Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mwanakijiji, I think ukisoma vizuri nimeainisha kwenye thread baadhi ya mambo aliyofanya Mkapa japo ilikuwa kwa kifupi (rejea thread). And yes, nakubaliana na wewe kuwa ilikuwa ni wajibu wake kufanya hayo mambo yote........

......in all fairness, Mkapa mwenye (one guy) asingeweza kuwa-monitor wote at once-kiasi cha kupelekea watu waliokuwa wamehadawa na tamaa zao (waliomuona mkapa anajaribu kurejesha nidhamu kazini na kuchonga dira ya uwazi ndani ya serikali) kuanza kuiba haraka haraka ili wapate chao mapema kabla screw haijawa tighten up zaidi (Balali and all other guys/mafisadi, hili unafahamu mkuu).......

Ukichukua yote hayo, kisha ukalinganisha na kile alichokifanya Mkapa ndani ya kipindi cha miaka kumi (japo ilikuwa ni wajibu wake), utaona kuwa Mkapa alijitahidi and he deserves some credit.
Ni vigumu kuamini kuwa mtu yeyote anayeweza kunena haya uliyonena ni mtanzania aliyekuwa akiishi nchini katika kipindi hicho cha usultani wa BMW. Nimepitia thread zote humu kwa mara ya pili na sijamwona mchangiaji hata moja anayekataa kuwa BMW hakufanya lolote zuri. Lakini tukiweka kwenye mizani mazuri ambayo alituahidi wakati akiomba kura zetu na hivyo kuwa wajibu wake na mabaya aliyojitumbukiza kuyafanya nje ya wajibu wake, there is no way we can give him a pass, period.

Kwenye hii mada hatujaribu kumlinganisha na mtu mwingine yeyote yule. Tunachopima ni utendaji wake baada ya kupata ridhaa ya wananchi awaongoze kuelekea neema. Mengi tu yametajwa humu na ukiweza tu kuvua hiyo miwani inayokufanya uone pumba ni machele utakubaliana na wengi hapa JF. Kwanza jiulize, kwa nini tumchukie BMW - wengine all we know about him ni kuwa alikuwa Raisi aliyeua tumaini la watanzania na ambaye athari za maamuzi yake mengine tutaishi nayo kwa muda mrefu.

Wengi wa hao unaowataja ni watu ambao walikuwa pamoja naye katika kipindi chote alichokuwa madarakani. Kuna hizi jitihada za kujaribu kutenganisha ofisi ya raisi na serikali hasa pale mambo yanapokwenda mrama lakini watendaji hao hao wanapowajibika ipasavyo, sifa zote zinamwendea huyo Raisi. Hakuna ujuha unaozidi huu na ukweli ni kuwa THE BUCK STOPS WITH THE PRESIDENT. Wateteaji wa UFISADI wa BMW wasitafute mabangusilo, aliyemwangusha BMW ni yeye mwenyewe na tamaa zake za KIFISADI.
 
Bongotz,

Hongera sana kwa kuomba msamaha. Umeonesha uungwana wa hali ya juu kwa vile ni wachache sana kati yetu huwa wanaomba msamaha wakigundua wamekosea.

Issue ya Mkapa ni ngumu sana ukichukulia yanayoendelea sasa hivi Tanzania. Wanasiasa wengi sana huwa wakifanya makosa yoyote yale kiutendaji au kwa mambo binafsi, mambo yao mazuri huwa yanasahauliwa haraka sana - Mfano mkubwa ni Tony Blair. Binafsi nisingepoteza sana muda wangu kumlaumu au kumsifia Mkapa maana sioni kama hiyo itasaidia chochote kinachoendelea sasa hivi Tanzania.

Oh, thanks kijana...

Ni kweli: at some point,we need to come to our sense and realize that no matter how fiercely we can debate hapa JR either kwa kumlaumu au kumsifia Mkapa, Kikwete, and those other guys, bado hali ya uchumi nchini itazidi tu-tank, na hali za wananchi wa kawaida itaendelea kuwa mbaya zaidi endapo kama sensible & decisive actions hazitachukuliwa mapema(nasi/wadau tulio na uchungu na motherland).

As a matter of cats, nimeamua kuwa badala ya kuendelea ku-debate hapa JR usiku na mchana (mpaka mishipa ya damu inanisimama), ni vema nianze ku-mobilize watu, tukusanye pesa, then tuanze kuchimba visima vya maji safi mikoani.

As the old saying goes, "words without action mean nothing no matter how you might want to embroider them."
 
Pamoja na kurasa zote hizi 26 hadi hivi sasa haujatolewa ushahidi wowote wa kisayansi kuonesha kuwa moja, Tanzania ilikuwa nafuu zaidi kiuchumi chini ya utawala wa Mkapa kuliko awamu mbili zilizomtangulia, b. Kwamba maisha ya Watanzania yalikuwa bora zaidi wakati wa Mkapa kuliko wakati mwingine wowote, na tatu, kwamba katika yote Mkapa alibakia msafi.

Kilichotolewa ni maneno ya fallacy of pseudoobviousness.. as my philosophy professor used to call it.. Ms. Alice Von Hilderbrand..
 
Oh, thanks kijana...

Ni kweli: at some point,we need to come to our sense and realize that no matter how fiercely we can debate hapa JR either kwa kumlaumu au kumsifia Mkapa, Kikwete, and those other guys, bado hali ya uchumi nchini itazidi tu-tank, na hali za wananchi wa kawaida itaendelea kuwa mbaya zaidi endapo kama sensible & decisive actions hazitachukuliwa mapema(nasi/wadau tulio na uchungu na motherland).

As a matter of cats, nimeamua kuwa badala ya kuendelea ku-debate hapa JR usiku na mchana (mpaka mishipa ya damu inanisimama), ni vema nianze ku-mobilize watu, tukusanye pesa, then tuanze kuchimba visima vya maji safi mikoani.

As the old saying goes, "words without action mean nothing no matter how you might want to embroider them."

Unaonyesha ku discount mchango wa JF, kwamba si kitu.Hasha, mchango unawapa watu mwangaza, magazeti yanakuja kuchota hapa, upinzani unakuja kuchota hapa, watu wa serikali wanakuja kuchota hapa,TISS na CCM wana snoop hapa -wakitaka kuchota wachote tu-

Wabinge wanapata muelekeo na kupima maji hapa, issues zinapelekwa bungeni.Juzi John Cheyo kam-lambast Sinclair bungeni, issue imetoka hapa hapa.Tafuta habari.

Kwa hiyo usitake kututaka tuamini kuwa kuchimba visima na wananchi ni jambo la maana zaidi ya michango itakayotolewa hapa.Wewe unaweza kwenda kuchimba visima huko, hapa kuna watu wakiamua kulivalia njuga swala la maji wanaweza kupiga pressure bajeti iongezwe, wanaweza kuwahamasisha wananchi katika scale kubwa zaidi, wanaweza kuongea na wabunge kutokana na mtandao huu.
 
BongoTz,
Haya sasa maneno isipokuwa mkuu hivyo visima tafadhali sana viwe vya pump... Visima vingi ni makazi ya mbu wanaoleta Maleria pia kuna uchafu wa viwanda (toxic) inabidi kujihadhari zaidi na uchimbaji visima ambavyo kimazingira tunaharibu badala ya kutengeneza..
Leo nimecheka sana kuona rais wetu akihutubia wananchi wilayani huko Tanga akiwa ktk gari la wazi tena ktk barabara ya vumbi..
Yaani imenipa kufikiria sana kama kweli tumeisha piga hatua hata kidogo zaidi ya kumwona huyu mwanamke Mama yetu Tanzania akipakwa makeup usoni, huku kwapa zinatoa funk la nguvu!.. Unajua tena asilima 90 ya wananume wanaamini kabisa ktk roho zao kuwa Uzuri wa mwanamke TABIA lakini ktk matendo na hali halisi ya mwanamme - Uzuri wa mwanamke ni recemption (sura, umbo na rangi!)..
Hayo Maendeleo bandia!
 
As a matter of cats, nimeamua kuwa badala ya kuendelea ku-debate hapa JR usiku na mchana (mpaka mishipa ya damu inanisimama), ni vema nianze ku-mobilize watu, tukusanye pesa, then tuanze kuchimba visima vya maji safi mikoani. As the old saying goes, "words without action mean nothing no matter how you might want to embroider them."

What is this? Mkuu kila kitu kiina wakati na mahali pake, na kuna msimu wa kila kitu, forum ni mahali pa ideas, kama vile bungeni na kwenye kongamano, huwazi kufanya hayo unayodai bila ya kuwa na ideas au elimu ya kutosha on it, na hapa ndio tunakuja kuchota elimu halafu when th time is right tutayahamishia kwenye vitendo, nafikiri ni suala la common sense tu sikudhani kuwa litakuwa ni suala la kuazna kupoteza muda kuelemishana, au?

Topic ya Mkapa kuwa clean umeianza mwenyewe, sasa unapewa majibu unasema nini tena?
 
Pundit! Kudos.. waache waikandie, na waidharau JF kwa maangamizi yao wenyewe... uzuri wa watu wanaotoa mawazo pasipo kutegemea kipato au malipo ni kuwa wanatoa mawazo kwa uhuru pasipo hofu au hisia ya kujali nani anasikiliza mawazo hayo. Mengi tunayoyasema hapa, watu wengi kwenye utumishi serikalini wanayafikiria lakini wengi wanayamezea... lakini sasa hivi usishangae watu wana mawazo kama haya huko huko Bongo lakini wananyoshea kidole kuwa yanatoka JF ili kuyapa credibility.

Na kuna mengine ambayo yanatoka hapa na hapa peke yake and we are proud to play a miniature part katika kushiriki katika mjadala wa Taifa letu. Hata walioko nyumbani si wote wanachimba visima!!
 
What is this? Mkuu kila kitu kiina wakati na mahali pake, na kuna msimu wa kila kitu, forum ni mahali pa ideas, kama vile bungeni na kwenye kongamano, huwazi kufanya hayo unayodai bila ya kuwa na ideas au elimu ya kutosha on it, na hapa ndio tunakuja kuchota elimu halafu when th time is right tutayahamishia kwenye vitendo, nafikiri ni suala la common sense tu sikudhani kuwa litakuwa ni suala la kuazna kupoteza muda kuelemishana, au?

Topic ya Mkapa kuwa clean umeianza mwenyewe, sasa unapewa majibu unasema nini tena?

This is a pragrammatic approach mkuu. Sisemi kwamba hii forum ni irrelevant (hapana), ila nimeamua tu kuchukua different approach. Approach ya kutafuta solutions/take action. Ningependa kuku-encourage wewe na wadau wengine pia muungane nami ktk hili. Coz it seems obvious to me that approach ya kulaumu pekee yake, imeshindwa kabisa kuzaa positive results.
 
BongoTZ,
Tatizo ni kwamba sisi tunapoona Kijani wewe mwenzetu unaona Njano.Sasa hiyo approach itaanzia wapi mkuu..
 
...Wewe unaweza kwenda kuchimba visima huko, hapa kuna watu wakiamua kulivalia njuga swala la maji wanaweza kupiga pressure bajeti iongezwe, wanaweza kuwahamasisha wananchi katika scale kubwa zaidi, wanaweza kuongea na wabunge kutokana na mtandao huu.

Kweli Pundit? Ningependa kuona hilo ulilosema " pressure bajeti iongezwe" likitokea, lakini I've serious doubts if it will ever happen kwa speed hii. Bado sijaona stratergy (hapa JF) ya kufanya hilo unalolisema likafanikiwa. Perhaps it will take 90yrs (even 150 yrs) kwa speed hii...( And I will be dead by then).
 
Oh, thanks kijana...

Ni kweli: at some point,we need to come to our sense and realize that no matter how fiercely we can debate hapa JR either kwa kumlaumu au kumsifia Mkapa, Kikwete, and those other guys, bado hali ya uchumi nchini itazidi tu-tank, na hali za wananchi wa kawaida itaendelea kuwa mbaya zaidi endapo kama sensible & decisive actions hazitachukuliwa mapema(nasi/wadau tulio na uchungu na motherland).

As a matter of cats, nimeamua kuwa badala ya kuendelea ku-debate hapa JR usiku na mchana (mpaka mishipa ya damu inanisimama), ni vema nianze ku-mobilize watu, tukusanye pesa, then tuanze kuchimba visima vya maji safi mikoani.

As the old saying goes, "words without action mean nothing no matter how you might want to embroider them."

Wewe nenda kachimbe visima tu, utachimba visima vingapi kabla ya kupata kibyongo? Wakati mwenzako balozi wa Canada Tanzania badala ya kwenda kuchimba visima kule kwao yeye ameweka kambi pale Dodoma kushawishi wabunge wetu aendelee kupata dhahabu ya dezo kwenda kujenga mabomba ya maji ya kuoga na kuogelea! Here at JF is were we make politics matter. Bila siasa nzuri na utawala bora watavifisadi hata hivyo visima utakavyochimba!

Asha
 
One, sikuhizi visima havichimbwi kwa jembe. Teknolojia ya kuchimba visima ime-advance mno (na uvumbuzi wa teknolojia bado unaendelea). So naomba nikutoe wasiwasi kuwa hicho kibyongo hakina ubavu.

Second, mijadala inayoendeshwa hapa JR ni mizuri, ila let's be realistic: do you real think kuwa kinachojadiliwa hapa kina-influence hali ya kisiasa nchini kwa namna moja ama nyingine? No, I personally don't. Isipokuwa, endapo kama tutamia hizi idea zinazoletwa hapa JR (na wachangiaji) na kuamua ku-take action, basi hapo nitakubalina na wewe. Otherwise, it just words. I mean a kind of therapeutic exercise to get anger/hate out of our sytems. Which is a good thing kwa sasa.
 
Mkuu,

Nimevumilia kuona jinsi unavyotumia kipaji chako cha kuvuruga mjadala na nimeona nami nichangie kidogo.

Mkuu, ulitoa thread na watu wakakuelewesha kwamba haikuwa imekaa sawa ingawa ulikuwa mkali kidogo na ukawa unatoa maneno mabovu, lakini ukaona kwamba wanachama wenzio waliopo hapa JF wana nguvu katika hoja zao na ukakubali kushindwa.

Baada ya kukubali kushindwa ukawa na wazo la ukomavu wa akili na ukaona uombe radhi kwa kutumia maneno yasio busara na nafikiri hata wewe ukashangaa jinsi wanachama wenzio tena wakikusaidia na kukubali upungufu wako.

Sasa naona bado unaelekea kulekule kwenye ile thread yako ya kwanza, mkuu katika thread hii una-apologise au unazungusha mambo?
 
No, I think mada hii imebadilika mkuu. Kinachojadiliwa hapa sasa hivi si kinginecho bali approach gani nzuri ya kubadili hali ya mambo nchini. I think unahitaji ku-catch up mkuu...
 
The way to approach hali ya nchini mwetu ni kwa mheshimiwa raisi Kikwete kubadili baraza la mawaziri kila baada ya miezi sita na kuhakikisha anapata wale watu ambao watamalizia yale ambayo Mkapa aliacha.

Mkapa aliahidi katika kampeni zake pale jangwani kwamba angefanya economic reforms ambazo zingeirudisha tena Tanzania katika competitive edge na nchi zingine za Afrika.

Hata wakati ule nilimwona Mkapa kwamba ni mtu mwenye akili, mwaminifu na angeleta nidhamu katika serikali.

Sio siri mengine aliyofanya yamesemwa hapa.

Lakini Mkapa alihitaji his right-hand man ili amsaidie kufanya yale (si UFISADI)ambayo alikua aliyafanya-kukuza uchumi na kuuendeleza.

Hii ni kauli ya Mkapa kwa jarida la kimataifa la Herard Tribune:

International Herald Tribune

07-13-2004

As a leader of a least developed country, I speak from experience when I say that poverty is too complex a phenomenon, and the strategies for fighting it too diverse and dependent on local circumstances, for there to be one silver bullet in the war on poverty. We have learned the hard way over the years. We have experimented with all kinds of ideas.

Kwa hio ni vipi mzee huyu ambae alikuwa na mipango thabiti ya kukuza uchumi wetu, aliweza kutenda na mengine ndio kitendawili kwangu.
 
Hii ni kauli ya Mkapa kwa jarida la kimataifa la Herard Tribune:

International Herald Tribune

07-13-2004

As a leader of a least developed country, I speak from experience when I say that poverty is too complex a phenomenon, and the strategies for fighting it too diverse and dependent on local circumstances, for there to be one silver bullet in the war on poverty. We have learned the hard way over the years. We have experimented with all kinds of ideas.

It's a pretty nice quote Richard. And yes, poverty is a very complex phenomenon... (I coud not disagree more).
 
This is a pragrammatic approach mkuu. Sisemi kwamba hii forum ni irrelevant (hapana), ila nimeamua tu kuchukua different approach. Approach ya kutafuta solutions/take action. Ningependa kuku-encourage wewe na wadau wengine pia muungane nami ktk hili. Coz it seems obvious to me that approach ya kulaumu pekee yake, imeshindwa kabisa kuzaa positive results.

Umeamua kuchukua different approach, ya kumshangilia mkapa, baada ya kuzidiwa hoja sasa umeamua kwenda kuchimba visima? hiyo ndiyo unaita different approach?

Mkuu sisi tunapiga kelele hapa, tunasogezea viongozi wengi wakuu hizi ideas, kuna zinazofanyiwa kazi, ni nyingi mno kwamba hata hautwezi kuzihesabu, kuna zinazokataliwa kwa kukosa hoja nzito, na kuna zinazofanyiwa kazi na magazeti yetu pia, licha ya wananchi wanaokuja kuchota elimu,

Baaada ya kukusoma kidogo,unaonekana kuchanganya ishu mbili tofauti hapa, nazo ni moja ya siasa za online na Cummunity Activism, hiyo unayotaka kufanya sasa huko ya kuchimba visima, inaitwa siasa za community activism, hii unayoifanya hapa JF inaitwa online activism, sisi mkuu tulichofanya ni kutumia huu huu mtandao kuwaomba wananchi tunaowajua wamchangie mama Kilango, hela za kuongeza kwenye mfuko wa visima 30 anavyotarajiwa kuvijenga huko Same East, ndio maana ya kuutumia mtandao kwa faida ya taifa letu, lakini kufanya hivyo sio sababu ya kuwatukana wananchi wengine hapa kuwa hii JF ni kupiga kelele tu, hilo take it back mkuu,

Otherwise, next time jaribu kutafuta topic safi na uwe na hoja za kui-back up, maana hii uliyojitwika hivi karibuni ya kutaka kushindana na jamii kuwa Mkapa hana makosa, mara mkapa hakuna ushahidi, mara oooh ni matatizo ya familia, sijui kama kweli utafanikisha lengo lako la kuchimba visima namna hii, maana si unaona ilivyoku-back fire!
 
Richard,

Hayo maneno mazito mkuu na huyu Mkapa pamoja na elimu yake aliweza sana kusema na kuandika lakini vitendo vyake ndio kama hivyo tena.

BongoTz,
Katika kutafuta wapi tuelekeze nguvu zetu ni muhimu sana tufahamu wapi tumetoka, tuyachambue makosa yetu wananchi na hata viongozi wetu..Sasa tunapoona kwamba kuna utatampya alotuachia Mkapa inakuwa kazi nyingine mpya kutatua matatizo yalilojenga ghorofa baada ya kurundikana...
Leo hii wewe na mimi hatujui wapi pa kuanzia, pamoja na kwamba mwenzetu unaanza na visima vya maji..
Mkuu, kumbuka vizuri miaka ya 70 wakati hali yetu kiuchumi ilikuwa mbaya sana lakini maji yalipatikana kila wilaya hasa miji mikubwa. Umeme kwa miji ya mikoa na daadhi wilaya ulikuwepo na uliendelea kujengwa zaidi. Utakumbuka Dar ulikuwepo wa kumwaga yaani sikumbuki kukatiwa Umeme iwe tupo Mbowe ktk kujirusha ama majumbani mwetu.. Huu ni wakati tulikuwa hohehahe hatuna mbele wala nyuma..
Leo hii baada ya maendeleo yanayodaiwa, Umeme limekuwa swala jipya, maji swala jipya kiasi kwamba ktk karne hii ya 21 tunafikiria bado wananchi ni jukumu lao kuchimba visima!..Kweli maneno yako changes zitakuja baada ya miaka 150 maanake nionavyo mimi tunarudi nyuma..
Na tatizo kubwa la wananchi hasa wale wanao support hawa Wakoloni weusi ni pale wanapoona upo mwendo ingawa ni wa kurudi nyuma lakini macho yao yanatazama mbele.. kwao hatujasimama!..hivyo ubishi kwao ni kuwepo kwa mwendo (movement)!
Wito wangu kwako na wengine wote ni kwamba tutazame tulikotoka isije kuta tunarudi pale pale tulipoanzia harakati za kudai Uhuru ama kuondokana na Utumwa!..That is a fact mkuu msifanye dhihaka hata kidogo! Ni muhimu sana tuangalie tulikotoka na kuweka record ya kila makosa yaliyotangulia..

Leo hii ukiwauliza viongozi wetu wengi tu kuhusiana na kubinafsisha - Ni wapi tulikosea hata Mkapa mwenyewe hawezi kukubali yalikuwa makosa pamoja na kwamba mashirika karibu yote yaliyobinafsishwa yamebwaya ktk utoaji huduma...Haiwezekani makosa ni mfumo wa kubinafsishwa hata kidogo kwani zipo nchi kibao zimefanya hivyo na wamefanikiwa..Je, sisi tulikosea wapi?.. hamtaki kutazama kabisa..
Hapa ndipo sisi tumeweza kujenga hoja zetu baada ya kuyatazama mashirika hayo, tumegundua kwamba UFISADI ndio umetumika ktk UBINAFSISHAJI.. Viongozi wetu hawakutazama kabisa maslahi ya Taifa bali yao wenyewe ktk kujiandaa kwao na Ubepari!..wote hawa walikuwa maskini tofauti na wenzetu nchi za Ulaya!.. Kina Mkapa ndipo walipona mwanya wa kujinufaisha ili muda wao waliopoteza ktk siasa usije kuwa ni hasara kwa familia zao..
Kama nilivyokwisha sema siku zote kwa mswahili KUIBA ni SIFA!... mtu akiwa benki na kashindwa kabisa kuiba wakati nafasi ya kuiba ipo huitwa JUHA!..
Mkapa kama reflection yetu sisi wote hakutaka aonekane JUHA kwa maana hiyo nakubaliana na wewe kuwa Mkapa ni SAFI yaani kaweza kuiba pale mwanya ulipopatikana..Mjanja yeye!
 
...next time jaribu kutafuta topic safi na uwe na hoja za kui-back up, maana hii uliyojitwika hivi karibuni ya kutaka kushindana na jamii kuwa Mkapa hana makosa, mara mkapa hakuna ushahidi, mara oooh ni matatizo ya familia, sijui kama kweli utafanikisha lengo lako la kuchimba visima namna hii, maana si unaona ilivyoku-back fire!

No, no, no Marshall soma thread vizuri mkuu. Please don't take my words out of context. Next time if you wanna construe my words, try at least to construe them correctly.

P.S. Visima lazima ni chimbe mkuu. Sioni kama kuna ubaya ktk hilo.
 
P.S. Visima lazima ni chimbe mkuu. Sioni kama kuna ubaya ktk hilo.

Sawa sawa sisi tunatuma hela tu huko vinachimbwa na pia tunatoa ajira in process kwa wachimbaji, hilo halina tatizo wewe endelea tu!
 
Back
Top Bottom