. Slaa, au kumuuliza Mkapa alipataje mali zote alizonazo in 10 years, tena the matter of fact in 6 years baada ya kifo cha Mwalimu 1999? Je mabalozi wa nje waliopo bongo wanaouiuliza serikali kuhusiana na orodha ya mafisadi, how do you describe them as far as this uzalendo thing is concerned?


2. [
B]Who told u Mengi ni rafiki wa Mkapa? And why not Msuya?[/B]

This one ni kutokana na maneno yake mwenyewe in private, kuwa "....hata Mengi who I thought to be my friend....", viongozi wote wa juu huwa ni marafiki wa kawaida wa Mengi, akiwa rais alikuwa akisafiri na huyo mkuu kila wakti kwenye ndege yake binafsi, je mkuu umeshawahi kusaifiri na Mkapa kwenye ndege yake binafsi akiwa rais kama Mengi? Mengi alikuwa hata rafiki wa Mwalimu pia, what is wrong with that? Hivi ninahitaji kuambiwa na mtu kuwa rais hawezi kusafiri na mtu yoyote kwenye ndege yake binafsi unless ni kiongozi mwenzake au kama ni Mengi, kama Mkapa alipvyokuwa akifanya basi ni rafiki yake?


3.
Huenda tupo hapa kuwaangalia wenzetu tu lakini vivuli vyetu vikawa vinatusumbua
;

Vivuli? Vipi hivyo? Hawa kina Adam Lusekelo wanaaoukemea ujinga wa serikali tena kwenye magazeti ya serikali hiyo hiyo wana vivuli gani hivyo? If that is the case tunafanya nini hapa forum? Basi tufunge hii forum maana kila tunalolikemea serikali ni vivuli vyetu vinatusumbua tu au? Why waste time na mkataba wa Buzwagi, wakati kumbe tatizo ni vivuli vyetu vinatusumbua? I mean pamoja na wananchi mbali mbali kutoa sababu nyingi za sisi kuwepo hapa forum, ukweli ni kwamba kazi yetu muhimu hapa inatakiwa kuwa kuikosoa serikali, in the wake ya magazeti na media zetu za taifa kununuliwa na Mtandao, na tutaendelea na tabia hiyo hiyo hapa bila kujali nani anahusika au chama gani kinahusika,

vivuli? wananchi wanaowazomea mawaziri huko mikoani na vijijini wanasumbuliwa na vivuli gani mkuu? Makamba anpowatukana wapinzani bongo anakuwa anasumbuliwa na kivuli kipi Mkuu?


4.
Nina mashaka na uzalendo wetu huu,rudini hapa TZ muungane na hao waandishi na magazeti mkamshitaki tujue moja kuwa kweli sasa haki itatendeka kwa walio wengi

Uzalendo kwako ni kuikosoa serikali ukiwa bongo tu? Sasa kina Seif Khatibu, wanahangaikia nini kuzungumzia tuhuma kwenye Redio za kina MMJ walioko nje? Kwa nini rais wetu anafungua tawi la CCM London, wakati kwa your thinking wananchi walioko nje sio wazalendo, isipokuwa walioko bongo tu? What a hoja?

Kuhusu kushitakiwa, hilo halina haraka ukweli upo kuanzia IPTL, Radar, Ndege ya Rais, Mikataba ya madini, it is only a matter of time tu mkuu atatinga mahakamani, kinachihitajika kubadilika ni upepo tu wa siasa, viongozi kama Sozigwa hawana hayo matatizo ya kuishi kwa wasi wasi kama mstaafu wetu, maana hata na yeye anajua kuwa wafadhili wakiweka mguu chini ashitakiwe anakwenda na maji, kwenye hilo mkuu muulize Taylor Wa Liberia kilichomtokea, wengine wakinyolewa ni vyema kuanza kuweka maji tayari!

5.
JF iachane na mitizamo binafsi juu ya watawala,

JF kama chombo cha media kilicho huru na kilichoandikishwa kisheria, hakihusiki na mawazo yako binafsi, wala ya kwangu kwa hiyo tuwe waangalifu na hilo mkuu in the future, JF isilaumiwe kwa mawazo ya watu binafsi!


6.
niliwahi kuyaona maoni ya binadamu mmoja humu,alishauri ni vema tukawaiga Wamarekani,When ur through with presidency, to them u become the saint

Ingekuwa ni kweli Clinton asingenyang'anywa Licence ya uwakili wa binafsi, baada ya kutoka urais kwa ajili ya kesi yake na Monica, hii hoja si kweli, Nixon alipewa alternatives, kati ya kushitakiwa akiwa rais au kujiuzulu hatashitakiwa, akachagua kujiuzulu kwa hiyo na hii hoja ni hafifu kama haipo kabisaa, huko Us ndio hawataki mchezo kabisaaa, ndio maana ilibidi Clinton amlipe dola laki saba Bibie Jennifer Flowers baada ya kutoka urais, kwa kulazimishwa na sheria!

7.
na ndiyo hoja ya JK,ukiweza kupita tanuru la mamlaka pasipo kugunduliwa na kushitakiwa basi wewe ni mstaafu bora wa jumba jeupe;He is out of Magogoni house,he is the third saint from Magogoni,mwacheni akapumzike,mkubalini ni rais wenu wa tatu,ndiye mwenye nuru na wakubwa duniani hilo halina ubishi
,

Idd Amin, aliwezaje kuwa mwenyekiti wa OAU, ni kwa sababu alikuwa ni rais wa Uganda na alikuwa na nuru na wakubwa, je inapunguza nini kuhusiana na uwezo wake mdogo wa uongozi akiwa rais? Savimbi na Mobutu je hawakuwa na nuru na wakubwa wa dunia, au Botha na Smith, je hawakuwa na nuru na wakubwa? Je umesahau kuwa Osama naye pia alishawahi kuwa na nuru na wakubwa USA ambao ndio hasa waliomtengeneza kuwa what he is today? Kwa nini na hwa tusiwakubali kuwa ni walikuwa na nuru kama Mkapa na wakakubalika na wakubwa wetu USA na UK?


8.
kama tunadhani tuko sahihi kuendelea na kuwa This day na kulikoni basi ni vema tuwaulize wakubwa wa sasa kama waliweza kudhibiti media zote juu taarifa ya Slaa walishindwa vipi kudhibiti taarifa za Kulikoni na This day? Wana agenda yao ya kumzima Ben Mkapa lakini bahati mbaya hawajui madhara ya zoezi hilo,sidhani kama Ben alizuia ripoti ya Warioba kwa hofu au shinikizo la Mwalimu tu,kuna mengi yanafanyika ila hamtaki kuyasema.

Aliyemchagua Warioba na kamati ya rushwa alikuwa Mwalimu au Mkapa? Mwalimu anahusika vipi na taarifa ya uchunguzi wa Warioba kutotolewa to the public? Na Warioba kwa nini hakwenda Elimu na Sayansi kwa swahiba? Leo maswahiba wakubwa under Mwalimu, kwa nini Warioba na Mkapa hawaelewani tena? Thisday/Kulikoni kama kweli yana shida ya kuharibu sifa za Mkapa kwa kuhsinikizwa na Mtandao, then kwa nini yanamtwanga Gavana na Mbunge Mkono pia? WHY? Ni nani anyesema kuwa taarifa za DR. Slaa zilidhibitiwa? Mbona wananchi tunazo? Mbona makataba wa Buzwagi kila mwananchi anao?

Ni dhana potofu sana kwamba wananchi wakimjadili rais wao wa zamani basi wanajiunga na Mtandao kumuangamiza rais wa zamani, hapana, hapa forum sijui ni ishu gani ambayo wananchi wamewahi kuikwepa, na kama tunatumiwa na Mtandao basi hawafanyi kazi nzuri, hebu angalaia topic zote humu forum uniambie kuwa tunatumiwa na Mtandao, another joke!

9.
The only way to delete Ben is by kuvunja rekodi zake na maaskari wake makini wa miavuli,Lowasa hatasahau kuachwa kwake ktk baraza 1995-97 licha ya kuwa Alhaj Mwinyi aliwaombea kazi mbele ya wajumbe wote Mkutano mkuu wa CCM,kumbuka kauli yake ya kwanza juu ya matatizo ya umeme -

Kwanza Mkapa, ana bahati kubwa sana kwamba we gave him a big chance akiwa rais hatukumtwanga sana, kwa sababu he was smart enough kutudanganya mapaka alipoondoka ndio ukweli ukaanza kupatikana, as opposed na serikali ya sasa ambayo hata haijamaliza term ya kwanza tayari tunaitwanga, kwa hiyo we were more than fair kwa Mkapa na urais wake, serikali ya sasa haijavunja rekodi ya wizi wake hilo ni kweli, na pia haijavunja rekodi ya mazuri yake ambayo huwa tunaaambiwa na wazungu tu lakini sisi wenyewe wananchi hatuyaoni, sasa what that tells you kuhusu huyo rais anyesifiwa na wazungu kama kina Savimbi na Mobutu, lakini wananchi hawayaoni hayo mazuri? Maana under Mwinyi angalau wananchi walitajirika na hakusakamwa na jeshi hata siku moja, as the case na Mkapa, rekodi ipo mkuu kuwa mkuu aliwafanyiwa kazi njema wazungu kama unavyodai, hilo sijui kama litavunjiwa rekodi na serikali ya sasa!

10.
Ikulu itaongozwa na binadamu ambaye sifa yake kuu ni udhaifu ;ikumbukeni kauli ya mheshimiwa Bill Clinton
"I did not have sexual relations with that woman." - Clinton
Todate USA inamkubali kwa uwezo wake mkubwa wa kushawishi na kuthubutu ktk harakati za maendeleo.

Ohh yah! Maendeleo ya hesabu hewa ni kweli kama ya Mkapa, unayoyasifia, hivi mkuu umeshawahi kusoma undani wa kesi za kina Ken Lay na Enron? Mkuu unajua toka Clinton aondoke madarakani ma-CEO wangapi wamefungwa? Kama USA ingekuwa inamkubali kiasi hicho cha kwako basi Gore asingeshindwa mkuu, Clinton alikuwa kiongozi safi halina ubishi mana hakuwa mwizi hata siku moja, huko Us huwa hawazimii na viongozi wezi hata siku moja, ni sawa kabisa Ikulu kuongozwa na mdhaifu wa kina mama, lakini sio udhaifu wa kuiba, ndio maana tunampa heshima Muungwana na Clinton, maana sio wezi, ila hatutakuwa na suluhu na viongozi wezi hata kama ni Karamagi,

Clinton, ametoka madarakani akiwa hana hela kabisa wala mahekalu ndio maana mke wake akachaguliwa, can you imagine mke wa mstaafu wetu akigombea ubunge? Mdogo wake tu wananchi walimkataa kwa kumchukia dada mtu, sasa iweje dada mwenyewe akiingia! Clinton hawezi kulinganishwa na kina mkapa, ni matusi makubwa, mkuuu!

11.
Why not Ben William Mkapa? Kila heri waungwana

Hakuna mwenye tatizo na mkapa wala kiongozi yoyote wa nchi yetu, tatizo ni kama wamevunja sheria kwa makusudi, na sidhani kama kwenye hii forum tumeshawahi kuwa na macho ya kuchagua yupi wa kumpiga mawe, Mkapa anashambuliwa kwa rekodi yake mwenyewe, IPTL, Radar, Ndege Mbovu ya rais, mikataba mibovu ya madini, kupanda kwa gharama za uchaguzi, ni rekodi ambazo zimetokea under hsi watch, kwa hiyo hatujali sura ya mtu au kiongozi, hapa forum kila kiongozi huchambuliwa kama alivyo, nothing personal that is pure nonesense, in the future mkuu ukitaka kumtetea mkapa weka rekodi, achana na ishu za binafsi maana hakuna mwenye shida naye za binafsi hapa, na hizi hoja za ubbinafsi it is about time hapa forum tukaachana nazo,

Ahsante Tuendelee kukata ishu mkuu, ila hapa haangaliwi kiongozi wala sura yake, isipokuwa rekodi yake! Utakapokuwa tayari kurudi karibu tena mkuu!
 
The debt repayment is a key part of the economic reform plan of President Olusegun Obasanjo, who is also planning a string of privatisations, tax reform, and greater transparency in order to boost the economy and attract foreign investors.
Nigeria has already been removed from an international credit blacklist, and now has credit ratings similar to other emerging market countries such as Turkey and Ukraine. That means the government is now able to borrow money on international capital markets on favourable terms.

Different from HIPC

Nigeria has followed a different path from other African countries who have been burdened with debt.
It was not included in the list of highly indebted poor countries (HIPC) that were eligible for 100% debt relief from official lenders, the IMF, and the World Bank, due to its oil wealth. However, those countries have been subject to stringent conditions and long delays before they qualified for debt relief.
Nigeria has been able to negotiate its own debt deal at its own pace because it has the funds to partially pay off its creditors, who were happy to accept a smaller overall payment in return for cash upfront.


Hizi ndio zinaitwa good record za rais mstaaafu, kila kitu hapo juu kinajisema chenyewe, sio ujanja ujanja tu! na hili ni gazeti la huko huko majuu, sasa hakuna yenye rekodi za Mkapa huko majuu?
 
1.

What is next, ni tunamuomba kila wakati rais......,

Ahsante Tuendelee kukata ishu mkuu, ila hapa haangaliwi kiongozi wala sura yake, isipokuwa rekodi yake! Utakapokuwa tayari kurudi karibu tena mkuu!


Hapa Mzee umekata ishu kinoma!! Chukua 5
 
fisadi ni neno linalotokana na neno la kiarabu FASAD.
na maana yake ni muharibifu.
sasa mtu anaetumia mali ya serikali kwa uharibifu, anaewacha watu wengine waharibu na anaeidhinisha uharibifu huo na yeye anakubalika kuitwa FISADI.
kwa maana hiyo, viongozi waliojilimbikizia mali (kwa kuharibu taifa lao), waliotuwekea viongozi waoza, waliowaita wageni waje watuharibie nchi wote tunawaweka kwenye kundi la MAFISADI.
mkapa kama anaingia hatoki, na hilo pia ni kwa kikwete na karamagi.
 
Bravo Bravo FMES kumkoma nyani giladi mchana kweupe huku unamwangalia usoni.
 
Na kwa kipimo gani hasa mjomba umeweza kujua upeo wangu wa kufikiri ikiwa hapa tu unashindwa kwa hoja na kuanza vioja vya mashambulizi ya nguoni!.mbona unaanza kutoka nje!...

Mkuu wewe mwenye kujua kiswahili bila kutumia kamusi inaweza kweli kusema neno upeo mdogo ni tusi la nguoni? Naona baada ya kushindwa hoja sasa unaanza kulala ili kupata sympathy kwamba umetukanwa ilhali hakuna aliekutukana.

I Can tell you by no stretch of the swahili language neno upeo mdogo linaweza kunasabishwa na tusi la nguoni.

Swali langu dogo tu kwako je hii tafsiri ya neno Fisadi iliyotolewa na wataalam wa kiswahili unakubaliana nayo au la?

ES

Naona sasa unaanza kutoa kauli za kukinzana, hapo awali ulisema hivi ktk post # 25

mambo yote uliyoyasema mkuu kuwa Mkapa ameyafanya kwa Tanzania, hayana tofauti kubwa sana na Clinton aliyoyafanya US, lakini mkuu huyo ametoka urais akiwa lamost hana hata senti moja, ni baada tu ya kutoka urais ndio ameanza kukusanya hela kwenye speech na vitabu,

Then all over suddenly kwenye post # 59 unakuja na usanii huu;

Clinton, ametoka madarakani akiwa hana hela kabisa wala mahekalu ndio maana mke wake akachaguliwa, can you imagine mke wa mstaafu wetu akigombea ubunge? Mdogo wake tu wananchi walimkataa kwa kumchukia dada mtu, sasa iweje dada mwenyewe akiingia! Clinton hawezi kulinganishwa na kina mkapa, ni matusi makubwa, mkuuu!

Mkuu sasa hapo tushike lipi au ndio usanii at its best.....

Mambo ya flip flopping, only in JF!
 
Marshall ES,
Suala la rada Waingereza, kupitia kwa waziri wao, walishaeleza kwamba mkataba ulisainiwa wakati wa Mzee Ruksa.Mkataba wa IPTL nao ulisainiwa na serikali ya Mzee Ruksa.

Kuhusu mikataba mibaya ya madini, naomba kwanza tuelekezwe mikatana hiyo ilisainiwa mwaka gani. Mimi nina mashaka kwamba mikataba hiyo ilisainiwa wakati wa Mzee Ruksa na alichofanya Mkapa ni kwenda kufungua migodi tu.

Pia ni vizuri tukaelewa kwamba ni serikali ya Mzee Ruksa ndiyo waliopitishwa sheria mpya ya uwekezaji ktk madini na nishati. Sheria hiyo ndiyo mzizi wa dhuluma na uporaji wote unaoendelea.

Pamoja na hayo, nakubaliana na wewe kwamba Mkapa ana kesi ya kujibu katika masuala kama, ununuzi wa ndege ya Raisi, mkataba wa Tanesco na Netgroup, na umiliki kampuni ya kusambaza umeme toka Kiwira.
 
I thought mining Act ni ya mwaka 1998! Was mzee Ruksa still President by then? Sheria hizi kapitisha Ben, tuache kumsakama mzee wa watu bure. Sasa atleast na sisi tumeona..na hii ya Buzwagi nani kasaini? Iam sure huu mkataba usinge-leak..tungedanganywa kama kawaida...conspiracy theories kibao..Lakini tumeona, Mkataba umesainiwa juzi juzi tuu, kwa hiyo hata hayo ya Ruksa wengine tunaona tunamwagiwa mchanga wa macho, wamesaini akina Mkapa na kundi lake na wala sio Ruksa. Unless muiletee hiyo mikataba ya IPTL na MINGINE TUIONE! Vinginevyo tunaamini kwamba Ruksa anarushiwa mpira tuu.
 
Masanja,
Kulingana na ripoti ya Dr.Slaa, mikataba ya migodi ya Nzega, na Kahama[Bulyankulu],ilisainiwa mwaka 1990, na 1994. Raisi wetu wakati huo alikuwa Mzee Ruksa.

Mgodi wa Nzega ulifunguliwa mwaka 1998 na ule wa Kahama nadhani ulifunguliwa mwaka 2001. Ndiyo maana nikaeleza kwamba ipo migodi ambayo Mkapa alifanya kazi ya kuifungua tu.

IPTL nayo unataka kusema tunarusha mchanga tunapodai ni Mzee Ruksa ndiyo alituingiza kwenye balaa hilo? Huna habari kwamba Mkapa na Rutabanzibwa walikwenda mpaka kwa msuluhishi wa kimataifa ili tuhurumiwe ktk mkataba huu?

Mimi sisemi kwamba Mkapa hana makosa. Infact, nimesema Mkapa anahusika na mkataba wa Tanesco na Netgroup, ununuzi ndege ya raisi, na umiliki wa kampuni ya umeme ya kiwira.

Kila mtu abebe msalaba wake. Nyerere abebe madhambi yake, Mwinyi abebe ya kwake,Mkapa naye abebe msalaba wake, na Kikwete naye tumlaumu kwa ya kwake.

NB:
Kama huu mkataba wa Buzwagi tunaambiwa ni afadhali, hebu fikiria Bulyankulu na Nzega kuna hali gani.
 
Back
Top Bottom