Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Recta,
Mkuu unachoshindwa kuelewa ni kitu kimoja tu.. Kwamba kwa kutumia katiba hiyo hiyo mtu anaweza kukiuka sheria kwa kutumia sera za chama. Kwa mfano Hitler na ubaya wake wote ule alitumia katiba ya nchi yake kufanya yote aloyafanya akilindwa na sera za NAZIs..Mugabe kwa ushenzi wake anatumia katiba ya nchi yake akilindwa na sera za Chama..
Mkapa pia ameyafanya yote aloyafanya kwa kutumia Katiba lakini akilindwa na sera za chama chake CCM..
Azimio la Zanzibar ni moja ya sera za CCM ambazo zilimwezesha kiongozi kuanzisha mradi wake ama kuingia biashara..hakuna chama wala wananchi waliohusishwa na azimio hilo. hata hivyo wakati sera hii ikijengwa hakuna hata kifungu kimoja kinachomruhusu ama kumpa nguvu kingozi wa serikali kujiuzia mradi wa serikali ama kuweka sheria ya kuuza hizo mali za Umma kwa viongozi..Alichofanya Mkapa na sera na Ubinafsishaji ni kinyume cha miiko/ maadili ya Uongozi sawa na dalali kujiuzia yeye mwenyewe mali aliyopewa dhamana ya kuiuza sokoni...

Kwa hiyo tunapozungumzia swala la sheria na katiba ya nchi halihusu maamuzi ya sera au Maazimio ya chama CCM wala mipango endelevu/ bomoa ya kiongozi aliyeshika maradaka...Hata huyo Bush aliposhughulikia swala la magaidi na kufungua kwa jela ya Guatanamo Bay limezua utata kutokana na hatua zilizofuatia namna ya ku deal na hao magaidi..Ni makosa yanayomwangukia Bush kukubali baadhi ya torture zitumike lakini hakuna kifungu ndani ya katiba ya Marekani inayoruhusu mateso hayo..
Obama amekusudia kuifunga jela hiyo na Wamarekani wanaweza kabisa kumsimamisha Bush kwa makosa yaliyofanyika ambayo katumia cheo chake kuhalalisha mateso..Kosa la Mkapa halikuwa Ubinafsishaji kama navyoweza kusema kosa la Bush halikuwa kufungua gereza la Guatanamo Bay isipokuwa kosa la Mkapa ni kutumia vibaya madaraka ndani ya katiba kwa kukiuka miiko ya Uongozi bora kama Bush ambavyo amekiuka miiko ya Uongozi bora pale alipotumia torture kinyume cha Uongozi bora..
 
Mkapa should be the most wanted,issue zote zinazomshuhulisha bwana kikwete chazo chake ni Mkapa.tatizo kikwete amekuwa mgumu kutoa maamuzi.

mkuu, cahnzo chake si Mkapa, chanzo chake ni JK mwenyewe. Kwa miaka 10 alikuwa anajipanga kuuupata urais bila kuwa na malengo ya uadilifu na nidhamu ktk serikali yake.we angalia baraza la mawaziri lilivyo na matanuzi wanayofanya.
Alichotaka ni kuupata urais tu.Baada ya kuupata anashindwa kutumia mamlaka aliyonayo kikatiba hata kufanaya maamuzi ya msingi Yeye kama Yeye. Ikulu hatulii,labda kama anataka kuvunja rekodi ya mkuu wa kaya aliyetembea sana kwa kipindi cha miaka mitano ya mwanzo ktka kutawala kaya hii.
Kasome historia john F Kennedy aliutafuta urais wa USA kwa miaka mingapi.Na alipoupata alifanya nini kwa nchi hiyo kiasi kwamba leo ukimwambia mmarekani JF Kennedy ni bogus unawezazusha kosovo.
 
Tangu thread hii ianze, nimejaribu kusoma line by line kuona ni kosa gani kubwa hilo ambalo baadhi ya watu wanaling'ang'ania ili Rais Mstaafu ashitakiwe nalo, nimeshindwa kuliona (Naomba msaada kwa hilo). Kosa ambalo linaelekea kusemwa-semwa sana ni ununuzi wa mgodi wa Kiwira. Jamani, kama mnajua miiko ya uongozi, nadhani umefika wakati kuiweka hapa ili hoja ziwe na nguvu zaidi. Maana ni dhahiri kuwa Katiba imeshawashinda. Na Serikali makini haiwezi kuingia Mkenge ambao baadhi yenu mnaotaka waingie (kuvunja Katiba). Miiko ya uongozi/Maadili ya uongozi au sheria inayomnyima mtu yeyote mwenye dhamana ya Urais kufanya biashara ni ipi? Miiko ya uongozi au sheria inayomnyima kiongozi yeyote kununua mashirika, makampuni au asset yoyote inayomilikiwa na serikali (mali ambayo inatakiwa kuuzwa) ni ipi? Hivi mnajua kuwa katika bidders wa Mgodi wa Kiwira kuna alie-bid kwa shilingi moja (TZS 1/=) tu?

Nadhani umefika wakati tutafakari na kushinikiza mambo ya msingi zaidi ya kutaka kuoneana, ama kukomoana. Mzee wa watu amefanya kazi nzuri, aachwe apumzike. Urais sio kazi rahisi namna inavyofikiriwa. Anastahili kupumzika baada ya kazi nzito na nzuri kwa Taifa hili.

Recta,

Unachanganya mambo. Kesi niliyoanzisha kuhusu Mkappa ni kuhusu kuwajibika na matumizi mabaya ya madaraka. Ukiangalia kwa makini, nimeweka vipengele ambavyo nimeashiria kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka.

Hilo la Kiwira au yeye kujibinafsisha wala sikulitaja na si sababu ya kumfungulia mashitaka.
 
Duh! Inasikitisha na kushangaza sana kuona bado kuna watu wanaona kelele zinazopigwa na Watanzania ndani na nje ya nchi za kumchunguza Mkapa na maovu yake alipokuwa madarakani na kisha kumfungulia mashtaka ni kutaka kumuonea au kumkomoa!!! Tumuonee au tumkomoe Mkapa ili iweje!!!!?

Akichunguzwa kama hakuna maovu yoyote aliyoyafanya kwa kutumia wadhifa wake basi kutakuwa hakuna ushahidi wa kumtia hatiani, vinginevyo asimamishwe kizimbani kujibu tuhuma dhidi yake na kama akionekana na hatia basi sheria iachwe ifuate mkondo wake.

Tunawaona wenzetu wa South Afrika wanamsimamisha kizimbani Zuma ambaye anakaribia kuwa Rais wa nchi hiyo kwa tuhuma za rushwa dhidi yake, sisi bado tunaogopa kumsimamisha kizimbani mtu aliyekwishamaliza awamu yake!!!! Wacha nchi yetu iendelee kuwa kichwa cha mwendawazimu na kuwa nyuma kimaendeleo miaka nenda miaka rudi maana hawa wahuni wanaojifanya ni viongozi na kuwachagua watuongoze hata wanapofanya maovu bado tunawatetea tu!!! eti tunataka kuwaonea na kuwakomoa!!! Mtu anajiuzia Kiwira na nyumba kwa bei ya bure kabisa na katika mazingira ya kutatanisha, kashfa ya rada, ndege ya Rais, TANESCO n.k. yote hayo hamyaoni!!!! Kazi kweli kweli!!! 😕 😕
 
Recta,
Mkuu unachoshindwa kuelewa ni kitu kimoja tu.. Kwamba kwa kutumia katiba hiyo hiyo mtu anaweza kukiuka sheria kwa kutumia sera za chama. Kwa mfano Hitler na ubaya wake wote ule alitumia katiba ya nchi yake kufanya yote aloyafanya akilindwa na sera za NAZIs..Mugabe kwa ushenzi wake anatumia katiba ya nchi yake akilindwa na sera za Chama..
Mkapa pia ameyafanya yote aloyafanya kwa kutumia Katiba lakini akilindwa na sera za chama chake CCM..
Azimio la Zanzibar ni moja ya sera za CCM ambazo zilimwezesha kiongozi kuanzisha mradi wake ama kuingia biashara..hakuna chama wala wananchi waliohusishwa na azimio hilo. hata hivyo wakati sera hii ikijengwa hakuna hata kifungu kimoja kinachomruhusu ama kumpa nguvu kingozi wa serikali kujiuzia mradi wa serikali ama kuweka sheria ya kuuza hizo mali za Umma kwa viongozi..Alichofanya Mkapa na sera na Ubinafsishaji ni kinyume cha miiko/ maadili ya Uongozi sawa na dalali kujiuzia yeye mwenyewe mali aliyopewa dhamana ya kuiuza sokoni...

Kwa hiyo tunapozungumzia swala la sheria na katiba ya nchi halihusu maamuzi ya sera au Maazimio ya chama CCM wala mipango endelevu/ bomoa ya kiongozi aliyeshika maradaka...Hata huyo Bush aliposhughulikia swala la magaidi na kufungua kwa jela ya Guatanamo Bay limezua utata kutokana na hatua zilizofuatia namna ya ku deal na hao magaidi..Ni makosa yanayomwangukia Bush kukubali baadhi ya torture zitumike lakini hakuna kifungu ndani ya katiba ya Marekani inayoruhusu mateso hayo..
Obama amekusudia kuifunga jela hiyo na Wamarekani wanaweza kabisa kumsimamisha Bush kwa makosa yaliyofanyika ambayo katumia cheo chake kuhalalisha mateso..Kosa la Mkapa halikuwa Ubinafsishaji kama navyoweza kusema kosa la Bush halikuwa kufungua gereza la Guatanamo Bay isipokuwa kosa la Mkapa ni kutumia vibaya madaraka ndani ya katiba kwa kukiuka miiko ya Uongozi bora kama Bush ambavyo amekiuka miiko ya Uongozi bora pale alipotumia torture kinyume cha Uongozi bora..

Mkuu Mkandara, nimekupata. Ila napingana na wewe kiasi fulani, hasa unapolinganisha makosa ya Mkapa na ya viongozi kama Bush, Mugabe na Hitler.

Mkuu, nadhani unajua kuwa kuna sheria za nchi na sheria za kimataifa. Bush na Hitler wanaweza kuwa wametumia Katiba zao kufanya waliyoyafanya. Ila sheria za kimataifa haziruhusu wao kufanya hayo. Kwa nyongeza tu, Viongozi hao wawili (Bush na Hitler) walikiuka haki za binadamu na walisababisha umwagaji damu wa watu wasio na hatia. Guantanamo Bay (mali ya US) ilitumika kuvunja zaidi haki za binadamu kwa kutesa watu bila kuwafungulia mashitaka. Matumizi ya Guantanamo Bay yalikuwa sahihi (kasoro katika uvunjaji wa haki za binadamu).

Kuhusu Mugabe, hali ni tofauti. Kwa kuwa tu yeye anakiuka sheria za nchi yake, na pia kwa uhakika Katiba ya nchi hiyo. Kwa vyovyote vile, Katiba ya nchi ya Zimbabwe inamtaka afanye mambo kwa maslahi ya Taifa, alinde uhai na haki za wananchi wote bila ubaguzi na alinde uhuru wa nchi yake. Ukiangalia kwa makini, utagundua kuwa anavunja Katiba ya nchi.

Kuhusu tuhuma zinazoongelewa hapa jamvini kumhusu Rais wetu mstaafu, ni tofauti kabisa. Kwanza Katiba haijavunjwa, inamlinda na mashitaka yoyote aliyoyafanya akiwa Rais. Lakini pia, nimeomba nipewe vifungu vya utawala bora alivyovivunja. Ningeshukuru sana Mkuu kama ungeainisha vifungu hivyo na hatia yake. Maana hivyo ndivyo makosa yeyenyewe. Umezungumzia Azimio la Zanzibar. Ni Azimio lililotoa ruhusa kwa kiongozi kumiliki mali na kufanya biashara halali ili kumuongezea kipato. Kama amevunja matakwa ya Azimio hilo, ningependa kujua kivipi. Nionavyo mimi hadi sasa hakuna hatia yoyote bayana zaidi ya kutaka kumuonea Mzee yule. Maana hakuna kesi iliyo bayana. Tuendelee kuelimishana.
 
Recta,
Sasa mkuu untafuta uzito wa kesi zao kulingana na mtazamo wako.. Unapovunja sheria umevunja sio swala la haki za binadamu kuwa msingi wa wa mashtaka...Isipokuwa ni utumiaji wa madaraka vibaya kuvunja sheria fulani ambayo imetokana na haki fulani..
Hakuna kiongozi hata mmoja kati ya hao Hitler na Bush ambaye amejilimbikiza mali akiwa rais, tena kwa kujibinafsishia mali ya Umma kuwa yake binafsi, hivyo makosa yao hayawezi kufanana na ya Mkapa..Labda huyo Mugabe na pia swala la kujilimbikiza yeye mali halina uzito zaidi ya kile kinachotazamwa na umoja wa Mataifa, wao wanatazama katiba yao na sheria zao nje ya zile za Zimbabwe.. Na Wazuimbabwe wenyewe wanaweza kabisa kumsimamisha Mugabe kwa kosa la kujilimbikiza mali hata kama halihusiani na Ubinafsishaji bali Utaifishaji.

Kwa hiyo hata Bush na Hitler nilichohusisha zaidi ni kutovunjwa kwa katiba ya nchi zao zaidi ya hawa viongozi kuweka sera zinazortuhusu nguvu zaidi kutumika ili kulinda hiyo katiba. Kwa mfano ni ktk kutekeleza katiba inayohusiana na Usalama wa Taifa maswala ya Ugaidi yakapewa Kipaumbele.. How to deal with them na hata hatua ya kwenda vitani Iraq na Afghanstan ni sera zinazoambatana na kuilinda hiyo katiba.. Katika matukio ya vita hivi tumeona ukiukaji wa sheria za ndani Marekani na kimataifa ikiwa ni pamoja na haki za binadamu na pia kinyume cha utawala bora ktk sheria za Usalama wa Taifa..
Kwa hiyo Bush na Hitler wangeweza kabisa kusimamishwa na mahakama za ndani kwa matumizi mabaya ya katiba ya nchi zao inapofikia swala la Usalama wa Taifa..

Mkapa vile vile ni ruksa ya bunge lake ambalo lilikubali kubinafsisha which is not wrong lakini kubinafsisha huko hakuna maana viongozi wake wachukue mali zile...hakuna kifungu chochote cha sheria kinachomruhusu Kiongozi kuchukua mali au kuji binafsishia mali ya Umma..
Mbali na hilo la Kiwira, mkuu wangu kuna mengi Mkapa kayafanya kwa jeuri kama rais na sera zake ambazo hazikuwa ktk kulinda maslahi ya Taifa..
 
Recta,

Unachanganya mambo. Kesi niliyoanzisha kuhusu Mkappa ni kuhusu kuwajibika na matumizi mabaya ya madaraka. Ukiangalia kwa makini, nimeweka vipengele ambavyo nimeashiria kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka.

Hilo la Kiwira au yeye kujibinafsisha wala sikulitaja na si sababu ya kumfungulia mashitaka.

Ndugu yangu Rev. Kishoka, maelezo yangu hapo juu hayakuhusiana na hoja yako pekee. Nimeongelea hoja nyingi zilizotolewa.

Matumizi mabaya ya ofisi ni hoja inayojadilika. Ila kama wengine wanaotuhumiwa ni lazima ibebe jinsi alivyotumia hayo madaraka yake vibaya. Kusema aliyatumia vibaya peke yake haitoshi.

Duh! Inasikitisha na kushangaza sana kuona bado kuna watu wanaona kelele zinazopigwa na Watanzania ndani na nje ya nchi za kumchunguza Mkapa na maovu yake alipokuwa madarakani na kisha kumfungulia mashtaka ni kutaka kumuonea au kumkomoa!!! Tumuonee au tumkomoe Mkapa ili iweje!!!!?

Akichunguzwa kama hakuna maovu yoyote aliyoyafanya kwa kutumia wadhifa wake basi kutakuwa hakuna ushahidi wa kumtia hatiani, vinginevyo asimamishwe kizimbani kujibu tuhuma dhidi yake na kama akionekana na hatia basi sheria iachwe ifuate mkondo wake.

Tunawaona wenzetu wa South Afrika wanamsimamisha kizimbani Zuma ambaye anakaribia kuwa Rais wa nchi hiyo kwa tuhuma za rushwa dhidi yake, sisi bado tunaogopa kumsimamisha kizimbani mtu aliyekwishamaliza awamu yake!!!! Wacha nchi yetu iendelee kuwa kichwa cha mwendawazimu na kuwa nyuma kimaendeleo miaka nenda miaka rudi maana hawa wahuni wanaojifanya ni viongozi na kuwachagua watuongoze hata wanapofanya maovu bado tunawatetea tu!!! eti tunataka kuwaonea na kuwakomoa!!! Mtu anajiuzia Kiwira na nyumba kwa bei ya bure kabisa na katika mazingira ya kutatanisha, kashfa ya rada, ndege ya Rais, TANESCO n.k. yote hayo hamyaoni!!!! Kazi kweli kweli!!! 😕 😕

Ndugu yangu Babu Ataka Kusema, mimi sijabishia hoja ya kumchunguza mtu yeyote. Ninaamini uchunguzi wowote utakaofanywa utasaidia kuona ni kwa kiwango gani kelele zinazopigwa na watu hao waliopo nje na ndani ya nchi zina mantiki au ukweli wowote. Hilo sina wasiwasi nalo na linaweza kufanyika. Ninaloona si sahihi, ni kumpeleka Rais mstaafu huyo Mahakamani kwa kigezo cha matumizi mabaya ya madaraka. Nadhani hilo linaeleweka bila kulisemea zaidi. Uwezekano wowote wa kumshtaki ni mdogo sana. Niamini tu kwa hilo. Katika mambo nisiyopenda kuyafanya nikiwa na akili zangu, ni kujidanganya. Na hilo nakuhakikishia ndio msingi wa ninayosema hapa. Hakuna uwezekano wowote wa kumshtaki Rais Mstaafu kwenye mahakama zozote hapa nchini. Na hasa kwa mashtaka mnayoyasema. Si kwa matakwa yangu, ila hiyo ndio hali halisi.

Mfano wako wa SA kumshitaki Jacob Zuma haulingani na mada iliyopo. Jacob Zuma si mTanzania na wala halindwi na Katiba yetu kwa namna yoyote. Pili yeye si Rais na wala hajawahi kuwa Rais. Kwa hiyo mfano huyo hauingii katika hoja iliyopo hapa.

Kama nchi yetu itakuwa au imekuwa Kichwa cha mwendawazimu, hilo ni suala la kuamua kwenye uchaguzi na mabadiliko ya Katiba yetu. Na wala sikubishii wala kuongelea hilo. Mkapa ameshamaliza muda wake, na hana nafasi tena ya kutumikia kwa wadhifa huo. Kama tunataka yasijirudie mambo hayo, ni lazima kubadilisha Katiba, na kufuta vipengele vyovyote vinavyoacha mwanya kwa Kiongozi wa juu kumiliki/kujipatia mali akiwa anatumikia Taifa (kama inawezekana).
 
Recta,
Uwezekano wowote wa kumshtaki ni mdogo sana. Niamini tu kwa hilo. Katika mambo nisiyopenda kuyafanya nikiwa na akili zangu, ni kujidanganya. Na hilo nakuhakikishia ndio msingi wa ninayosema hapa. Hakuna uwezekano wowote wa kumshtaki Rais Mstaafu kwenye mahakama zozote hapa nchini. Na hasa kwa mashtaka mnayoyasema. Si kwa matakwa yangu, ila hiyo ndio hali halisi...
Kwa maelezo hayo hapo mkuu tuko page moja!...
 
Maparoko achaneni na Mkapa

Ansbert Ngurumo
Tanzania Daima~Sauti ya Watu​

“KATIKA maisha haya, nje ya kaburi, kuna mambo mawili yenye thamani kubwa kuliko yote, sifa yetu na uhai wetu.

Lakini tunaweza kupoteza sifa kwa kufanya jambo dogo sana lisilo la heshima kama vile kupiga mluzi mahali pasipo pake na wakati usio wake.’’

Kauli hii iliyotolewa na daktari na mshairi wa Kiingereza Nathaniel Cotton (1707-1788), inafaa kutusaidia katika tafakuri ya mjadala unaoendelea juu ya tuhuma zinazomkabili Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Kwa bahati mbaya, mjadala huu umemfanya Rais Mkapa aonekane kama rais wa maparoko.

Nitafafanua katika matumizi ya kawaida ya neno hili. Paroko ni padri kiongozi wa parokia ndani ya jimbo linaloongozwa na askofu. Linatumiwa zaidi na Wakatoliki.

Lakini kwa matumizi ya makala hii, nitalikuza kumaanisha viongozi wa dini na wanasiasa waliojitokeza kujenga ‘hoja za kidini’ kuanzia Zanzibar, Mtwara hadi Tabata, Dar es Salaam, hivi karibuni kumtetea Rais Mkapa dhidi ya tuhuma anazorushiwa.

Nitataja baadhi yao na kujadili hoja zao kwa kifupi. James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, ana pendekezo jipya. Anakerwa na dhana na harakati zinazoendelea dhidi ya viongozi wastaafu na walio madarakani waliotumia madaraka yao kifisadi. Anasikitika kwamba jamii imekengeuka kiasi cha watu kuacha kuitana ndugu, wakahamia kwenye uheshimiwa, na sasa imefikia mahali watu wanaita wengine mafisadi.

Anapendekeza harakati za sasa dhidi ya ufisadi zibadilishwe mwelekeo, badala ya kuwakamata na kuwachukulia hatua watuhumiwa, uanzishwe mfumo wa maridhiano ya kitaifa kuhusu mkengeuko huu wa kimaadili.

Ndivyo nilivyomwelewa, baadhi ya viongozi wa dini, katika matukio na nyakati tofauti za kiibada, wamenukuliwa wakikemea tabia ya wananchi kumghasi Rais Mkapa kwa kumuita fisadi.

Wanadai kwamba hata kama ana makosa, rais mstaafu lazima apewe heshima yake, apongezwe na kuenziwa kwa mema na makubwa aliyolitendea taifa hili na kamwe asiitwe fisadi.

Wamekerwa zaidi na tabia ya vijana kuwazomea vigogo, akiwemo Rais Mkapa, na kuwaita mafisadi, tena mmoja alifika mahali akaacha mahubiri rasmi kwenye misa ya mazishi, akazama kwenye utetezi wa Mkapa, huku akinukuu Biblia kwamba tusimhukumu Mkapa ili tusije tukahukumiwa. Wengine, akiwemo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, wamejaribu kuwakatisha tamaa wote wanaotaka Rais Mkapa aondolewe kinga ya kikatiba ili afikishwe mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili au hata ikibidi kutoa ushahidi katika kesi zinazowakabili wasaidizi wake wa karibu kama atahitajika.

Hoja ya Zitto ni kwamba haoni kama hatua ya kumwondolea Rais Mkapa kinga ina faida kwa taifa. Anaogopa madhara (asiyoyajua) yanayoweza kumpata rais mstaafu binafsi, warithi wake kimadaraka na taasisi nzima ya urais, iwapo tutaruhusu utamaduni wa kuwaondolea marais kinga yao ya kikatiba, hawa na wenzao ndio ‘maparoko’ ninaowazungumzia.

‘Uparoko’ wao unatokana na ujumbe wao wa ‘kiroho’ wanaowapatia Watanzania msamaha wa jumla jumla.

Ujumbe wao unakuzwa na nafasi walizonazo katika jamii. Ni watu wenye wafuasi, na wenye ushawishi.

Wana ujumbe mzito tusioweza kuupuuza. Ndiyo maana tunaujadili, tatizo lao ni moja. Wanajua, lakini hawajajikita katika kujadili kwa kina asili ya harakati hizi za ufisadi na jitihada za kutaka kuondoa kinga ya Rais Mkapa.

Hawajajiuliza: Iweje Rais Mkapa aliyeungwa mkono na Watanzania mwaka 1995 na 2000 ‘Mr. Clean’ aliyeingia Ikulu kusafisha wala rushwa leo ndiye anaandamwa kwa tuhuma nzito nzito?

Ni lini ‘mtu safi’ alibadilika na kuwa Mr. Dirty? Ni kipi kilimbadilisha? Tunakidhibiti vipi kisiwabadilishe wengine?

Kosa wanalofanya baadhi yao ni kutokujenga hoja inayojitosheleza. Mbatia amejitahidi. Lakini hoja yake ni ya kiroho, si ya kisiasa.

Anastahili apewe mimbari, ahubiri upendo, msamaha na amani. Kama hatapata mimbari hiyo makanisani, anaweza kuanzisha asasi ya kutoa ushauri kwa wakosaji na wakosewa juu ya msamaha na maridhiano.

Zitto naye amejaribu, lakini hoja yake ni dhaifu kwa kuwa inaambatana na woga. Hajui kitakachotokea baada ya kinga ya rais mstaafu kuondolewa.

Zaidi ya hayo, hajafafanua vya kutosha kuhusu tija ya kitaifa anayoizungumzia, akidhani haitapatikana kwa kumwondolea rais mstaafu kinga ya kutoshitakiwa.

Maana Rais Mkapa anatuhumiwa kwa kujihusisha au kuhusika na baadhi ya miradi inayotiliwa shaka, hasa kwa kuzingatia kwamba alijiingiza kwenye biashara akiwa rais wa nchi, baadhi ya miradi anayohusishwa nayo ina maslahi kwa umma.

Kama waliokuwa wasaidizi wake wanatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na kupoteza mabilioni ya shilingi za Watanzania na kama kesi zao zina tija kwa taifa, kwa nini mashitaka dhidi ya Mkapa yasiwe na tija kwa taifa?

Kwa mfano, kama alitetea na kuidhinisha ununuzi wa rada ya kijeshi au ndege ya rais katika mazingira tata, na kama tayari yameonekana mazingira ya rushwa ambayo yamekuwa baadhi ya makovu ya utawala wake, kwanini mashitaka dhidi yake yasiwe na tija kwa taifa?

Maana hatuwezi kumshitaki bila kumwondolea kinga. Na ikiondolewa ya Mkapa, hata wanaofuata baadaye watajihadhari na matumizi mabaya ya ofisi kuu ya umma.


Itatoa mfano na onyo hata kwa watumishi wa chini, Wataogopa msumeno wa sheria. Rasilimali zetu zitapona. Kuanzia siku hiyo, hata rais aliye madarakani, na wote watakaogombea na kushinda, watajua kuwa urais ni utumishi, si ufalme.

Kama wao wanatutisha kwa sheria wanazotutungia, ni wazi kwamba na sisi tutawatisha kwa kuwaondolea kinga inayoendekeza ufisadi. Hii ni tija kwa taifa.

Jambo moja ambalo watetezi wote wa Rais Mkapa wanakosea ni kutazama tu utukufu wa urais wa Mkapa, wakasahau makandokando ya urais wenyewe. Wanatazama heshima na sifa ya urais, hawatazami kama rais mwenyewe anaheshimika au ametawala kwa kujiheshimu na kulinda sifa hiyo.

Hawawezi kututhibitishia kwamba, hivi sasa tunavyozungumza, Rais Mkapa ana heshima wanayodhani kwamba anayo mbele ya jamii.

Zaidi ya hayo ni kwamba Watanzania hawajamhukumu Mkapa. Kwa hiyo, hoja ya msihukumu, msije mkahukumiwa, haina nafasi hapa.

Wanachofanya Watanzania ni kumtuhumu. Na tuhuma hizi haziwezi kuondolewa kwa mahubiri na utetezi wa maparoko.

Mfumo wa kisheria nchini hauwapi maparoko mamlaka ya ‘kuwasafisha’ watuhumiwa, hata kama ni ndugu zao, rafiki wao, au hata waamini wanaotoa sadaka kubwa.

Baadhi ya wahubiri hawa wanajua, na wamekuwa wanatufundisha sisi kuwa njia ya kupata msamaha wa makosa yetu ni kuungama, na kujuta na kutubu dhambi. Hawajawahi kutufundisha kwamba kosa likitendwa na rais linapungua uzito, halihesabiwi kabisa au haliadhibiwi. Jamii ile ile wanayoifundisha uadilifu, ndiyo inatumia misingi hiyo hiyo na akili za utambuzi wa mema na mabaya kujua kwamba kiongozi wao alikosea, na anastahili kuchukuliwa hatua ili kuwaonya wengine wasitumie nafasi zao vibaya.

Nadhani viongozi hawa wa dini wanajisahau, wanataka kuendekeza ushirika wao na watawala kama walivyofanya watangulizi wao, wamisionari walioshirikiana na wakoloni kufundisha Waafrika utii na unyenyekevu wakati rasilimali zinaporwa, na wananchi wanafanywa kondoo wa kafara ndani ya nchi zao. Hatuwezi kurudia kosa hilo.

Na kwamba Rais Mkapa alifanya mazuri mengi wakati wa utawala wake, kwa hiyo asituhumiwe kwa mabaya aliyotenda, ni hoja ya kitoto.

Dhambi na neema ni vitu viwili tofauti na vina matokeo tofauti, Hao wanaopelekwa mahakamani leo wana orodha ndefu ya mazuri mengi waliyotenda.


Hayajadiliwi kwa sababu hayahusiki. Hata hivyo, mengine waliyatenda si kwa hiari yao bali kwa kutimiza wajibu wao – tuliowapatia. Hawastahili sifa ya ziada. Wala hayatoshi kunyamazisha wananchi wanapojadili ufisadi.

Wakati mwingine tunapopima mazuri na mabaya, uzito wa mabaya ndiyo unagusa zaidi maisha ya wananchi.

Na wananchi wanapotazama maisha ya neema wanayoishi watawala wetu, wakiyalinganisha na uduni wa maisha yao wenyewe, wanagundua kuwa mazuri ya watawala yamebaki vitabuni, adha zinazotokana na makosa ya watawala ndizo zinaifanya nchi iwe ilivyo – maskini, hohehahe, huku ikiwa imejaa rasilimali zisizomithilika.

Tayari maparoko hawa wanataka kutengua mafundisho yao wenyewe kwamba hata Mungu husamehe wanaotubu.

Tutaanza kuwatuhumu nao kwamba wanasafisha njia ya ufisadi. Vile vile, ni vema maparoko wakajikumbusha saikolojia ya makosa, na wasipuuze kauli ya kiongozi mwenzao wa dini, Askofu Mwingereza, Joseph Hall (1574-1656), kwamba sifa ya mtu ikishaharibika inaweza kujengwa tena, lakini siku zote macho ya jamii yatakuwa yanang’ang’ania pale penye kovu lililoharibu sifa hiyo.

Ndicho kinachofanyika kwa Rais Mkapa na wengine. Mazuri aliyofanya si tiketi ya kufanya mabaya. Lakini ukweli wa ziada ni kwamba Rais Mkapa hakufanya mazuri bila kuwezeshwa na sisi walipa kodi. Aliomba kazi tukampa. Kodi tukalipa. Tukamtunza akiwa Ikulu. Tukamlipia pensheni atakayokula hadi kifo chake.

Kama amejiingiza kwenye ufisadi, basi hana shukrani na hastahili utetezi huu, kwa staili wanayotumia maparoko.

Kama tungegoma kulipa kodi, hata baadhi ya hayo mazuri yake yasingetekelezwa. Kwa hiyo, Watanzania wana kosa gani kumuhoji mwajiriwa wao anayetuhumiwa kutumia vibaya ofisi yao?

Wana kosa gani kuhoji biashara za mwajiriwa wao waliyemlipia kila kitu hadi mwisho wa maisha yake, hasa kama biashara zenyewe zina utata, na zinaleta mgongano wa masilahi?


Ikumbukwe pia kuwa si kazi ya Watanzania kulinda sifa ya Rais Mkapa au kiongozi yeyote.

Ni kazi yake mwenyewe kulinda sifa yake na uhuru wake. Sifa kwa kiongozi ni mzigo na akishaipoteza hawezi tena kuwa huru. Vijana watamzomea kwa sababu amepoteza uhuru.

Watetezi wa Rais Mkapa lazima wajue kwamba wananchi wanampenda Mkapa; lakini wanachukia makosa yake.

Wanajua kuwa asipohojiwa au kuchukuliwa hatua kila mtu atajua kuwa urais ni kichaka cha ufisadi, nafasi ya watawala kuibia wananchi na kutokomea bila kuguswa.


Kama alivyosema mshairi na mwandishi wa riwaya na maigizo, William Shakespeare, heshima ya kiongozi ndiyo uhai wake, Watanzania ni watu wema wanajua maana na mipaka ya maadili na heshima kwa viongozi.

Wana uwezo wa kugundua kuwa viongozi wamepoteza sifa na heshima. Wanawajua viongozi wanaoishi kwa woga na hofu. Na wakikutana nao wanawazomea kama ishara ya kufikisha ujumbe mzito kwao, na kutokubaliana na baadhi ya matendo yao.

Kama vijana wanamzomea Rais Mkapa au yeyote kwa kumuita fisadi, ni kielelezo cha sifa na heshima yake inayoonekana kwa vijana hao.

Si kwamba huyu amechafuliwa kwa kuitwa fisadi, bali amejichafua kwa kuruhusu ufisadi uingie ofisini mwake - ofisi aliyokabidhiwa na vijana hao hao.

Tusisahau kauli ya Rais wa tatu wa Marekani, Thomas Jefferson (1743-1826) kwamba sifa na utukufu wa urais havimsaidii chochote rais mwenyewe, bali vinamwongezea uhasama na vinampotezea marafiki.

Kama Rais Mkapa anachukiwa na amepoteza marafiki ni kwa sababu ya urais wake na jinsi alivyoutumia. Utetezi na mahubiri ya maparoko haviwezi kumrejeshea Rais Mkapa marafiki anaowapoteza. Ni kazi yake kuwarudisha.

Heshima hainunuliwi na hailazimishwi. Tanzania ina watu wengi wema na wabaya kuliko Rais Mkapa.

Mbona hatuwajadili? Mbona hatuwazomei? Kuna sababu ya ziada. Na sababu hiyo ndiyo inakuwa msingi wa tija (kwa taifa) ya tuhuma dhidi yake. Tukiwazuia vijana kumzomea, huku tukiziba mianya ya kisheria ya kumchukulia hatua, tunaweza kutabiri kwamba hatua watakayochukua vijana hao itakuwa na nafuu kuliko kumzomea?

Jambo ambalo watawala, maparoko na mashabiki wao wanapaswa kujifunza sasa ni kwamba wananchi wamepunguza imani yao kwa serikali kwa sababu viongozi wenyewe wameonekana hawaaminiki.

Na kama maparoko wanataka tuwapuuze hata wao, waendelee kutetea makosa ya vigogo.


Labda wananchi wametambua na kuzingatia ukweli wa kauli ya Rais Mstaafu wa Marekani, Ronald Regan, kwamba “Serikali si mfumbuzi wa matatizo yetu, bali serikali ndilo tatizo lenyewe.” Tatizo hili haliwezi kuondoka tusipowachukulia hatua waliolisababisha, wanaolilinda na wanaolishabikia.

Kwa maoni yangu, na kwa mujibu wa sheria zetu, Rais Mkapa bado hana hatia. Ametuhumiwa tu.

Aachwe ajitetee katika mkondo wa kisheria unaokubalika. Kumtetea na kumlinda kupita kiasi kunaleta wasiwasi na kuongeza uzito wa tuhuma – hasa pale kazi hiyo inapofanywa na ‘maparoko.’

Mkapa hakuwa rais wa maparoko. Watuachie rais wetu tumalizane naye. Maparoko wasitetee, bali wakemee maovu yote, hata ya watawala.
 
Hawa maparoko huenda siyo watumishi wa Mungu; ama wanataka kuficha aibu kutokana na ukweli kuwa Mkapa alikuwa muumini wao.
 
Wakatoliki, kama walivyo Waislamu wanakuwa na raha ya AINA yake KIONGOZI MKUU wa NCHI anapokuwa wa dhehebu/dini yao. Wanachofaidika na hilo bado ni kitendawili kwangu.
 
Hawa maparoko huenda siyo watumishi wa Mungu; ama wanataka kuficha aibu kutokana na ukweli kuwa Mkapa alikuwa muumini wao.[/QUOTE]

Kanisa katoliki lime-panic sababu wengi waliokamatwa na kutuhumiwa kama watuhumiwa wakuu kwa ufisadi wengi asilimia zaidi ya 90 ni wakatoliki na waliosomea shule za wakatoliki kuanzia akina Mkapa,Balali,Chenge,Mramba n.k na walikuwa ndio wachangiaji wao wakubwa kwenye halfla mbalimbali za kanisa hilo na wageni wao heshima kwenye uchangiaji pamoja na ukibaka wao.

Kilio cha maparoko hao ni kupungua kwa wachangiaji kutokana na kesi hizo za ufisadi maana hata wale mafisadi ambao hawajashikwa wanaogopa kujitokeza kuchanga mapesa kanisani mengi kwenye halfa za uchangiaji kwa kuogopa kufuatiliwa.

Maparoko kilio chao ni kilio cha sadaka kupungua.Wangependa mafisadi wasikamatwe ili waendelee kuneemeka na michango ya mafisadi makanisani mwao.Kanisa halikaliki kutokana na njaa ya kupungua sadaka na wafadhili wengi wa nje hawatoi misaada kwa kanisa katoliki kama zamani.Tegemeo lao kubwa lilibakia kwa mafisadi.

Njaa ndizo zinawafanya maparoko wapige yowe hata kwenye misiba badala ya kuwalilia marehemu wanaowazika wanalilia mafisadi waliokamatwa na wanaotarajia kukamatwa !!!.Hivi ni sahihi mtu kulilia mtu mwingine kwenye msiba wa marehemu mwingine? Hao maparoko nao wanaendekeza mno njaa mpaka hawaoni ukweli kwa kupofushwa macho ya roho zao na hela za kifisadi kwenye chombo cha sadaka laaniwa.shenzi type.
 
Wote wanaomtetea Mkpa wafahamu jambo moja la msingi alililotufanyia watanzania wote. Ni sera ya uchangiaji elimu, matibabu n.k LEo hii tunashuduia migomo ya wanafunzi sababu ni hiyo hiyo.Tujiulize chanzo ch uchangiaji huo ni ini. Awamu ya pili hapakuwa na sera hiyo .Kilichotokea awamu ya tatu nini nini ? Au ndio ilikuwa njia ya kutafuta ulaji ?

Huyu jamaa imeshadhihirika nidio mwenye kumiliki Kiwira mining. Lets us wait and see what comes next.......
 
Mkapa akumbana na jipya jingine
ATAKIWA APANDE MAHAKAMA YA THE HAGUE



RAIS wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ambaye amekuwa akisakamwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi, huku akitakiwa kuvuliwa kinga na kupandishwa kizimbani, sasa anakabiliwa na tuhuma nyingine nzito; anatakiwa afikishwe Mahakama ya The Hague baada ya Wapemba kuuawa Januari 27, 2001.


Mauaji ya Wapemba hao yalitokea mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais wa Zanzibar wakati Amaan Abeid Karume alipotangazwa mshindi na kusababisha wapinzani kuandamana kupinga ushindi huo. Serikali inasema ni watu wasiozidi 27 ambao waliuawa, lakini wapinzani wanasema ni zaidi ya 100.


Na wazee wa Pemba walioshiriki kuandaa barua ya kuuomba Umoja wa Mataifa uwasaidie kupatikana kwa serikali huru ya kisiwa hicho, ndio walioibua hoja hiyo wakisema wanakusudia kumfikisha rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa Mahakama ya The Hague kutokana na mauaji waliyoyaita ya kikatili ya Wapemba yaliyotokea Januari 27 mwaka 2001.


Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, katibu mtendaji wa wazee hao, Hamad Ali Musa, alisema tayari walishafikisha suala hilo kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa kwani mauaji hayo yalitokea wakati viongozi hao wakiwa madarakani.


Idadi ya watu waliouawa baada ya kutangazwa kwa matokeo iliibua mjadala na katika mahojaino na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Mkapa alionekana kupata hasira baada ya mtangazaji kumweleza kuwa idadi ya waliouawa ni zaidi ya 100.


Mkapa alisema katika kipindi hicho cha Hard Talk kuwa, anashangaa waandishi kuokota habari wakati mtoaji rasmi wa taarifa kama hizo ni serikali.


Musa pia alisema wanakusudia kumfikisha katika mahakama hiyo aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi, Omary Mahita wakidai kuwa, damu iliyomwagika bila hatia katika kipindi hicho haiwezi kufumbiwa macho na hivyo ni muhimu haki itendeke na sheria kuchukua mkondo wake.


Kiongozi huyo alisema, hivi sasa wapo katika mchakato wa mwisho wa kutafuta mawakili watakaosimamia kesi yao ipasavyo wakati itakapoanza kusikilizwa.


Katika suala la kumfikisha Waziri Seif Khatib mahakamani, Musa alisema kuwa, mapema mwishoni mwa mwezi huu mchakato huo utakuwa umekamilika, kwani mawakili wa kusimamia kesi hiyo tayari wameshapatikana.


"Ni vema viongozi wetu wakaelewa kuwa hakuna haja ya kuwafumba midomo watu wanapotafuta haki zao za msingi. Waziri Khatib alitufumba midomo kwa kutumia nguvu za dola na ndiyo maana tukawekwa ndani," alisema Musa.


Katika hatua nyingine, mjumbe wa kikundi cha wazee hao, Ally Makame alisema bado wanaendelea kuzitaka jumuiya za kimataifa kushughulikia suala la kisiwa hicho kujitenga na kuwa na dola yake kwani hatua iliyopo hivi sasa inaonyesha dhahiri kuwa watu wake wameendelea kudhalilishwa kila siku.


Alisema mapema mwezi uliopita walipeleka maombi yao ya kutaka kujitenga katika ofisi za Umoja wa Mataifa, lakini walijibiwa kuwa Pemba haina sababu za kujitenga kutokana na ukweli wa mambo kwamba, Rais Jakaya Kikwete anashughulikia mpasuko uliopo ndani ya Zanzibar.


"Jambo hili ni uongo kwani suala letu halihusiani kabisa na masuala ya siasa, katika suala la kutaka Pemba iwe na dola yake si suala la CUF, ni suala letu wananchi, hivyo ni vema viongozi wakafahamu jambo hili," alisema Makame.


Alisema baada ya kupokea majibu hayo ya awali ya barua yao kutoka UN, tayari wameshaandika barua nyingine wakieleza hisia zao kuwa, kama suala la mpasuko lisiposhughulikiwa mapema, hali itakuwa mbaya tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2010.


"Wapemba hawatakubali kuendelea kufedheheshwa kama wakimbizi, hivyo ni vema mashirika ya UN yakaanza kujiandaa mapema kupokea wakimbizi nchini Kenya wakati wa uchaguzi," alisema Makame.


Baada ya vurugu hizo za mwaka, watu kadhaa kutoka Pemba walikimbilia Shimoni, Mombasa wakisaka hifadhi ya kisiasa.


Juni mwaka jana kikundi cha wazee 12 wa Kisiwa cha Pemba waliibuka na kuzua hoja ya kutaka kujitenga kwa kisiwa chao kwa madai kuwa, serikali ya CCM inawabagua kimaendeleo.

Source: Mwananchi
 
Wakatoliki, kama walivyo Waislamu wanakuwa na raha ya AINA yake KIONGOZI MKUU wa NCHI anapokuwa wa dhehebu/dini yao. Wanachofaidika na hilo bado ni kitendawili kwangu.

Hizo ndo tunaziita Dhana za KIJINGA..
 
Hawa maparoko huenda siyo watumishi wa Mungu; ama wanataka kuficha aibu kutokana na ukweli kuwa Mkapa alikuwa muumini wao.

Haya ndo maoni ya ma-pundits wa JF..

Kwa hiyo 'maparoko' ndo waliomtuma Mkapa?

Kaazi kweli kweli..
 
Kanisa katoliki lime-panic sababu wengi waliokamatwa na kutuhumiwa kama watuhumiwa wakuu kwa ufisadi wengi asilimia zaidi ya 90 ni wakatoliki

Hivi unajua DIMENSION ya Kanisa Katoliki au unataka kuwaingiza kingi waso na upeo wenzako na hizi stori za vijiweni?

Hivi una akili timamu? Yaani unasema eti Kanisa Katoliki lilikuwa linategemea michango ya kina Che Mkapa?

JF ina kila aina ya mitindio duh..
 
Hawa maparoko huenda siyo watumishi wa Mungu; ama wanataka kuficha aibu kutokana na ukweli kuwa Mkapa alikuwa muumini wao.[/QUOTE]

Kanisa katoliki lime-panic sababu wengi waliokamatwa na kutuhumiwa kama watuhumiwa wakuu kwa ufisadi wengi asilimia zaidi ya 90 ni wakatoliki na waliosomea shule za wakatoliki kuanzia akina Mkapa,Balali,Chenge,Mramba n.k na walikuwa ndio wachangiaji wao wakubwa kwenye halfla mbalimbali za kanisa hilo na wageni wao heshima kwenye uchangiaji pamoja na ukibaka wao.

Kilio cha maparoko hao ni kupungua kwa wachangiaji kutokana na kesi hizo za ufisadi maana hata wale mafisadi ambao hawajashikwa wanaogopa kujitokeza kuchanga mapesa kanisani mengi kwenye halfa za uchangiaji kwa kuogopa kufuatiliwa.

Maparoko kilio chao ni kilio cha sadaka kupungua.Wangependa mafisadi wasikamatwe ili waendelee kuneemeka na michango ya mafisadi makanisani mwao.Kanisa halikaliki kutokana na njaa ya kupungua sadaka na wafadhili wengi wa nje hawatoi misaada kwa kanisa katoliki kama zamani.Tegemeo lao kubwa lilibakia kwa mafisadi.

Njaa ndizo zinawafanya maparoko wapige yowe hata kwenye misiba badala ya kuwalilia marehemu wanaowazika wanalilia mafisadi waliokamatwa na wanaotarajia kukamatwa !!!.Hivi ni sahihi mtu kulilia mtu mwingine kwenye msiba wa marehemu mwingine? Hao maparoko nao wanaendekeza mno njaa mpaka hawaoni ukweli kwa kupofushwa macho ya roho zao na hela za kifisadi kwenye chombo cha sadaka laaniwa.shenzi type.

Hizi ndizo kauli za aibu. Mtu anawezaje kufikiria kuwa kuna dhehebu linalohitaji watu wachache wakaibe ili liweze kustawi. Mawazo gani haya?
 
Mfa maji,

Naomba nikukosoe kidogo. Suala la kuchangia elimu halikuanza na Mkapa hata kidogo ila lilianza wakati Mkapa akiwa waziri wa elimu ya juu wakati huo Rais akiwa Mzee Ruksa!. Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kilifungwa kwa miezi 9 kwa kisingizio cha wanafunzi kumtukana Rais matusi ya nguoni lakini ukweli ni kwamba tulikuwa tunapinga suala la kuchangia elimu ya juu kwani tulijua sasa elimu ya chuo kikuu itakuwa ni ya watoto wa wenye nacho na sisi watoto wa wakulima hatutasoma tena. Hivyo suala la kuchangia elimu lilianza wakati wa awamu ya pili!!!!.

Kuhusu hili la maparoko, namuunga mkono mtoa hoja, maparoko wakae kimya!!!!! na wakitaka kuchangia mawazo yao ni sawa wachangie kama Mtanzania mwingine yeyote lakini si wakati wa misa!!!!!
 
Back
Top Bottom