Mkurugenzi wa TRC, Kadogosa asema “Hatuna makubaliano yoyote ya kubadilisha mkandarasi wa SGR”

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Maswali kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa kuhusu Mradi wa Reli ya SGR.

Swali: Kuna changamoto kadhaa na malalamiko yanayoripotiwa na Wafanyakazi wa SGR hasa Lot 3 na 4, nini kinachoendelea?

JIBU: Changamoto kwenye miradi mikubwa ni jambo la kawaida, muhimu ni kuzitatuwa, zipo baadhi ya Lots zimekaribia kuisha.

Swali: Ni kweli Mkandarasi Mkuu wa SGR, Yapi Merkezi ameishiwa fedha na yupo njiani kukabidhi Mradi kwa Mkandarasi mwingine katikati ya Mwaka 2024?

JIBU: Mpaka sasa kimkataba Yapi Merkezi ndiyo contractor, hatuna makubaliano yoyote na Yapi Merkezi, ya kubadilisha Mkandarasi na hawawezi ku-handover kazi kwa Mkandarasi mwingine bila ya makubaliano na TRC.

MASWALI MENGINE
- Mkandarasi Mkuu, Yapi amesema atapunguza zaidi ya Wafanyakazi 600, TRC mmekubaliana na uamuzi huo na je hauwezi kuathiri ujenzi wa Mradi?

- Wafanyakazi wanaopunguzwa wanalalamika kuhusu stahiki zao wanazotakiwa kulipwa ni kidogo, utaratibu wa kuachana upoje?

- Inadaiwa Mkandarasi hajaingiza michango ya NSSF kwa zaidi ya miezi 10

- Kwa nini malalamiko mengi hayasikiki kutoka Mkandarasi wa Lot 5

- Mradi utakamilika lini kwa kila Awamu?

JIBU: Maswali uliyoniuliza ni ya Mkurugenzi wa Yapi Merkezi au uongozi wa Yapi kujibu.

===================
  • Awamu ya 1 Dar es Salaam – Morogoro (Km 300)
  • Awamu ya 2 Morogoro – Makutupora (Km 422)
  • Awam ya 3 Makutupora –Tabora (Km 294)
  • Awamu ya 4 Tabora – Isaka (Km 130)
  • Awamu ya 5 Isaka – Mwanza (Km 249)

==============

Hoja ya Yapi kudaiwa kukabidhi Mradi, soma hapa = Wafanyakazi SGR Itigi tumeandama, watulipe stahiki zetu kabla hawajaondoka
 
Mikataba ilisainiwa na Viongozi tuliowachagua wenyewe na tuliowaruhusu wenyewe wawepo madarakini.

Yangu ni hayo tu!

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Wakubwa ni fahamisheni kadogosa si alitolewa au hii imekaa je.
Ndio aliteuliwa na jiwe alikuwa manager wa mikopo katk bank ya tab

Masanja Yuko app kimadawa tu Wal siyo weleni alipazwa Muda mrefu awe mahkamanik
 
Wafanye vyote wavavyojua watufungulie barabara za majumba sita na njia panda ya airport wanatuletea usumbufu mkubwa sana kwenye usafiri.
 
Huyu Kadogosa should have gone when the TRC board was dissolved!! Kwa serikali yeyote makini huyu bwana na board yake wangefungwa kwa kosa la kuhujumu shirika.

As long as he is still with TRC huo mradi wa SGR utazidi kututesa wa lipa kodi kwa kuongezewa tozo na kodi!
 
Back
Top Bottom