Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mimi nataka kutoa credit kwa Mkapa. Naomba mniambie mambo aliyoyafanya ambayo hayakuwa sehemu ya wajibu wake na kazi yake aliyoombea kura. Ni yeye aliyepita mara mbili kwa wananchi akiomba kura ili apewe nafasi ya kuongoza nchi yetu na mara zote wanananchi wakamuamini, na akaenda kufanya mambo ambayo alitakiwa kufanya.

Sasa ni yapi ambayo aliyafanya nje ya wajibu wake na kazi yake ili tumpe sifa?

vinginevyo, kila mtu anayefanya kazi yake aliyoajiriwa kufanya anahitaji kupewa sifa?

BongoTZ naomba uniambie tu kwa maneno mepesi (unaweza kuoutline) ni nani alichofanya ambacho anastahili credit, kitu ambacho hakikuwa sehemu ya kazi yake?

at least tunakaribia kuelewana jambo moja..kuwa...mkapa alifanya kazi ...ila unasema hastahili pongezi kwa kuwa ni wajibu wake...lakini hapo hapo ujuwe kuwa ukimpa mtu kazi unao wajibu wa kusifu pale katika yale anayofanya vema...kama vile utakavyomponda kwa yale anayokosea..

what we want is the balanced traetment.....sio kupinga tu..
 
Sioni credit yoyote ya kumpa Fisadi Mkapa, ndiyo aliongeza makusanyo ya mapato kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na wakati Mwalimu Nyerere au Mwinyi Mzee wa Rukhsa walipokuwa madarakani. Je, makusanyo hayo makubwa ya kodi yalisaidiaje kuinua viwango vya maisha ya Watanzania kwa ujumla.

Je, mahospitali yetu yalipatiwa vitanda na vifaa vingine muhimu? Je, mashule yatu yalipatiwa madarasa yenye hadhi na madawati kwa wanafunzi? Je, ajira kwa Watanzania ziliongezeka au mishahara iliongezeka kutokana na ongezeko hilo la makusanyo ya mapato? na maswali mengine chungu nzima.

Na majibu ya maswali hayo yote ni HAPANA. Hivyo hastahili kupewa credit yoyote labda na WB na IMF ambao takwimu zao zilikuwa zinaonyesha uchumi wa Tanzania ulikuwa kati ya asilimia 4 mpaka 6 kila mwaka wakati fisadi alipokuwa madarakani, lakini ukweli unabaki kwamba Watanzania walio wengi hawakuona ahueni yoyote kiuchumi wakati alipokuwa madarakani.
 
Phillemon mikael,
Jamani hivi lini tutakuja tumia vizuri neno hili credit!..
Pundit kesha waeleza vizuri kabisa kuwa mabaya ni 10 (-) na hayo mazuri ni 5...umebaki na kitu gani?..
Hata yule mtu alokaa mtihani akaambiawa ame fail mtihani haina maana kakosa maswali yote!.. Labda niuweke kiutalawa ni kwamba huyo Mkapa ktk kundi la D na F...
Na tatizo lako kubwa ni pale uliposhindwa kuelewa kwamba viongozi bora wapo nchi zote duniani na kuiwa kwetui nje inasaidia kuweza kuona nini maendeleo...
Labda mwenzetu mwepesi wa Kusahau kwamba ktk kipindi cha Mkapa umeme ulikatika kabisa, Reli ya kati ilisimama kabisa, shirika la ndege lilikufa kabisa, Maji yalikuwa hayapatikani kirahisi mji wote wa Dar...
Mkuu biula vitu hivyo kweli unaweza kuhesabu mafanikio ama unachukua mafanikio kwa kutazama hali halisi yaani Mkapa ameweza kufanya nini baada ya kuua miundombinu yote!... sii rahisi kabisa nchi kuwa bado ina amani ktk hali hiyo, hivyo labda tuzungumzie kipande hicho cha kushangaza!
 
Wakulu wananchi wengi wanapotea na kushindwa kujua Mkapa ni fisadi kwasababu hatukupata habari zake kwa uhuru alipokuwa madarakani, lakini kingine alijitahidi sana kuhakikisha anakoroma kwa nguvu anapoona mambo yanataka kwenda mrama kidogo. Kwa akili yangu nakumbuka hata viongozi waliokuwa sambamba na yeye waligeuka wababe kwa mambo mengi, mojawapo ni Mahita aliyegeuka kuwa mbabe hata kwa askari wenzake. Pia Mkapa aliiba baada ya kubadili kidogo hali iliyokuwepo baada ya Mzee Ruksa kuondoka na kuacha rasilimali zetu nyingi zikiwa bado intact. Mkapa alivyokuja akaleta sera nyingi za kula na mojawapo ilikuwa ni ubinafsishaji, hapa ndio nchi yetu ilianza kupataniwa bei na wageni. Kikwete alipopokea aligonga msumari kwa kusema Mkapa aliweka msingi safi sana, sasa sisi ni kuendeleza tu.... IMEKUWAJE? Mkapa sio kama tulivyokuwa tunamwona, alikula zake za kutosha na alikoroma tusijue.
 
Rais aliyetuletea kina Rostam na Lowassa, eti akumbukwe kwa mazuri? Hapa ndio ninazimia na sisi wabongo!

..mukulu..historiua inaonesha wazi kuwa..rostam pekee ndiye
alianza kujulikana kisiasa kwenye KAMPENI YA MKAPA 1995..akiwa moja ya mjumbe wa ile timu along na kina warioba ,generali ulimwemgu twaha,ets.....

huyu lowassa aliiinuliwa na MALKECELA...kikwete alikutwa na WARIOBA mtwara na lindi ..akiwa waziri mkuu wakati wa yale mafuriko ...alimkuta kule ni katibu wa ccm wilaya ..newala,alipomueleza mzee MWINYI ndio aliyeamua kumuinua na kumchagua mbunge wa viti maalumu na naibu waziri wa nishati chini ya AL NUR KASSAM[enzi hizo akiwa MAJOR JAKAYA MRISHO KIKWETE]

KWA KIFUPI LOWASSA NA ROSTAM ...ndio waliombeba kikwete zaidi mbele....kwani hata ule uchaguzi wa 1995 waliolishana yamini KIKWETE ALIJUA NI MSINDIKIZAJI TU...HAKUWA NA UMAARUFU...UMAARUFU ALIUPATA GHAFLA BAAADA YA LOWASSA KUPIGWA FYEKEO NA NGUVU ZOTE ZA VIJANA KUHAMISHIWA KWAKE...AMBAZO BAADAYE ZILIWASABABISHIA MAJERAHA SUKWA SAID SUKWA..NA ...JOHN JOHN GUNINITA....

stand to be corrected!!
 
Katika Sheria kuna Fundamental mistakes na Warranty, sasa kwenye mkataba kukiwa na fundamental mistake then mkataba ni batili, lakini kosa likiwa Dogo, then issue ya kufanya ni kurekebisha hilo tatizo, na mkataba unaendelea. Basing on those fact, ningependa kusema mkapa alifanya Fundamental mistakes katika uongozi wake , hivyo inapelekea uongozi wake kuwa mbovu, kama Pundit alivyosema -10 + 5 = -5.
Hizo Fundamental mistakes alizo fanya ni
1. Kulazimisha Net group kuingia Tanesco, na matokeo yake tumeyaona.
2 Suala la Radar , ambayo ilipingwa na wataalam including ICAO
3Kuuza Nyumba za Serekali kwa kisingizio kwamba anataka kusaidia wafanyakazi, wakati hatua hiyo ni short term, kwa sababu, je wafanyakazi wanaojiriwa sasa wata pata wapi nyumba zao Binafsi?
Kwa sababu alikuwa anatakiwa kuweka mradi endelevu nao ni kuanzisha kwa Mortagage Finance.
4 Reli waliuwa kwa maksudi ili waweze ku-justify ubinafsishaji. na zaidi ya hapo huo ubinafsishaji utahusisha capital flight, na kuwa hostage wa muwekezaji. na kama tukitaka kujitoa itakuwa kama ilivyo kuwa iptl , kwamba ukivunja mkataba pay iptl 100 million usd.
5. kutokuwa na policy endelevu ya uzalishaji wa umeme.
6. kuiuwa atc , kwa kuingia mkataba mbovu na sa, na hapo ni baada ya kuwa tulipata kuanzisha alliance na sa ambayo ilikufa, wakati wa Alhaji Ali Hassan.
Kuingia mikataba mibovu ya madini, matokeo yake TBL wanalipa kodi kubwa kuliko kwenye Madini, then kulikuwa hakuna haja ya kuyachimba hayo madini.
na zaidi ya hapo akielezwa mzee hapo unaingia shimoni, anakuwa mbogo, so alikuwa anaelewa kabisa kwamba anatupeleka shimo, lakini madhali yeye ni raisi au anafaidika na hilo jambo then it was right for us kuingia humo shimoni.
 
You know I posted this thread to test and see how smart or foolish Tanzanians really are, and most of you (indeed) have proved to be the latter.

Foolish people.

Acheni kukaririshwa mambo na inner circle wa Kikwete hapa!

Be smart people
.

Ndugu acha jazba huo ndo ukweli wenyewe: Ukimweka Mkapa kwenye mizani kuhusu utendaji wake utaona unalemea negatively. Kuhusu mazuri aliyoyafanya ni vema ujue hakuwa akitulipa Watanzania fadhila yoyote bali alitimiza wajibu wake kwa yale tuliyomtuma na kumpa kazi tukufu pale Ikulu. Tujiulize Ndugu Bongo, Je, Mkapa alifanya zaidi ya yale tuliyomtarajia kufanya au alifanya kwa kiwango cha chini? Jibu unalo mwenyewe- Mkuu Mkapa alikuwa busy na deals zake na inner circle wake;

Mkapa ndo aliyeweka misingi ya ufisadi nchini mwetu- He is a father of corruption na mambo yanayotokea sasa ni matunda tu ya misingi ya ufisadi ya aliyoiweka Mkapa!

Hatuna haja ya kumzunguzia Kikwete hapa na inner circles wake, kinachoonekana hapa ni mgawanyiko wa hao inner circles wa Mkapa, Kikwete akiwa mmoja wao kwa hiyo suala la kukaririshwa mambo na inner circles wa Kikwete hapa hakuna maana kama wapo hao inner cirlcle wa Kikwete basi wao ni Pionneers tu wa Misingi ya Ufisadi iliyowekwa na Mkapa mwenyewe na kwa hali ilivyo Kikwete aliwadanganya Watanzania tu kwa kauli tamu na ndoto za mchana-hajafanya kitu na hatafanya kitu.

Tujiulize- Hivi waweza kujenga jengo kubwa la ghorofa kwenye msingi mbovu? La, haiwezekani. Nionavyo mimi WaTz tuna kazi ngumu sana na kubwa, anachofanya Kikwete ni kuziba nyufa tu katika msingi uliojengwa na Mkapa kwa hiyo ujenzi wa Taifa letu hausongi mbele. Kikwete anajua wazi kuwa kauli na ahadi zake zote haitekelezeki kwa hiyo kinachofanywa na hao inner circle wa JK (kama wapo) ni kutuangaliza WaTz nyuma ili tumtupie lawama Mkapa kwa haya yanayotokea sasa lakini hata wenyewe hawataepuka lawama kutoka kwetu maana tunawataka nao watimize sehemu yao na tutawahukumu.
 
Rais aliyetuletea kina Rostam na Lowassa, eti akumbukwe kwa mazuri? Hapa ndio ninazimia na sisi wabongo!

Hapo sasa!! Ukweli ni kwamba bila Kikwete kuwabeba, Lowasa na Rostam wasingekuwepo kwenye duru za kisiasa za Tanzania. Watanzania wengi wanaopienda nchi na kumtakia mema Kikwete walimshauri na hata kumkemea asimteue Lowasa kuwa waziri mkuu, akawadharau, halafu leo kuna watu wanataka tumsifie JK kwa kujiuzulu kwa Lowasa, mtu ambaye hakupaswa kupewa hiyo nafasi in the first place?!

Tatizo letu watanzania tuna tabia ya kuchangamkia matokeo ya tatizo badala kuangalia chanzo cha tatizo lenyewe, ndiyo hawa jamaa wataendelea kutuchezea hadi kesho.
 
KWA KIFUPI LOWASSA NA ROSTAM ...ndio waliombeba kikwete zaidi mbele....kwani hata ule uchaguzi wa 1995 waliolishana yamini KIKWETE ALIJUA NI MSINDIKIZAJI TU...HAKUWA NA UMAARUFU...UMAARUFU ALIUPATA GHAFLA BAAADA YA LOWASSA KUPIGWA FYEKEO NA NGUVU ZOTE ZA VIJANA KUHAMISHIWA KWAKE...AMBAZO BAADAYE ZILIWASABABISHIA MAJERAHA SUKWA SAID SUKWA..NA ...JOHN JOHN GUNINITA....

Hii ni kawaida kabisa kwenye siasa. Lakini hakuna aliyemlazimisha Kikwete kumteua Lowasa kuwa waziri mkuu huku akijua atakuja kuwa mzigo kwenye utawala wake.
 
Hii ni kawaida kabisa kwenye siasa. Lakini hakuna aliyemlazimisha Kikwete kumteua Lowasa kuwa waziri mkuu huku akijua atakuja kuwa mzigo kwenye utawala wake.

Kikwete mwenyewe tayari ni mzigo kwa watanzania. Pinda ambaye amemrithi mzigo Lowasa naye anaonekana kuwa mzigo mwingine. Sasa ch kufanya ni kuitupa chini mzigo yote then tuanze upya!!!!
 
sawa hawafai sasa nani anafaa? mwingine ndo kishavuta 3m hata ikulu hajafika! yule nae kajaza mashemeji kwenye chama hadi tatoo kaamua kulala mbele, yule ustaadhi alienda yuno kwa mbwembwe mara karudi shuta kilichomtoa huko siri yake.
 
Nafikiri tukiongea kiutafiti huwezi kusema kuwa Mkapa hakufanya kazi,katika kipindi chake shillingi ilistabilize kuliko wakati mwingine wowote.Ikumbukwe kuwa alichukua nchi wakati inflation iko double digits.Kuna mambo kama ya MMEM,MES kwa upande wa Elimu kama wewe ni mfuatiliaji wa maswala ya elimu utabaini hiyo ilikuwa a good initiative.Barabara zilijengwa tuu hasa njia ya kati ambayo kwa sasa imesimama na mengine mengi tuu.Hao waliovunja mkataba wa ATC wameleta nini?habari zilizopo hata mafuta ya kurusha ndege hakuna, kukodi ndege mbovu n.k. Ni kweli kuna mambo aliyovurunda kama wengine waliomtangulia lakini hatuwezi kuacha kumpa credit ingawa bwana Pundit anajaribu kutumia standard one mathematical analysis,i beg to differ.
 
hiyo yote ilikuwa miradi ya world bank, imf na other international donors ikiwa ni masharti ya kufutiwa madeni, sio intiative zake, alipopewa kufanya intiative zake ni madudu matupu, ndio hiyo radar, ndege ya raisi, net group, madini ya dhahabu, tanzanite, almasi, kiwira , na mengineyo sasa sijui huyu utamwita kiongozi mzuri au apewe credit.
eg ndogo tu ya tanzanite, kwa nini soko lake lisingekuwa hapa hapa tanzania kwamba inakatwa na kusafishwa hapa na kuuzwa hapa hapa, pili kuweza kukusanya madeni, ya tanesco ni kuweka luku sehemu ambazo wadeni wengi ni sugu, na kwa ofisi za serekali wangeweza ku-complement umeme wao kwa kuweka solar power angalau kuwasha taa (Bulb).
Kuhusu nyumba za Serekali, hiyo Building Agency ingepewa Mkopo hata na World Bank wakabomoa Nyumba za Zamani na Kujenga Nyingi zaidi katika hayo hayo maeneo, kuzipangisha, whether ni kwa wafanyakazi wa serekali au watu Binafsi or let say priority one wafanyakazi wa serekali, askikosekana mtu yoyote mwenye pesa yake kwa mkataba maalumu.
Hiyo ndio inaitwa miradi endelevu , wenye kuweza kujiendesha wenyewe na kujiongezea thamani, kinyume cha hapo ni ujinga , ujinga, ujinga.
ATc yaani tumeshindwa kuwa na wafanyakazi wachache na dedicated na kuweza kufanya kasafari kamoja ka kuja ulaya atleast hadi London then watu wanapata connection zingine, kama amsterdam , geneva , bonn, etc etc, maana national airline ni pride of the nation na means of advertisement. sio SAA, ni ujinga ujinga ujinga. tena uliotukuka
 
Kikwete mwenyewe tayari ni mzigo kwa watanzania. Pinda ambaye amemrithi mzigo Lowasa naye anaonekana kuwa mzigo mwingine. Sasa ch kufanya ni kuitupa chini mzigo yote then tuanze upya!!!!

He he he!! kwi kwi kwi! Very smart move zero. I really like your idea (a lot)! And from this day on: You shall be called no more zero, but one.

Hasta la vista, Kikwete, Pinda, Membe, and...( that other guy)
 
Mimi nataka kutoa credit kwa Mkapa. Naomba mniambie mambo aliyoyafanya ambayo hayakuwa sehemu ya wajibu wake na kazi yake aliyoombea kura. Ni yeye aliyepita mara mbili kwa wananchi akiomba kura ili apewe nafasi ya kuongoza nchi yetu na mara zote wanananchi wakamuamini, na akaenda kufanya mambo ambayo alitakiwa kufanya.

Sasa ni yapi ambayo aliyafanya nje ya wajibu wake na kazi yake ili tumpe sifa?

vinginevyo, kila mtu anayefanya kazi yake aliyoajiriwa kufanya anahitaji kupewa sifa?

BongoTZ naomba uniambie tu kwa maneno mepesi (unaweza kuoutline) ni nani alichofanya ambacho anastahili credit, kitu ambacho hakikuwa sehemu ya kazi yake?

Mwanakijiji, I think ukisoma vizuri nimeainisha kwenye thread baadhi ya mambo aliyofanya Mkapa japo ilikuwa kwa kifupi (rejea thread). And yes, nakubaliana na wewe kuwa ilikuwa ni wajibu wake kufanya hayo mambo yote. Ila pia kumbuka kuwa (rejea thread) nimeanisha hali halisi ya nchi aliyoipokea toka kwa mzee Ruksa coupled na uharibifu uliokuwa umefanywa na mzee Mchonga na sera zake za ujamaa, conditions alizokuwa amewekea na shirika la fedha dunia/nchi wahisani (ulipaji madeni n.k), pamoja na terrible supporting casts waliokuwa wamemzunguka ( ambao ndio waliokuwepokipindi hicho na hata sasa hivi bado ndio waliopo bado/mzunguka Kikwete) . Ambao, in all fairness, Mkapa mwenye (one guy) asingeweza kuwa-monitor wote at once—kiasi cha kupelekea watu waliokuwa wamehadawa na tamaa zao (waliomuona mkapa anajaribu kurejesha nidhamu kazini na kuchonga dira ya uwazi ndani ya serikali) kuanza kuiba haraka haraka ili wapate chao mapema kabla screw haijawa tighten up zaidi (Balali and all other guys/mafisadi, hili unafahamu mkuu).

Ukichukua yote hayo, kisha ukalinganisha na kile alichokifanya Mkapa ndani ya kipindi cha miaka kumi (japo ilikuwa ni wajibu wake), utaona kuwa Mkapa alijitahidi and he deserves some credit.

P.S. ukitaka maelezo zaidi: nipatie email yako nitakutumia maelezo kwa kirefu. Maana hapa JR naingia time ambayo niko break, na sitapata muda mzuri wa kukuelezea mazuri yote aliyoyafanya Mkapa kwa muda mchache ninaokuwa nao (esp. hapa). As matter of fact, I know for sure kuwa for a smart guy like you utakuwa unajua already mema na mazuri ambayo Mkapa ameyafanya na sioni kama nitakuwa na magic language ya kuku-pursuade kama mpaka sasa hivi bado uko skeptical na kila kilichoandikwa humu.
 
Mkapa may deserve some credit as some of you his supporters claim here, except for one big cloud: ufisadi. That will be Mkapa's tombstone whatever good he may have done in his 10 years in power. History is always never kind to these kinds of people.
 
Pease know that I'm not your enemy. I'm one of you in this battle against ufisadi. All I was trying to do is to stir a honest conversation about this whole ufisadi thing. Coz I personaly feel that mzee Ben is being mistreated here. so when I used the term "foolish" yeasterday, it was not my intention to offend/mock anyone. I wish if only I had chosen the right word—and I apologize for that.

I'd have also to say that since the very first day I joined this forum (JF), I have read tons of convincing arguments from different smart people whom I have yet had a chance to shake hands with (maybe someday I will). So I respect you all.

And having said that, I still hold to the belief that "Mkapa ni mtu safi."

Thanks.

Bongotz,

Hongera sana kwa kuomba msamaha. Umeonesha uungwana wa hali ya juu kwa vile ni wachache sana kati yetu huwa wanaomba msamaha wakigundua wamekosea.

Issue ya Mkapa ni ngumu sana ukichukulia yanayoendelea sasa hivi Tanzania. Wanasiasa wengi sana huwa wakifanya makosa yoyote yale kiutendaji au kwa mambo binafsi, mambo yao mazuri huwa yanasahauliwa haraka sana - Mfano mkubwa ni Tony Blair. Binafsi nisingepoteza sana muda wangu kumlaumu au kumsifia Mkapa maana sioni kama hiyo itasaidia chochote kinachoendelea sasa hivi Tanzania.
 
Jamani turudi nyuma kabla hatujalaumu mtu yeyote...
Lowassa kabla ya Kikwete kuchukua Urais

1. LOWASSA served as Minister of State in the Prime Minister's Office during President Ali Hassan Mwinyi's second term. He unsuccessfully sought the nomination of Chama cha Mapinduzi (CCM) as its presidential candidate in 1995 and was then a backbencher in Parliament until he was appointed Minister for State, Vice President's Office - Environment & Poverty in 1997. Following the Tanzanian general election, 2000 he was appointed Minister of Water and Livestock Development. He gained a high profile as a minister of Water and Livestock Development..

2. Rostam Aziz... He was CCM treasurer since 2005 mwezi sina hakika! lakini kabla ya Uchaguzi 2005, record zote zinazohusiana na Rostam kuwa tresurer CCM wakati wa Mkapa zimefutwa kutokana na tuhuma za EPA. Kama mtakumbuka kuna siku kabla ya uchaguzi wakati Mzee Es alipotupa habari za Rostam niliingia ktk website ya CCM na kuona kuwa Rostam alikuwa treasurer nikatoa hata link, lakini leo hii huwezi kuipata wala ku access record ile.
Habari za kuaminika ni kwamba bibie Marehemu Salome Mbatia ambaye alikuwa treasurer kabla ya Rostam alikuwa njiani kukana ukweli kuwa yeye ndiye alihusika na ukwapuaji wa fedha za EPA kama treasurer wa chama during Campaining for KiKwete...Kabla hajafanya hivyo -Hatunaye tena! - Mungu amlaze mahala pema peponi!...
Sasa iwe vyovyote vile ukweli ni kwamba Rostam alikuwepo madarakani CCM toka wakati wa Mkapa..Nina hakika kabisa kwa haya ninayoyasema...
Jamani mwee Mkapa na Kikwete lao moja kama........, lakini tunachojaribu kuangalia hapa ni Mkapa Mwenyewe.. Je alikuwa kiongozi bora?...Jibu ni hapana! nani alikuwa nani haiwezi kusaidia kitu wala kumwondoa mtu katika Ubaya...Hapa anazungumziwa Mkapa mkitaka kuzungumzia Kikwete ipo mada yake na Mzee Es kashika mkoba huko!
 
Back
Top Bottom