Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Philip Magani, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi NBC, ni rafiki mkubwa wa Ben Mkapa, na wanatoka eneo moja. Inasemekana kwamba Gavana Daudi Balali naye amekula sana kwa kushirikiana na Mkapa.

Watanzania kazi tunayo, maana inaonekana kila tunayemwamini anatugeuka. Mkapa,Daudi Balali,.....the list goes on and on.
 
Bubu, hebu sasa sema. Amefanya kazi ya siasa ionekane tamu sana na kusaidia kujenga matajiri wa kitanzania halisi wengi.
 
He has done better economically and below par in the war against corruption. My verdict is, overall he has done good job. Well done Cha Mkapa!
 
Mwanakijiji,

Imetoka gazeti la jana, kurasa ya tatu. Kichwa cha habari kilikuwa MKapa Kuwa Muwazi na mkweli Kuhusu Utajiri wako.
 
We voted him into office so that he can do a good job and not otherwise. If he did it, well and good! that's what was expected from him.

If he did something contrary to the Tanzania Leadership Code, he should equally be accountable.
 
Naomba nikuulize: Ni dhambi kwa Rais kufanya
biashara? Ni dhambi Rais kuanzisha kampuni na kukopa
na kisha kulipa deni? Je bado unaishi zama za Azimio
la Arusha? Ni viongozi gani wanaruhusiwa kuanzisha
makampuni na kukopa...mawaziri na makatibu wakuu? Kwa
nini iwe nongwa kwa Rais?
Kwa leo..nasubiri majibu
 
Shy.. masuala ya Dhambi waulize wachungaji..!!

Kinachofanywa gizani lengo lake kufichwa!! Kama siyo vibaya kwanini hakusema wakati ule kuwa anaanzisha kampuni... na alitumia vipi ofisi yake ya Urais kufanikisha biashara zake... tatizo siyo yeye kuwa na biashara au mtu yeyote yule kwani sisi ni nchi ya kibepari... tatizo ni kwanini kwa kutumia ofisi yake ajipendelee?
 
Naomba nikuulize: Ni dhambi kwa Rais kufanya
biashara? Ni dhambi Rais kuanzisha kampuni na kukopa
na kisha kulipa deni? Je bado unaishi zama za Azimio
la Arusha? Ni viongozi gani wanaruhusiwa kuanzisha
makampuni na kukopa...mawaziri na makatibu wakuu? Kwa
nini iwe nongwa kwa Rais?
Kwa leo..nasubiri majibu

Assuming alilipa.........
How do we know kuwa alilipa?
 
Naomba nikuulize: Ni dhambi kwa Rais kufanya
biashara? Ni dhambi Rais kuanzisha kampuni na kukopa
na kisha kulipa deni? Je bado unaishi zama za Azimio
la Arusha? Ni viongozi gani wanaruhusiwa kuanzisha
makampuni na kukopa...mawaziri na makatibu wakuu? Kwa
nini iwe nongwa kwa Rais?
Kwa leo..nasubiri majibu


Shy,

Kwa sasa hatuko kwenye enzi za Azimio la Arusha tena kwa vile tuanfuata siasa za soko huru. hata hivyo siasa hizo za soko huru zinamzuia kiongozi kutumia nafasi yake kujilimbikiza mali kinyume na maadili ya nafasi zao. Ndiyo maana marais wa marekani hutangaza mali zao wakati wanaingia madarakani na kujitoa katika shughuli zozote za kibishara na investments zao kuziweka kwenye trusts ambamo wao wenyewe hawahusiki na maamuzi kiutendaji. Kama ilivyo kwa raia wote, rais pia hutakiwa kuripoti mapato na malipo yao ya kodi kila mwaka, na ole wake apatikane na mapato dubious. Je Mkapa alifanya lolote linalofanana na Rais wa Marekani ambao wao ndio vinara wa hili soko huria? Kama Mkapa angekuwa rais wa Marekani na akajulikana kuwa alianzisha kampuni na kukopa benki (inayomilikiwa na serikali kwa hisa nyingi kuliko wote - assuming kuwa benki ya aina hiyo ipo marekani) wakati akiwa rais wa nchi kilikuwa kinatosha kabisa kumfukuzisha kazi yake kwa aibu.
 
Angalieni huyu naye Kibaki wa siasa anavyosema. Watu wamesaliti elimu zao, wanatumia umaskini kuomba misaada nje, wakipata wanagawana huku maskini vijijini wanaendelea kuwa maskini. Huyu jamaa sasa ndio mshika mikoba ya Mkapa.

----- Original Message -----
From: Aziz Ponary Mlima
To: list@tanzanet.org
Sent: Wednesday, June 06, 2007 12:58 PM
Subject: Re: [tanzanet] FWD: Mkapa awe mkweli na muwazi.


Waheshimiwa, "Wasomi"

Niliamua kuwa kimya, lakini kwa suala hili nimaamua kuzungumza machacche hasa baada ya kuangalia hoja zinazotolewa na baadhi ya "Wasomi Wetu" ambao baadhi yao kama wakiwa na ujasiri kidogo na kuupata ubunge wanaweza kuukwaa uwaziri🙂 Mjadala mzima huu na yale yote yaliyoandikwa kwenye magazeti kwa mwandishi yeyote anayeheshimu taaluma yake na kuwaheshimu wasomaji wake taarifa tulizozisoma siku zilizopita zinatia wasiwasi kiwango cha "Journalism" tuliyonayo kwasasa au tuseme kwa yule aliyeandika makala hayo.

Kilichonifanya kujitupa kwenye mjadala huu siyo yule anayeandika kwa ajili ya kuuza magazeti bali hawa "Wasomi wetu" wanaoweza kupambanua mambo lakini bado wanatekwa katika uwigo wa uandishi usiotaka kutoa taarifa bali kutoa utashi binafsi. Tatizo nilionalo hapa hasa kwa wasomi wetu ni vitu viwili hasusani kwa wale amabo wapo ughaibuni au bado wanaendelea kuishi ughaibuni.

(1) Mazoea ya "Cash-Economy"
(2) Mitazamo iliyopitwa na wakati, "Outdated views"

Nikurudi katika kipengele cha kwanza cha hapo juu, (cash economy mentality) haswa kwa hawa ndugu zangu wasomi waliopo majuu wanaoshangaa mtu kuchukuwa mkopo na kununua nyumba kuna vitu viwili ambavyo ni obvious......

(a) Wanaishi nyumba za kupanga ughaibuni na wamezoe kununua magari mitumba🙂 kama utanunua gari jipya ughaibuni na hata Nyumbani siku hizi na una ajira inayoeleweka unapata MKOPO kama unakopesheka!

(b) Hali ilivyo nyumbani na kama ilivyo sehemu nyingine yeyote na hasa sisi tuliosomea masuala ya Mabenki na tumekwisha fanaya kazi hizo nyumbani na ughaibuni, Biashara kubwa ya BENKI ni Kukopesha! Na katika nchi yeyote iliyoendelea ukitaka kumjua JUHA au uonekane JUHA fikiria fikiria na fanya mambo kama upo kwenye "cash economy" watu wanakopa kununua magari, wanakopa kusoma, wanakopa kusomesha watoto, wanakopa kufungua makampuni na wanakopa kununua nyumba.

Kama HOJA hapa ni KIONGOZI wa nchi KUKOPA na KUNUNUA Nyumba, VIONGOZI wafuatao WALIKOPA na WALINUNUA NYUMBA wakiwa Madarakani:

Tony & Cherrie Blair (Hyde Park)
Bill & Hilary Clinton (New York)
Goran Person (Sweden)
John Major (Vauxhall Bridge, London-Uingereza)
Margreth Thatcher (Chester Square-London-Uingereza)
James Callaghan (Kennington-London,Uingereza)
Harold Wilson (Ashley Garden & Isle of Scilly)
Edward Heath (Salisbury-Uingereza)
Harold Macmillan (Birch Grove Estate,West Sussex)

Tatizo LIKOWAPI?

Tena nafikiri tukimwona KIONGOZI wa KIAFRIKA amekopa kununua nyumba hata kusomesha watoto wake au kulimia INABIDI TUMPONGEZE kwani anaweza kupiga simu kwa GAVANA NA WA BENKI na Kumwamuru Waziri wa fedha ampatie KIASI chochote bila maswali na kuondoka madarakani hana deni🙂

Nikirejea kwenye kukopa na kuanzisha shamba, mtu aliyekopa namni hii ni "MKULIMA" na wakulima wetu wote wangekuwa wanakwenda kwa mwendo huo tungekuwa tumeacha kilimo cha jembe la mkono🙂

Je Kunanzisha Kampuni mtu akiwa madarakani ni dhambi? Jibu ni HAPANA waulize TUME ya MAADILI , HAIKATAZWI, ilimradi kampuni yako haitegemei kupata "favours" zinazotokana na kazi au wadhifa "wako" wewe uliyeanzisha KAMPUNI hiyo.

Zaidi ya Hapo Kampuni ikiwa "LIMITED" ina "LEGAL PERSONALITY" inayojitegemea KAKOTI UPO? na hivyo inatenganishwa kisheria na mmiliki! na kwa KITAALUM, Kumiliki KAMPUNI ni KUMILIKI "HISA" JE WANGAPI LEO hii WANAHISA kwenye Makampuni? Tukianza na yale yetu kama Kiwanda cha Bia, Saruji, Oksijeni, Swissport, Sigara, UMOJA TRUST, na zinginezo? JE hawa WOTE waandikwe MAGAZETINI? Mbona huko ughaibuni haya hayaonekani kama yana mgongano wa maadili?


Nikipitia suala la Kuanzishwa KAMPUNI ya ANBEN LTD mwaka 1999. kuna vitu viwili hapa "Wasomi" inabidi kupambanua:
-Mwaka 2000 ulikuwa "Uchaguzi Mkuu" kama ilivyo kawaida yetu waafrika ukienda kwa Chifu au Ukikutana na "Chifu au Mtemi" huwa kanapelekwa KAKIBUYU ka pombe na ka-kuku" Profesa Mbele upo? Tanzania ni nchi ya Kidemokrasia mkataba wa kukaa IKULU kwa DHAMANA ya wapiga KURA ni miaka Mitano, na ikiisha watanmzania Tumekuwa na jadi ya kuwapa viongozi wetu zawadi kama ilivyokuwa tangu enzi za "Uchifu na Utemi" na kama ilivyo Chifu au Mtemi huwa hashitakiwi wala kudharirishwa hadharani. ndivyo hata taratibu ztu za KITANZANIA zilivyo, hivyo basi, ili kuepuka mambo kama KUKOPA na kushindwa kurejesha mkopo au hata kmapuni ikashindwa kutimiza masharti ya msingi, Busara na kwa Rais au Rais Mstaafu kuanzisha "LEGAL PERSONALITY" Limited Comapany ambayo INAWAJIOBIKA KISHERIA hii ni "COMMON SENSE, LOGICAL REASONABLE ACTION" kwa mtu yeyote anayeheshimu, UWAZI, na MISINGI ya SHERIA za DOLA.

Kampuni inaweza kuitwa Mahakamani lakini Rais au Rais Mstaafu ana "IMMUNITY" sasa KELELE sijuwi zinatoka wapi? au kitivo cha fikra kipo LIKIZO🙂?

Kwa kuhitimisha, ni muhimu tukahama kutoka kwenye cash economy mentality na kuingia ndani ya ULIMWENGU wa sasa, ndiyo Maana wenzetu Wahindi na Wayahudi na Wazungu wanapinga hatua kwenda mbele kwa kuwa wanatumia MASHIRIKA NA JUMUIYA ZA FEDHA zilizopo kufanya mambo ya KIMAENDELEO wakati sisi tunaimba oooooOh hatuna mitaji wakati mitaji imelala BENKI na ianawsubiri muweze KUKOPESHEKA, USINGOJE KESHo Aaanza LEO! Na wewe Utaweza Kununua Shamba na Kumiliki Ghorofa na hata Viwanda pia na kuendesha gari jipya na Kusomesha watoto hadi Chuo Kikuu kwa Mkopo!🙂

Siku njema!

Aziz
 
JK: Why I won`t do business from Ikulu


THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

PRESIDENT Jakaya Mrisho Kikwete yesterday made a categorical declaration that he is not interested in pursuing personal business dealings while occupying the highest public office in the land, in contrast to his predecessor Benjamin William Mkapa.

Answering a series of questions from local media editors after addressing the nation from State House in Dar es Salaam, the president said he has no plans to start his own private company with the first lady at Ikulu, like Mr Mkapa and his wife Anna did.

Instead, Mr Kikwete said after retirement he would be content with being just a simple farmer.

Asked about his predecessor's reported controversial 'entrepreneurship' pursuits while at State House, the president said his administration was prepared to let go the matter of Mr and Mrs Mkapa starting and operating a private business company, ANBEM Limited, from State House.

However, President Kikwete maintained that the government of the day would not hesitate to take action against any proven allegations of serious wrongdoing in the matter.

Delving further into the subject, Mr Kikwete said he personally believed it was not prudent for a middle-aged person to choose to make a debut into the world of private sector enterprise.

''There is a British friend of mine who once told me that you can't start engaging in business after reaching the age of 40,'' he said in response to a question from one local Kiswahili tabloid journalist.

Mr Mkapa was pushing 61 years old when he registered ANBEM Limited with Mrs Mkapa in 1999, with the official registration documents describing the then State House couple as 'entrepreneurs' and sole directors of the limited liability company.

Referring to a series of exclusive reports published by THISDAY in recent weeks on ANBEM Ltd and related business dealings, the president asserted that there was no need to pursue further investigations, noting that the hefty loans the company reportedly received from two local banks were repaid in good time.

He also tried to discourage such investigations into the personal affairs of retired presidents such as Mkapa and Ali Hassan Mwinyi before him.

''Sometimes that is why (political) leaders are tempted to change national constitutions to prolong their stay in power, for fear of being so investigated once they retire from office,'' he remarked.

The ANBEM Limited reports published by THISDAY have drawn very mixed feelings and ignited much heated debate amongst political observers, commentators and even actors, over the ethical considerations of Mr and Mrs Mkapa's actions while still at State House.

While some have argued that the couple did not break any law in registering their own private company while at Ikulu, others contend that the move - being mainly geared at ensuring personal gain - could well be interpreted as an abuse of office.

For example, it has been widely asserted that the reality of Mr Mkapa, as sitting president, having personal business interests or participating in personal business activities outside his official portfolio is likely to have in some part interfered with the exercise of objective and independent judgement, on behalf of Tanzanians as a whole, while on the job.

One seasoned lawyer and politician has gone so far as to point out various issues of serious conflict of interest and undue influence to consider in trying to balance such presidential and personal business affairs in a manner not likely to raise public questions and generate controversy.

''Tanzanian laws may be silent on the issue of the president doing business while in office�but is there any bank manager in the country who will say no to the president when he applies for a loan?'' he queried.

ANBEM Ltd was granted hefty loans of $500,000 (approx. 620m/-) and 250m/- from the National Bank of Commerce Limited and CRDB Bank in 2002.

Although it was eventually very quickly repaid, the NBC Ltd loan to ANBEM Limited was granted at a time of heated national debate over the privatization process surrounding the once state-owned bank, which the government formally sold off to South Africa's ABSA Group for a reported total price of just 15bn/- for 70 per cent majority shares in April 2000.

This was despite much opposition from a good number of legislators representing both the ruling CCM and opposition parties, all of whom were quite amazed by the cheap price quoted in the divestiture deal.

Privatization of the giant bank was also fiercely opposed by the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, until his death in 1999. Mr Mkapa's two tenures as president covered the period 1995-2005.

Outlining major priorities for his incoming government in a historic state-of-the-union speech on assuming the presidency on December 30, 2005, President Kikwete underlined the increasing need to root out corruption and unethical conduct by public officials before it all got out of hand.

''We must tighten mechanisms in place to ensure public officials do not use their offices for personal gain and self-enrichment,'' he said, adding for good measure: ''I am not against people getting rich. Indeed, I want everyone to have a better life. What I am against, is people using public offices for self-enrichment.''
 
Kuna haja ya kuwandikia BBC Panorama wachunguze na Rada za Tanzania.

Saudi prince 'received arms cash'

*Arms deals with the Saudis have been worth billions to the UK



BBC investigation
A Saudi prince who negotiated a £40bn arms deal between Britain and Saudi Arabia received secret payments for over a decade, a BBC probe has found.
The UK's biggest arms dealer, BAE Systems, paid hundreds of millions of pounds to the ex-Saudi ambassador to the US, Prince Bandar bin Sultan.

The payments were made with the full knowledge of the Ministry of Defence.

Prince Bandar would not comment on the investigation and BAE systems said they acted lawfully at all times.

The MoD said information about the Al Yamamah deal was confidential.

Up to £120m a year was sent by BAE from the UK into two Saudi embassy accounts in Washington.

There wasn't a distinction between the accounts of the embassy or official government accounts

The BBC's Panorama programme has established that these accounts were actually a conduit to Prince Banda for his role in the 1985 deal to sell more than 100 warplanes to Saudi Arabia.

The purpose of one of the accounts was to pay the expenses of the prince's private Airbus.

David Caruso, an investigator who worked for the American bank where the accounts were held, said Prince Bandar had been taking money for his own personal use out of accounts that seemed to belong to his government.

He said: "There wasn't a distinction between the accounts of the embassy, or official government accounts as we would call them, and the accounts of the royal family."

Mr Caruso said he understood this had been going on for "years and years".

"Hundreds of thousands and millions of dollars were involved," he added.

Investigation stopped

According to Panorama's sources, the payments were written into the arms deal contract in secret annexes, described as "support services".

They were authorised on a quarterly basis by the MoD.


Prince Bandar was Saudi ambassador to the US for 20 years

The payments were discovered during a Serious Fraud Office (SFO) investigation.

The SFO inquiry into the Al Yamamah deal was stopped in December 2006 by attorney general Lord Goldsmith.

Prime Minister Tony Blair said at the time it had been dropped because of national security concerns.

Prince Bandar, who is the son of the Saudi defence minister, served for 20 years as ambassador and is now head of the country's national security council.

Jane Corbin, from Panorama, explained that the payments were Saudi public money, channelled through BAE and the MoD, back to the Prince.

The SFO were trying to establish whether they were illegal when the investigation was stopped, she added.

And she said she believed the payments would thrust the issue back into the public domain and raise a number of questions.

Liberal Democrat Treasury spokesman Vince Cable said that if ministers in either the present or previous governments were involved there should be a "major parliamentary inquiry".

"It seems to me very clear that this issue has got to be re-opened," Mr Cable told BBC Radio 4's The World Tonight.

"It is one thing for a company to have engaged in alleged corruption overseas. It is another thing if British government ministers have approved it."

Panorama will be broadcast on Monday 11 June 2007 2030 BST
 
http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/6/7/habari1.php

Kikwete amlinda na ‘amshangaa' Mkapa

na Absalom Kibanda

RAIS Jakaya Kikwete amewataka waandishi wa habari kuachana na kile alichokielezea kuwa ni utaratibu wa kuwachunguza viongozi wastaafu hususan katika masuala madogo.

Kikwete, aliyekuwa akizungumza na wahariri na wakuu wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam jana, alitoa kauli hiyo wakati alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu shutuma zinazoelekezwa kwa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, juu ya uamuzi wake wa kusajili kampuni akiwa Ikulu na kuomba mkopo benki akijitambulisha kuwa mjasiriamali.

Akizungumza kwa tahadhari kubwa, taratibu na akiwa ametulia, Rais Kikwete alisema: "Sina hakika na hilo (kama Mkapa alifanya biashara Ikulu)…kwa maoni yangu, nadhani huu utaratibu wa kuwachunguza viongozi wastaafu katika mambo kama haya si mzuri sana."

Rais Kikwete alirejea msimamo wake alioutoa siku chache tu baada ya kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho kwa kusema, anadhani kuwa halitakuwa jambo jema kwake akiwa madarakani hivi sasa, kuanza kuwachunguza viongozi wakuu wastaafu kwa sababu tu ya mambo madogo yanayoandikwa katika magazeti.

Mbali ya hilo, akijigeukia yeye, kwa namna iliyoonyesha kutoafiki kuanza kufanya biashara katika umri mkubwa, Rais Kikwete alisema anaamini akianza kufanya biashara sasa, atakwama.

Bila kutaja jina la mtu, Kikwete (57) alisema rafiki yake mmoja Mwingereza alipata kumshauri kutoingia kwenye biashara akiwa na umri wa zaidi ya miaka 40, kwani atashindwa, ushauri ambao hadi hivi sasa umemjengea imani ya kuamini kuwa yeye hawezi kufanikiwa katika biashara.

Badala yake, Rais Kikwete alisema kwa mtazamo wake, anaona anaweza akafanikiwa iwapo atakuwa ama mkulima wa mazao kama mananasi au mfugaji wa ng'ombe.

Hata hivyo, alisema kwa kuwa yeye si mtu wa kuogopa, iwapo litatokea jambo kubwa ambalo litapaswa kufanywa uchunguzi dhidi ya kiongozi yeyote mstaafu, hatasita kufanya hivyo.

"Likitokea jambo kubwa tutalifanyia uchunguzi, kwani hatuogopi mtu, ingawa nadhani tukianza kufanya uchunguzi kwa kuwa tu mtu ameandikwa magazetini, hilo mimi halinifurahishi," alisema Rais Kikwete.

Akizungumzia tatizo la wanafunzi 29 Watanzania waliokwama Ukraine baada ya kushindwa kulipia gharama za masomo, Rais Kikwete alisema serikali haiwezi kufanya lolote kuwagharamia kwani walikwenda huko kwa utashi wao.

Aliwataka Watanzania kutambua kuwa, gharama za kumsomesha mwanafunzi mmoja nje ya nchi ni kubwa sana kulinganisha na kumsomesha nyumbani na hivyo iwapo watashindwa kumudu gharama hizo, ni vyema wakazingatia ushauri wa serikali wa kurejea nyumbani na kutafuta vyuo vya hapa.

Mbali ya hayo, mazungumzo kati ya rais na wahariri wakuu ya jana yalikuwa yakilenga mada kuu mbili; ya kwanza ikiwa ni mkakati wa serikali kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa Ukimwi kwa kuanzisha kampeni ya kitaifa ya upimaji wa virusi kwa hiari na la pili likiwa ni lile la kuongezeka kwa tatizo la utoro na ujauzito miongoni mwa wanafunzi wa kike katika shule za msingi.

Katika mazungumzo yake hayo, Kikwete alisema kampeni hiyo ya kitaifa ya kupima kwa hiari iliyokuwa ifanyike mwezi huu sasa imeahirishwa hadi Julai 14 mwaka huu.

Aliwataka viongozi wakuu wa serikali, wanahabari, na wananchi kwa ujumla kujitokeza kupima ili kupunguza na ikibidi kumaliza kabisa maambukizi mapya ya ugonjwa huo usio na tiba wala chanjo.

Alisema wakati wastani wa maambukizi ya ugonjwa huo kitaifa ni asilimia saba hivi sasa, lengo ni kuhakikisha kiwango hicho kinashuka ifikapo mwakani hadi kufikia asilimia 6.5.

Kuhusu madai ya baadhi ya viongozi wa dini kusema ugonjwa huo unaweza kutibika kwa maombi, Kikwete alisema iwapo hilo linawezekana, basi ni jambo la heri na faraja kubwa, ingawa wataalamu wa afya wamekuwa wakipingana nalo.
 
Aziz,

Mkapa hakukopa kununua nyumba; ingekuwa ni hivyo hiyo hakuna mtu angelalamika, kwani hata Nyerere ile nyumba ya msasani alikopa pesa THB. Matatizo ya Mkapa kimaadili kama presiednt ni mengi sana, mojawapo hapa ni kuwa wakati akiwa Rais wa Tanzania, kazi ambayo ni ajira ya saa 24 kila siku kwa siku 7 kwa wiki, alikuwa vile vile ni mkurugenzi wa kampuni ya binafsi ya ANBEN; kwa hiyo alikuwa akitumia sehemu tu ya muda wake kama president wa Tanzania na sehemu nyingine ya muda wake kama Mkurugenzi wa ANBEN. Hata hivyo alikuwa akipokea masilahi kamili ya president huku akijua kuwa hakufanya kazi hiyo kwa muda utakiwao. Kupokea malipo kwa kazi ambayo hukufanya ni wizi uliowahi kuongelewa siku nyingi sana na Nyerere.
 
Aziz,

Mkapa hakukopa kununua nyumba; ingekuwa ni hivyo hiyo hakuna mtu angelalamika, kwani hata Nyerere ile nyumba ya msasani alikopa pesa THB. Matatizo ya Mkapa kimaadili kama presiednt ni mengi sana, mojawapo hapa ni kuwa wakati akiwa Rais wa Tanzania, kazi ambayo ni ajira ya saa 24 kila siku kwa siku 7 kwa wiki, alikuwa vile vile ni mkurugenzi wa kampuni ya binafsi ya ANBEN; kwa hiyo alikuwa akitumia sehemu tu ya muda wake kama president wa Tanzania na sehemu nyingine ya muda wake kama Mkurugenzi wa ANBEN. Hata hivyo alikuwa akipokea masilahi kamili ya president huku akijua kuwa hakufanya kazi hiyo kwa muda utakiwao. Kupokea malipo kwa kazi ambayo hukufanya ni wizi uliowahi kuongelewa siku nyingi sana na Nyerere.

Duh! Mimi sigombei tena urais kama ndiyo hivyo ... itabidi iongezwe sifa ya kuwa rais ni lazima asiwe na mke/mume (na familia in gneneral) kwa vile kuna muda ataupoteza kuwapa huduma mbalimbali.
 
Duh! Mimi sigombei tena urais kama ndiyo hivyo ... itabidi iongezwe sifa ya kuwa rais ni lazima asiwe na mke/mume (na familia in gneneral) kwa vile kuna muda ataupoteza kuwapa huduma mbalimbali.


Naona kama wewe unataka kupotosha kama siyo utani tu. Kutunza familia yake ni sehemu ya marupurupu ya kazi zote hapa duniani, isipokuwa labda utawa tu. Kazi ya rais nayo inapata marupurupu hayo ya kutunza familia. Kinachoongelewa hapa ni kwa Rais kuwa mkurugenzi wa kampuni binafsi ya biashara.
 
Duh! Mimi sigombei tena urais kama ndiyo hivyo ... itabidi iongezwe sifa ya kuwa rais ni lazima asiwe na mke/mume (na familia in gneneral) kwa vile kuna muda ataupoteza kuwapa huduma mbalimbali.

Inachekesha!!!! kwikwikwiwkwiiiiiii!!!!!!!!!!

Mbona akina GW Bushi wana makampuni lakini bado ni marais wa nchi? Rais kuwa na mali si jambo baya provided mali hiyo haikupatikana kupitia influence yake kama rais wa nchi. Kuwa rais miaka kumi na kuendelea kuwa masiskini baadaye ni ujinga. Politics is not only about power it is also about monies!!!
 
Mr.0:

(1) Bush hana makampuni kama unavyodai, ameinvest kwa kutumia trusts ambazo yeye hana mamlaka nazo. Biashara yake ilikuwa ni ile timu ya baseball aliyouza baada ya kuwa gavana wa Texas. Wanasiasa wote wa federation ya marekani (siyo wa state na counties) hufanya hivyo wawapo madarakani, hawawezi kufanya kazi ya nchi halafu wakaendesha biashara zao kabisa aisee.

(2) Huwezi kuwa rais wa Tanzania halafu ukafa maskini kwa sababu nyingi tu. Lililofanyika hapa ni ulafi usiokuwa na sababu yoyote. Kwanza pension ya rais na marupurupu baada ya kustaafu ni makubwa sana. Halafu rais anayestaafu na sifa nzuri hutengeneza pesa nyingi sana kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na speaking fees, kama alizopata Nyerere, Clinton, Mandela, na vitabu vinavyoweza kutokana na hotuba zake.

Marais wanaotumia muda wa kazi kufanya bishara na kujilimbikizia mali ambazo baadaye wanazionea aibu huwa hawatendei haki raia wao kwa vile muda wa kutumia kutatua matatizo ya nchi wao wanautumia kufanya biashara zao binafsi.

Ikulu hakuna biashara kabisa aisee.

(3) kwa katiba ya Tanzania, rais ana influence kwa kila sehemu kwa hiyo sijui ben alifanya biashra gani ambayo influence ya rais haikutumika.
 
Back
Top Bottom