Mjerumani amchambua Lowassa, awashangaa Watanzania

Mjerumani amchambua Lowassa, awashangaa Watanzania

Wenye nchi hawana huruma kabisa na nchi yao ndiyo kwanza wanataka kumkabidhi fisi nchi yao,mpaka mzungu ambaye hafaidiki chochote na wenye ndiye anaewaonea huruma.

Kama kipindi kile cha lada ambapo wazungu walionea uchungu watanzania kwa jinsi walivyo ibiwa,wakawapeleka wezi kwenye mahakama zao,tena kwa kutumia kodi za wananchi wao na wakafanikiwa kuwaokolea watanzania mabilioni ya fedha yaliyokuwa yameibiwa,huku watanzania ndiyo kwanza wamelala fofofoo,wakiwapepea mafisadi wa nchini mwao badala ya kuwapeleka Mahakamani na sasa ndio hawa wanaotaka kuwakabidhi nchi wawatawale.

Kama watanzania wanashindwa hata kuwashughulikia mafisadi wa ndani,badala ya kuwapeleka jela wanawapa utawala mpaka mzungu aje awashitue kuwa hapa mmepotea, hakuna haja ya kusema kuwa tuko huru,labda kama tuko huru kwa maana ya kumuondoa mzungu nchini mwetu hapo sawa,lakini kwa upande mmoja bado tunatawaliwa na mafisadi na upande mwingine tunatawaliwa na wazungu ndiyo maana hatuwezi kufanya maamuzi magumu pasipokusaidiwa na wazungu.
 
kiloriti

Unakosea sana kutaja jina la mama wa mtu wakati hausiani na hoja! In short we ndie pure Tz anaeongelewa hapo akili fupi sana mi binafsi huyo lowasa jana ndio nimemuona anatuimbisha wimbo ule ule wa kikwete nothing more
 
Last edited by a moderator:
Usijitoe akili wewe.
Unakumbuka Pinda alivyolazimishwa na bunge amfukuze katibu wa nishati na madini alisemaje? Kumbuka vizuri pinda alichowajibu wabunge.
Serikali wewe iache tu kama ilivyo ndio maana madudu mengi sana

Mkuu sijajitoa akili niko timamu kabisa, Naweza nikasema Lowasa ni mpambavu wa karne huwezi ukajiuzulu kwa kesi ambayo itakuletea heshima mbovu, angalia Heshima aliyonayo mzee mtei alijiuzulu sababu msimamo wake ulikuwa haumfurahishi bosi wake. Kama Lowasa alishndwa kutuokoa kwenye jinamizi hili kwa style ya Mtei hata akiwa rais ataendelea na mfumo huo huo wa kulindana, hivi watanzania nani katuroga jamani?
 
Hvi wakati KANGI LUGOLA anataka kuvaa ki-ninja alitaka iweje vile???
Mbona suala la UADILIFU, UFISADI na RUSHWA huyu jamaa wa mvi hataki kusema????
 
Eti kipau mbele cha jamaa kitakuwa elimu huo uongo wa mchana kweupe.Ni elimu mbovu ndiyo inayowafanya mpaka leo mheshimike sasa kweli unaweza elimisha watu watambue janja yenu?.
Mtu anataja tu Elimu,ila hasemi ni njia zipi atatumia ili kuimarisha Elimu na hatimae Elimu imkomboe Mtanzania.
 
Mnaomtetea lowasa kwanini msitetee kwa hoja badala ya matusi?

Kama mimi nafuatilia nijue uhusika wa lowasa katika kashifa ya Richmond maana hata chama chake 2011 kilitaka kumfuta uanachama akiwa na pacha wenzie sasa leo mnatoa povu bila hoja how?
 
Hayo ni maswali ya msingi. Haijalishi yameulizwa na mzungu au mwafrika. Watanzania tunasahau haraka sana, tunaangalia sura na sio sera!
Maswali ya msingi, was he charged? Was he cleared? We are such myopic citizens!!!

tupe hoja kwa nn unasema ni fisadi, na kama kweli aliwah kushtakiwa wapi? na kama ndiyo aliwajibihswa na nani?
tulimuona Mramba aakienda segerea mbona ahuyu haatukumona?
tusiseme tu kama wagonjwa wa akili na hiki ndicho ninachikipinga mimi
haya ya kusema mjeruman kwan yy Mungu kila kitu kiwe sahihi kwake?
 
Watanzania kama kuku mtetea anayejua kuhesabu moja tu. Chukua yai lake kila siku ili mradi umwachie moja, ataendelea kutaga hapo bila kushtuka anaibiwa. Wajinga ndio waliwao.
 
Mtapaje mwiz EL msiambiwe ni kitanzi kiwenu?? Lowassa hatufai
 
Lowasa hafahi ni mla rushwa na fisadi simkubali hata kidogo na wala huwrzi kunibadilisha na hata ikitokea kashinda urais si kwa kura yangu Bali kwa wale tu wasiojielewa.Mungu tubariki watanzania tuongoze ktk maamuzi ya hekima
 
Who's that Mzungu kwa nchi yetu na kwako hadi uanzishe thread kabisa? So kwa kuwa kasema Mzungu ndo tuamini sio?

Waswahili wana msemo kuwa "Nyani haoni Kundule'. May be anatusaidia kutuambia kuna nini huko nyuma.
 
Mtoa mada eti anasema ana elmu ya chuo kikuu! halafu hajui kutofautisha kati ya mjeruman na mzungu,elimu....mzungu ni mtu hashga kutoka uingereza na maracphache u.s.a.kesho utakuja na hoja ya mchina kisa mweupe naye utamwita mzungu!
Ficha upuuzi wako,unalivunjia had hi jukwaa la magreat thinkers bhana
 
WAZUNGU NDIO WAIZI KABISA NA WANAFIKI TUACHE KUONA WAZUNGU NDIO WATU BORA ZAIDI/ jr
 
Tunazungumzia maisha ya watanzania unakuja tuletea habari za wazungu??who is Mzungu?

Unawezaje kutukana mzazi wa mtu kisa kamtaja lowasa kipenz chako?kwani kakosea nini kwenye hoja yake?nini ambacho kakisema kwa kumsingizia lowasa?

kuna haja ya watanzania kujitafakari sana,unawezaje kujenga matumaini kwa mtu muovu?amekutendea wema gani hadi usahau uovu wake mapema hivyo?kama ananunua mboga kwenu,ama kulipa school fees,kuwalipia matibabu ktk family yenu basi anastahiri kusimamia Marathi huko kwenu.

Tunazungumzia urais kama tasisi nyeti ambayo hupaswi kuitafta kuingia ispokua wananchi ndio waseme unastahili.Unategemea nini kama lostam Aziz,Tibaijuka,kingunge,karamagi,na wachafu wote kumsapoti muovu eti awe rais wa nchi hapo unayegemea
 
Yani wewe jamaa sasa una tofauti gani na K ya kitimoto?
Au ngeliless? Mjerumani kwanza hajui kingereza yeye anaongea kijerumani kwa hio english yake ni ya kuunga unga.
Wewe anakuuliza maswali sio kwamba hujui ila unasema tu i dont know kuepuka kutoa maelezo.
-umesababisha watz waonekane viazi mbelw ya mzungu wako.
-ina maana hujui kuwa Obama na Mke wa Clinton walienda ubungo kufanya nini?
-hujui kuwa Lowasa alihusishwa indirect na ule mkataba ila waliohusika ni makatibu wakuu wa mawizara?
:ungemjibu hata kwa kiswahili basi badala ya kuongea neno moja tu i dont know i dont know!
Pole.

Dah!!!wewe ndo unapotosha kabisa watu aisee,!!!uliza historia ya wajeruman ndugu,mjeruman ni mtu wa kwanza kujua kuzungumza na kuandika lugha za watu wengine au lugha za nchi nyingine Ulaya lakin uwa anapenda sana lugha yake,nina rafiki yangu yupo hapa tz ni mjeruman aisee anapiga english,kirusi,kifaransa,kitaliano,kiispanish na kiportugal tena vizuri kabisa,so german people acha chezea kabisa
 
Team Membe jana mmepigwa mmeenda tafuta kick ya mjerumani kwa kuwa anakuuliza maswali kana kwamba Jana hakuona kiongozi wa Safari ya Matumaini na yaliyojiri.

Je wao waliotutesa wakati wa ukoloni amekuambia tunavyowakaribisha na wewe ukiwa mmoja wao anatuonaje

Je baada ya hapo mlienda wote wapi?

Kipigo cha Jana kimekufanya Usiweze andika threats yako bila kutegemea mawazo ya mzungu?

Unadai umesoma kwa style hii umesoma kweli?

Tuachane na mzungu

Team Membe mnaweza anzisha uzi au sasa mnakutana na wafaransa?

Nijibu tuendelee au hata Team mwingine
 
Katika hali ya kunishangaza, nilikuwa nabadilishana mawazo na mzungu mmoja raia wa Ujerumani kwenye N.G.O yake. Katamka maneno yaliyonistaajabisha.

Tumeongea mambo mengi lakini baadae tukaanza kuongelea siasa. Akasema kuna yule aliekuwa waziri mkuu anaitwa Lowasa, nimeona sasa mnampenda sana. Mimi nikamjibu inaonekana kuna Watanzania wanampenda awe Rais. Yule Mzungu akaniuliza, si yule aliejiuzuru kwa sababu ya Corruption?, nikamjibu ndie huyo. Akasema, wakati ule alionekana amekula Rushwa, sasa anataka kuwa Rais na watu wanamuunga mkono!, akaongezea kwa kusema how can you easily forget?, how can you easily change your mind?, yaani mnawezaje kuwa wasahaulifu namna hii, mnawezaje kubadili fikra zetu haraka hivi juu yake?, hapo mimi nikabaki na kigugumizi. Akaongeza, au Lowasa amewahi kuwaelezea uhusika wake na hizo corruption?, mimi nikamjibu hapana. Akasema tena, Or was he cleared by the court? yaani, je Mahakama iliona hana hatia?, nikamjibu kesi haijawahi kwenda Mahakamani. Akauliza, then which criteria do you use support him?, yaani mnatumia kigezo gani kumuunga Lowasa mkono? nikamjibu kwakweli sijui wananchi wanatumia kigezo gani.

Yule mzungu akasema, anyway, you are such amazing country, with this style it may take you so many years to change. Yaani ninyi ni nchi ya ajabu, kwa style hii itawachukua miaka mingi kupata mabadiliko.


Nami nakubaliana nae yanayotokeaga Tanzania ni maajabu huwezi kuyakuta popote pale. Yaani huyu atakuwa anatupeleka kwenye SAFARI YA MATUMIZI, wala hakuna kitu kinachoitwa SAFARI YA MATUMAINI tuwe makini sana na hii taasisi ya URAIS
 
criteria ya vijisenti ndo maana watu wanamsupport.Yaani watanzaniani watu wa kuridhika sana,yaani laki tatu mtuakipewa yaani anaridhika kabisa

Sio watu wanaridhika,tatizo ni kwamba hawa watu wana nguvu na hata usipokula ela zake jua atapita tu,so bora ule ela na hata kesho akiwa Magogoni anaweza akakukumbuka,ukapata hata uku wa mkoa au ubunge wa viti maalumu
 
Back
Top Bottom