Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Oh!! Chief Masanja, Kidumu Cha Mapinduzii!!!! au kama si mwanachama wa CCM basi Habari Yako!!!

Ni kweli kwa asilimia 80 ya Watanzania waliona kwamba hawa watu wafaa ndiyo, lakini mimi naamini kwamba Tanzania nzima inaongozwa na MEDIA e.g Serikali wakitaka kuwajulisha waTanzania kwamba nini kinaendelea au taarifa yoyote waapitia MEDIA, Kiongozi akienda sehemu yoyote anataka na waTanzania wajue anatumia MEDIA ect. Sasa kwamfano MEDIA ikiamua kumchambua kiongozi au kigogo au mtu yoyote na kuyasema mambo mazuri au mabaya Je Watanzania Hawataamini???

Hata ukitaka kutangaza biashara yako unatumia nini?? ni MEDIA. MEDIA zote Magazeti, TV, Radio, Internet.

By the meantime,

Gazeti la Mwananchi
Na Na Mwandishi 'Wao' Linasema

Norway yasifu mazungumzo ya CCM, CUF

SERIKALI ya Norway imepongeza hatua ya Serikali ya Tanzania ya kuendeleza mazungumzo kati ya CCM na CUF na kusema yanatia moyo katika kufikia maelewano na hatimaye kuleta hali ya utulivu na amani visiwani Zanzibar.

Balozi wa Norway nchini, Jon Karleiv Andreas Lomoy, alitoa kauli hiyo jana, alipokutana na Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein, alipokwenda kujitambulisha ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi Lomoy alisema Tanzania ina sifa kubwa duniani ya kudumisha amani kwa kuwa imekuwa mstari wa mbele katika kusuluhisha migogoro ya kisiasa katika nchi za maziwa makuu.

Alisema anaamini ikiwa Tanzania itafanikiwa kulimaliza suala la Zanzibar katika mazungumzo yanayoendelea sasa baina ya vyama hivyo, itaendelea kung’aa na kujijengea heshima katika jumuiya ya kimataifa.

Balozi Lomoy alimweleza Makamu wa Rais kuwa ametiwa moyo na hatua kubwa ya maendeleo ambayo Tanzania imefikia hivi sasa, ikilinganishwa na miaka ya 80 wakati alipokuwa akiishi hapa nchini.

“Niliondoka Tanzania mwaka 1988. Sasa naona kuna mabadiliko mengi tu. Hapa Dar es Salaam penyewe tu inaonyesha kuna mabadiliko makubwa,” alisema.

Balozi Lomoy alitaja nyanja za biashara, utamaduni na utafiti kuwa ni maeneo ambayo yatatiliwa mkazo katika ushirikiano baina ya Tanzania na Norway.

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais alimhakikishia balozi huyo kuwa serikali ya awamu ya nne, kupitia ilani yake ya uchaguzi 2005 – 2010, imedhamiria kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wake.

Dk Shein alisema Ilani hiyo inasisitiza juu ya umuhimu wa kujenga uchumi wa kisasa na kuwawezesha wananchi kushiriki katika kujenga uchumi wa nchi yao kupitia mpango wa Mkukuta.

Aliishukuru serikali ya Norway kwa misaada yake ambayo imekuwa ikisaidia jitihada za Serikali ya Tanzania kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Alisema uhusiano kati ya Norway na Tanzania umeendelea kuimarika, hasa baada ya utiaji saini wa makubaliano ya hivi karibuni kati ya Norway na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kupeleka umeme kisiwani Pemba kutoka Tanga kupitia Bahari ya Hindi.
 
Habari Ndugu wana JamboForums,

Leo hii nimetoka na hii habari ambapo Rais Mstaafu amabaye pia ni Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi akiwaasa wana-CCM kusimama Imara. Soma Zaidi CHini

Mkapa: Wana-CCM simameni imara

52618695.Africa2005BenjaminMkapa_3.jpg

Rais Mstaafu wa JMT ambaye pia ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Ndugu Benjamin Mkapa.


Kutoka Gazeti 'letu' la Uhuru,
Na Anita Boma, Kisarawe


MWENYEKITI mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa amewataka wana-CCM kuendelea kusimama imara katika Chama bila kuyumbishwa na kelele za wapinzani.

Mkapa ambaye pia ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu alitoa wito huo juzi, alipokuwa akiwasalimia wanachama wa CCM katika sherehe za kumpokea alipokuwa kwenye ziara ya siku moja wilayani humo. Sherehe hizo zilizofanyika katika ofisi ya CCM wilaya.

Aliwataka wanachama kuendelea kusisimama imara katika Chama bila ya kuyumbishwa na kelele za wapinzani, kwani wamezoea kulalamika na kulaumu ovyo.

“Ukiona Chama kinaungwa mkono na wananchi kwa kiwango kikubwa, hao wanaolaumu na kupiga kelele ujue wanapayuka tu wakitaka kujaribu.
“Ninyi wanachama, wafuasi na mashabiki wa CCM mkiendelea kukipa nguvu Chama na kumuongezea Rais Jakaya Kikwete imani; mtakuwa mnanipa raha kweli kweli kwa kuwa kitadumu, kwani Chama Cha Mapinduzi kina uongozi makini na kimepata imani kwa wananchi,” alisema Mkapa.

Alisema CCM ni mkombozi wa wananchi na aliwataka Watanzania waendelee kukiamini na kukipa ridhaa ya kuongoza.

Mkapa aliwataka wanachama wa Kisarawe kufanya juhudi ya kuwarudisha wanachama waliopotea na kukimbilia vyama vya upinzani.

Katika ziara hiyo alitembelea shule ya sekondari ya Malumbo, ambapo aliombwa kuwa mlezi wa shule hiyo ya sekondari.

“Nimefurahia ujenzi wa sekondari, bidii ya wanafunzi na matokeo mazuri ya mitihani ya awali waliyofanya nimewakubalia kuwa mlezi wa shule ya sekondari ya Malumbo,” alisema Mkapa.
 
anasema anafuraha sana huyu michelin kwanini haswa? au kwa sababu amekingiwa kifua na jk katika rada?.mpuuuzi huyu
 
Hii habari iko light. Ukiona mkanda kamili ya aliyoyazungumza kisarawe utakereka zaidi!
 
anasema anafuraha sana huyu michelin kwanini haswa? au kwa sababu amekingiwa kifua na jk katika rada?.mpuuuzi huyu

tuattack kwa hoja si umichelin wake.
hamna baya kama anawaasa wanaccm wake, ina maana anawasiwasi wanaccm wanaweza hama kwakukosa imani na viongozi wao. changamoto ni wanaupinzani kutoa hoja nzito ili wananchi waone mapungufu ya ccm.
CCM wanahitaji critics nyingi ili waboreshe uongozi Lakini tukijadili umbo au kutukana bila hoja hatufiki wanajambo.
 
Mkapa .............ali achia uwenyekiti kama vile anakimbia jambo fulani...!!!
 
REVEALED: Mkapa family owns Bank M building

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

IT has now been revealed that the building housing the registered office of an upcoming new financial institution, Bank M (Tanzania) Limited, in Dar es Salaam is owned by former president Benjamin Mkapa and his wife Mrs Anna Mkapa.

The two-storeyed office building (pictured) is located at Number 8 Ocean Road, right adjacent to the official residence of the former president and first lady (inset photos) in the city’s affluent Sea View area.

Our investigations show that the couple bought the property, with certificate of title number 6809, from the Tanzania Building Works in 2002.

At the time, Mr Mkapa was still the sitting president of the United Republic of Tanzania, while Mama Anna served as the country’s First Lady.

President Benjamin William Mkapa and First Lady Anna Mkapa served in the highest office in the land from 1995 to 2005, when he concluded his second and final presidential term.

The inconspicuous building in a quiet neighbourhood of Upanga is now listed as the registered office of Bank M (Tanzania) Limited, a new bank in the pipeline which is understood to have some rather big-name members of the local business community as shareholders through their respective companies.

The bank, with an initial share capital of 6.5bn/-, is in the final stages of being launched after a registration process that started in February this year.

In the meantime, there are few signs of its pending arrival, with only a hardly visible signpost on the front boundary wall of the building where it is housed, and now revealed to be owned by the Mkapa family.

The signpost has the simple letter ’M’ printed on an austere logo.

According to our investigations, registered owners of the bank are Jayant Kumar Patel, alias Jeetu Patel, of Noble Azania Investments Limited; Vimal Mehta of Negus Holdings Limited; and Fidha Rashid, a prominent real estate developer and car dealer with Africarriers Limited.

Nimrod Mkono of the respected Dar es Salaam law firm Mkono & Co. Advocates, is also listed as one of the main shareholders of the bank through one of his companies, Equity & Allied Limited.

There are also two listed minority shareholders in the name of Sanjeev Kumar, a local banker, and Bhaskaran Nair, described as a business executive.

Records show that by February this year, the shareholding structure of the bank as officially filed was as follows: Negus Holdings Ltd (1.3bn/-), Noble Azania Investments Ltd (1.3bn/-), Africarriers Ltd (1.3bn/-), Equity and Allied Limited (1.3bn/-), Mr Kumar (650m/-) and Mr Nair (650m/-).

When contacted by THISDAY and asked to give more details about the bank’s shareholding structure, registration and licensing status, and other details, shareholder Jeetu Patel declined comment.

Instead, the Noble Azania Investments Limited representative referred our queries to Mkono, who has so far not been available for comment.

Apart from his status as a top local lawyer and representative of Equity and Allied Limited company in the new bank’s shareholding structure, Mkono is also the current member of parliament for the Musoma Rural Constituency, on a CCM ticket.

Efforts by THISDAY to contact the governor of the Bank of Tanzania (BoT), Dr Daudi Ballali, to confirm whether or not ’Bank M’ has been or will be issued with a formal banking licence, have also proved unsuccessful so far.

But our sources in the country’s banking sector have confirmed that the process of recruiting key staff for the new bank has been quietly proceeding, apparently in preparation of its imminent formal launch.

www.thisday.co.tz
 
Yebo yebo,
Angalia hiyo list hapo hapo, halafu ni kina Kumar, Nair, Chavda and so on...wanaulizwa maswali, wanaelekeza kwa Mkono...it is very interesting!
 
Theorem: President Mkapa, who happens to be the first president of Tanzania after the demise of President Nyerere, was the the chief builder of corrupt governement system in Tanzania with strong support of the British Prime Minister Tony Brair.

Proof: Straightfoward
 
Kwa sasa sina comments, navuta subira kidogo!
 
Tena nasikia Mzee Mkapa na mkewe ndiyo wamiliki wa Ngurdoto Hotel (Arusha).
 
Yebo yebo,
Angalia hiyo list hapo hapo, halafu ni kina Kumar, Nair, Chavda and so on...wanaulizwa maswali, wanaelekeza kwa Mkono...it is very interesting!


Ndugu yangu mimi na wewe tumeshapewa chetu milioni mbili mbili ili tuanzishe mradi wa kulima mchicha na kuuza maandazi. Hawa wenye kujua kutumia makaratasi na kalamu wacha wale nchi kilaini. Mkono naye ameweka Shs 1.3bn...hizi kesi za mikataba na wawekezaji zinalipa vizuri sana.
 
Back
Top Bottom