Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

hii hoja ni nzito na nitaijibu kwa umakini baadae kidogo, nasikiliza taarabu sasa hivi !!
 
Huyu mkapa nadhani tumfanye kama Chiluba alivyofanywa kwa kufunguliwa mashtaka nje ya nchi. Pale Tanzania chini ya CCM ataendelea kuyeya tu
 
Tumeona ya ANBEN, hatutaki kusikia ya SAKI

Na Mpayukaji Msemahovyo

Mkapa umefanya biashara Ikulu!

“SIAMINI kama mstaafu wetu, Benjamin Mkapa, tuliyemsifia kuwa ni Mr Clean, anaweza kutufanyia hivyo, Watanzania tuwe imara na tuamke na kumbana atuambie kulikoni.” Anaingia Mkurupukaji, anaimba hata hasalimii.

Mgosi Machungu hamkopeshi. “Mgosi hata hutiamkii umeona kuimba ndiyo dii?”

Kama aliyekuwa usingizini anatupa salamaleko na kuendelea. “Mwenzenu siimbi bali naomboleza kugundua kuwa kumbe Kampuni ya ANBEN ni Anna na Ben! Yaani hapa tumemvua nguo mwalimu.

Mkapa, Mkapa, unafanya biashara ukiwa Ikulu! Kweli mbwa hafanani na bwana wake.”

Mgosi anazidi kushangaa. “Mgosi mbona hatikuelewi!”

Mpayukaji naingilia. “Mgosi tatizo lenu ni kujali sana mambo ya tunguli na kudharau uchunguzi.

Hujui kuwa Ben na mkewe kumbe walikuwa wakikopa pesa walipokuwa Ikulu kiasi cha kuanzisha Kampuni ya ANBEN?”

Mgosi hajibu bali kujishika tama na kutamka neno ambalo haliandikiki. Hayo tuyaache.

Mpemba hana hamu na salamu, anachomekea. “Mie nilijua Nkapa si Mr Clean pale nkewe alipokopa pesa na kununua lile jumba pale Barabara ya Morogoro Road na asinkataze,”. Mbwa mwitu anaingilia. “Morogoro Road, maana road ni barabara,”

Mpemba haukubali uchitaaahiro na ukihiyo anajitetea. “Nafahamu sana. Sema hasira nimeghafilika yakhe. Mie najua Nkapa alikuwa alala yule nchaga ndiye kanzindua.”


Mkurupukaji naye hana simile anadonoa mic. "Taarifa nilizo nazo ni kwamba Mkapa na mkewe walianzisha ANBEN pindi tu walipotia mguu Ikulu.

Alipokufa Mchonga wakaisajili na kuendelea kujichotea pesa kwenye mabenki. Hadi naongea wanadaiwa kitu kama bilioni. Walizifanyia nini, nani anajua? Hata hiyo Fursa sawa ilikuwa ni fursa sawa kati ya nani na nani maana ukiwauliza akina mama iliwasadiaje, sijui kama wanajibu.

Mzee Maneno hangoji habari iishe analamba mic. “Mie nilijua walipofichua Waingereza. Nakumbuka yule Mama Shoto alivyotua uwanja wa ndege amefura utadhani angemtimua Mkapa.”

Kabla ya kuendelea Mbwa mwitu anamkosoa. "Ni Clara Short siyo shoto."

Mzee Maneno anasema. "Shoti hiyo hiyo huoni alipowekwa ndani na kupewa lugha tamu akaondoka kwa furaha akatuachia shoti zetu! Kweli wanasiasa ni uchwara hata wawe Wazungu kumbe Nkapa alikuwa akitwambia kwa mafumbo alivokuwa akiwaambia wenzake uchwara, hatukumuelewa!"

Mgosi naye anakwanyua mic. “Mie naona Kikwete aache kuingilia usaama wa nchi hii, aache Mkapa asimame atieleze tiandastandi kwanini yeye na mkewe wamefanya hivyo? Bado tinahisi japo si moja kwa moja, ana mkono kwenye rada, Tanesco, NBC tena na kuanzisha kampuni wakiwa madaakani.

Pia atiambie kwanini aliondoka bila kutaja mali zake na lile hekau la pale Ushoto alijenga kwa bei gani? Mimi naamini kuna mengi kuliko haya tinayoambiwa.”

Makengeza anadakia. “Kikwete hamtetei Mkapa anajitetea mwenyewe. Maana ukiangaria ilipotoka EOTFL imeingia WAMAAAA. Usishangae leo kusikia ANBEN. kesho ukakuta kumbe kuna SAJA, tena zimeungana.

Hapa ni ulaji mtindo mmoja. Huoni wahusika wa Richmond walivyojikausha utadhani watu hawaoni ujambazi tunaofanyiwa.

Sasa kama rais anawatetea wezi kazi yake ni nini hapo Ikuru, sasa hili naro atatwambia nini tumuelewe?"

Mpayukaji nami siwezi kuondoka bila kumwaga cheche, nakula mic. “Kumbukeni Jakaya alisema tumuache mzee Mkapa akatanue. Huenda yeye aliona mizigo ya aibu na kashfa alizo nazo vinatosha lakini akasahau kuwa pesa iliyoibwa kwenye rada na miradi mingine ni yetu siyo yao.

Hapa ndipo bomu letu linaloitwa Katiba linapaswa kubadilishwa haraka kama anavyolalama Mzee Mtei."

Mzee Kidevu naye anatia timu. “Nyie hamjui. Hapa ni kata mti weka mti. Toa kibaka weak kibaka.” Anakohoa na kuendelea. “Kwanza wa kulaumu ni sisi. Asiyesikia la mkuu? Maana Mchonga pamoja na kutuletea kinyago chake cha mpapure alisema wanaokimbilia Ikulu inabidi tuwaulize wanakimbilia nini huko?.

Je, sisi tuliwauliza? au tulishabikia sura na mipasho. Inabidi tukome na kujilaumu huku tukijipanga upya kuwakabili kwa kila hali.”

Matai anachomekea. “Wewe unataka kuvuruga amani sasa.”

Mzee Kidevu hakopeshi. “Amani au ukondoo katikati ya ujambazi? Amani gani iwapo Ikulu inatumika kufanyia biashara? Hivi nyinyi Watanzania nani aliwaroga? Yaani nyinyi mmeridhika na Ikulu yetu kuwa pango la wezi na wachumia tumbo?”

Msomi naona amesukuti muda mrefu. Maana kila anayeongea anamtazama ili achonge. Anatia guu. “Kusema ukweli Mkapa ameamua kujivua nguo. Yeye aliona ni siri. Tunajua kuwa ANBEN ilisajiliwa mwaka 1999 baada ya kuona Mchonga amekufa. Acha hiyo kuna na nyingine ya Ikulu humo humo.

Yaani tumekuwa wa ovyo kuruhusu Ikulu yetu ifanyiwe umachinga na uchafu huu!” Anatuangalia na kubwia tangawizi yake na kuendelea. “Hapa inabidi wananchi tuache woga tumtake rais achague moja, kuongoza au kumtetea huyo mwenzake. Hapa lazima wapinzani waungane na wananchi mitaani kuendesha migomo na maandamano ili tuwabane hawa.

Nakumbuka Mrema alishtuka mwanzo akasema huyu si Mr. Clean, akaonyesha jinsi alivyopokea bonge la dhahabu watu hawakujali. Sasa uwezo tunao, sababu zipo za kumhoji Mkapa. Maana nakumbuka ubabe wake akitukana waandishi kuwa ni uchwara na wana wivu wa kike na uvivu wa kufikiri. Hivi ni tamaa gani kwa rais aliyeko madarakani kujiingiza kwenye umachinga Ikulu?

Nyerere alisema ogopa rais anayetawaliwa na kushauriwa na mkewe lakini hatukuelewa.”

Anakohoa na kujifuta jasho na kuendelea. “Mie nachukia wanafiki sawa na nguruwe. Heri hata ya Mobutu maana alijionyesha alivyokuwa jambazi badala ya mashetani wanaojionyesha kama malaika.

Nchi hii inahitaji rais aina ya Mwanawasa badala ya kulindana. Sasa lazima tutoe shinikizo kwa rais maana nchi hii si yake kwamba Mkapa lazima aseme mbele ya umma, mbele ya sheria ili liwe somo kwa wengine.

Rais wetu namheshimu asitake tumdhanie vibaya. Yeye atakuwa mtu wa kashfa za wengine hadi lini?

Nyumba zetu kachuna, Richmond usanii, Mkapa oh! Mara mzee Mkapa. Hapa hakuna cha mzee Mkapa angetaka iwe hivyo angeigiza mfano wa mtu aliyembeba hadi akafika hapo alipokuwa hapaotei wala kujiandalia.

Kikwete badala ya kulipwa mshahara na marupurupu yetu kwa kumkingia kifua lazima aweke msimamo wake kama ni kulinda mali zetu au kuwalinda wanaoiba mali zetu. Hapa ndipo wapinzani wana kete ya wazi.

Wangeanza kuwashawishi wafadhili wenye akili kama nchi za Japan na Scandinavia kuanza kutoa shinikizo wanaotafuna nyumba yetu, wangeshughulikiwa.

Kumbe wakati Nyerere alisema tuwaogope kama ukoma alishajua kuwa wako wanakuja na sasa tunao!”

“Msomi sikubaliani nawe. Hapa ni suala la Watanzania kuingia mitaani kwa maandamano na migomo ili kieleweke kama kazi ya Jakaya ni kuwalinda wahalifu au kupambana nao.

Hawezi kukaa kwenye Ikulu ya wananchi na akaendelea kuwalinda wabaya wao.

Naye kama amechoka si atimke tu maana hatuoni hata sera wala la maana zaidi ya kashfa. Tumechoka sasa na isitoshe mtu mzima hasutwi.” Anachomekea Mchunguliaji aliyekuwa amenyamaza kitambo.

Msomi anaendelea. “Jakaya inabidi ajikumbushe Mkapa alivyokuwa na ubabe, sasa viko wapi anaishi kwa kujificha maana madhambi yake yanamfuata. Isitoshe miaka mitano au kumi si mbali, kesho anaweza kujikuta walipo kina Chiluba. Pia afahamu kuwa kutokuwa na miiko ya uongozi ni hatari kwa rais, maana watu wengi watajifanyia wanavyotaka lakini atakayeulizwa baadaye ni yeye.

Jamani mwalimu mbona ametuachia hazina ambayo tunaichezea kama mataahira!”

Jana nilikunywa sana. Wakati maongezi ndiyo yananoga, si tumbo la…. lilinishika. Kilichofuatia unafahamu! Tuonane wiki ijayo.


Makala -Tumeona ya ANBEN, hatutaki kusikia ya SAKI
 
Mkapa kavunja mwiko, Ikulu si patakatifu tena

Kristofa Kidanka

ILE kashfa ya ununuzi wa rada ilipokuwa imevuma wakati Rais Benjamin Mkapa akiwa madarakani, watu hawakuonekana kuhoji sana jinsi rais wao alivyokuwa akitumia muda wake wa kuwa ikulu.

Pengine hawakuwa na taarifa za kutosha au waliona kuwa ilikuwa mapema mno.

Tulimwona Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Clare Short, akija Tanzania akiwa amenuna; baada ya kuwa amehoji sana ‘deal’ hiyo ya rada na kuipinga kwa nguvu zake zote.

Kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam (sasa ‘wa Julius Nyerere’) alikwenda Ikulu.

Kina sisi tulibaki nje tukisubiri atakachosema atakapotoka huko kulikokuwa na kile kilichoitwa ‘mazungumzo ya faragha’ na viongozi wetu.

Kwa mshangao wetu, aliingia amenuna lakini akatoka anacheka. Alisema suala la rada wamelizungumza kwa kirefu na ‘ameelewa’. Akapanda ndege akaenda zake.

Huyu ni Waziri wa Uingereza aliyekuwa akipinga mpango wa Tanzania kununua rada kwa bei kubwa.

Binafsi niliwaza: “Viongozi wanazungumza lugha moja. Na kinachoweza kuzungumzwa kwenye magazeti si kile kinachoweza kuzungumzwa faraghani.

Kwa suala nyeti na la kiusalama kama la rada linaweza kuwa na maelezo ya kuridhisha zaidi faraghani, ndiyo maana wazee wameelewana. Sisi watu wa magazeti tusiwe na nongwa.”

Hata hivyo, majuzi tumepata habari za kushitusha: Kwamba ununuzi ule wa rada ulikuwa umegubikwa na lindi la rushwa. Uchunguzi umeonyesha kuwa wakubwa walikuwa wamechukua ‘cha juu’ kuuziwa rada kwa bei kubwa kupita kiasi.

Uingereza imefanya uchunguzi wake na kugundua ulaji wa kutisha. Nchi yetu imekuwa ikitafunwa na wenye meno.

Kutokana na hili, wapo waliomtaka aliyekuwa rais wakati huo ajibu maswali yetu kuhusu kashfa hii. Walikuwa na haki ya kufanya hivyo.

Mrithi wake, Rais Jakaya Kikwete akaja juu: “Hivi jamani kweli mnamtaka mzee Mkapa atoke huko aliko aje ajieleze? Ajieleze nini? Hebu mwacheni mzee wa watu apumzike!” aligomba Rais Kikwete.

Kwangu mimi sikuona mantiki yake. Na mtoa hoja hakuieleza. Alitumia zaidi hisia: Kwamba ‘mzee Mkapa aachwe apumzike’.

Nilitarajia Rais Kikwete aseme kwa nini Rais wa Awamu ya Tatu asijieleze kwetu jinsi alivyotumia dhamana tuliyompa? Alitakiwa aseme kwa nini Benjamin Mkapa asitoe maelezo juu ya watu walio chini yake kupokea hongo na kuhatarisha taifa?

Na alitakiwa aseme kwa nini mzee Mkapa asihusishwe na kashfa ya rada. Kama haya yangekuwa si lazima kutoka kwa Mkapa, angeyatoa yeye mrithi wake aliyemkingia kifua. Hakuna lililofanyika. Tukanyamaza.

Mengi yalitufanya tunyamaze. Mojawapo ni kuwa Rais Kikwete alisema Uingereza bado wanachunguza kwa kina suala hilo na kwamba tutadai ‘chenji’ yetu iliyozidi katika ununuzi ule ambao umedaiwa kuwa ulikuwa na bei kubwa kupita kiwango.

Lakini kwa hili la watumishi wetu serikalini kupokea hongo tumenyamaza kwa kuwa sisi ni Watanzania. Tunaodumisha ‘amani na utulivu’.

Ni lazima tunyamaze ili tuwe na amani. Amani kama ya makaburini ambako, tofauti na sokoni, kuna ukimya mkuu na utulivu. Nani apige kelele?

Leo kumezuka suala jingine zito sana. Kwamba akiwa Ikulu, Rais wa Tanzania alisajili kampuni ya biashara na kuendelea kufanya biashara huku akikopa katika benki kadhaa hapa nchini.

Tangu mwaka 1999, Benjamin Mkapa na mkewe Anna, walikuwa wakurugenzi wa ANBEM Limited. Lakini hawakuwahi kujitokeza hadharani kama wafanyabiashara, ila tulimjua mzee Mkapa kama rais na mkewe Anna kama mwanaharakati wa ukombozi wa wanawake akiongoza Taasisi ya Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).

Tunataka maelezo kutoka kwa mzee Mkapa. Na katika hili, tunamuomba Rais Kikwete akae pembeni. Asimkingie kifua. Tunataka atueleze japo kwa kifupi sana kwa nini alitumia muda aliokuwa ikulu kufanya biashara?
Tunataka aseme kwa nini ANBEM Limited iliyoanzishwa ikulu na kuendeshwa na rais aliyeko madarakani huku ikiwa kampuni binafsi isifilisiwe na kurudishwa kwa wananchi.

Habari kwamba tangu mwaka 1999 watu wawili walikuwa wakiendesha kampuni binafsi ya biashara kutoka ikulu ya Tanzania si habari ndogo.

Pamoja na kuwa sisi tunaweza kuwa ‘wavivu wa kufikiri’, ‘malofa’ na ‘waandishi uchwara’, lakini tunahitaji majibu yenye hoja nzito kutoka kwa Benjamin Mkapa.

Habari zinasema Juni 21, 1999, mwaka aliofariki Mwalimu Julius Nyerere, Benjamin Mkapa na mkewe Anna walisajili kampuni binafsi iitwayo ANBEM Limited.

Kampuni hiyo ilipata hati ya usajili yenye namba 36547. Ilipofika mwaka 2005, wakati Mkapa alipokuwa anastaafu urais, kampuni yake ilikuwa na madeni yanayofikia kiasi cha shilingi milioni 750, zilizokopwa kutoka benki mbalimbali.

Swali ni kwamba, Rais wa Tanzania aliwezaje kuwa mfanyabiashara mkubwa kiasi hicho bila kuwapo kwa mgongano wa masilahi dhidi ya washindani wake kibiashara? Mikopo hii kutoka benki mbalimbali hapa nchini ilipatikana kati ya Julai na Desemba 2002 wakati Mkapa alipokuwa bado Rais wa Tanzania, je, iliwezekana kumtenganisha Benjamin Mkapa na madaraka ya urais walipokwenda kuomba mkopo?

Rais Mkapa alitangaza mali zake alipokuwa akiingia madarakani, lakini hakufanya hivyo alipokuwa akiondoka, licha ya watu wengi kumtaka atangaze ili tujue kama ametumia ikulu kujineemesha.

Anapokuwa madarakani, rais ni kiongozi wa wote na ndiyo maana anaangaliwa kwa kila kitu ili awe mtu huru asiyehangaika.

Anapaswa kuwa mwamuzi kati ya watu wanaogongana wakati wakitafuta riziki. Hapaswi kuwa naye mtafutaji anayegongana na watafutaji wenzake huko.

Ndiyo maana Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kutuasa kuwa ikulu ni mahali patakatifu na si pa kufanya biashara.

Je, haitakuwa sahihi kutamka kwamba, Ben alivunja mwiko huo na kupafanya ikulu mahali pa kufanyia biashara?

Mwalimu alishangaa kwamba katika miaka yake 23 ya kukaa ikulu hakuona biashara yoyote lakini watu walionekana kuwa tayari kutumia fedha kuitafuta ikulu.

Hapa alimaanisha kuwa, ni dhambi kwa mtu tuliyemweka ikulu kufanya biashara kwa kuwa si mahali pake.

Nakumbuka wakati wa uongozi wake, Rais Mkapa alikwenda nchini Malawi alikokutana na kiongozi wa huko, Bakili Muluzi, kati ya mengi aliyoyasema pia alisema kuwa kuna dhana miongoni mwa Waafrika kuwa kiongozi bora anastaafu akiwa maskini.

Alipingana na dhana hii na kusema kuwa si dhana sahihi. Nami nilikubaliana naye wakati ule na ninakubaliana naye sasa, lakini sikubaliani na dhana ya kiongozi kutumia muda wake wa ikulu kufanya biashara binafsi. Pengine nina mning’inio wa Azimio la Arusha.

Ni vigumu kumtenganisha mtu na cheo chake, hivyo Mkurugenzi wa ANBEM Limited anapoomba mkopo papo hapo akiwa Rais wa Tanzania, anakuwa juu ya waombaji wengine, na kwamba ikiwa fursa ni chache, basi mkopo utatolewa kwa ANBEM na si kampuni nyingine. Hii ni kibinadamu.

Viongozi wetu wamevunja Azimio la Arusha lililokuwa limeweka misingi ya kiutu katika uhusiano wa kijamii na maadili ya uongozi. Hili tunalijua. Je, ina maana kuwa tumeua kabisa maadili ya uongozi katika nchi hii?
Lakini pamoja na kwamba Azimio la Arusha halipo tena, nadhani bado tunahitaji rais atakayekuwa hana upande wakati tunapogombania mkate wa kila siku na si mtu anayenyang’anyana nasi uwanjani.

Kwa rais kukaa ikulu kabla ya kwisha kipindi cha kwanza akasajili kampuni ya biashara, na pia akaingia tena katika kinyang’anyiro cha urais; akaomba mkopo benki na kuendesha biashara yake kutoka ikulu, tunahitaji maelezo.

kidanka@hotmail.com

Makala -Mkapa kavunja mwiko, Ikulu si patakatifu tena
 
Kama kuna mtu anaweza kutupatia makala ya Denis Msaki katika gazeti la Mwananchi la leo Ukurasa wa sita, "Mkapa amedhihirisha kuwa yu mkweli na muwazi" ambayo imemtetea na kukejeli wanaohoji kuanzisha kwake kampuni. Pia makala ya jana katika Daily News ukurasa wa nne inayofanana kwa kila kitu na hii ya Msaki, tukiwekewa humu itasaidia maana hazipo katika mtandao
 
Tahariri Habari nyingine zaidi!
Mkapa aachwe astaafu kwa amani
Mhariri
HabariLeo; Wednesday,May 30, 2007 @00:02

KATIKA siku za hivi karibuni, tumeshuhudia baadhi ya magazeti yakiandika habari zinazodaiwa
kuwa za uchunguzi kuhusu mikopo ambayo ilitolewa na benki hapa nchini kwa kampuni inayohusishwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na mkewe Anna.

Kwa ufupi, taarifa hizo zinahusu mkopo ambao inasemekana Mkapa aliupata kutoka benki mbili za hapa nchini, na ambao ameshaurejesha. Mkapa, kama Mtanzania yeyote yule ana haki ya kuwekeza katika biashara na ana haki ya kupata mkopo. Isitoshe, ametuonyesha kwamba mtu anapokopa kwenye tasisi za fedha, lazima arejeshe.

Kinachotushangaza ni namna ambavyo habari hizo zimeandikwa, kwani kuna wakati hazizingatii maadili ya uandishi wa habari ambayo yanakemea mtindo wa kuweka maoni ya mwandishi katika taarifa ambayo sio maoni au uchambuzi.

Inatuwia vigumu kuamini kuwa taarifa hizo ni za uchunguzi wa kawaida kwani uchunguzi makini ungeliangalia namna benki zinavyotoa mikopo kwa wafanyabiashara kwa ujumla na sio mtu mmoja tu. Kwa hali hiyo tulitegemea kuwa magazeti hayo yangeanza mikopo iliyotolewa
na wafanyabiashara wengine, ambao baadhi yao bado wanadaiwa na taasisi za fedha.

Tunachoona sisi, na bila shaka Watanzania wengine, ni dalili ya wazi ya kumuandama Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu kwa sababu ambazo hazina msingi zaidi ya chuki.

Aidha wale wanaomwandama hawaoni mbali, kwao wanachokiona ni Mkapa na sio ustakabali wa nchi hii.

Tanzania imeonyesha njia kwa nchi za Afrika kwa kuwa na mpangilio mzuri wa urithi wa kisiasa wa kidemokrasia ambao umeshuhudia viongozi wetu wakikabidhiana madaraka baada ya kumalizika kwa vipindi vyao vya kidemokrasia.

Mfumo wetu wa kisiasa umewezesha viongozi wetu wameheshimu vipindi vyao vya kuongoza nchi na kamwe hawajatafuta mbinu za kujiongezea muda ili waendelee kutawala ili kulinda maslahi yao binafsi kama ambavyo tumeshuhudia katika baadhi ya nchi nyingine za Kiafrika.

Tumeshuhudia baadhi ya marais waliostaafu katika nchi hizo wakisakamwa hadi kufikia hatua za kugawa nchi.

Kwa bahati nzuri kwa Tanzania, marais wetu wanakabidhiana madaraka na kila mmoja anajenga kwenye misingi iliyowekwa na mwenzake. Urithi huu umetuwezesha kujenga umoja nchini mwetu.

Watanzania wana safari ndefu ya kujiletea maendeleo na wasingependa kurudishwa nyuma kwa namna yoyote ile.

Mkapa amefanya mengi kwa taifa hili na tumpe nafasi ya kustaafu na kupumzika bila bughudha yoyote.

Mhariri wa Habari Leo, leo amerejea kauli ya JK "Mwacheni Mzee Mkapa Apumzike"! kufuatia kuandamwa kwa bosi wake wa zamani BWM kuhusu na matumizi ya madaraka ya Urais kufanya biashara zake binafsi.

Naona pressure imekuwa kubwa sana na hasa baada ya aliyekuwa Rais wa Zambia, Chiluba kushtakiwa mahakamani na kukutwa na hatia huko Uingereza!

Kama wameshatoa kweny gazeti lao bila shaka walishatuma onyo kwa gazeti la THISDAY. Tuone kama THISDAY watatishika au wataendelea kutupa habari za Ujasiriamali wa Mzee Mkapa akiwa Ikulu.

Mimi nadhani Chilubanization iendelee na ikiwezekana Mahakama (kupitia Mkono & Co,. kama mbia mwenzake) ndiyo imsafishe Mzee wetu BWM au yeye mwenyewe BWM akanushe.
 
nilipokuwa pwani ya Tanga miaka ile nakumbuka msemo mmoja ambao ni wa kweli hapa.. "akutukanaye hakuchagulii tusi"!! Hili ni tusi la nguoni!
 
Halisi,

Wanafiki siku zote hawakosekani Tanzania. Nimegundua kwamba waandishi wengi wa habari Tanzania huyaweka maneno mdomoni mwao kwa sababu ya Ulaji
...Utakuta mwandishi anaandika vitu ambavyo kavitunga yeye mwenyewe badala ya kumhoji Mkapa na kunukuu maneno ya Mkapa, msemaji wake ama wakili wake!..Na kibaya kuliko yote siku zote hawafanyi uchunguzi kabisa!... Wanafiki hua ni kati yetu sisi wenyewe!

News (habari) Tanzania ni mawazo ya mwandishi, uchaguzi na hukumu ni ya mwandishi kupamba upande anao penda yeye!...

Hivi hawa waandishi wanafahamu ni kiasi gani cha mali yao kimetumiwa vibaya na hawa viongozi? Hivi kweli wanafahamu kwa nini kila mwaka Benki yetu Kuu hupeteza mafedha kibao ya mikopo toka nje?... hata siku moja hawajiulizi unakuwaje hta benki yetu KUU inafikia kuungua moto!...

Kwa hiyo isikupe homa maanake hata Yuda aliyemsaliti Yesu alipata wafuasi wengi sana na leo hii dunia nzima inawapigia debe nje ya imani zao.
 
Ebu wenzangu someni maneno haya ya mwandishi:-

Aidha wale wanaomwandama hawaoni mbali, kwao wanachokiona ni Mkapa na sio ustakabali wa nchi hii.
Tanzania imeonyesha njia kwa nchi za Afrika kwa kuwa na mpangilio mzuri wa urithi wa kisiasa wa kidemokrasia ambao umeshuhudia viongozi wetu wakikabidhiana madaraka baada ya kumalizika kwa vipindi vyao vya kidemokrasia.

Ukiyasoma maandishi haya dhahiri kweli akutukanae hakuchagulii tusi...hasa pale nyani asipoweza kuliona K... lake!
 
Mwanakijiji,

Mhariri anadai wanaomwandama Mkapa hawaoni mbali, wanachoona ni Mkapa tu na sio mustakabali wa nchi.

Yaani huyu Mhariri anataka kutuambia Rais Mstaafu Mzee Mkapa ndiye anyeamua mustakabali wa nchi yetu kwa sasa! Yeye (Mhariri) ndiye haoni mbali maana ikiwa kila Rais anayeingia madarakani ataigeuza Ikulu kuwa ni duka la familia yake basi mustakabali wa nchi yetu utakuwa shakani.

Wakati umefika Chilubanization must take place!
 
jamani.. nitawajibu waandishi uchwara kama hawa!!! ambao hawaoni linginei isipokuwa mustakabali wa matumbo yao...
 
Wanatufata nafasi ya kuwa kwenye 'pay roll' ya mzee,kama wachezaji mpira wavyotatuta nafasi kwenye 'first eleven' ya kocha.
 
Kaka Mkandara kwa kweli nami hilo limenikera sana! We are together against huu umbu-mbu-mbu wa Mhariri wa Habari Leo, bila shaka hiyo kazi amepewa tu bila kuwa na sifa zinazostahili, labda ni Mwana CCM.

Nchi hii, kila kitu siasa tu! Hata mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yetu ni siasa! Siasa, siasa, siasa itatufikisha wapi? Nahofia itaua mustakabli wa nchi yetu.
 
Kaka Mkandara kwa kweli nami hilo limenikera sana! We are together against huu umbu-mbu-mbu wa Mhariri wa Habari Leo, bila shaka hiyo kazi amepewa tu bila kuwa na sifa zinazostahili, labda ni Mwana CCM.

Nchi hii, kila kitu siasa tu! Hata mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yetu ni siasa! Siasa, siasa, siasa itatufikisha wapi? Nahofia itaua mustakabli wa nchi yetu.



Pole Ibrah,
Mustakabari upi wewe unautaka?mbona siku nyingi tumeshapoteza mwelekeo nchi hii ina kwenda hea hea sasa.
Juzi nimesikia budget yetu ya ikulu imevuka kwa zaidi ya bilioni 950 na mwaka wa hesabu/pesa unaisha mwezi ujao,jaribu kufikiri kidogo.
Nyuma pale Prof.Lipumba aliposema 'safari za nnje sio lazima' tulimtazama mara mbili mbili sasa tunayaona.
 
Haya haya mwanangu... Mwanakijiji!..
Hakika chama kipya kianzishwe haraka!... watu wapo alisema Mwl. Nyerere!
 
nnarudi tena, nimekumbuka kuna mwana JF mmoja kipindi cha nyuma alisema yeye atajikomba kwa kulinda maslahi binafsi ndo ya huyo mwandishi, nnaamini alioyaandika sio yalio ndani ya fuadi yake. ila anaamini akiandika hivyo atakuwa kajikomba kwa wahusika na mambo yatakuwamazuri.

hapa ndipo tunapopoteza credibility ya wengi, mkJJ NNNAKUPONGEZA NA NNAKUOMBEA MUNGU USIMAME HAPO HAPO JAPOKUWA UTAKUWA UNANUKA SIFA MBAYA NYINGI TU MBAYA KWA WASIOPENDA KUAMBIWA NYEUPE NYEUPE.
 
Back
Top Bottom