A
Anonymous
Guest
Mchongo upo hivi, kwa siku kadhaa sasa kazi zimesimama, hatufanyi chochote cha maana kwa kuwa mafuta ya Disel kwa ajili ya kuendeshea mitambo hayapo.
Uongozi umetuambia wazi kuwa Disel ndio ishu lakini hilo haliwezi kuwekwa wazi badala yake wametangaza kufanya maamuzi mengine ya kupunguza muda wa kufanya kazi.
Tumewekewa tangazo kuhusu kupunguzwa muda wa kufanya kazi, lakini ukweli ni kuwa hata huo muda ambao tunaenda kazini hatufanyi chochote.
Serikali iangalie huu mradi kwa ukaribu, ni wa kwetu Watanzania, hivyo zigo lote likiachwa kwa Mkandarasi bila kujali ana mapungufu au la.
Majibu ya TRC kuhusu uhaba wa Dizeli soma hapa - TRC yajibu madai kuwa kuna uhaba wa Mafuta ya Dizeli kwenye Mradi wa SRG