Kichuguu,
Mkuu tatizo la sheria sio swala la sisi kujua alivyoupata mradi wa Tanesco ama mingineyo isipokuwa inatutaka sisi kutoa ushahidi against yeye tukisha fanya uchunguzi wa njia zilizotumika..Mkapa hana haja ya kuzitoa hizo njia unless sisi tuwe na ushahidi kwanza kuthibitisha kwamba alikiuka sheria..
Sasa kama kuna mmoja wetu anazo hizo njia haramu zilizotumika nadhani itakuwa mwanzo mzuri..
Kama ningekuwa mimi na sii mwana CCM ningesema weka ndani itajulikana baadaye! lakini Kikwete sio Dikteta anatafuta haki na kuna hatari kubwa kama hatachukua hatua za Kisheria kuna watu nyuma ya huyu jamaa na wenzake wanaweza kuzua balaa ya kwa kutumia Udini, sasa hivi tu kuna watu wanaamini swala la Yona na Mramba limesababishwa na Kisasi..
tatizo wote tunajua Yona na Mramba walitumia vibaya madaraka yao na kujilimbikiza mali lakini hatuna ushahidi tosha zaidi ya kutumia hoja ya walitumia vibaya madaraka yao!..
Kichuguu,
Mkuu tunarudi kule kule kuwa katiba inamlinda Mkapa tofauti na hao kina Yona, Mramba, Karamagi na wengine...Bunge pekee ndilo linaweza kuirudisha sheria ya kuwajibisha viongozi waliotumia madaraka yao vibaya na pengine uchunguzi kufanyika zaidi ya hapo mkuu chukulia kama baba kajamba!
Kichuguu,
Mkuu tunarudi kule kule kuwa katiba inamlinda Mkapa tofauti na hao kina Yona, Mramba, Karamagi na wengine...Bunge pekee ndilo linaweza kuirudisha sheria ya kuwajibisha viongozi waliotumia madaraka yao vibaya na pengine uchunguzi kufanyika zaidi ya hapo mkuu chukulia kama baba kajamba!
Jamani si jk katika hili alishajibu kwamba hawezi kumshitaki kwa sababu nchi haitakalika? au mimi ndiye nimesahau nini?
Mkuu labda sijakuelewa.. Ni maamuzi gani alofanya Mkapa ambayo kayafanya kama Mkapa na sio rais wa Tanzania!..Mkandara, mimi sikubaliani na hili la katiba inamlinda Mkapa. Katiba inamlinda Mkapa kwa maamuzi aliyoyafanya kama Rais wa Tanzania na siyo maamuzi aliyoyafanya kama Mkapa
Bubu ataka Kusema,
Mkuu labda sijakuelewa.. Ni maamuzi gani alofanya Mkapa ambayo kayafanya kama Mkapa na sio rais wa Tanzania!..
Kwani access na nguvu ya yote aliyoyafanya na tunayodai kayafanya ni kwa sababu alikuwa rais wa Tanzania na hayapingani na Azimio la Zanzibar - Uporaji.
Na kuhusu rada mnatakiwa kuthibitisha kuwa alipewa rushwa, hapo ndipo katiba haiwezi kumlinda lakini yeye kama rais mstaafu hatakiwi kujieleza kwa mtu yeyote kabla ya mashtaka!.. Ni jukumu letu sisi kuwa na ushahidi kwanza hata kama tunajua kajamba yeye!
Mkuu bado sijakuelewa naomba ufafanuzi wa yeye kufanya maamuzi hayo kama Mkapa..Alipoamua kufanya biashara akiwa Ikulu uamuzi ule haukuwahusu Watanzania. Pia alipoamua kutupora mgodi wa Kiwira na kuwashinikiza wakuu wa TANESCO wakati ule kusaini mkataba na 'kampuni' alifanya maamuzi yale kama Mkapa na siyo kama Rais wa Tanzania.
Bubu ataka Kusema,
Mkuu labda sijakuelewa.. Ni maamuzi gani alofanya Mkapa ambayo kayafanya kama Mkapa na sio rais wa Tanzania!..
Kwani access na nguvu ya yote aliyoyafanya na tunayodai kayafanya ni kwa sababu alikuwa rais wa Tanzania na hayapingani na Azimio la Zanzibar - Uporaji.
Na kuhusu rada mnatakiwa kuthibitisha kuwa alipewa rushwa, hapo ndipo katiba haiwezi kumlinda lakini yeye kama rais mstaafu hatakiwi kujieleza kwa mtu yeyote kabla ya mashtaka!.. Ni jukumu letu sisi kuwa na ushahidi kwanza hata kama tunajua kajamba yeye!
Bubu ataka kusema,
Mkuu bado sijakuelewa naomba ufafanuzi wa yeye kufanya maamuzi hayo kama Mkapa..
1. Azimio la Zanzibar lilimruhusu kufanya biashara haikueleza kama Ikulu hapafai wala haparuhusiwi, ndio Ofisi na makazi yake kama rais na sio Mkapa..
2. Uwezo wa kupora Kiwira mtu kama Mkapa bila kuwa rais aliwezaje... na mashrti gani yalikuwepo ambayo hakuyafuata!..
I think one important thing JamiiForum is missing is the concrete plan of action. We increasingly debate without moving forward. It's time now to put our debate, analysis, perspectives, etc. into action. The constitution allows us to sue Mkapa. In the process we we be able to debate whether this man has immunity or not for the dirty he commited while in Ikulu. Kikwete could not initiate every move. We need to push him. The president needs our support now more than ever.
NGOS, MEDIA, LAYERS ASSOCIATION, OPPOSTION PARTIES, BLOGERS......LET US DO SOMETHING NOW. LET US SUE MKAPA RIGHT AWAY! YES WE CAN!
Kichuguu,
Mkuu nakueleweni nyote isipokuwa nasimama upande wa pili kuona kama sisi tunao ushahidi tosha wa kumsimamisha Mkapa mahakamani. Chukulia tu kwamba mimi ni mwajiriwa upande wa utetezi kumwakilisha Mkapa ktk hoja za hapa lakini haina maana namuunga mkono ama siamini kwamba hakuhusika na hujuma za uchumi wa nchi yetu.
Mkuu nachokiona hapa kulingana na hoja zilizotangulia ni matokeo ya kile tulichokiona Mkapa kisha simamisha. Sawa na muuza unga aliyejenga nyumba lakini hata siku moja hajakamatwa na unga.. Hiyo nyumba sio ushahidi wa kuuza unga na hata kama tukifanya uchunguzi biashara yake ya kuuza nguo za India au Pakistan inaweza kuvunja tuhuma zote halali..Kinachotakiwa ni ushahidi zaidi, uchunguzi zaidi na pengine Kikwete anayafanya haya bila wananchi kufahamu.. unajua tena FBI..
Pamoja nayote haya, hakuna hata mmoja wetu anayefahamu mali za Mkapa zilipatikana kwa njia gani zaidi ya kusema haramu.. je alifanya nini kinyume cha sheria hadi tuite haramu....No one knows!
Pili, discussion yote hii ni ktk kutafuta njia za kumshitaki Mkapa kama rais mstaafu na sio Mkapa.. Huo ndio msisitizo wangu na ndio sababu sote tumetazama katiba kama inamlinda, laa sivyo sioni sababu ya kutazama katiba ikiwa yeye ni Mkapa na binadamu kama sisi...Ndani ya katiba kuna kipengele hicho kinachomhusu rais peke yake tofauti na sheria nyingine zinazowahusu watu wote...Mimi na wewe hatuwezi kuwa impeached isipokuwa kiongozi wa nchi na sio Mkapa..sheria ipo kwa WHO is he/she hilo jina imetokea tu kuwa jina lake linaitwa Mkapa.
Viongozi wa Kiafrika ni Miungu na sheria zilizowekwa zimeambatana na Azimio linalomruhusu wala sio yeye pekee yake.. Viongozi wote wa chama wamenufaika na madaraka tuliyowakabidhi. waziri wa Utalii walifungua ofisi za Utalii, Kilimo walinunua mashamba, Afya wakafungua mahospital, Elimu wkafungua mashule lakini wote wametumia ujanja ujanja kuweza kuficha madhambi yao na kisheria inakuwa kazi sana kuwabana wote kwa sababu kwanza hilo Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu Conflict of interest..na haikuwa dhambi kama ilivyokuwa Takrima ktk uchaguzi uliopita..
Sasa ikiwa leo hii tukiondoa takrima na kuiharamisha Je, tunaweza kutumia sheria hiyo mpya kuwahukumu viongozi waliopita ktk uchaguzi wa 2005..kisheria sidhani!
Ndio maana msisitizo wangu ni kujaribu kuwaonyesha nyote kwamba kuhusiana na Mkapa tumesha liwa wakuu zangu. hakuna mtu humu JF ambaye atafurahi sana kuona Mjomba katinga Kisutu ama mahakama yoyote zaidi yangu... nina usongo na mtu yule isipokuwa nikitazama possibility kisheria sioni ndani kabisa zaidi ya kuwepo Mageuzi/Mapinduzi ya utawala...
Kikatiba, he is above the law wajomba!
Hapana Mchukia fisadi, Tanzania itakalika tu tumechoka na hawa wanaojivisha ngozi ya uongozi ili kuwafisadi Watanzania ili kukidhi uroho wao wa utajiri wa haraka haraka kupitia migongo ya Watanzania. Na Mkapa ni mmoja wa mafisadi hao ambaye inabidi sheria iachwe ifuate mkondo wake.
Tunaotaka rais Mkapa ashitakiwe tunataka haki ifanyike kwa wizi wa mali ya umma alioufanya akiwa Ikulu. Na si kwa sababu za maamuzi aliyoyafanya akiwa rais. Ukilielewa hilo utatuelewa.Kwa kweli mimi binafsi nasikitishwa sana jinsi watu makini sana hapa JF tunavyotumia muda mwingi sana hapa kumshupalia mzee Mkapa kwa makosa aliyoyafanya akiwa ikulu! hili swala la kuzungumzia kumpeleka Mkapa mahakamani halina maana kabisa, ni wendawazimu tu! hizi ni fikra hafifu kabisa ambazo ni hatari sana kwa demokrasia ya nchi, kama mkapa amefanya kosa akiwa rais, basi ni wajibu wa rais anayefuata kutengua hayo maamuzi 'mabaya' ya rais aliyetangulia na nhi ikaendelea mbele, mfano tu tunamsikia Obama akiainisha maamuzi ya rais Bush ambayo yeye atabalisha mara atakapoingia ikulu...hatumsikii Obama akisema atampeleka rais Bush mahakamani kwa maamuzi yake mabaya sana yaliyoigharimu Marekani na dunia kwa ujumla! lakini katika nchi yetu maskini kabisa, watu makini kabisa tumejisahau kabisa na kuongelea hili kama vile ndilo jambo muhimu kabisa na kusahau kwamba wananchi wetu wanazidi kuteseka na serikali yetu kwa kweli inahitaji msaada wa kifikra ya jinsi ya kumnasua mtanzania kwenye umaskini uliokithiri. whether we take Mkapa to court or not does not have effect on the livelyhood ya mtu mtu wa kawaida, lakini kama the sitting president can reverse his decisions, hiyo inaweza kusaidia jamii.
Nimesema hapo juu kwamba swala la kukimbilia kuondoa immunity ya rais mstaafu na kumpeleka ni hatari sana kwa demokrasia kwa sababu inaweza kuanzisha madikteta kwa sababu rais ataona kwamba akistaafu atashitakiwa na kusumbuliwa hivyo ni vyema apiganea abakie madarakani. Mimi nafikiri tuige wenzetu wa nchi za magharibi hususan marekani wanavyofanya, rais anayeingia madarakani aweze kutengua maamuzi ya rais aliyetangulia na kumwacha mstaafu aendelee kuishi bila bughudha. narudia tena kusema hili la kumsakama Mkapa aondolewe kinga ni sawa na 'kuuza dume kwa ajili ya kesi ya kuku'... Watanzania tuna matatizo mengi mazito kabisa yanayohitaji uchambuzi mzuri wa wana JF.