Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Bwana Mkandara,

Naoana tuko na mawazo sawa! Point zako kali na somo la bure JF. Ila nataka kukufahamisha kwamba umenifungua macho kiasi kikubwa. Kumbe wa jamaa wanakimbilia ardhi kwa ajili ya madini? Ndiyo maana Mkuranga kumekuwa deal kwa sababu ya fununu za mafuta. Mimi siku zote nimekuwa nashangaa kama kweli Viongozi wetu wanajifanya wanalima mbona hayo mashamba hatuoni yanazalisha kitu.

Nafikiri wao ndiyo walitakiwa waaonyeshe mifano wananchi badala yake wanang'anga'ania madaraka mpaka wafe. Afer all wote wamekulia vijijini lakini wanaogopa kurudi huko kuinvest kwenye kilimo. Mimi niliposikia ex PM anastaafu siasa anaenda kulima nilifikiri anaenda kufanya kitu cha maana, then nikasikia ana kashamba ka hekari 30 - 40 na vingombe vichache vya maziwa. Baada ya muda yuko US anasoma, hapo ndipo nilipoona kichekesho. Kama kilimo tayari ni mtaaramu kwenye hiyo fani. Kumbe ilikuwa danganya toto watu wasahau ili ajirudishe taratibu kenye mapolitics. Kwa nini asitumie influence yake kuwaincourage wananchi kulima kwa yeye mwenyewe kuwa mfano?
 
Mr. Zero,

Mzee Kawawa analima Uyoga, sijui mashamba yake makubwa kiasi gani.

Mkapa naye ana shamba Morogoro, yeye kalipwa madeni yake wakulima wadogo wadogo hawajalipwa. Sasa huyu ambaye alitakiwa kuongoza mapambazo dhidi ya hao wanunuzi wa mazao, badala yake yeye anakubali kulipwa chake huku maskini wanasota.

Kama ulivyoandika hapo juu, hawa wastaafu walitakiwa wakachukue mashamba ya matunda kama kule Tanga, wao ndio wawe chanzo cha soko na utaalamu kwa wakulima wenye mashamba madogo madogo na wao wangetafuta soko la ndani au nje kwa ajili ya hao matunda. Lakini wanajiita wakulima ili kudanganya Watanzania tu, vya kuchinja hawawezi hao, wamezoea vya kunyonga.
 
Watanzania aisee hoja simtetei mtu hapa huu ni ukweli tu
Unajua watanzania wanatatizo moja hawapendi kumuona mtu akifanikiwa mfano BM hata kama kaiba lakini kafanikiwa, anatoa misaada mbali mbali kajiusisha kwenye mambo ya ukimwi na kadhiliki kiufupi pesa ipo. Ingekuwa mkapa katoka kama Dr Omar ali juma mungu aiweke roho yake mahali pema watu wangefurahi sijui ama mngemcheka hajatumia nafasi yake vizuri? Mimi binafsi nikiwa raisi siwezi kuto jiendeleza kimaisha bwana na kama mtu anasema sio kweli basi huyo mnafki.
Lakini kama hauja abuse cheo chako kama wazee wengine mfano mabutu na wengine basi sioni kama kuwa na shamba nikosa. Na hamna mtanzania anaweza akasema mkapa kaiba kama kina mabutu share zake nyingi watu wanazijua
Watu wengi hawaelewi kwanini wakubwa wananunua mashamba kwanza shamba ni bei poa. Kama hamjui mpaka mapori yanauzwa bongo sio mbuga za wanyama mapori. Mtu anaona bora anunue shamba million 10 kuliko jumba la million 200 likamkosesha usingizi. Vifaa vya kilimo havina kodi. Kuna mikopo mingi tu unaweza ukazoa ukiwa na shamba
 
Mr.Ziro,
Ndio maana kila siku nawambia kuwa CCM hupanga vitu kwa manufaa yao kabla ya Katiba ama sheria kufanyiwa marekebisho. Hilo la viongozi kuwa wafanya baishara lilisha pangwa toka Mwinyi akiwa madarakani ktk awamu yake ya pili. Lakini mengi waliyafanya kwa kificho kwani Mwl. alikuwa bado hai. Hotel zote kubwa Dar ni mali za vigogo hayo majina ya wahindi ni kamba tu..huwezi kupata kiwanja karibu na Polisi Officers mess hata kidogo enzi za mchonga.
sasa tembelea milima ya Uruguru, Handeni, Sumbawanga, Usukumani na mkoa wa Mara kote viongozi wamekamata ardhi kubwa na hawalimi kitu chochote...Tena wengi wao hawana nasaba wala ukazi wa maeneno hayo! zaidi utaona wanatuma watu huko nchi za nje kuwatumia vifaa vya kutafutia na kuchimba madini!...Wameajiri watu wa Stamico kutafuta madini tu. Hapa mjomba sheria ya mtu kumiliki ardhi haijatoka bado na wanaifanyia kazi usiku na mchana!...(USIKU - ktk kamati za ufundi) kwa hiyo siku ikija toka sheria, asilimia 10 ya wananchi hao viongozi wetu ndio wameshika asilimia 80 ya ardhi yenye rutuba ama madini.. kwa hiyo deal lolote la madini ni kati yao na hao wawekeshaji. Je, hapa kuna tofauti ya kiongozi wetu na Kaburu wa Zimbabwe?

Kwa hiyo kumpa support Mkapa ni kukubali kutoyaona malengo yao. Mkapa ameyafanya yote kwa makusudi na akijua vizuri kwamba cheo chake na kumiliki kampuni ni makosa makubwa lakini hapo hapo ktk Katiba wamepitisha sheria ambayo inaruhusu viongozi kumiliki biashara. hawakutaja viongozi gani? na wala kuweka ibara inayohusu conflict of interest!... walijua wazi kuwa sherria wanayo wao mkononi na katiba peke yake ndiyo inaweza kuwakwamisha hasa Azimio la Arusha!
Kama alivyosema Kichuguu, mashamba ambayo JK amezungumzia ni shamba dogo tu ambalo hata marehemu babu yangu alikuwa na kubwa kuliko hili la JK.
Kiongozi kuwa Mkulima, mfanyabiashara kama wa South ambayo ni full time job nadhani hiyo ni nje kabisa! Muhimu tuelewe sababu kubwa zilizosababisha kuweka sheria... ikiwa ni conflict of interest pamoja na nafasi ya kiongozi wa serikali kuhudumia nyumba mbili - kama vile tofauti za ndoa kati ya mke na mwanaume. Sheria inayomruhusu mume kuoa zaidi ya mke mmoja inaweza kabisa tafsirika kama ni kuwadhalilisha wanawake ama ni sheria inayowafunga wanawake kwani wao hawana ruksa ya kuoa waume zaidi ya mmoja...Hapa hata utumie logic , sayansi na kadhalika bado kutakuwepo na utata wa kufafanua sheria ama mila kama hizi. lakini ikiwa ndio tamaduni na mazingira yenu ni vitu ambavyo havihitaji ibara kuelezea zaidi. hapa nachoona wengi wanajaribu kuweka hii ndoa kwa kulinganisha mwanamme na mwanamke bila kujali kwamba Mkapa ni mwanamke akiwa kiongozi na rais wa nchi.
Pia kumbuka kwamba tuliposema viongozi wanaruhusiwa kufanya biashara haina maana kuwa rais ama kiongozi yeyote wa serikali anaweza fungua Benki KUU!, tutaonekana ni wenda wazimu, lazima tuelewe kuna limit ya kila ruksa!..common sense tu inatakiwa.
Kitendo cha Mkapa ni sawa kabisa na baba aliyembea na mwanae! tutaweka kila sababu za kusema kwani Mkapa si mwanaume, ama mwanaye hana haki ya kuchagua mume ama kwani hawawezi kuzaa!... bado itabaki kuwa rais kufungua na kumiliki kampuni ni kitendo haramu kabisa...

Sizzla, Hata Saadam Hussein aliyafanya mazuri kwa maskini kuliko Bush!.. Hitler vilevile! hata Alex Masawe ni mtu mzuri sana kwa wale tunaomjua!
 
Mkandara,
Asante kwa jibu lako kwa Sizzla. Hizo hela anazotumia Mkapa kwa ukimwi hazitoki mfukoni mwake. Actually ameanzisha hiyo Foundantion kwa madhumuni ya kupata michango kutoka foundations za kigeni kama vile Carter Center etc, kwa hiyo tusidanganyike kuwa Mkapa kafanikiwa na anatoa huduma. Kufanikiwa binafsi hiyo inawezekana ikiwa mtu unakubali kuwa kiongozi mla rushwa na mpaka hapa hatuna ushahidi unaoashiria kuwa Mkapa alijitahidi kuepuka rushwa kama alivyofanya Mwalimu alipokuwa uongozini.
 
Sizzla,

Unamwongelea nani? The Vulture Mkapa na kundi lake? Wanazunguka nchi mbalimbali wakiwaambia wazungu jinsi Watanzania walivyo maskini na wanavyohitaji misaada. Wakifika TZ wanawatambia Watanzania jinsi Tanzania
ilivyo na neema sasa mabank yote yanakopesha bila wasiwasi.

Hawana tofauti na vultures, wanasubiri Watanzania waangamie zaidi kwa malaria na ukimwi ili wazidi kupata misaada.

Shame on them, umewahi kujiuliza Mkapa ana wafanyakazi wangapi ambao wanalipwa na serikali? Zaidi ya nusu ya pesa wanazopewa haziendi kwa Walengwa.
 
JK kakwepa hoja za ANBEM au diplomasia?

JK: "Sina hakika na hili kama tatizo na kukopa au kuanzisha kampuni. Lakini naamini kiongozi kufanyabiashara ili mradi tu amefuata taratibu zinazokubalika si tatizo. Lakini mimi sioni kama ni uungwana kuwachunguza au kuwafuatafuta viongozi wetu wastaafu eti kwa sababu tu imebainika ameanzisha kampuni au alikopa na amerudisha mkopo haraka.

SWALI: Kwanza hana HAKIKA, lakini pia anasema "haoni ni UUNGWANA kuwachunguza viongozi wastaafu na kuafuata fuata, je, nchi sasa inaendeshwa kwa UUNGWANA na si UTAWALA BORA? atapataje uhakika bila kuchunguza? Je, atajuaje kafuata utaratibu bila kuchunguza? Atajuaje kama mkopo umelipwa na mhusika ama MAFISADI aliowauzia RASILIMALI ya TAIFA?

JK: "Sioni kama ni utaratibu mzuri mimi leo kwa sababu tu kuna hisia na hakuna ushahidi wowote mzito nikaanza kumchunguza Mzee (Ally Hassan) Mwinyi, Mkapa au Mwalimu Nyerere" .

SWALI: Haoni kama ni utaratibu mzuri na kwa sababu ya hisia, ina maana UTARATIBU mzuri unajengwa kwa vigezo gain, inawezekana pia si utaratibu mzuri kumchunguza ama kumfikisha mahakamani mfanyabiashara wa mihadharati wakati aliichangia CCM katika uchaguzi lakini je, utaratibu mzuri unaanzia wapi? Kwa walala hoi wanaoiba viazi kujaza matumbo na kuuwawa kwa kuchomwa moto? Utaratibu mzuri unaanzia kwa vizee vyenye macho mekundu wanaouwawa Shinyanga na Mwanza? Utaratibu mzuri unaanzia kwa Machinga wanaoganga njaa mitaani Kariakoo?
Pili, anasema kwa sababu ya HISIA tu, ina maana Rais sasa anazungumzia HISIA, atawezaje kupata ushahidi bila kuagiza uchunguzi huru? Lakini pia kwa nini anawataja Mwinyi na Nyerere wakati hoja haiwahusu? Mwinyi na Nyerere wamestaafu muda mrefu na hadi sasa hakuna aliyeibuka na hoja nzito kama alizo nazo Mkapa na pia Mwinyi anaonekana mitaani hadi watu wanaanza kujenga hoja kwamba inabidi aombwe radhi kwa kusakamwa yeye na mkewe Sitti bila kuwapo hoja zenye mashiko wakati Nyerere hadi umauti hakuwa na utajiri wowote na mkewe Maria alitaka kuporwa hadi kiwanja sasa kwanini anawahusisha? Je, kwanini watu wasijenge hoja kwamba naye si msafi ndo maana anataka kujenga hoja mapema asiulizwe akistaafu?

JK. "Mimi hilo halinipendezi ila ikitokea kuna ishu nzito na ushahidi ukawa wa wazi kwamba kuna kiongozi amejihusisha na masuala maovu hapo sitasita kuchunguza."
"Sifikirii kufanya biashara nikiwa Ikulu. Kwanza mimi huwa sipendelei sana kufanya biashara. Nimejifunza kuwa mkulima na mfugaji zaidi.
"Tayari nimeanza kulima na kufuga ng'ombe. Kule kwetu ukiwa na ekari 20 za mananasi wewe ni mkulima mkubwa sana," alisema Rais Kikwete.
" Namkumbuka rafiki yangu mmoja Mwingereza aliniambia, ukipitisha miaka 40 kabla hujaanza kufanyabiashara, achana nayo ukianza ni maumivu. "

SWALI: Rais anasema hakuna issue nzito kwa Mkapa kufanya biashara akiwa madarakani halafu anasema yeye hatofanya biashara sasa na hata baadaye, je, kama hakuna issue kwanini nayeye asifanye biashara? Maana hakuna asiyependa maisha bora kama alivyoahidi kwa kila Mtanzania akiwamo yeye mwenyewe. Halafu issue nzito na ushahidi wa wazi ataupata wapi bila kuchunguza?
 
Rais mstaafu si anapata 80% ya mshahara, huduma nyingine kama usafiri wa ndani na nje/matibabu/mishahara ya walinzi,madereva,wasaidizi na watumishi wengine vyote vinatoka serikalini?
 
Nafikiri tatizo letu sisi Watanzania tunataka JK awe mwamuzi wa haki nchini, Mkapa anatakiwa kuwa codemned kwanza na wanasheria wetu. Hii ni kazi ya judge mkuu kama ilivyofanyika Peru ama tunatakiwa kuwa na kitu kama Congressional commission yenye wawakilishi toka vyama vyote!... hata hivyo hawa jamaa wetu inabidi JK afahamu kuwa they are Untouchables ndio maana tunakwenda kwake!

Halisi, JK kazidi sana uungwana kiasi kwamba sasa hivi anavurunda kabisa! wananchi are calling for an ethics investigation! yeye anakuja kutetea vitu ambavyo yeye mwenyewe hana usshahidi wa kutengua madai ya wananchi....wakati anafahamu fika kwamba mambo mengi machafu yalifanyika na ndio maana wananchi wengi walimchagua yeye wakitegemea kuwa atakuja yashughulikia maswala ya rushwa hizi kubwa kubwa!..Na hivi kweli wananchi wakishusha ushahidi tosha ataweza kuufanyia kazi?...Na kwa kiasi gani anachotakja ushahidi huo uwe ili aweze kuamini kuwa habari hizi sio HISIA!

Mr. President, just launch an investigative panel of the ethics committee, truth will always prevail! That's all we asking.
 
Mkandara,
Kama JK kashindwa kuwachukulia hatua wauza madawa ya kulevya na wala rushwa baada ya kukiri hadharani kuwa majina anayo, na leo ni miezi zaidi ya nane. unategemea atasema nini juu ya hili?
 
Kumshurutisha JK kuanza kusumbuana na Blaza Ben ni kuangalia suala hilo bila ya umakini.


Quote:Originally Posted by Halisi
JK: "Sioni kama ni utaratibu mzuri mimi leo kwa sababu tu kuna hisia na hakuna ushahidi wowote mzito nikaanza kumchunguza Mzee (Ally Hassan) Mwinyi, Mkapa au Mwalimu Nyerere" .


Wengi wetu tunapenda kuona mambo yanafanyika ili kufurahisha nyoyo zetu bila ya kuangalia umuhimu na athari za suala hilo kwa jamii yetu kwa ujumla. Jibu la JK hapo juu linasema kila kitu kwamba kuna vichaka havina haja ya kuchunguliwa. Tukianza Blaza ben itakuja Mzee Mwinyi halafu Mwalimu halafu tunajikuta tumemaliza kubomoa kila nguzo zilizotumika kujenga taifa letu ambalo hata kama tuna maoni tofauti lakini ni taifa la kujivunia.

Kama mnakumbuka mara tuu baada ya maneno kuhusu Blaza Ben kuanza kuchukuwa kasi Baba Askofu Pengo alimfanyia misa maalumu Blaza Ben na "mkewe". Kwangu mimi ule ulikuwa ujumbe tosha. Keeeeep out

Sasa tukianza huko tuwe tayari kusikia ya Mzee Mwinyi na misa maalumu kufanywa na kina Basalleh na Ponda....na wao wakitoa ujumbe ...Keep out you bloody "kafiri"

Then boom, tunajikuta hata tukikosa concentration kwa matatizo haswa ambayo ni kuwa na mfumo unaoruhusu hayo tunayolalamikia kutokea. Taifa letu bado halina mfumo na nyenzo za kiutendaji za kuweza kushughulikia baadhi ya masuala bila ya kuhatarisha kubomoka kwake. hata kama tunadhani mambo ni shwari lakini ukweli hali ni tete mno kisiasa na hata wale ndugu zangu wa upinzani ambao wangependa kufaidika na hili na mengineyo kisiasa wanajua hilo. Huo ni ukweli ambao tunapaswa kuutambua na kuukubali.

Ndugu zangu, hisia za kisiasa na uanasiasa ni kitu kimoja....uongozi wa nchi ni kitu kingine.....

Tujaribu kufungua vichwa vyetu kung'amua busara za misimamo ya Kaka JK hata kama inaumiza moyo mnoooooo

Tanzanianjema
 
Nashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri, nadhani sasa ni RUKSA kufanya lolote, nilikua sijafahamu, kumbe SIKUANGALIA kwa umakini, japo sikumshurutisha JK, nakubali mara zote huwa siko makini. Nakubaliana na wewe pia kwamba kumfuata fuata Blaza Ben ni kuharibu utaifa, naomba radhi kwa hilo maana sikujua kwamba utaifa ni kwa waheshemiwa, sisi wadharauliwa na watoto wetu kule Ukraine walale mbele, wao hata wakifa utaifa hautaharibika kwa kuwa hawana faida yoyote kwa Taifa hili na pengine hawana faida kwa MATUMBO YETU sisi wenye nafasi hata ya kuandika humu ndani, seuse wale ambao hata VIBATARI kwao ni ANASA. Ahsante sana kaka TANZANIANJEMA naamini ni kweli kabisa kwako na wenzako wanaosoma UK, CHina, US etc kwa fedha za serikali kweni TANZANIA NI NJEEEMA sana na munahitaji mshikamano wa kitaifa, WAKOME WANAOTHUBUTU KUTAKA KUVURUGA AMANI NA UTULIVU WETU, eti tu kwa sababu MTU KAJIPATIA KIHALALI KABISA MKOPO NA KUWA MJASIRIAMALI pale LUTHULI 15, (EOTF) sasa WAMA bila kulipa pango wala umeme. SAMAHANI SANA AMANI NA UTULIVU IDUMU ILI TUENDELEE KUISHI KWA NA KUPATA KUANDIKA KUZIMA HOJA HUMU NDANI
 
Uoga ndio unaondama....ila itakapofika wakati wananchi wakiondoa woga basi nchi itasimama IMARA....Nature ya nchi yetu siku zote tumekuwa tukiambiwa utavunja AMAN unarudi nyuma................
 
Pamoja na mantiki ya JMK, makosa aliyofanya BWM kama rais wa nchi hayawezi kufananishwa hata kwa punje moja na makosa ya AHM na JKN. Huyu bwana alikuwa akifanya mambo yale kwa makusudi kabisa kwa faida yake mwenyewe na huku akijua kabisa kuwa hilo ni kosa na ndiyo maana alikuwa akificha. Hao waliomtangulia nao walifanya makosa mbali mbali lakini ya kwao ama yalikuwa ya kiutendaji bila kujinufaisha wenyewe au walifanya kwa uzembe bila wao wenyewe kujua kuwa ni makosa. Tukiruhusu Ben apite bila kuulizwa, tutakuwa tumetelemsha sana hadhi na utakatifu wa ofisi ile kubwa ya nchi ambayo ndiyo inayoidhinisha watu kunyongwa au kuwekwa kizuizini. Vile vile hatutakuwa na haja ya kuwa na TAKURU, na vitendo vya rushwa kwa ngazi zote vitakuwa vimeruhusiwa. Tunategemea kuwa ofis ya Rais itachukuliwa kwa standard kubwa katika mambo ya rushwa lakini analosema JMK ni kuwa rushwa katika ofisi ya rais ni ruksa.
 
TanzaniaNjema,

Sheria ni msumemo brother, ukianza kuchagua ya Ben yakawatofauti na ya Mtikila, hiyo sheria sio msumeno tena bali chujio.
 
viongozi lazima wawajibike na matendo yao hususan yale ambayo sio kwa maslahi kwa taifa.

nadhani ni vyema pakiwepo taratibu ambazo zinaweza kutumiwa pindi kiongozi anapo-abuse mamlaka aliyopewa. kama itawezekana hilo wakati kiongozi yupo madarakani ni vyema na kama itabidi taratibu zifuate atokapo madarakani ni vyema. nia ni viongozi kujua kwamba watashughulikiwa pindi wanapo-abuse madaraka yao.
 
ANBEM Limited: Operated from the first lady`s office



THISDAY REPORTERS
Dar es Salaam

FORMER president Benjamin Mkapa and first lady Anna Mkapa operated their private business company, ANBEM Limited, from a registered office within the official State House walls in Dar es Salaam, THISDAY can now reveal.

According to our investigations, documents setting up ANBEM Limited in 1999 listed its physical address as Plot Number 15, Luthuli Road � which is a government building forming part of the Ikulu estate.

It is also the building allocated for use as the official office of all sitting first ladies.

Further investigations have shown that 15 Luthuli Road was also the registered physical address of the Equal Opportunities for All Trust Fund (EOTF), a non-profitable organization established by Mrs Mkapa in June 1997.

EOTF's stated objectives include: ''To initiate, design, promote, facilitate and support the empowerment of the disadvantaged segments of Tanzanian society.''

But it has now been confirmed that even as EOTF steadily built a name in this area of activity over the years, ANBEM Limited was also operating from the same State House building maintained by taxpayers' money.

Mr and Mrs Mkapa, whose two tenures at State House covered the period 1995-2005, registered ANBEM Limited in 1999, with the official registration documents describing them as 'entrepreneurs' and sole shareholders/directors of the limited liability company.

Stated objectives of ANBEM Ltd include: ''To carry on business and to act as merchants, general traders, warehouse, stockists, shopkeepers and operators of supermarkets, commission agents and carriers.''

Official records also show that the company listed the Ikulu building as its registered office in annual returns signed by both directors (Benjamin William Mkapa and Anna Mkapa) between 1999 and 2005.

In 2002, ANBEM Limited was granted hefty loans of $500,000 (approx. 620m/-) and 250m/- from the National Bank of Commerce Limited and CRDB Bank respectively. Both loans have since been cleared.

It was at the end of Mr and Mrs Mkapa's second and final term in office in 2005, that both the ANBEM Limited and EOTF offices were relocated away from Ikulu.

The 15 Luthuli Street building, situated right inside the State House boundary walls, is currently being used by Wanawake na Maendeleo Foundation (WAMA), another NGO established and run by the sitting first lady Ms Salma Kikwete.

Since THISDAY started running exclusive reports on ANBEM Limited and related business dealings, a growing national debate has ensued over the ethical considerations of Mr and Mrs Mkapa�s actions while still at State House.

While one school of thought argues that the couple did not break any law in registering their own private company while at Ikulu, another contends that the move - being mainly geared at ensuring personal gain - could well be interpreted as an abuse of office.

Issues of possible conflict of interest and undue influence, on the part of a sitting president endeavouring to balance official responsibilities and private business affairs, have inevitably been brought up.

Speaking to local media editors last week, incumbent President Kikwete said his administration was prepared to let go the matter of Mr and Mrs Mkapa starting and operating a private business company from State House.

But he maintained that the government of the day would not hesitate to take action against proven allegations of serious wrongdoing in the matter.

President Kikwete also declared that he personally had no intention of engaging in private business dealings while occupying the highest office in the land.
 
Naona JK aende Zambia kwa mwamawasa aone mambo wanafwanywje. Chiluba has now been ordered to vacate his mashion with funitures valued at 250K USD as part of recovering the monies he squandered during his term in office. Haya mambo yanaweza kufanyika bongo kama tuko serious. Ila tatizo speed ya watoo wa vigogo wanavyovamia siasa nafikiri watu wanaogopa visasi siku za mbeleni!!!!!!
 
Ikulu kuna Biashara gani..........'Mwl J.K Nyerere'

Waungwana nadhani bado mnakumbuka ile speech maarufu ya Mwl. Nyerere alipokuwa akiwazodoa wale waliokuwa wanataka kwenda ikulu kwa udi na uvumbi akiwauliza kwa mshangao..Ikulu kuna biashara gani?

Kwa ushahidi wa hapo juu kutoka 'This day' sio tu maneno ya Mzee wetu Nyerere yanamuumbua Mh. Rais mstaafu, BWM bali ni ni jambo la kuhuzunisha na kusikitisha kwa wale wengi tulioamini Mzee wa Uwazi na Ukweli atasimama ktk 'moral & ethical grounds' za Mzee Nyerere gwiji na mpikaji wa wanasisa wengi wa Tz.

Swali , je kweli walala-hoi tulio chini katika 'food chain' tutasalimika ikiwa vigogo huko juu wanajinufaisha wenyewe na familia zao kwa kutumia migongo ya public offices walizo nazo.

Na hayo mabenki yetu yalikuwaje yakatoa mikopo kwa ofisi ambayo 'address yake ni state house'.
Je mabenki yetu yalitishwa kwamba wasipotoa mikopo watapoteza leseni zao au kufungwa jela?..... Benki zetu zinatambua nafasi yake ktk jamii??? Au ndio ile perception za kizamani, Bankers are greedy and non-caring and non-considerate.

Je Mh. Kikwete anahitaji ushahidi upi zaidi ya huo wa THIS DAY kutaifisha mali hizo zilizochumwa kwa kutumia majengo ya walipa kodi wa Tz.

MH. RAIS JK, Kumbuka watz walikUpa ushindi mkubwa wa kishindo 80% kwa matarajio wewe ndio utakekuja kuwa nuru ya ukumbokozi kutoka kwa wanasiasa waliotumia ofisi za umma vibaya kwa manufaa yao, na matatizo mengine yanaousibu umma wa Tz.

It is only sensible to set up 'independent enq. commitee' to investigate this matter further and take appropriate actions where necessary.

Any proceeds recovered from the individual who abused his power whilst in office can carefully invested in HOSPITALS, SCHOOLS AND EDUCATION, and it will set precedent to future leaders that no one is above the law.
Kama baadhi ya wachangiaji walivyoainisha mzee Nyerere na Mwinyi kama walikuwa na makosa yao basi ni either 'technical or negligence' and wewre not intetionaly acted as this one comes to light.

We still have faith in you Mr. President and dont let us down!!
God bless Tanzania & Africa
and protect us from the evil of selfish leaders.
 
Back
Top Bottom