Naona Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi ndiye anakosekana katika hii picha. Ni kweli, picha inaonyesha mshikamano. Masuala ni mengi walioshikamania, labda tuanze na suala la RADA. Msimamo wa watu waliopinga ununuzi wa RADA haujabadilika toka wakati ule. Ni watu walewale, na maneno waliyoyasema wakati ule, ndio wanayoyasema leo hii. Lakini hawa waheshimiwa wawili kwenye hii picha, msimamo wao wa wakati ule unaeleweka kwani walisimama kidete kutaka kutetea huo uchafu, na hata kuthubutu kutumia vyombo vya dola kuwapiga ngwala waliotaka kuwapinga.
Leo hii, ni hawa hawa waheshimiwa wawili na katika jambo hilohilo la wakati ule la Rada. Hata hivyo, misimamo yao ya sasa haieleweki. Raisi Kikwete anasingizia serikali ya Blair. Mkapa ameuchuna, lakini wapiga debe wake wanasema alirithishwa mkataba kutoka kwa Mwinyi. Ukiondoa Tanzania, labda na nchi nyingine chache, sijawahi kuona kiongozi wa nchi anasimamia kidete jambo fulani, tena ikiwezekana kupitia ncha ya upanga, alafu kesho anakuwa na msimamo tofauti unaopingana na ule wa jana katika jambo hilohilo, bila kutakiwa kueleza kwa nini amebadilisha msimmo wake.
Kila kiongozi anasingizia urithi. Mbona wote walirithi nchi yenye madini, samaki, na mashirika ya Umma. Viko wapi hivyo vitu? Mbona waliridhishwa nchi ambayo watu wake walikuwa wanasomeshwa shule bila kukopwa, tena na msosi wa bure juu. Kwa nini wasiendeleze huo urithi? Mkapa acha ghiriba, kwani mikataba mingi katika kipindi chako cha uongozi inafanana kama mapacha. Kuna tofauti gani kati ya mkataba wa RADA na ule wa kununua nyumba ya ubalozi Italy? Si mambo yale yale ya kuongeza bei? Je nao uliridhishwa kutoka kwa Mwinyi?
Mbona mnataka kumsingizia mzee ruksa? Au kwa sababu ni mtu mwema? Please, give me a break! Anyway, one that renders thinking and re-thinking of ones own position in regards to RADAs fracas. Nonetheless, the less intellectual eyes of a sheriff might yearn for Ali Hassan Mwinyis confession, but those critical by the jury would demand that of Benjamin Mkapa. Well, folk like me in the sidewalk wait for neither a jury, nor a sheriff to make up my mind. Humbleness is none other than the vicissitude of an intellectual. Had it been Mkapas abode, calling upon him to excuse himself of the imbroglio thus far created, cannot be a second guess. GO AHEAD MR. MKAPA. DO IT. It takes a man, a real man to say wananchi, I am Sorry.