Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mkuu FMES,
HIvi mzee Mkapa akiwekwea Ndani wewe utafaidika na nini?

sio suala la mtu binafsi kufaidika. kama ni kufaidika ni kwetu sote - watanzania. na hii itakuwa faida ya leo na kesho.
kama atafikishwa mahakamani na kupatikana na makosa, say ya kujiuzia 'mali' kwa bei poa au rushwa etc inamaana kuwa utakuwa utaratibu wetu kwa siku zijazo kuwachukulia hatua za kisheria marais wetu wa kifanya makosa. kwa atakae fuata halitokuwa jambo jipya.
na yeye atakuwa madarakani akijua akiharibu kifuatacho ni kisutu.
nina uhakika kama kuna makosa ben aliyafanya hakutegemea kama angeweza tinga kisutu. alijua anakinga ya wakat ule na ujao - akishastaafu.
watu wengi hatufanyi makosa/dhambi/uhalifu kwa sababu ama tunamuogopa mungu au taratibu/miiko au sheria za nchi au vyote. mwingine anaweza asiogope viwili vya mwanzo lakin akaogopa cha mwisho ambacho ni sheria. na siku hiz ndicho hasa kinachoogopwa. sasa gembe hujaona faida hapo bado?
1. viongoz wetu/watu wote watakuwa chini ya sheria
2. tutakuwa tumekubali kuwa binadamu ni binadamu tu hata kama ana akili kama 'einstein' na mkubwa kama 'goliati'
3. binadamu ana udhaifu wake kama binadamu na hivyo anaweza tenda baya au zuri
4. binadamu amezungukwa na binadamu wenzie - wabaya kwa wazur na wote hao wanamuinfluence kwa namna moja au ingine
5. mali za 'taifa' zinakuwa 'salama' zaidi maana awaye yeyote hata kama atazitamani kias gani atakuwa anaogopa 'kujimilikisha'
6. rushwa itapungua kwa kuogopa kutinga mahakamani baadae
7. kwa kuwa uraisi wa nchi ni ngazi ya 'mwisho' ya 'mafanikio' ya binadamu kutinga mahakamani ukishatoka uraisini itakuwa aibu. hivyo mtu atajitahidi kutenda yaliyo sawa aibu isije mkuta
8. etc.

kuna haja gani ya watu wenye heshima mbele ya jamii kuanza kushtakiwa>?

mambo yote ya maana au ya ovyo popote pale yana buniwa, kuanzishwa, kusimamiwa na watu wenye heshima katika jamii.
mara ingine mabovu yanafanywa ilihali wanajua kuwa ni mabovu. kwanini wasihukumiwe kama wamekosea? lingekuwa kosa moja au la kwanza tungesema bahat mbaya.
hebu angalia ujerumani kipindi cha hitler na marafiki wake. cheki pale rwanda na majirani zao burundi. chungulia zimbabwe. angalia mtafaruku wa kenya. vurugu au mauaji au vyote vilianzishwa na kusimamiwa na watu wenye heshima katika jamii.
au unataka kuniambia hitler alikuwa haheshimiwi?
 
Mkuu FMES,
HIvi mzee Mkapa akiwekwea Ndani wewe utafaidika na nini?kuna haja gani ya watu wenye heshima mbele ya jamii kuanza kushtakiwa>?
.

Hivi hiyo heshima unayosema inashuka tu kama MANA toka juu au unafanyiwa kazi? Kwamba vyovyote utakavyofanya ili mradi wewe ni Rais utaheshimiwa? Cheo cha urais kweli kina hadhi ya juu nakwa sababu hiyo kimewekewa taratibu na masharti ya namna ya kukitumikia.Tatizo linakuja, je mtu tunayempa cheo hicho anatambua usafi na heshima ya cheo alichopewa? Na kama anafahamu anafanya juhudi gani kuilinda heshima ya cheo alichopewa?

Mkapa tulimpa cheo hicho chenye hadhi na akaki-abuse(Kukitumia kinyume na masharti yake. Hivyo kwa uchafu wake akakichafua cheo hicho na kutuchafua watanzania pia. Tunataka aende mahakamani ili akatueleze kwa nini hakufuata taratibu za kukitumikia cheo hicho.

Pili watanzania tutafaidika kwa mengi, lakini mojawapo ni kujenga utawala wa sheria na kupeleka ujumbe kwa viongozi wote wa sasa na wajao kuwa. NI MARUFUKU KUTUMIA DHAMANA UNAYOPEWA KUWAIBIA NA KUJIKATIA ROBO TATU YA MKATE WA TANZANIA PEKEE YAKO NA FAMILIA YAKO.
Tunakosa huduma nyingi kwa kuwa pesa ambazo zingetumika kutoa huduma hizo, zimechukuliwa na watu wachache kinyume cha taratibu kwa tumia mgongo wa cheo alichopewa.
Hatufaidiki ipasavyo na mali asili zetu kwa kuwa watu wanatumia vibaya dhamana tulizowapa kwa kusaini mikataba mibovu kwa makusudi ili kujinufaisha wao. Na hii wanaifanya kwa kuwa kutumia power ya uongozi.

Hakuna rais mstaafu ambaye anaheshima kama Madiba(N.M), lakini alitinga kortini kujisafisha kuwa yeye ni safi tena akiwa bado ni rais. Lakini mpaka leo heshima yake haijashuka si Afrca tu bali Duniani, kwa kuwa kweli alikuwa safi.

Sisi tunataka kama kweli Mkapa ni safi na mtu anayeheshimika, basi aende akatuthibitishie usafi na heshima hiyo mahakamani.
 
Heri ya X-mas na mwaka mpya wadau.


Pamoja na kwamba nakubaliana kabisa na Dr. Slaa kwamba Mh. Mkapa hana kinga... kulingana na kipengele cha katiba kwenye mambo aliyofanya binafsi...

Sikubaliani na Mtanzania yeyote yule ambaye anadhani kumshitaki Mkapa ni sawa na kumshitaki kiongozi mwingine...

Angalieni mbali wakuu... kwa ajili ya usalama na utengamano wa Taifa... naomba Mkapa asipelekwe Mahakamani hata kama ametenda makosa...

Over and Out

Mimi pia sina mengi ya kuandika mkuu!Lakini niweke angalizo tu.Wakuu nyinyi endeleeni na mchakato wa kumburuza mkapa mahakamani na endeleeni kumshawishi Kikwete ili abadili msimamo wake.Lakini yote hayo yakikamilika basi mjiandae na kusambaratika kwa taifa la tanzania.

Enyi watanzania,

Tusiwe wajinga kiasi cha kutumiwa na watu wa manufaa yao,Na nawaomba sana huku nikitumia nguvu za ziada kuonya na kuwaambia tusiwe chujio la kuchuja yale ya wanasiasa wa maji taka.

Kwa kifupi,kuamua kumpeleka Mkapa Mahakamani ni kuangamaiza taifa hili.wananchi wenzangu Ndiyo itakuwa mwanzo wa kuanguka kwa CCM na kuanguka kwa CCM kutapelekea nchi hii kuyumba .

Nasema mie simo na tuendelee kumuombea Dr. Slaa!

Mwalimu nyerere alishasema Bila CCM madhubuti nchi itayumba![/SIZE]

<
<rant>
Mtumeeee! Astakafululahi! Yes wangu! F.u.c.k! Huwa naamini inatakikana kila mtu awe huru kujenga mawazo yake na imani zake. Sasa naanza kuamini hii inabidi ibadilike maana ni hatari ... Naanza kuona kama democrasia ni kosa kubwa sana, whoever thought of it first must be in hell right now, pengine ni heri kuwa na ma-dikteta wenye akili kuliko kuwa democrasia iliyo jaa watu wanaofikiri na makalio.

Kwa sasa nataka kuamini kwamba ndugu zetu hapo juu mnatania, la sivyo go have your selves checked by a competent doctor ... psychosis huwa ina dalili zake ... or are u guys having enough sex these days?
</rant>

lol
Nimeshindwa kujizuia kucheka nilipokuwa nasoma hizo posts...
Waheshimiwa mawazo yenu mazuri, ila sidhani kama wengi hapa watukubaliana nanyi ...



Disclaimer: I didn't type anything between <rant> and </rant>. It wasn't me kabisa ...
 
Ndugu Mwanjelwa,
Mimi ni Mtanzania, ninfuatilia kwa makini na kwa ukaribu zaidi mambo ya siasa za Tanzania. Asante kwa kuonesha upumbavu wako wa kukubaliana na machafu, wizi na ufisadi. Inaonesha wazi kwamba wewe ni moja kati ya mafisadi ama umefaidika na ufisadi huo ama si mtanzania halisi kama akina Mkapa, balali na Rostam wenye uraia wa nchi mbili mbili.

Kama unashindwa kuona na kuelewa uchafu wa Mkapa na kundi lake basi bila shaka una matatizo ya akili.
Mkapa ni mwizi, Jambazi na muuaji na ndiye chanzo cha matatizo yote ya sasa ambayo serikali ya Jakaya imekutana nayo.

Daniel Yona na pesambili Mramba hawakufanya wizi pekee yao, bali walifanya na bosi wao Mkapa na ushaidi upo, uuzwaji wa nyumba za serikali na mashirika ya umma ulilenga zaidi kumtajirisha Mkapa na kundi lake na wala si kwa faida ya watanzania na Tanzania.

UKWELI UNABAKI KUWA UKWELI KWAMBA MKAPA NDIYE BABA WA MAFISADI. NI LAZIMA AKAMATWE, ANYANG'ANYWE MALI ALIZOIBA NA AFUNGWE BILA KUCHELEWA.

Ohh, samahani mkuu, nilikuwa sijakuona. Kumbe na upo? Pole sana kwa uelewa wako unaokutosha wewe tu. Tumshukuru Mungu kwa kuwezesha mtu kupumua bure bila kujali haiba yake.
 
- Thisday ya leo kuna waziri mkuu wa zamani anayechunguzwa na uchunguzi ukimalizika tu one way to Kisutu, we are right on the track!
 
Heri ya X-mas na mwaka mpya wadau.


Pamoja na kwamba nakubaliana kabisa na Dr. Slaa kwamba Mh. Mkapa hana kinga... kulingana na kipengele cha katiba kwenye mambo aliyofanya binafsi...

Sikubaliani na Mtanzania yeyote yule ambaye anadhani kumshitaki Mkapa ni sawa na kumshitaki kiongozi mwingine...

Angalieni mbali wakuu... kwa ajili ya usalama na utengamano wa Taifa... naomba Mkapa asipelekwe Mahakamani hata kama ametenda makosa...

Over and Out


sawa mdau hatutampeleka mahakamani, kama ambavyo kipindi cha mwinyi wizi wa midhahabu na mi almasi hakukuwa na hatua yeyote iliyochukuliwa, na Kikwete achukue Mikumi na Manyara au Bulyankulu, na atakae kuja achukue mlima kilimanjaro awe anapeleka watalii, kwa ajili ya usalama wa Taifa letu.
Hell NOOOOO usalama upi wakati tunashindwa kulinda mali zetu au ni kwa ajili ya usalama waoooo.....Nishachoka mie
 
msimsahau na mama Anna Mkapa,to me anaweza kuwa ndie Imelda Marcos wa bwenyenye Mkapa, coz siamini kama Mkapa alikuwa na guts za ku-accomplish yote bila force ya yule fisadi mkimya wa kike...nadhani ana mchango mkubwa sana katika kulipoteza taifa ndani ya miaka 10 ya Mkapa!!

hee! Mwizi ni nani mbona tunavuruga mambo basi waambie wasimsahau na mama mgonja, mama Mramba, na mama yona? makubwa aliyeiba ndie akamatwe sio tu kwasababu mke au mumewe ni active then useme akamatwe ...
 
Pamoja na ugumu wa kufanya maamuzi ya maana unaoonekana ndani ya Wanasiasa wetu na Viongozi kuhusu kufungua kesi ya matumizi mabaya ya madaraka kwa Mkapa, kuna haja ya shinikizo la nguvu la kuleta mabadiliko ya katiba ambayo si kwamba yataondoa au kufafanua kinga kwa Rais bali kutaleta uwajibikaji na kujenga Demokrasia mpya Tanzania ambayo inatawaliwa na kunyanyaswa na CCM.

Laiti kama Kikwete angejaribu basi kufanya hilo....
 
Kuna malalamiko kadhaa yanayoendelea miongoni mwa watanzania juu ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Ben Mkapa kutaka afikishwe mahakamani kwa sababu za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka wakati wa utawala wake.

Lakini binafsi napenda kuungana na kauli iliyowahi kutolewa na JK rais wa sasa wa Tanzania kumwacha Mkapa astaafu wa amani.

Nasema hivi kwa sababu kwa kumfikisha mahakamani Mkapa tutakuwa tunakiuka sheria na katiba ya nchi ambayotumeiweka wenyewe.

Istoshe Mkapa kajitahidi sana kama kiongozi kulinda amani ya nchi, kuimarisha miundombinu hali ambayo iliwafanya watanzania wengi kumpa sifa nyingi kwa utendaji wake mzuri wakati wa urais wake.

Kikubwa sisi kama watanzania tufanyeni kazi na tuachane na porojo porojo za Mkapa, Mkapa, tufanyeni kazi za kimaendeleo tuachane na Mkapa Katiba inamlinda
 
Mwandikie PM Mkuu FMES...Hii thread tulishazungumza sana..tukate ishu
 
Kuna malalamiko kadhaa yanayoendelea miongoni mwa watanzania juu ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Ben Mkapa kutaka afikishwe mahakamani kwa sababu za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka wakati wa utawala wake.

Lakini binafsi napenda kuungana na kauli iliyowahi kutolewa na JK rais wa sasa wa Tanzania kumwacha Mkapa astaafu wa amani.

Nasema hivi kwa sababu kwa kumfikisha mahakamani Mkapa tutakuwa tunakiuka sheria na katiba ya nchi ambayotumeiweka wenyewe.

Istoshe Mkapa kajitahidi sana kama kiongozi kulinda amani ya nchi, kuimarisha miundombinu hali ambayo iliwafanya watanzania wengi kumpa sifa nyingi kwa utendaji wake mzuri wakati wa urais wake.

Kikubwa sisi kama watanzania tufanyeni kazi na tuachane na porojo porojo za Mkapa, Mkapa, tufanyeni kazi za kimaendeleo tuachane na Mkapa Katiba inamlinda

Ntaramuka,
Hii ni Nchi huwezi kumwacha mhalifu apete; nobody is above the law, even if he was a president, he souldn't steal! Hata kama analindwa na sheria basi hiyo sheria ishapitwa na wakati inabidi tui-amend! Lazima tuzibe ufa, sio kila rais akija basi aibe kwa sababu sheria inamlinda!
 
Mkapa ni MHUNI sana. Tena uhuni wa Mkapa unatisha.
Alipoona kuwa marupurupu ya Urais na hela zote ambazo kakusanya kwa kufanya kazi Tanzania na nje ya Tanzania miaka yote hiyo hazitoshi, akaona afikirie mbinu mpya za kukusanya VISENTI vingi tu kwa siku wakati akienda kupumzika na kusubiri aende mbele ya Pilato mkuu wa ulimwengu.
Mkapa akajua kuwa hatafaidi hela za kubinafsisha mashirika. Kaliza Tanesco, Air Tanzania, NBC, BoT, Bandarini, Kodi, Ndege, Rada, nk. Alipokusanya hizo zote akaona kuwa bado hazitoshi (kwanza muone, kakaa mkao wa Mfalme Jeta vile). Akaanzisha IPTL ili akusanye kwenye UMEME. Kwenye Maji (DAWASCO) nako akawekeza. Alipoona hizo zote hazitoshi, akajiuzia nyumba za serikali na hii ni baada ya kufanyia matengenezo makubwa. Wao wakalipa ghalama za matengenezo tu.
Kama hiyo haitoshi, akaJIPA kiwanda cha makaa ya MAWE kiwira ambacho kumbe hata kufanya biashara hajui, kiwanda kinakufa sasa. Hee, wewe mahela yote hayo ya nini? Hushibi mtu wewe? I think Mkapa ni mfano hai wa BLACKHALL inayomeza kila kitu, hadi mwanga. Angeliweza kukubadilisha wewe Ntaramuka na Gembe ili mwe EURO 1,000,000. basi angelifanya hivyo bila hata ya kufikiri mara mbili.
Take this Mfalme Jetta aka BLACKHALL to Kisutu. This will give more chance next prezidaaa awe anaheshimu katiba na watu wake. Yes, as soon as possible, AMINA.
 
Issue siyo kumsakama rais mstaafu Mkapa. Issue ni matendo ya kifisadi aliyoyafanya yeye kama Ben Mkapa na sio kama rais. Japo mimi sio mtaalamu wa katiba, kinga ya rais mstaafu kutofikishwa mahakamani inahusu maamuzi yoyote aliyoyatenda kama rais kwa mujibu wa taasisi ya urais, lakini uvunjaji wowote wa sheria uliofanywa na Mkapa at personal capacity kama Ben, hauna kinga yoyote.
Hakuna mahali popote kwenye katiba palipomkataza rais asifanye biashara akiwa ikulu, hili ni suala la morals na sio sheria.
Suala la kisheria linakuja pale ambapo mchakato wa ubinafsishaji wa Kiwira umepindishwa ili kuifavour kampuni ya AnnBen, hapa ndipo kwenye tatizo.
Uamuzi wowote Mkapa alioufanya kama AnnBen ni uamuzi binafsi na hauna kinga yoyote ya kisheria.
Pia naungana na msimamo wa JK kumwacha apumzike kwa amani kama heshima, na hana haja ya kuhukumiwa na sheria za nchi, 'lawa of the land' bali tayari ameshaanza kuhukumiwa na 'The law of the Karma' ambapo dhamira yake inamsuta and he'll suffer the cuenseqenses of his past actions.
.
 
Kuna malalamiko kadhaa yanayoendelea miongoni mwa watanzania juu ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Ben Mkapa kutaka afikishwe mahakamani kwa sababu za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka wakati wa utawala wake.

Lakini binafsi napenda kuungana na kauli iliyowahi kutolewa na JK rais wa sasa wa Tanzania kumwacha Mkapa astaafu wa amani.

Nasema hivi kwa sababu kwa kumfikisha mahakamani Mkapa tutakuwa tunakiuka sheria na katiba ya nchi ambayotumeiweka wenyewe.

Istoshe Mkapa kajitahidi sana kama kiongozi kulinda amani ya nchi, kuimarisha miundombinu hali ambayo iliwafanya watanzania wengi kumpa sifa nyingi kwa utendaji wake mzuri wakati wa urais wake.

Kikubwa sisi kama watanzania tufanyeni kazi na tuachane na porojo porojo za Mkapa, Mkapa, tufanyeni kazi za kimaendeleo tuachane na Mkapa Katiba inamlinda

Hapa mkuu umechemsha! Ni sehemu gani katika katiba inamlinda Mkapa. Dr Slaa hivi majuzi tuu amefafanua hili suala la katiba kumlinda Raisi wa nchi, ila kuna ulazimu wakuangalia kwa undani ili tuelewe.

Binafsi, Mkapa achunguzwe na kama kuna alichovurunda basi kuna ulazimu awajibishwe. Watanzania hatuwezi kusota eti sababu mtu fulani "Is above the Law"?

This should apply to viongozi wote tuliowapa ridha yakutuongoza.
 
Jamani hapa tusichanganye mambo,mwizi ni mwizi awe Rais,Waziri,Askofu au padri n.k.Kama Rais kunamambo na sheria anapashwa kiziheshimu.Kitendo cha kuifanya Ikulu kitengo cha bihashara au kubinafsisha mali ya umma(kiwila)n.k ni vitendo ambavyo Mkapa amekiuka miiko ya uongozi.Kama mambo yataendelea hivi tusije tukashangaa Kikwete baada ya kumaliza muda wake akainunua Ikulu na kuifanya nyumba yake ya kuishi na kuchukua mgodi wa Buzwagi kwani hawezi kushitakiwa kuondolewa kwa kinga kwa Rais na Mkapa kufikishwa mahakamani kuua funzo kwa wanaofuata na kua makini katika kutoa maamuzi mbalimbali.Advocate Jasha
 
JK: I won`t reveal corrupt suspects

2009-01-08 11:30:53
By Mary Edward, Dodoma​

The Chairman of the ruling Chama cha Mapinduzi President Jakaya Kikwete yesterday said that all government leaders and others suspected to have abused office or taken part in corrupt practices would face justice.

He called on people who wanted him to name the suspects to bear with him as state organs were still investigating and that once the investigations were over, names of the suspects would be made public by the relevant organs.

Opening the general meeting for CCM women wing (UWT) here, President Kikwete said he would not reveal the suspects because the whole move was not intended to humiliate people but rather to let justice take its course.

``I know some people would like to see me reveal people they suspect are corrupt. This is not the right procedure. Let the state machineries do their work.

The idea is not to humiliate people. The names will be made public once the investigations are completed`` he said.

Two former ministers Daniel Yona and Basil Mramba and retired permanent secretary in the treasury Gray Mgonja have already been arraigned for allegedly abusing office and occasioning loss of 11.7bn/- to the government.

Twenty one people have also been taken to court allegedly for stealing from the Bank of Tanzania`s External Payment Arrears (EPA) account.

Dwelling on the CCM's women wing elections which started yesterday night, Kikwete said it was high time the ruling party brought some changes by having an educated leadership cadre.

He said due to the many challenges facing the world, it would be impossible for illiterate leaders to cope with global issues.

``It is upon UWT to make sure that its leaders are well-schooled. If we cannot invest in education in this era of science and technology, then for sure we will be left out,`` he said.

He called on UWT members to elect good leaders who would act as catalysts for development.

Kikwete lashed out at some CCM members who he said were behaving contrary to party ethics.

``There are some CCM members whose actions are contrary to what the party believes in and stands for,`` he said.

On school pregnancies, Kikwete called on the women`s wing to help the government in fighting the vice.

He said the government would continue to build hostels in public secondary schools so as to make sure that all students lived in hostels.

Earlier on, the UWT outgoing chairman Anna Abdallah alleged that some candidates were bribing voters.

Sophia Simba, who is the Minister in the President`s office (Good Governance), Janeth Kahama Special Seats MP and Joyce Masunga also Special Seats MP are contesting for the UWT`s top post.

SOURCE: Guardian
 
Waungwana,

Miye Mchungaji nimeleta hoja kufungua kesi kutokana na matumizi mabaya ya madaraka, kama vile Mramba, Mgonja na Yona wanavyokaangwa. sasa kutumia madaraka vibaya kuna kinga gani Kikatiba au kisheria?

Hilo ni moja, la pili ni la tuhuma za Ufisadi, hili ni kosa la jinai, nalo lina kinga gani Kikatiba na Kisheria?
 
Mimi naongezea tu na kifo cha Makamo wa Rais Hayati Muheshimiwa Dr Omar Juma inasadikiwa Mkapa ndie chanzo cha kifo chake naomba na hili litiwe pindipo akifikishwa mahakamani kwani kuna utata wa kifo chake.
 
• Paroko atumia misa ya kumuaga Malima kumsafisha







ORODHA ya viongozi wa dini na kisiasa wanaoonekana kukerwa na tuhuma zinazoelekezwa kwa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa zinazidi kuongezeka.

Baada ya padri mmoja wa Kanisa Katoliki wa Mtwara na mwingine wa Zanzibar kueleza dukuduku lao dhidi ya wale wanaomshambulia rais huyo mstaafu safari hii ameibuka kiongozi mwingine wa Kikristo kumtetea.

Aliyeibuka katika mwelekeo huo huo safari hii ni Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Kristo Mfalme, Tabata, Jijini Dar es Salaam, Claudio Fadhili, ambaye jana aliungana na viongozi wenzake wa Kikristo kumtetea rais huyo mstaafu.

Paroko Fadhili alitoa kauli hiyo wakati akihubiri kwenye misa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri wa gazeti la HabariLeo, Cassian Malima aliyefariki dunia katika hospitali ya Aga Khan, Ijumaa iliyopita.

Kwa mujibu wa paroko huyo, kitendo cha baadhi ya watu wakiwamo watoto wadogo kumzonga Mkapa kwa kumuita fisadi mitaani na katika maeneo mengine ni cha kutomtendea haki rais huyo mstaafu ambaye alisema wakati wa utawala wake wa miaka 10 alilifanyia taifa hili mambo mengi ya manufaa.

Akitoa mfano alisema mema mengi ya kiuchumi yakiwamo yale ya kuimarisha mfumo wa miundo mbinu ambao umeshuhudia kuwapo kwa barabara nyingi nzuri ambazo matundani yake yanawafaidisha Watanzania hadi leo hii, ni matokeo ya kazi kubwa iliyofanywa na serikali aliyoiongoza Mkapa katika kipindi cha kati ya mwaka 1995 na 2005.

Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu, wakiwamo viongozi wa serikali, vyama vya siasa, wanahabari na wananchi wa kawaida, Paroko Claudio alisema pamoja na ukweli kwamba Mkapa kama binadamu anayo mapungufu yake, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba, wakati akiingia madarakani, hali ya uchumi wa taifa ilikuwa ni mbaya, kabla ya yeye kuiongoza serikali na kuiboresha.

‘‘Hivi sasa mambo haya yamesababisha hata wenzetu wa nje waanze kutucheka na kujiuliza hivi hawa ni wale Watanzania tuliowafahamu? Nchi inaelekea kubaya, hili suala la ufisadi, mtu mzima kama rais mstaafu Mkapa anaitwa fisadi...

Tunasahau kwamba Mkapa huyu alifanya kazi kubwa kuinua uchumi wa nchi...nasikia mtu anapita barabarani hata watoto wanapiga kelele fisadi huyooo! Tunakwenda wapi kama taifa?” Alihoji paroko huyo huku akiwaomba radhi waombolezaji waliofika hapo akisema anajua kwamba hapo hapakuwa sehemu sahihi ya kufikisha ujumbe wake huo.

Huku akinukuu maandiko kutoka katika Biblia, yasemayo ‘msihukumu, msije mkahukumiwa’ paroko hoyo aliwaonya watu kuacha kuwatuhumu wenzao kwa sababu tu ya kuendekeza ubinafsi wao.

Alisema Watanzania wanapaswa kutambua kuwa, mambo ya namna hii yanaweza kusababisha amani ya nchi ikapotea na heshima ya watu ikashuka hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

“Amani ya nchi inaweza ikapotea, watu wamebaki kulaaniana, mtu akionekana ana uwezo kidogo anaitwa fisadi, watu wataogopa kujiletea maendeleo kwa kuogopa kuitwa mafisadi,” alisisitiza paroko huyo.

Kauli hiyo ya paroko imekuja siku chache tu baada ya kiongozi mwingine wa kidini wa Zanzibar, Askofu Mstaafu wa Kanisa Anglikana visiwani humo, John Ramadhani, kutoa matamshi yenye mwelekeo huo huo wa kumtetea rais huyo mstaafu.

Askofu Ramadhani katika mahubiri yake ya hivi karibuni aliyotoa katika Kanisa la Mkunazini mjini Unguja, alimuelezea rais huyo mstaafu kuwa alikuwa mmoja wa viongozi waliokuwa mstari wa mbele kuheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala bora enzi za uongozi wake.

Kiongozi mwingine ambaye naye hivi karibuni alisikika akipinga juhudi za watu kutaka Mkapa afikishwe mahakamani ni Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ambaye aliwalaumu wale wanaotaka kuondolewa kinga kwa kiongozi huyo mstaafu.

Mbatia ambaye alikuwa akifungua Mkutano Mkuu wa NCCR-Mageuzi uliomchagua kuendelea kukiongoza chama hicho kwa miaka mingine mitano, alisema hatua ya kumpandisha Mkapa kizimbani kwa makosa yoyote aliyofanya wakati akiwa madarakani kunaweza kusababisha vurugu.

Mbali ya viongozi hao wawili, kauli zenye mwelekeo huo huo zilitolewa pia na Mnajimu maarufu wa Afrika Mashariki, Sheikh Yahya Hussein ambaye alisema juhudi zozote za kujaribu kumfikisha mahakamani Mkapa haziwezi kufanikiwa kutokana na ukweli kwamba wakati wa utawala wake kiongozi huyo aliwatetea wanyonge.

Sheikh Yahya ambaye alikuwa akitoa utabiri wake wa mwaka 2009, alisema pamoja na tuhuma hizo nyingi kuelekezwa kwa Mkapa kiongozi huyo mstaafu alikuwa akitarajia kuteuliwa kuongoza moja ya taasisi muhimu kimataifa katika kipindi cha kati ya mwezi Aprili na Juni mwaka huu.

Kauli za viongozi hao zinakuja wakati kukiwa na shinikizo kutoka kwa watu mbalimbali wanaotaka Mkapa afikishwe mahakamani kujibu tuhuma mbalimbali za ufisadi ambazo ziliibuka wakati akiwa mahakamani.

Wakati kukiwa na shinikizo hilo, tayari baadhi ya wabunge akiwamo Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa, wameshaonyesha nia ya kuandaa hoja binafsi na kuiwasilisha bungeni ya kutaka Mkapa aondolewe kinga ya kisheria aliyonayo akiwa rais mstaafu.

Mbali ya wabunge hao kuonyesha nia hiyo, Spika wa Bunge, Samuel Sitta ameshapata kukaririwa zaidi ya mara moja akisema alikuwa tayari kupokea hoja binafsi yenye mwelekeo huo wa kutaka Mkapa aondolewe kinga hiyo ya kisheria ambayo inazuia kumfikisha mahakamani rais mstaafu kwa maamuzi aliyofanya wakati akitekeleza madaraka yake ya urais.

Source:Tanzania Daima
 
Tangu thread hii ianze, nimejaribu kusoma line by line kuona ni kosa gani kubwa hilo ambalo baadhi ya watu wanaling'ang'ania ili Rais Mstaafu ashitakiwe nalo, nimeshindwa kuliona (Naomba msaada kwa hilo). Kosa ambalo linaelekea kusemwa-semwa sana ni ununuzi wa mgodi wa Kiwira. Jamani, kama mnajua miiko ya uongozi, nadhani umefika wakati kuiweka hapa ili hoja ziwe na nguvu zaidi. Maana ni dhahiri kuwa Katiba imeshawashinda. Na Serikali makini haiwezi kuingia Mkenge ambao baadhi yenu mnaotaka waingie (kuvunja Katiba). Miiko ya uongozi/Maadili ya uongozi au sheria inayomnyima mtu yeyote mwenye dhamana ya Urais kufanya biashara ni ipi? Miiko ya uongozi au sheria inayomnyima kiongozi yeyote kununua mashirika, makampuni au asset yoyote inayomilikiwa na serikali (mali ambayo inatakiwa kuuzwa) ni ipi? Hivi mnajua kuwa katika bidders wa Mgodi wa Kiwira kuna alie-bid kwa shilingi moja (TZS 1/=) tu?

Nadhani umefika wakati tutafakari na kushinikiza mambo ya msingi zaidi ya kutaka kuoneana, ama kukomoana. Mzee wa watu amefanya kazi nzuri, aachwe apumzike. Urais sio kazi rahisi namna inavyofikiriwa. Anastahili kupumzika baada ya kazi nzito na nzuri kwa Taifa hili.
 
Back
Top Bottom