Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Yebo Yebo,

Masaki anastahili pongezi lakini hapaswi kuwa mfano wa kuigwa moja kwa moja.

Anachosema Masaki ni kwamba kwa kuwa wanaoiba ni walewale tuwaache sisi tufanye mambo mengine. (anamaanisha kama ni mwizi yuleyule anakuja kukuibia wewe mwache kaendelee kufanya kazi kwa bidii uje umletee naye andelee kuiba). Unaweza kweli kuiga mfano kama huu?

Anaendelea kusema kwamba yeye anasadia yatima "WACHACHE" kwa jasho lake( naamini nchi ingeweza kusaidia yatima WENGI kwenye bilioni 12 za 30% ya RADA kuliko hao yatima anaowasaidia yeye, na hajui kwamba hizi pesa ni zake zilizotokana na kodi yake na yangu kwa hiyo hizi nazo ni JASHO LETU).

Ni kweli kwamba hao YATIMA wachache watakukumbuka milele lakini WATANZANIA ambao wengi ni YATIMA kutokana na BABA YAO Tanzania yenye neema kufa na MAMA yao MAISHA BORA kwa kila mtanzania kufariki watawakumbuka zaidi wakina Mwanakijiji na wengine kwa kazi wanayoifanya.

Ni kweli sio lazima uwe Mbunge kuleta mabadiliko na si lazima uwe mwanasiasa(meaning: Kiongozi wa Chama cha siasa) kuleta mabadiliko katika jamii ya watanzania hawa masikini.

Ila ni LAZIMA uwe MWANASIASA kama unavyofanya MWANAKIJIJI(Kazi nzuri kaka) na wengine humu, unaweza pia kuwa MAMA THERESA/PRINCESS DIANA(i mean-mtoa misaada kwa yatima toka kwenye jasho lako ama jasho la jirani zako) kama ambavyo anafanya MASAKI. Lakini jua hata mwanakijiji na wengine huwa tunasaidia yatima kama ufanyavyo ila nakubaliana nawe si lazima kujitangaza!

JJ
 
Yebo Yebo,

Masaki anastahili pongezi lakini hapaswi kuwa mfano wa kuigwa moja kwa moja.

JJ


Nakubaliana na wewe ujumbe wa Masaki una sehemu 2...mimi sikuwa specific lakini nakubaliana na yeye kwenye sehemu hiyo ya pili. Kuna wentezu wengi watanzania ambao wangeweza kufanya mamba mengi kwa kadri ya uwezo wao lakini hawafanyi kabisa..japo kidogo. Mfano: Imagine kuishi UK/USA/Canada n.k ukaamua kumsomesha mtoto wa jirani yako katika shule ya serikali itagharimu kiasi gani...not much ndio maana nikasema kwa hapo Masaki anastahili kuigwa.

Tanzania itajengwa na wenye moyo...wakiwamo JJ Mnyika, Mwanakijiji, Mkandara, Lunyungu, DrWHo na wengine wengi humu ambao wako tayari kutumia muda wao kutoa mwanga na mitazamo yao kwa wengine.
 
Wanangu Wadogo Zangu, Chief Naingia Kwa Mara Ya Kwanza Baada Ya Kuona Mambo Yamekuwa Moto Na Vijana Mnaitaji Kuelekezwa Jinsi Mambo Yanavyokwenda.

Mimi Nataka Niwaambie Kitu Kimoja,jana Mlikuwa Mnanyonya Maziwa Na Wazazi Wenu Je Leo Mnataka Kurudia...nafikiria Jibu Naona La Muafaka Nio Hapana. Wengi Wetu Tungependa Leo Tuwanyonyeshe Maraha Baada Ya Kutufikisha Hapa Tulipo.

Mie Kwa Kuona Hili Na Mengineyo Naomba Tufanye Kwamba Masuala Ya Mwinyi Na Mkapa Yanafahamika Na Nafikiri Ni Vyema Tukayaacha Na Kuganga Ya Jakaya.

Wanangu Wazee Wangu Waliwahi Nihusia, Ukitaka Maendeleo Usiangalie Kivuli Chake. Tuangalie Nini Tunafanya Na Sio Kuangalia Ulifanya Nini?

Nafikiri Ujumbe Umefika. Ambaye Hajaelewa Basi Nakaribisha Maswali.
 
John Mnyika,

Ndoto ulizonazo sana sana zitakufikisha bungeni tu lakini sio kuhahakisha kwamba hizo 30% za rada zinawafikia wananchi! Mambo hayo hayatatokea kwenye kizazi hiki! Unaweza ukawa na mtazamo mzuri sana kuhusu maendeleo ya nchi hii, lakini utakapogundua uoza na vikwazo vilivyopo basi utaka kata tamaa! Hilo nina uhakika nalo kabisa ! Na utajikuta umejiunga nao tu katika kuwafuna Watanzania wasio na mtetezi wa kweli (If you can't beat them, join them!)

Binafsi namuheshimu sana Jenerali Ulimwengu kama mzalendo halisi ambaye hakutana kurudi nyumakatika kuhahakisha Tanzania inakuwa nchi yenye neema! Sasa naona naye kakata tamaa wala haandiki tena!

Wazalendo wengi sana tangu enzi za Nyerere wameishia kuwa frustrated tu! Angalia wasomi wangapi wa enzi za Nyerere ambao wako mitaani hawathaminiki? (Ukiacha wale ambao walikubali kuingia kwenye mfumo uliokuwepo). Tena walisomeshwa kwa pesa nyingi za wavuja jasho wa Tanzania. Tatizo lilikuja pale walipokuja na mawazo mbadala! Fikiria kuwa na mawazo mbadala kwenye enzi za "zidumu fikra sahihi za mwenyekiti"!

Nchi haithamini michango ya wasomi na wala nchi haina falsafa ya maendeleo, bado eti unategemea maendeleo, haiwezekani. Lets call a spade , a spade here and not a big spoon! Mimi siyo mwanasiasa na wala sitakaa niwe! Mimi ni mzalendo tu ambaye sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa! Mara nyingi huwa nashabikia sana hoja kuliko porojo za kisiasa!

Tuchukulie mfano, Mbowe ambaye anategemea kugombea urais mwaka 2010 (nina imani hiyo)....Sasa hivi tunaambiwa anasoma digrii tatu kwa wakati mmoja! Jamani, hata Albert Enstein hakuwa na akili kiasi hicho! Tena anasoma digrii tatu katika mabara matatu na nchi tatu tofauti! Watanzania hawa masikini wasishangae kufikia mwaka 2010 kuambiwa Mbowe ana PhD! Hicho ni kiini macho kwa Watanzania masikini wasio na elimu! Ni dhuluma.

Ndio maana nasema, ni bora kujiwekea malengo madogo yanayotekelezeka kama vile kusomesha watoto yatima kumi, kuliko kujiwekea malengo makubwa yasiyotekelezeka kama kuahidi Watanzanai nchi imiminikayo maziwa na asali ndani ya miaka kumi. Hiyo HAIWEZEKANI! Historia inatuthibitishia hayo kwa kuangalia nchi nyingi zilizoendelea, iliwachukua miaka zaidi ya mia moja, tena wakiwa na viongozi jasiri, wachapa kazi, wasiojilimbilikizia mali na waliokuwa tayari kufanya kazi kwa faidi ya kizazi kijacho! Katika nchi hizo, viongozi hao wana enziwa sana mpaka leo! Je Tanzania ya leo tunao? Wawe wa chama tawala au cha upinzani, je kweli wapo?????
 
Masaki Mwanangu Habari Za Jioni,

Samahani Kama Nitakuwa Naingilia Uhuru Wako Wa Kuchangia Ila Kuna Suala Limenigusa Hasa Uliposema Kwamba Mbowe Ana Soma Degree Tatu Kwa Sasa.

Hebu Nambie Wewe, Inakuwaje Na Ana Weza Vipi? Mie Nimeshtuka Sana Kuona Hili. Sasa Huyu Bwana Na Ndg. Yangu Wa Kule Kiraracha Kama Nimeandika Vizuri, Watakuwa Na Tofauti Gani?

Mie Ninachojua Ni Kwamba Mh. Mbowe Ana Degree Tayari , Maana Kwa Kupambana Na Jakaya Na Kupata Asilimia Ile Ni Ushindi Kwake. Mie Binafsi Nilikuwa Simjui Kabla Ya Uchaguzi.anyway, Umezungumza Vitu Vizito Lakini Nataka Nikuambie Mwanangu Kwamba Hii Forum Imekuwa Na Maana Nyengine Sasa?

Wewe Sema Na Msemaje Wa Chadema Nasikia Bwana Mnyika Naye Anasema.mimi Nataka Tu Nisikie Kwa Upande Wa Mnyika Anasemaje Juu Ya Hili.
 
Masaki,

Mnyika, Mwanakijiji, Mwanasiasa, Mzee Es, DrWHO, Mwanagenzi nk hatujakata tamaa bado kama wewe ulivyoamua kusalimu amri.

Chunguza historia duniani, mabadiliko yamekuwa yakitokea pale ambapo jamii imekata tamaa lakini pakawepo kikundi cha watu wachache wenye kuweza kuona nyuma ya ukuta.

Hapa JF watu wengi ni wa namna hiyo. Wenye hisia za If u can't fight them join them si wengi sana hapa. Huwa wanakuja na kuondoka. Nakuomba Masaki usije na kuondoka.

Jenerali alikuwa kimya, lakini umeona hivi karibuni alivyotoa kauli kali kama mjumbe wa bodi ya hakielimu? Alisema wazi kwamba serikali ya namna hii ni ya kifashisti etc etc(mwenye ile quote iliyotolewa na mwananchi ampe Masaki).

Hilo la Mbowe limeshajadiliwa sana http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=987 ingia huko ukachangia hili suala. Usitupoteze malengo ya mjadala aliouanzisha mwanakijiji.

Na naona mnakuja kwa kasi, huyu mwingine aliyeingia anaitwa Chief Mayunga, yeye hataki tujadili past. Anataka kulinda nini wakati haya mengine ya past ndio tunayalipa hivi sasa?

IPTL mpaka leo inapandisha bei yetu ya umeme. Tuvumilie mpaka lini. Kikwete aliahidi kushughulikia hii mikataba, alichoanzisha mwanakijiji ni kuvuta kumbukumbu za nani ni nani katika nini ili iwe rahisi kushughulikia.

We are looking for leaks and leads so as to exercise the power of recall.

Hili si suala la vyama vya siasa pekee. Ni suala lako Masaki kama mwananchi.

Nathamini mchango wako kwa hao yatima. Fungua post kuhusu michango kwa yatima tutachangia hoja huko. Thread hii tuache tujadili nani alifanya nini lini?Viongozi wetu wa serikali na mikataba waliyoingia. Usitukatishe tamaa. Nani aliwaza kwamba ipo siku Kikwete ambaye alitetea ununuzi wa RADA huko nyuma atakuja kutoa kauli kwamba kama kuna cha juu waingereza inabidi waturudishie?

Jamani eeeh, endeleeni ni 'issues'!

JJ
 
Mnyika,

Nashukuru kuona kwamba angalau bado wapo Watanzania wachache wenye moyo kama wewe na wengine hapa JF! Kwanza nitafarijika sana siku nikiona angalau 20% tu ya yale ambayo nayaona yanawezekana kufanyika Tanzania yanafanyika!

Lakini siasa zetu Waafrika ni za ajabu sana! Kenya nadhani ndio wanaongoza kwa hilo la nani alikuwa nani wakati wa dili na kashfa hii na ile! Lakini je ni nani kafikishwa mahakani mpaka leo? Hakuna! Kwa sababu ni wale wale tu! Mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya!

Siasa za kinafiki ndio chanzo cha karibu matatizo yote duniani!!
 
Masaki,

Unawajibu wa kuundoa huo UNAFIKI kwa kuacha kuunga mkono siasa za KINAFIKI za If u cant fight them join them!.

JF inatimiza wajibu huo. Tuunge mkono hapa kwa kuchambua mambo hapa kwa maslahi ya taifa.

Mambo yote ya kianikwa najua ipo siku WATAFIKISHWA MAHAKAMANI na wasipofikishwa kwenye mahakama ya sheria ya kiserikali basi WATAFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA WANANCHI.

Na kila kitu kikiwekwa wazi hapa hata MAJAJI na MAHAKIMU watasimamia UHURU na HAKI. Na mawakili wauongo watajifunika nyuso zao kwa MAJOHO YAO.

Yametokea nchi nyingine, kwa nini yasitokee Tanzania.

Mwanakijiji na wengine, endeleeni na hoja yetu ya msingi.

Mimi wakati wa Mwinyi nilikuwa mdogo sana-sikumbuki majina ya viongozi wa wakati huo na sasa niko mbali na maktaba yangu.

JJ
 
Chief Masanja,
Nahene! Karibu sana ukumbini. Lakini ushauri wako kuwa usitizame kivuli unaweza kujikuta unarudia yale yale yaliyofanyika katika kivuli. Kuna thread inayoendelea kati ya Mwinyi Mkapa na Kikwete nayo ni kuwa walaji au wafujaji ni wale wale. Sasa lazima utizame nyuma uone kidonda kimeanzia wapi ili uweze kujua dawa inayohitajika. Wabheja!
 
Mwana Kijiji
Kumradhi Maalim Wangu Hio Lugha Hapo Juu Sijaielewa? Ni Kiswahili Au, Maana Lugha Zilizoruhusiwa Humu Ni Kisw Na English

Samahani Nitoe Tongo Za Macho Just Nimeipenda
 
Kwanza Habari Za Leo Wanangu Na Wajukuu Zangu.

Chief Nimerudi Tena Siku Ya Leo , Huku Nikishukuru Mungu Wa Majebele Na Masanja Mwana Magu Kwamba Ng'ombe Wote Ni Wazima Na Watu Wangu Wanaendelea Kuniombea Uzima Huku Afya Ikipambazuka.

Mwanangu Mnyika, Naomba Uelewe.nilipokuwa Nasema Hivyo Sikumaanisha Kwamba Tusiangalie History. Sababu Bila Ya History Nafikiri Hata Mimi Nisingekuwapo Na Watu Hawa Wanaoniamini Na Wewe Pia Usingekuwapo Na Chadema. Swali Ni Kwamba Chadema Imetoka Wapi Na Wewe Umekujaje Hapo Duniani. Nirejee Kwenye Mada.

Nilichokianisha Jana Ni Kwamba Kuna Mambo Mengi Sana Yametokea Tanzania. Labda Nikupe Mfano Mmoja, Wakati Watu Wanaenda Kwenye Vita Na Nduli Iddi Amini Nafikiri Utaungana Na Mimi Nikikuambia Kwamba Tulikuwa Tunakomboa Maeneo Yetu Ambayo Yalikuwa Yanataka Kukaliwa Kimabavu. Tanzania Kama Nchi Huru Tusingekubali Kuingilia Katika Mipaka Yetu. Lakini Angalia Madhara Yaliyotupata Baada Ya Vita Ile? Je Kweli Tukae Tuangalie Ni Nani Alitupeleka Vitani Au Ni Kwa Nini Tulitumia Technique Zile.....mimi Naona Kwa Busara Za Majebele Hapana. Ni Vyema Tukaangalie Wapi Tunakwenda Na Nini Tunafanya Ili Kuleta Maendleo Ya Kweli.

History Inaandikwa Na Ni Ukweli Wa Yale Yaliyotokea. Hakuna Kitakacho Fichwa. Kubwa Kama Kiongozi Ni Uangalie Nini Na Nani Anakwamisha Maendeleo Ya Sasa Ili Tuweke Kuweka Au Kumuweka Sawa Au Ikiwezekana Kama Ni Kiongozi Aondolewe. Sidhani Kama Kuna Lisilowezekana. Ukikaa Ukiangalia Nyuma Mwanangu /mjukuu Wangu Hautokwenda Mbele.

Baba Yangu Majebele Mwana Masanja Alinifundisha Kitu Ambacho Ni Muhimu Kwa Watu Wote Na Napenda Ukae Nacho Kwa Kuwa Naamini Una Macho....usiogope Kivuli Chako, Kwani Huyo Ni Wewe! Jiamini Utafanikiwa.ninachoweza Sema Mimi Ni Kwamba Viongozi Wa Sasa Waangalie Nini Tunaweza Fanya Ili Tuweze Kuwa Na Nchi Yenye Maendeleo Na Watu Tusahau Yote Yale.

Hakuna La Kuficha Yalitokea, Je Turudie Tena ! Mwinyi Amepita Na Nyerere Alikadhalika.

Mimi
Chef Masanja Wa Majebele
 
Chief Masanja

Wewe ni chief eh! ..............................

Longa Chief
 
Jamani, ni nani aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi 1993-1997?
 
Mwanakijiji

Hii list itakusaidia:
Name: Government of Tanzania
HQ Country: Tanzania
Date Founded: 26 Apr 1964
Website: http://www.tanzania.go.tz/

Past and present personnel listed in our People database
People are listed alphabetically. This list includes people who are currently in the stated positions or who have formerly held these positions. Dates are given wherever possible. The list is not necessarily exhaustive for this institution.
Abdalla, Anna
Minister of Works & Labour (1995 - 2000)
Minister of Health (2000 - 2006)
Aboud, Muhammed
Controller and Auditor General (1964 - 1996)
Presidential Advisor on Economic Affairs (1996 - 2000)
Ali, Hon. Fatma Said
Member of Parliament
Minister of Culture and Community Development (1985 - 1989)
Minister of State of Civil Service by the President (1989 - 1991)
Minister of State of Civil Service by the President (1993 - 2000)
Deputy Minister of Communication and Transport (2001 -)
Amour, Dr. Salmin
Second Vice President (1990 - 1995)
Apiyo, Timothy Odele
Principal Secretary - Ministry of Commerce and Industry (1969 - 1974)
Chief Secretary and Head of the Civil Service (1974 - 1990)
Babu, Abdul Rahman Mohamed
Minister of Planning
Bilali, Dr. Mohamed Gharib
Permanent Secretary - Ministry of Science, Technology & Higher Education (1990 - 1995)
Bomani, Paul Lazaro
Minister of Natural Resources and Cooperative Development (1960 - 1962)
Minister of Finance (1962 - 1965)
Minister of Economic Affairs and development Planning (1965 - 1970)
Minister of Commerce, Industry and Mining (1970 - 1972)
Ambassador to the USA (1972 - 1983)
Minister for Mineral Resources and Mining (1983 - 1984)
Minister for Lands, Natural Resources, Tourism and Housing (1984 - 1986)
Minister for Agriculture and Marketing (1986 - 1988)
Minister for Labour and Social Welfare (1988 - 1989)
Minister for Local Government, Marketing, Cooperative and Community Development (1989 - 1990)
Chenge, Andrew
Attorney General (1995 - 2006)
Minister of East African Co-operation (Mar 2006 -)
Chiligati, John
Minister of Home Affairs (04 Jan 2006 -)
Chitepo, Herbert Wiltshire
Director of Public Prosecutions (1962 - 1966)
Diria, Ahmed Hassan
Ambassador to the United Arab Republic (1965 - 1968)
Ambassador to Zaire (1968 - 1970)
Ambassador to India (1970 - ?)
Minister of Information (1989 - 1990)
Foreign Minister (1990 - 1993)
Minister for Labour and Youth Development (1993 - ?)
Doriye, Professor Joshua
Permanent Secretary of the Planning Commission and Privatisation in the Office of the President (2001 -)
Jamal, Amir Habib
Minister of Urban Local Government and Works (1959 - 1960)
Minister of Finance (1965 - 1972)
Minister for Commerce and Industry (1972 - 1975)
Minister of Finance and Planning (1975 - 1977)
Minister of Communications and Transport (1977 - 1979)
Minister of Finance (1979 - 1983)
Permanent Representative to the UN Specialised Agencies (1986 - 1991)
Juma, Omar Ali
Vice President (22 Nov 1995 - 04 Jul 2001)
Jumbe, Sheikh Aboud
Minister of State in the Vice President’s Office (1964 - 1972)
Vice President (1972 - 1984)
Kaduma, Ibrahim Muhammad
Foreign Minister (1975 - 1977)
Kahama, Clement George
Minister for Home Affairs (1959 - 1961)
Ambassador to West Germany (1965 - 1966)
Minister of State for Capital Development (1980 - 1983)
Minister of Natural Resources and Tourism (1983 - 1984)
Minister of Cooperatives and Marketing (2000 - 2006)
Kambona, Oscar
Foreign Minister (1963 - 1965)
Minister of Regional Administration (1965 - 1967)
Minister of Local Government and Rural Development (1967 - 1967)
Karume, Sheikh Abeid Amani
Vice President (1964 - 1972)
Karume, Ali Abeid
Deputy Ambassador to the United States (1989 - 1994)
Ambassador to Belgium (1996 - 2002)
Ambassador to Germany (2002 -)
Kawawa, Rashid Mfaume
Minister of Local Government and Housing (Tanganyika) (1960 - 1961)
Prime Minister (Tanganyika) (22 Jan 1962 - 09 Dec 1962)
Vice President (Tanganyika) (Dec 1962 - Apr 1964)
Second Vice President (1964 - 1977)
Prime Minister (17 Feb 1972 - 13 Feb 1977)
Minister of Defence (1977 - 1980)
Khatib, Mohamed Seif
Minister of Home Affairs (2000 - 2003)
Minister of State in the Prime Minister's Office (Feb 2003 - Jan 2006)
Information, Sports and Culture (04 Jan 2006 -)
Khatibu, Abdisalaam Issa
Deputy Minister of Finance (1995 -)
Kikwete, Lieutenant-Colonel Jakaya Mrisho
Deputy Minster of Energy (1988 - 1990)
Minister of Water, Energy and Minerals (1990 - 1994)
Minister of Finance (1994 - 1995)
Foreign Minister (1995 - 2005)
President (21 Dec 2005 -)
Kinana, Abdulrahman Omar
Head of Delegations to Conferences of the Front-Line States, SADC, OAU, UN, & Non-Aligned Movement
Deputy Minister of Defence and National Services (1985 - 1990)
Member of Parliament (1985 - 1995)
Deputy Minister of Foreign Affairs and International Relations (1990 - 1991)
Minister of Defence and National Service (1991 - 1995)
Special Envoy of the President to the Great Lakes (1995 - 1996)
Kombe, Lieutenant-General Imran H
Director - Department of Intelligence & Security (1983 - 1996)
Lipumba, Professor Ibrahim Haruna
Presidential Advisor on Economic Affairs (1991 - 1993)
Lowassa, Edward Ngoyai
Minister for Environment & Poverty (1988 - 2000)
Minister of Lands and Human Settlement Development (1993 - 1995)
Minister of Water and Livestock Development (2000 - 2005)
Prime Minister (30 Dec 2005 -)
Luhanjo, Philemon
Permanent Secretary - Ministry of Foreign Affairs (? - Jan 2006)
Chief Secretary and Head of the Civil Service (Jan 2006 -)
Lumbanga, Matern Yakobo Christian
Permanent Secretary - Ministry of Home Affairs (1990 - 1991)
Permanent Secretary - Ministry of Industry and Trade (1991 - 1992)
Permanent Secretary - Ministry of Lands, Housing and Urban Development (1992 - 1995)
Chief Secretary and Head of the Civil Service (1995 - 2006)
Permanent Representative to the United Nations (Apr 2006 -)
Magembe, Professor Jumanne
Minister for Labour, Employment and Youth Development (2006 -)
Makamba, Yussuf
Regional Commissioner for Dar es Salaam (1995 - 2006)
Makame, Hasnuu
Minister of Health
Minister for Communication and Transport
Minister for Natural Resources and Tourism
Minister for Information and Tourism
Minster for Capital Development (1975 - 1979)
Malecela, John Samuel
Permanent Representative to the United Nations (1964 - 1966)
Foreign Minister (1972 - 1975)
High Commissioner to the UK (1989 - 1990)
Prime Minister (09 Nov 1990 - 07 Dec 1994)
Malima, Professor Kighoma Ali
Minister of Education
Minister of Finance (? - Dec 1994)
Mapuri, Omar Ramadhani
Minister of State in the Prime Minister's Office (2000 - 2003)
Minister of Home Affairs (Feb 2003 - Jan 2006)
Ambassador to China (Jun 2006 -)
Meghji, Zakia Hamdan
Minister of Health (1995 - 1997)
Minister of National Resources and Tourism (1997 - 2006)
Minister of Finance (04 Jan 2006 -)
Migiro, Asha-Rose
Minister for Community Development, Women’s and Children’s Affairs (2000 - 2006)
Foreign Minister (04 Jan 2006 -)
Mkapa, Benjamin William
Press Secretary to the President (1974 - 1976)
High Commissioner to Nigeria (1976 - 1977)
Foreign Minister (1977 - 1980)
Minister for Information and Culture (1980 - 1982)
High Commissioner to Canada (1982 - 1983)
Ambassador to the USA (1983 - 1984)
Foreign Minister (1984 - 1990)
Minister for Information and Broadcasting (1990 - 1992)
Minister for Science, Technology and Higher Education (1992 - 1995)
President (23 Nov 1995 - 21 Dec 2005)
Mongella, Gertrude
Member of the Central and National Executive Committee
Minister of State for Women’s Affairs (1982 - 1986)
Head - Social Services Department (1982 - 1991)
Minister of Lands, Natural Resources and Tourism (1985 - 1987)
Minister Without Portfolio (1989 - 1990)
High Commisioner to India (1991 - 1993)
Mramba, Basil
Minister of Finance (Nov 2000 - Jan 2006)
Msuya, Cleopa David
Prime Minister (07 Nov 1980 - 24 Feb 1983)
Prime Minister (07 Dec 1994 - 28 Nov 1995)
Mtawali, Dr. Charles Vincent
Permenant Secretary - Ministry of Health (1962 - 1968)
Mtei, Edwin
Minister of Finance and Planning (1977 - 1979)
Mtulia, Professor Idris A
Principal Secretary - Ministry of Health
Principal Secretary - Ministry of Higher Education
Principal Secretary - Ministry of Water and Minerals
Mwakawago, Daudi Ngelautwa
Member of Parliament (1970 - 1990)
Minister of Information and Broadcasting (1972 - 1977)
Minister of Information and Culture (1982 - 1983)
Minister of Labour and Manpower Development (1983 - 1987)
Minister of Industry and Trade (1987 - 1987)
Permanent Representative to the United Nations (1994 - 2003)
Mwandosya, Professor Mark James
Principal Secretary - Ministry of Water, Energy and Minerals (1990 - 1992)
Principal Secretary - Ministry of Industries and Trade (1992 - 1993)
Minister of Communication and Transport (2000 - 2006)
Minister of State for the Environment (04 Jan 2006 -)
Mwanyika, Johnson
Attorney General (04 Jan 2006 -)
Mwapachu, Juma Volter
Ambassador to France (2002 - 2006)
Mwinyi, Ali Hassan
Minister of Health (1972 - 1975)
Minister for Home Affairs (1975 - 1977)
Ambassador to Egypt (1977 - 1982)
Minister for Natural Resources and Tourism (1982 - 1983)
President (05 Nov 1985 - 23 Nov 1995)
Nagu, Dr. Mary Michael
Minister for Community Development, Women’s and Children’s Affairs (1995 - 2000)
Minister of State in the Office of the President (2000 - 2006)
Minister of Justice and Constitutional Affairs (04 Jan 2006 -)
Ngatunga, Samuel Emillian
Head - Health Information & Research Policy & Planning Division - Ministry of Health (1990 - 2003)
Deputy Secretary - President's Office, Public Service Commission (2004 -)
Ntiro, Professor Sam Joseph
High Commissioner to the UK (1961 - 1964)
Nyalali, Honourable Justice Francis
Chief Justice (1976 - 2000)
Nyang'anyi, Mustapha Salim
Ambassador to the USA (1995 - 2002)
Ambassador to the United Arab Emirates (2002 -)
Nyerere, Mwalimu Julius K
Foreign Minister (Tanganyika) (1961 - 1963)
Prime Minister (Tanganyika) (01 May 1961 - 22 Jan 1962)
President (09 Dec 1962 - 05 Nov 1985)
Foreign Minister (1965 - 1972)
Palangyo, Peter
High Commissioner to Canada
Rashid, Major General Makame
Ambassador to Malawi (Apr 2004 -)
Rwegasira, Joseph Clemence
Foreign Minister (1993 - 1995)
Salim, Dr. Salim Ahmed
High Commissioner to India (1965 - 1968)
Foreign Minister (1980 - 1984)
Prime Minister (1984 - 1985)
Deputy Prime Minister (1986 - 1989)
Samatta, Honourable Justice Barnabas
Chief Justice (2000 -)
Sarungi, Professor Philemon
Minister of Health
Minister of Education (? - 2001)
Minister of Defence (2000 - 2006)
Sayore, Simon Fundi
Commissioner - Presidential Parastatal Sector Reform Commission (Feb 2000 -)
Sekule, William H.
Director of Public Prosecutions (Oct 1979 - Apr 1987)
Shareef, Dr. Abdulkader
Ambassador to Saudi Arabia (1990 - 1995)
High Commissioner to the UK (1995 - 2000)
Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation (2000 - 2006)

Inaendelea.................
 
Endelea............
Shein, Dr. Ali Mohammed
Deputy Minister of Health (1995 - 2000)
Minister of State in the President’s Office for Constitution and Good Governance (2000 - 2001)
Vice President (Jul 2001 -)
Sokoine, Edward Moringe
Prime Minister (13 Feb 1977 - 07 Nov 1980)
Prime Minister (24 Feb 1983 - 12 Apr 1984)
Sumaye, Frederick Tluway
Prime Minister (28 Nov 1995 - 30 Dec 2005)
Tarishi, M. Kibenga
District Executive Director - Kisarawe District Council (Sep 1997 - Sep 1999)
Assistant Director of Local Government Co-Ordination, Heading Disrict Authorities (District Councils) - Ministry-Regional Admin. and Local Government (Sep 1999 - Nov 2000)
Acting Director of Local Government Co-Ordination - Ministry-Regional Admin. and Local Government (Nov 2000 - Dec 2000)
Acting Director of Local Government Co-Ordination, President's Office - Ministry-Regional Admin. and Local Government (Dec 2000 - May 2002)
Chairperson, National Task Force-Legal Harmonization - President's Office,Regional Admin+Local Government (Jan 2002 - Jan 2004)
Commissioner - Local Government Service Commission (Apr 2002 - Jan 2004)
Director of Local Government Co-Ordination, President's Office Government - Ministry- Regional Admin. and Local Government (May 2002 - Jan 2004)
Utouh, Ludovick
Controller and Auditor General (Aug 2006 -)
Wakil, Idris Abdul
Second Vice President (1985 - 1990)
Warioba, Joseph
Vice President
Prime Minister (05 Nov 1985 - 09 Nov 1990)
Yona, Daniel
Minister of Finance (1997 - 2000)
Minister of Energy and Mineral Development (2002 -)
 
Mwanakijiji

Defence Kinana, Abdulrahman Omar
Head of Delegations to Conferences of the Front-Line States, SADC, OAU, UN, & Non-Aligned Movement
Deputy Minister of Defence and National Services (1985 - 1990)
Member of Parliament (1985 - 1995)
Deputy Minister of Foreign Affairs and International Relations (1990 - 1991)
Minister of Defence and National Service (1991 - 1995)
Special Envoy of the President to the Great Lakes (1995 - 1996)
 
Ole, asante... so Kinana was the Minister of Defence when the Rada issue first was brought up to the UK government. Anybody know who was the Chief Secretary (Katibu Mkuu) wa Wizara hiyo wakati huo?
 
John Mnyika,

Ndoto ulizonazo sana sana zitakufikisha bungeni tu lakini sio kuhahakisha kwamba hizo 30% za rada zinawafikia wananchi! Mambo hayo hayatatokea kwenye kizazi hiki! Unaweza ukawa na mtazamo mzuri sana kuhusu maendeleo ya nchi hii, lakini utakapogundua uoza na vikwazo vilivyopo basi utaka kata tamaa! Hilo nina uhakika nalo kabisa ! Na utajikuta umejiunga nao tu katika kuwafuna Watanzania wasio na mtetezi wa kweli (If you can't beat them, join them!)

Binafsi namuheshimu sana Jenerali Ulimwengu kama mzalendo halisi ambaye hakutana kurudi nyumakatika kuhahakisha Tanzania inakuwa nchi yenye neema! Sasa naona naye kakata tamaa wala haandiki tena!

Lakini siasa zetu Waafrika ni za ajabu sana! Kenya nadhani ndio wanaongoza kwa hilo la nani alikuwa nani wakati wa dili na kashfa hii na ile! Lakini je ni nani kafikishwa mahakani mpaka leo? Hakuna! Kwa sababu ni wale wale tu! Mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya!

Mzee Masaki Heshima yako Mkuu,

Napenda kukatiza kidogo mahudhui ya mada hii kwa kuchangia katika baadhi ya hoja zako ulizozitoa katika kipindi tofauti. Kama Haki Elimu wangejiunga na Serikali, walimu wangepata mishahara yao on time? Kama Oxfam international wangejiunga na mataifa tajiri duniani, tungefutiwa madeni? Kama Galileo Galilei angesalimu amri kwa busara za uongozi wa kanisa katoliki za kuamini kuwa mbinguni ni juu na kuzimu ni chini, tungejua ‘what goes around comes around”? Kama Martin Luther King Jr angebwaga manyanga kwa wazungu, bintie Condi angeiona promised land? Kama Mzee Madiba angenyoosha mikono kwa Botha, Kikwete angekuwa anakatiza hivyo viwanja kweli? Si vema kuangalia tunapokwenda bila kujua tulipotoka na mahala tulipo. Ndio tunahitaji ‘mwendo kasi”lakini wenye mwelekeo ‘vector quantity” na wala sio ‘kasi” isiyo na mwelekeo ‘scalar quantity” ama sivyo tutagonga mwamba. The longervity of our journey is no longer important, what matters most is the quality our lives through that journey.

Nadhani anachofanya Mwana kijiji ni kutafuta ‘common denominator” Itatusaidia kujua ni akina nani wanatukwamisha ili tuwateme. Mbinu hii itatusaidia kuhepa makosa waliyoyafanya wakenya. Moi alifanikiwa kuwatema waliomzidi kete katika udokozi. Waheshimiwa waliotemwa, walijikusanya na kuunda vyama vya upinzani. Ilifikia mahala KANU ikawa imeoza na kuwa pango la mizoga. Maisha ya wakenya wengi yalikuwa taabani na KANU ilishindwa kujisafisha. Vyama vya upinzani vikaungana ili kuiondoa KANU madarakani. Kumbe ule muungano wa upinzani uliwajumuisha vibaka waliokuwa ndani ya KANU na wakaiba zaidi ya waliobaki. Wakenya hawakutaka kutambua kuwa muungano wao na vyama vya upinzani ulikuwa mithiri ya ule wa Fisi na Mbuzi walioshikana mikono kwa ajili ya kudai marisho bora. (Fisi –viongozi wa upinzani: Mbuzi- wananchi wa kenya).

Hata waliotaka kudadisi kama afanyavyo Mwana Kijiji sasa hivi, yaani kujua uhalali wa upinzani wa mtu kama Gerorge Saitoti, walizimwa na slogan ya ‘anything is better than Moi”. Hivi ndivyo wakenya walivyouvaa Mkenge. Well, majuzi wakati akiongea baada ya mazishi pale Kakamega, Moi aliwasihi wakenya wamsamehe Kibaki. Just imagine, Eti Moi ana credibility ya kumkingia kifua Kibaki? Makosa walioyafanya wakenya, ni sawa na CCM iendelee kufanya madudu, alafu mwaka 2010 waheshimiwa kama vile Kiula, Kigoda, Magufuri, Lowasa, Mramba, Lamwai, Fundikira, Mkapa, wajiengue CCM na kuungana na chama cha Mrema, alafu sisi tuwe nyuma yao kwa lengo la kuunganisha upinzani ili kuiondoa CCM madarakani. Mtu makini akituuliza kulikoni tusema ‘anything is better than CCM”. Inatupasa kucheza mahepe sasa hivi ili kuhepuka hiki kilema cha maisha kama kilichowasibu majirani zetu.

Kwa matendo, Ulimwengu uliyemtaja ametufundisha mambo makuu mawili. Njia halali za kutumia elimu ili kubadili mazingira yetu bila kuwa na mtaji wa fedha. Gazeti la Rai lilianzishwa kama kijarida na watu watano; Salva, Bwambo, Shoo, Ulimwengu, na yule marehemu mtunzi wa mashahiri. Tofauti na wamiliki wa magazeti ya udaku yanayoibuka kama uyoga kwa kusukumwa na mitaji mikubwa ambayo upatikanaji wake ni wa utata, hawa waheshimiwa watano hawakuwa na mtaji wa kifedha isipokuwa ule wa mawazo katika fani zao. Waliyaweka mawazo yao kwenye maandishi katika mfumo wa kijarida na kuwauzia watu. Bidhaa iliyotokana na mawazo yao ilipendwa na watu kwa sababu ya ubora wake. Fedha waliyoipata kutokana na yale mauzo ya mwanzo ya mawazo yao ndio ikachapisha magazeti ya Rai. Mwanzo idadi ya magazeti ilikuwa ndogo kama vile mia moja, mia mbili, elfu moja, likaongezeka gazeti la Dimba, Mtanzania na mpaka likawa shirika kubwa la Habari Corporation.

Ulimwengu sio mtu aliyekata tamaa. Binafsi, nadhani yeye ndiye anatuona sisi kama wale waliokata tamaa. Walichotufundisha hawa waheshimiwa nikuwa mtaji uko kichwani mwako. Mathalani, wanasheria wetu wanapohitimu chuo kikuu, wangeiga mfano wa ulimwengu na kuachana na tabia ya kulalama kuwa hawawezi kujiajiri kwa sababu hawana mtaji wa kifedha. Kadili ya Ulimwengu, mtaji ni ujuzi walioupata katika fani yao ya sheria. Itazame nchi yetu ambapo watu wanauziwa haki zao za msingi, rushwa iliyokithiri, uonevu na unyanyasaji usio kifani, viongozi wanaovunja sheria za nchi, utapeli na ukanyabwoya usioelezeka, ufisadi, mikataba mithiri ya ile ya Abushiri, uvunjaji wa katiba unaofanywa na watawala, pamoja na maovu mengine mengi.

Katika mazingira kama haya, haingii akilini kumkuta mwanasheria anatantalika maofisini akitafuta ajira, na wengine kuishia kupata kazi zisizo fani zao. Tazama tunavyokabiliwa na uhaba wa bidhaa zilizo imara. Mfano, matofari mengi yanayotengenezwa mitaani, ukilipiga ngumi linamomonyoka. Kwa nini kisitokee kikundi cha wahandisi watano waliokubuhu katika masuala ya kemikali, wakachanganya simenti na mchanga ili kupata bidhaa isiyomengenyuka ovyo hata ikigongwa na chuma, alafu ikanunuliwa na kuwawezesha kupata mtaji wa kujenga kiwanda. Ulimwengu alitufungulia njia kwa matendo-Kijarida-Rai -Habari Corporation.

Kitu cha pili alichotufundisha Ulimwengu ni tabia ya kujitegemea kimawazo kwa kutanguliza uzalendo badala ya urafiki na njaa. Pia, tabia ya kupenda kusoma na kuandika. Magazeti mengi nchini kwetu yanamilikiwa na watu wanaopenda kujizalilisha huku wakiganga njaa. Ni majuzi tu wakati Raisi wetu aliyatolea uvivu kwa kuyakemea kutokana na kilemba cha ukoka wanachomvika, wakati hali halisi hazionyeshi hivyo. Rai ya Ulimwengu ilipomfikisha Mkapa madarakani mwaka 1995, Iligeuka na kuanza kutumia safu ile ile kuikosoa serikali kwa kusaidia kumulika wala rushwa, kupinga mauaji ya raia wasio na hatia, kuchochea mijadala ya maendeleo kwa nguvu ya hoja, na kuisifia serikali pale ilipofanya jambo jema. Bahati mbaya, nchi yetu imesheheni watu wenye ugonjwa wa kujizalilisha wanaodiliki kulamba hata matapishi ya watawala wetu. Hawa waheshimiwa hawakufurahishwa na mienendo ya Habari Corporation. Kwao, Mkapa alikuwa ni kasisi mkuu, kama vile Yesu na mitume wake. Hawakuchelewa kushika upanga na kumkata Ulimwengu sikio. Mkapa hakuwa na miujiza ya Yesu ya kurudisha sikio papo kwa papo. Wote tunajua yaliyotokea.

Habari Corporation ilishakuwa kubwa kiasi cha kutokuweza kuendelea bila kutegemea fedha kutoka kwa wateja, hasa zile zitokanazo na matangazo. Serikali ikapiga kwanja matangazo yote na shirika likaanza kuingia madeni makubwa. Hapakuwa na jinsi isipokuwa kubwaga manyanga na kusalimu amri kwa wenye nazo (Rostam). Hata hivyo huo sio mwisho wa Ulimwengu. Hapa kwa Mfugwa Mbwa, tunasema unaweza ukanilamba shaba, but you can’t kill my spirit. Ulimwengu anaweza kuwa asiandike, lakini amefanikiwa kutengeneza jeshi kubwa lisilo kifani. Mimi binafsi, najaribu kufuata nyayo zake ingawa sina kipaji kama cha kwake. Sasa hivi nimetingwa, lakini nikipata nafasi nzuri nitaandika sana. Vilevile nimekwisha soma maandiko mengi ya waandishi wa makala mbalimbali katika magazeti yetu ambao wanakubali kuwa bila hawa waheshimiwa watano uandishi wao ungekuwa mashakani. Unaweza usiyaone maandishi ya ulimwengu lakini yapo ya chipukizi wake.

Je maandishi yanasaidia? Maandishi ni kirutubisho cha ubongo. Hata hivyo, Kamuulize Chigwemise kuhusu madhara ya kitabu cha Uongozi na Hatima ya Tanzania. Viongozi wetu kwa muda mrefu wamezoea kufanya mauzauza na kupeta bila mambo yao kuwekwa kwenye maandishi na kutunzwa kwa ajili ya vizazi vijavyo. Naamini Mkapa alifanya ujinga wote ule kwa sababu tulimwachia Ulimwengu peke yake. Jambo Forum ilikuwa bado hajaweza kupenyeza mawazo yake na kuwafikia watanzania waliowengi kama ilivyo sasa hivi. Kipimo cha ufanisi katika maandishi ya sasa ni mienendo na tabia ya sasa ya serikali. Ukiona wanafanya mambo utafikiri bado wako kwenye kampeni, ujue msumari umegonga mfupa.

Majuzi Raisi amepewa taarifa kuwa kuna barua iliyoandikwa na mtanzania inatumika kama kielelezo cha hoja katika Bunge la Uingereza ambalo yeye mwenyewe hajapata bahati ya kulihutubia. Kesho yake alijibu mapigo kwa kuhitisha mkutano na wakuu wa vyombo vyote vya habari, kitu ambacho alikuwa hajawahi kufanya kwani alikuwa anaongea kupitia kwenye luninga na radioni. Alijitahidi kutumia udhaifu wa wanahabari wetu wasiopenda kujishughulisha ili kupotosha Umma. Hata hivyo, siku iliyofuatia alifunguliwa mlango na makala iliyonyoosha ukweli alioukuwa amepindisha. An orthodox style, but very effective, yaani banda bandua, au ‘qui pro quo”. Exit plan yake ikawa kuwaondoa wanafunzi madarasani na kuwavalisha jezi za chama ili kuonyesha mshikamano. Viongozi wetu hawakuzoea mashambulizi ya uhakika na yenye mwelekeo, ndio maana wanatumia fedha kujaribu kufunika aibu ‘desparate moves”.
 
mzee Kyoma... umenifanya ninywe maji ya baridi kuteremshia hoja zako.. nimezipenda hasa hilo la Kina Lowassa, na wengine wahame CCM wakienguliwa halafu tuwaunge mkono... that is exactly what happened in Kenya!
 
Back
Top Bottom