Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Naona kama wewe unataka kupotosha kama siyo utani tu. Kutunza familia yake ni sehemu ya marupurupu ya kazi zote hapa duniani, isipokuwa labda utawa tu. Kazi ya rais nayo inapata marupurupu hayo ya kutunza familia. Kinachoongelewa hapa ni kwa Rais kuwa mkurugenzi wa kampuni binafsi ya biashara.

Kichuguu,

Sijapotosha wala kutania. Nilitafakari sana kabla ya kuandika hayo maneno.

Na utata unazidi pale tunapomtaka Rais aliyepo madarakani asifanye biashara au kumilki kampuni binafsi, na wakati huo huo tunao wafanya biasahara na wakurugenzi wa kampuni zao binafsi wanaotaka kuwa marais. Inabidi tuwazuie hawa ama tutaifishe hizo kampuni zao kabla ya kuwaapisha (wakishashinda uchaguzi) ama itakuwaje? Maana kwa vyovyote vile bado wataendelea kunufaisha hizo kampuni zao hata kama kuna watakaokuwa wanakaimu ukurugenzi or whatsoever!

Ndugu zake watakaokuwa wanamiliki kampuni au biashara mbalimbali wanaweza kunufaika kwa njia hiyo pia, licha ya kwamba huyo Rais atakuwa si mfanyabiashara (akiwa madarakani).

Na ni kwamba Katiba yetu tuliyo nayo iko kimya katika haya yote. Wala haisemi kuwa ukishakuwa Rais basi unanyimwa uhuru wako kama raia kujiongezea kipato (kwa kufungua biashara ama kampuni binafsi) kwa kufuata sheria zilizopo. Kwanza inawezekana ni fursa ya kipato ulichonacho kwa wakati huo ndiyo imekusukuma kutimiza malemgo yako uliyojiwekea kwa muda mrefu.

Nimejaribu kuielewa "common sense" tunayotaka kiongozi aitumie katika mazingira hayo, bado inanirudisha kule kule tu kwamba common sense yangu mimi ni kufuata taratibu na sheria zilizowekwa. Kuna ubaya gani hapo?

Mr. Zero,

Unajua imenibidi nicheke wakati naandika jina lako (nimeikumbuka katuni ya Mtanzania, teh teh teh).

Maneno yako ni mazito. Hata mimi naona ni muhimu kutumia fursa zilizopo kihalali kutimiza malengo yetu ya kupata maisha bora. Vinginevyo turudi kwenye katiba kama nilivyojaribu kuhoji hapo juu.
 
Ila siasa ya Marekani ni wachache sana wanaoingia ni malofa..
 
Kichuguu,
Chukua tano. Ukishakuwa rais huwezi kufa lofa au maskini.
Na kama kuna watu wanaona kuwa hakuna tatizo kwa rais wa nchi kuanzisha kampuni yake binafsi akiwa Ikulu, basi bado tuna njia ndefu kweli kweli.
 
Kichuguu,
Even if Bush doesn't have companies it doesn't mean that he does not have interest in some companies. Nijuavyo mimi marais wengi wa America ni matajiri either through inheritence or other ways but they are all rich. Sioni njia ambayo inaweza kumtajirisha mtu sustainably bila kuwa na investments au companies. Anyway, kwa maelezo yako hawa marais wakiwa madrakani wanauza makapuni yao. Je wakimaliza term zao inakuwaje? wanaanzisha biashara nyingine au hawaruhusiwi kufanya tena biashara maishani mwao?

Kuhusu other means za kujipatia kipato, sidhani kwamba marais have to follow the same ways of living and making monies after their terms in office. Umaarufu wa JKN, Mandela na the likes huwezi ukalinganisha na akina AHM and BWM. Hivi kweli vitabu vya hawa jamaa niliowataja (kwa mfano) nani atavinunua? Personally I can't!!!!!

Personally, sioni tatizo la rais kuwa tajiri provided that hakuiibia nchi. So far sijaona solid convincing evidence kwamba huyu BWM alichota.

USHAURI WA BURE!!!
 
Mr. Zero,
Wamarekani walijipitishia sheria kuepusha "conflict of interest," kuwataka marais wao wanapoingia Ikulu biashara zao waziweke katika kile kinachoitwa "blind trust." Rais hana ruhusa ya kuchunguza kinachoendelea katika hiyo blind trust wakati akiwa mamlakani. Akimaliza muhula wake basi anaweza kurejea kwenye biashara zake. Wenzetu waliona mbali siku nyingi.
P.S. Yaani hutanunua kitabu alichoandika Mwinyi au Mkapa? he, he, he!
 
Jasusi,
Hii ndio shida kubwa ya sisi Wadanganyika. Nafikiri sababu kubwa inayowafanya wengi kumuunga mkono Mkapa ni kwa sababu wanafahamu kuwa mais wa nchi nyingine na hasa US ni matajiri!.. Kwa hiyo judgement yao ni kuwa lazima viongozi wanafanya biashara hata wakiwa madarakani!...
Hii ndio dhana iliyotumika ktk kutangaza mageuzi ya mfumo wa biashara nchini!...Milango wazi ya biashara basi kila mtu leo hii ni mfanya biashara wametupa kabisa majembe yao! na ndio dhana hii iliyotumika kulizika Azimio la Arusha!.. wananchi wengi hawakufahamu kabisa kilichokuwa kibindoni kinachofuata!.... Kama nilivyosema hii ilisha Pangwa na viongozi wa CCM miaka mingi toka Mwinyi akiwa madarakani ....Smooth criminals!
 
Jasusi,
Sioni kitu ambacho AHM anaweza kuandika kunicovince kusoma kitabu chake labda BWM kidogo.

Anaway, sijaribu kumtetea Nkapa, ila sheria nyingi zinazotumika US haziko practical kwetu. Kitu ambacho unaweza kutusaidia ni kusuggest new measures of doing things our way but we can't borrow everything from the WEST without looking at our real situation!!!
 
Ila tukumbuke kwamba katiba yetu inatamka ibara ya nane kuwa nchi hii ni ya misingi ya ujamaa na kujitegemea.

Kama ndivyo kuna maadili ya viongozi kwenye ujamaa na leo nanukuu mbili tuu.

1.Asiwe na hisa kwenye kampuni lolote.

2.Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabila au ya kibepari.

Hapa MKAPA amekosa tena sana kwani ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya kiongozi.

Tuache kutetea uyovu jamani hata Mungu hapendi.
 
Mr. Zero,
O.K, now you are talking. Sheria za Marekani huenda kweli zisiwe practical kwetu. Lakini kumbuka na sisi tulikuwa na sheria kali za uongozi. Hukuruhusiwa hata kujenga nyumba ya kupangisha. Maybe that was an extreme, lakini baada ya kuzika Azimio la Arusha, one would have thought kuwa viongozi wataendelea kubanwa na maadili. Huwezi leo kuwa share holder katika kampuni ya Vodacom na wakati huo huo upitishe sheria bungeni za kuidhibiti Vodacom. But that is now happening in Tanzania. Sheria zilipitishwa bungeni chap chap za kuinyang'anya Mobitel frequencies ambazo zilichukuliwa na Vodacom, eti kwa ajili ya national security kumbe ilikuwa ni stomach security. Baadaye ikabainika kuna viongozi lukuki ambao wana shares katika kampuni hiyo. Mwalimu was right. You can't serve 2 masters. Pale ambapo maslahi ya umma yanagongana na maslahi ya kampuni, viongozi wetu wanapaswa kuwa upande wa umma na si upande wa Vodacom.
 
Jasusi,
Hii ndio shida kubwa ya sisi Wadanganyika. Nafikiri sababu kubwa inayowafanya wengi kumuunga mkono Mkapa ni kwa sababu wanafahamu kuwa mais wa nchi nyingine na hasa US ni matajiri!.. Kwa hiyo judgement yao ni kuwa lazima viongozi wanafanya biashara hata wakiwa madarakani!...
Hii ndio dhana iliyotumika ktk kutangaza mageuzi ya mfumo wa biashara nchini!...Milango wazi ya biashara basi kila mtu leo hii ni mfanya biashara wametupa kabisa majembe yao! na ndio dhana hii iliyotumika kulizika Azimio la Arusha!.. wananchi wengi hawakufahamu kabisa kilichokuwa kibindoni kinachofuata!.... Kama nilivyosema hii ilisha Pangwa na viongozi wa CCM miaka mingi toka Mwinyi akiwa madarakani ....Smooth criminals!

....unataka kusema,hii leo azimio la arusha lina maana?au unakumbukia enzi hizo?


nb:habari za siku?
 
Mr. Zero,

Hivi unajua rais Clinton alitoka Ikulu akiwa na madeni? Sasa hayo mambo ya
kwamba ukiwa rais wa USA lazima uwe tajiri sio wakati wote ni ukweli. Clinton
hata wakati anaingia Ikulu bado alikuwa sio tajiri. Alikuwa na uwezo na watu wakamuunga mkono.

Case ya Monika na uchunguzi mwingine vikammaliza, akatoka ana minus. Baada ya kumaliza muda ndio kaandika vitabu na kutengeneza pesa ya maana.

Hata Blair na mkewe labda watatengeneza pesa baada ya kuondoka Ikulu. Kwasasa pato lao limepungua maana hata mshahara mkubwa ambao mkewe angepata kama Blair asingelikuwa PM, sasa hapati tena.

Ila wakitoka hapo ndio wanaanza kutengeneza pesa lakini sio wakiwa Ikulu.

Huyo Aziz anatumia ujinga Watanzania juu ya mifumo na sheria za nchi zingine kutaka kudanganya. Mifano yote aliyotoa sio sahihi, anatumia ukweli mdogo kufanya conclusion ambayo haiwi supported na facts.
 
Mr. Zero,
O.K, now you are talking. Sheria za Marekani huenda kweli zisiwe practical kwetu. Lakini kumbuka na sisi tulikuwa na sheria kali za uongozi. Hukuruhusiwa hata kujenga nyumba ya kupangisha. Maybe that was an extreme, lakini baada ya kuzika Azimio la Arusha, one would have thought kuwa viongozi wataendelea kubanwa na maadili. Huwezi leo kuwa share holder katika kampuni ya Vodacom na wakati huo huo upitishe sheria bungeni za kuidhibiti Vodacom. But that is now happening in Tanzania. Sheria zilipitishwa bungeni chap chap za kuinyang'anya Mobitel frequencies ambazo zilichukuliwa na Vodacom, eti kwa ajili ya national security kumbe ilikuwa ni stomach security. Baadaye ikabainika kuna viongozi lukuki ambao wana shares katika kampuni hiyo. Mwalimu was right. You can't serve 2 masters. Pale ambapo maslahi ya umma yanagongana na maslahi ya kampuni, viongozi wetu wanapaswa kuwa upande wa umma na si upande wa Vodacom.

....kazi yako ya ujasusi[utani kidogo]....kwani ni siri kwamba tuna walafi wengi kwenye nafasi za uongozi....halafu...ni kwa ulafi wetu wa gongo,komoni,pingu,bia za mafungu,pilau,kuku wa kukaanga[hamna wanaojua kuchoma kuku kama wareno wa nandos]na nyama ya kuchoma[mtanisamehe wakenya....haiitwi nyama choma!]ndio vinatufanya kuwaweka walafi madarakani?

tutavuna tulichopanda na si vingine!....tutajiju haswa!
 
Dar si Lamu,
Aaaah mjomba tunakumbukia tu....njaa tena babuuuu!

Mr. Zero,
Anaway, sijaribu kumtetea Nkapa, ila sheria nyingi zinazotumika US haziko practical kwetu. Kitu ambacho unaweza kutusaidia ni kusuggest new measures of doing things our way but we can't borrow everything from the WEST without looking at our real situation!!!

Statement nzito sanaaaa!...lakini ajabu ni kwamba tunameza kila mfumo from WEST kama walivyo upika...Kisha sisi tunatengua sheria zetu bila sababu ya kimsingi. I mean - Zero, kweli nambie wewe - Ni sababu gani hasa inayofanya sheria imruhusu Kiongozi wa serikali kuwa mfanya biashara?.

Kisha tazama JK alivyokuwa mjanja aliposema biashara yake yeye - Ukulima na Ufugaji!.. hakika jibu hilo ndilo limetupa picha kamili kulingana na mazingira yetu. Miaka yote wazazi wetu, machief wetu wote walikuwa wakulima na shughuli za shamba hazihitaji muda wa rais, chief ama mzazi 24/7. Sisi wote humu ni wakulima, hizo koo zetu zimetoka ktk ukulima. Wafanyakazi wengi wana mashamba yao na hata maprofessa wa chuo kikuu, madaktari na hata wafanya biashara wote wana mashamba toka enzi za Nyerere! Azimio la Arusha halikupiga marufuku Ukulima ambacho ni kipaji tulichojaliwa na Mungu....
 
Kama katiba inasema hivyo na wao hawajaamua kuvivuta hivyo vipengele basi vitumike kuwamaliza!

katiba ya CCM inasema TZ ni nchi ya ujamaa na kujitegemea lakini siku hizi utasikia watz wanasema tena katika majukwaa kuwa enzi zile za ujamaa na siku .....

Ni kwa nini katiba isibadishwe ili UJAMAA NA KUJITEGEMA KIONDOKE NA WAWEKE .....??

KWA HALI ILIVYO SASA HUKO TANZANIA SI RAHIHI KWA bM KUSHITAKIWA!


HIVI KARIBUNI SIKU TATU ZILIZOPITA NILIONA KICHWA CHA HABARI

JK AMESEMA HATAWAHOJI AU HOJI UTAJIRI WA MARAISI WA WALIOMUTANGULIA NA KUWA UTAMADUNI WA KUHOJI MARAIS WALIOTANGULIA HUSABABISHA MARAIS WENGINE KUBADILI KATIBA ILI WATAWALE MILELE!!!!!!??!!!!!!??~?? (GAZETI LA NIPASHE?)

WALA SIKUTAKA HATA KULISOMA!

JE KUNA SUNSTANCE HUMO KATIKA HIYO SABABU!

UPANDE MWINGINE WA SHILINGI NI KUWA UKIWA RAIS WA TANZANIA IBA SAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAANA.

HUTAULIZWA!
BYE FOR NOW AND TODAY!
 
Mr. Mkandala,

Sijui kilimo tunakichukuliaje TZ!! Kilimo naonavyo mimi ni kazi kubwa na nzito kuliko ku-run a small company. Nitakupa mfano nilioona kwenye nchi za kusini mwa Afrika. Farming kwenye nchi za kusini (RSA, NAM) wazungu wamekuwa wakiifanya kama full time activity na wamepata mafanikio makubwa sana. Baada ya uhuru wa nchi hizi serikali zimeingiza mambo ya land redistribution hivyo wakachukua baadhi ya mashamba na kuwapatia wazawa. Hii imepunguza productivity kwa kiasi fulani kwa vile watu wamepewa kisiasa na hivyo wanafanya farming kama wanavyofanya vibosile wa TZ. Watu wanaofanya kazi na wana mashamba ukiongea nao watakueleza ugumu wa farming wakati unafanya kazi. Wengi watakuambia they are occupying land for future use. Farming haikupi muda wa ku-enjoy life in town because it is difficult and need a lot of skiils and attention. Ndiyo sababu vijana wanakimbia vijijini kuogopa kilimo (JOKE!!!). Ukulima wanaouzungumzia TZ siyo farming as bussiness ni njia wanaitumia kujipatia peace of land kwa ajili ya wajukuu wao.
 
Mr Zero Ilonga, na Icadon,

Nadhani mmeshajibiwa maswali yenu yote mliyokuwa mmenielekezea ingawa nimechelewa kuyaona. Nashukuru Jasusi, Mtanzania na Mkandara kwa kutoa ufafanuzi. Ni bahati mbaya sana kuwa watanzania tunataka kuiga mambo ya mitelemko tu bila kujua kuwa kila mtelemko huwa una mpando pia. Tunatumia sweeping statements kudai kuwa marais wa wote marekani ni matajiri kwa hiyo marais wetu pia wawe matajiri bila kuruhusu sheria za kimaadili zinazowabana marais wa kimarekani kutumika kwa marais wetu.
 
Kichuguu,

Mambo ya utajiri wa marais wa US nilizungumzia bila kuwa na uelewa mkubwa wa American politics with regard to this issue. However, that was not my main point if you have been reading between the line in all posting I have made in this issue.

My main points were siyo lazima tuige what is in the US or West, vilevile sikuona ubaya wa rais kuwa na makampuni provided that there is no confrict of interest. Hicho kilimo watu wachojidai wanafanya, kama watakichukulia very serious na kurun farms commercially itakuwa sawasawa na mtu kuwa na company wakati yuko madarakani. Kama ungekutana na watu wanaorun big commercial farms nafikiri ungenielewa nasema nini, here people talk in >1000 hecters. Now imagine puting infrastratures and machinery in such business!!! Siyo mambo ya kusema kwetu tunalima mananasi na machungwa, nikistaafu nitaenda kuwa mkulima. Hiyo ni danganya toto wanajaribu kuoccupy ardhi kijanja kutoka kwa wazaramo kwa ajili ya wajukuu wao. Ndiyo maana kila moja anakimbialia kununua karibu na Dar. Kwanini wasiende arusha, iringa, mbeya, rukwa ambako kuna kilimo cha uhakika wakainvest huko?
 
Mr.Zero,

Kweli kilimo nyumbani ni tofauti na nchi nyingi sana, lakini hadi sasa hakuna ubaya kabisa kwani ni sehemu ndogo sana ya ardhi yetu inatumika, nadhani chini ya asilimia 10 ya ardhi inatumika kwa kilimo. Kwa hiyo mimi binafsi natazama kilimo kwa mapana kama hayo ya nchi za south lakini bila kuondoa wakulima wadogo wadogo ambao kusema kweli hawakushika ardhi yenye rutuba kama ilivyo huko South, mashamba yetu yote yako karibu na miji yetu mikubwa na midogo.
Ukienda sehemu za Mara huko Siari mpakani na Kenya utaona ardhi kubwa ilivyoachwa, na utaona tofauti iliyopo kati ya nchi hizi mbili. Ukivuka mpaka tu utaona mashamba makubwa ya miwa heka kwa maheka... huu ndio Ukulima ambao tunauhitaji Tanzania na bahati mbaya serikali haitazami kabisa mbinu za kukuza kilimo kama hicho zaidi ya wao viongozi kugawana ardhi kubwa za mashamba na wasilifanye kitu. Wote hope yao ktk mashamba haya ni uwezekano wa kuwepo na madini!.. just imagine hiyo ndio vision ya viongozi wetu. Hata ukulima wenyewe ni ktk kutegemea kuiba maliasili za nchi kwa madai ya kwamba ardhi hiyo ni mali yao!.. wale wasukuma wa Buliyanhuru hawakuwa na sheria ya kuwalinda wao ila sasa utakuja sikia kuwa adrhi fulani ni ya rais ama waziri fulani.

Kenya wao wamefanya mpango mmoja mzuri sana, mathlan tuseme zao la Miwa. Kampuni moja kubwa ya kutengeneza sukari imeingia nchini kuwekesha lakini tazama jinsi ilivyo chezwa.
Kampuni hiyo huwa ina wakadiriaji wake ambao hutembelea mashamba ya wenyeji, huko hutazama ukubwa wa shamba na kutoa makadorio ya pato la shamba. Sasa kama wewe Mr.Zero una heka zako 10 na ukilima wa miwa unategemea kuzalisha kitu kama millioni 10 kwa mwaka. Hii kampuni inakupa offer ya millioni 15 kwa mwaka kulitumia shamba lako wewe kuzalisha miwa yao. Kwa hiyo wao wanaleta mashine zao kulima, wanapanda na kuvuna kisha mwisho wa mwaka wewe unaenda ku collect millioni zako 15! for doing almost nothing na ardhi bado ni mali yako. Hapo wewe unapata nafasi ya kushughulika na maswala mengine kabisa!....
Kenya wamefanya hivi ktk zao la Chai, kahawa na mazao mengine mengi ambayo makampuni makubwa yamekodisha ardhi kwa wananchi (mkataba) kutokana na msukumo wa serikali kuongeza kilimo!..Kizuri zaidi ni kwamba Makampuni haya hujenga viwanda nchini kumalizia process ya zao, yaani finished product inatoka Kenya moja kwa moja sio tena kusafirisha mali ghafi nje.
Tanzania tunashindwa kitu gani?..tena basi sisi ardhi ni mali ya serikali hatuna haja kabisa ya wazungu wakulima wa South ambao wao watatuzunguka tu ktk soko na ulipaji kodi. Makampuni yapo makubwa yenye interest za kilimo kwani sasa hivi mashirika haya yamegundua kufuatilia zao toka chini hadi finished product! Inakuwa kama walivyotaka wao na gharama ni ndogo!.Taratibu mpango wa soko la dunia la mazao linaanza kufa!...mali inatoka mashambani hadi kuwa finished product bila kwenda sokoni! Makampuni yanakuwa na uhakika wa uzalishaji na supply ktk nyanja zote mbili - Ukulima na Kiwandani.
 
Mr. Zero: Afadhali umekuja kabla sijaondoka.

Ni kweli kuwa kurun commercial farming ni sawa kabisa na kurun kampuni ya bishara na umesema kweli kabisa rais hawezi kutumikia madaraka ya urais sawasawa wakati anaendesha biashara ya kilimo. Nadhani wachangiaji walio support farming activities kama shughuli za ziada walikuwa wakiongelea medium scale farming siyo large scale farming.

Kwa mtazamo wangu ni kuwa, serikali yetu illifanya makosa sana ilipoamua kuvunja Azimio la Arusha na kuunda Azimio la Zanzibar kuruhusu viongozi kuwa wafanya biashara kwa kuiga Marekani bila kujua system ya US inavyofanya kazi. Ni kama wewe ulivyokuwa unadhani kuwa wanasaiasa wa marekani ni wafanyabiashara.

Pamoja na makosa hayo, bado waliacha kifungu cha sheria kinachomzuia mtumishi wa serikali kutumia nafasi yake ya kazi kwa manufaa binafsi. Kwa kawaida kifungu hiki kinamzuia mfanya kazi wa serikali asitumie rasilimali zote za serikali na dhamana ya cheo chake kuendesha biashara zake binafsi: kwa mfano kutumia stationary za serikali, kutumia magari, computer, simu na watumishi wa serikali walioko chini yake pamoja na kutumia jina la cheo chake. Kulingana na madaraka aliyonayo rais wa Tanzania kwa mujibu wa katiba, idadi na aina ya watumishi wa serikali wanaomzunguka na raslimali za serikali anazotumia kila siku kwa saa 24, kifungu hiki kinamzuia kufanya biashara kwa sababu nyingi tu unazoweza kuainisha.

Swali la kujiuliza ni lile lililoletwa na Ilonga kuwa je kama mtu tayari ni mfanyabiashara, ina maana haruhusiwi kuwa rais? hapo kweli ni ngoma kali. Ndiyo maana kweli tunahitaji kuwa na katiba mpya.
 
Back
Top Bottom