BongoTz
JF-Expert Member
- Nov 3, 2006
- 272
- 3
Sawa sawa sisi tunatuma hela tu huko vinachimbwa na pia tunatoa ajira in process kwa wachimbaji, hilo halina tatizo wewe endelea tu!
Now we're in the same page, Marshall.
Sawa sawa sisi tunatuma hela tu huko vinachimbwa na pia tunatoa ajira in process kwa wachimbaji, hilo halina tatizo wewe endelea tu!
...Ni muhimu sana tuangalie tulikotoka na kuweka record ya kila makosa yaliyotangulia..
Leo hii ukiwauliza viongozi wetu wengi tu kuhusiana na kubinafsisha - Ni wapi tulikosea hata Mkapa mwenyewe hawezi kukubali yalikuwa makosa pamoja na kwamba mashirika karibu yote yaliyobinafsishwa yamebwaya ktk utoaji huduma...Haiwezekani makosa ni mfumo wa kubinafsishwa hata kidogo kwani zipo nchi kibao zimefanya hivyo na wamefanikiwa..Je, sisi tulikosea wapi?.. hamtaki kutazama kabisa...
BongoTz BongoTz has no status.
Member Join Date: Fri Nov 2006
Re: Mkapa ni mtu safi... Period!
Kuna mengi yamesemwa/andikwa kuhusu Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa: "Oh, mkapa ni fisadi," "Mkapa alitumia madaraka ya Urais vibaya," "Mkapa ajitete mbele ya umma," "Blah... blah... blah..."
Lakini ukweli ni kwamba: ni Mzee Ben, na sio Mzee ruksa, wala this Kikwete guy, ambaye ameifanyia nchi hii mema na mazuri. Ikumbukwe kuwa baada ya uchaguzi mkuu wa 1995, Mkapa alipokea nchi iliyokuwa katika hali mbaya kupindukia.
Rushwa ilikuwa imekithiri. Pato la taifa lilikuwa chini. Ukwepaji kodi ulikuwa katika kiwango cha kuogofya. Na miundo mbinu ilikuwa imechoka kupindukia.
Ni chini ya utawala wa mzee Ben ndipo watanzania kwa mara ya kwanza tulipoanza kuona sera ya taifa kuhusu uchumi ikipewa kipaumbele. Miundo mbinu ikiboreshwa. Pato la taifa likikua. Na kamba dhidi ya vita ya rushwa ikikazwa.
Lakini pia katika viongozi tuliowahi kuwapata, ukimuacha Mwalimu, ni Mkapa peke yake aliyekuwa na ubavu wa kupinga kuendeshwa na nchi za Magharibi. Mwinyi alikuwa anajikojolea wahisani wakikohoa, Kikwete (sote tumeshuhudia) anacheza samba kila mara nchi za magharibi zikimuamuru afanye hivyo.
Yes, kuna mabaya amabayo Mkapa ameyafanya ktk kipindi cha miaka 10 akiwa ikulu: (1) mikataba mibaya hususani madini (ambayo hata hivyo ni mwanasheria mkuu ndiye anapaswa kulaumiwa);(2) kumuachia mke wake a-dictate badhi ya shughuli za kiserikali ( one of his weakness). (3) kujihusisha na bishara akiwa ikulu (which is a minor thing)...
Cha msingi hapa ni kujua kuwa Mkapa sio Malaika bali mwandamu. na kama mwadamu, naye pia anahadawa na tamaa ya kuwa na maisha yaliyotulia. You know, financial security and all those things, kwa ki-inglish.
Hitimisho: Hapa suala ni kwamba, Kikwete and his inner circle wameshaona kuwa wamechemsha big time, hivyo wanachokifanya ni kumchafulia mzee Ben jina ili watu wasipate fursa ya ku-compare utawala wake (mtalii Kikwete) na ule wa mzee Ben (mtu safi).
1. Ni nani serikalini aliyeamua mgodi wa Kiwira uuzwe? Kama kuna kikao chochote cha baraza la mawaziri kilichokaa ili kuamua mgodi wa Kiwira uuzwe basi tungepata kujua ni mawaziri gani waliohudhuria kikao hicho, kilifanyika tarehe gani na wapi.
2. Ni nani aliyefanya tathmini na kuamua kwamba mgodi wa Kiwira ulikuwa katika hali mbaya (pathetic condition) na hakuna chochote kiliachoweza kufanywa na serikali ili kubadilisha hali hiyo.
3. Hayo "madeni mengi mno" yaliyokuwepo katika mgodi wa Kiwira yalisababishwa na nini? mishahara ya wafanyakazi? kuchimbua makaa ya mawe toka mgodini? Tunataka maelezo ya kina na tuambiwe deni hilo lilikuwa ni kiasi gani na nani amelilipa deni hilo (Tuna wasi wasi kwamba deni hilo lilipwa na serikali kabla ya mafisadi Mkapa na mwenzie kujimilikisha mgodi huo)
4. Je, kuna zabuni yoyote iliyotangazwa katika magazeti mbali mbali ya Tanzania kwamba serikali iliamua kuuza mgodi huo? ilitangazwa tarehe zipi na katika magazeti gani? Na kama zabuni haikutangazwa basi tupewe sababu za msingi kwa nini zabuni ya kuuzwa Kiwira haikutangazwa hadharani.
5. Kama zabuni ilitangazwa tungependa kujua kamati ya wajumbe wa kuzitathmini zabuni mbali mbali zilizotumwa na waombaji ilikuwa na watu wangapi na tungependa majina yao yatangazwe hadharani.
6. Ni lini kamati ya kutathmini zabuni hizo ilikaa na kuammua kwamba zabuni kutoka kwa mafisadi Mkapa na Yona ndiyo ilyoshinda? Pia tungependa kujua hao waombaji wengine walikuwa tayari kuununua mgodi wa Kiwira kwa kiasi gani?
7.Ni wajumbe gani toka TANESCO, Wizara ya Nishati na Ikulu walikuwemo katika kuujadili mkataba uliosainiwa kati ya TANESCO na Kiwira wa shilingi 326 billioni? Tungependa tupatiwe majina na nyadhiza zao.
- na ni chini ya utawala wa Mkapa ndipo wizi mkubwa kabisa katika Benki Kuu umetokea!
- Ni chini ya Mkapa Usalama wa Taifa was compromised kwa kubadilisha sheria ya usalama na kuunda picha ya kitu kinachoitwa Usalama wa Taifa na hivyo kuruhusu wezi kuingia hadi jikoni kuiba huku picha hiyo ikiwa imesimama mlangoni!
- Ni chini ya Mkapa Sheria mbovu ya Madini ya 1998 imeandikwa ambayo ilifungua mlango kwa upotevu wa mabilioni ya shilingi katika sekta hii muhimu kwa uchumi.
- Ni chini ya Mkapa sheria mbili za fedha zenye mambo ya ajabu ziliandikwa 2001, 2004 ambazo pamoja na sheria nyingine ziligeuza tanzania kuwa kisima cha uchotaji wa fedha na kuzirusha nje.
- Ni chini ya Mkapa makampuni feki yaliyoundwa na kuchota fedha za umma ikiwemo Meremeta yalipoundwa na yeye mwenyewe akiwa ni mmoja wa watu waliojua nini kinaendelea!
- Ni chini ya Mkapa kwa mara ya kwanza Rais wetu alitumia nafasi yake kuingia kwenye ubia na taasisi iliyo chini na hivyo kuvunja sheria ya maadili ya viongozi - na hili si dogo, ni kubwa mno! Nchi nyingine rais anaondolewa na Bunge!
- Ni yeye aliyemteua Mwanasheria Mkuu mbovu kabisa katika historia ya Tanzania huru
Hitimisho:
Mkapa alifanya aliyoyafanya na katika aliyoyafanya aliyoyafanya kwa kuyafanya vibaya kabisa ni yale aliyoyafanya ambayo hataki kuyazungumzia kuwa aliyafanya!
Nilipoandika hii thread couple of weeks ago, boy, kidogo tu watu wangenimwagia mafuta. Lakini nimefarijika kusikia kuwa wahisani wa nje nao wameliona hili na kuamua kukubaliana na mimi: Mkapa is arguably one of the finest Presidents Tanzania has ever produced.