DOKEZO Wafanyakazi SGR Itigi tumeandama, watulipe stahiki zetu kabla hawajaondoka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hivi ndivyo ilivyo katika Camp ya Itigi, sisi Wafanyakazi wa Mradi wa Reli ya SGR, tumeandamana hadi kwa HR wa Mkandarasi Mkuu wa Mradi, Yapi Merkezi tukitaka kujua majaaliwa ya stahiki zetu baada ya kufukuzwa kazi.

Mkandarasi Mkuu ametangaza punguzo la Wafanyakazi, sasa kila tukiuliza kuhusu maslahi yetu ya kusitishiwa mkataba na mafao ya NSSF hatupati majibu.

Asubuhi ya leo tarehe 8 Desemba 2023 tumeamkia kwa HR atueleze kwa kuwa taarifa tulizonazo ni kuwa kuna uwezekano wa Yapi kukabidhi mradi kufikia Julai 2023.

Inamaanisha hivi sasa tunatakiwa kujua kila kitu kinachoendelea kuhusu maslahi yetu, kwani Yapi akiondoka itakuwa ngumu kupata stahiki zetu.

Kila tukiwauliza wanasema tusiwe na wasi kwamba kuna Mkandarasi mwingine anakuja, tunajua kama ni kweli Serikali itusaidie kulipwa kila tunachotakiwa kulipwa.

Majibu ya TRC = Mkurugenzi wa TRC, Kadogosa asema “Hatuna makubaliano yoyote ya kubadilisha mkandarasi wa SGR”
 
TRC wanajua yoote....Kadogosa ame over stay pale....hakuna Eng mwingine pale ambadili ?
 
Back
Top Bottom