Katika hali ya kunishangaza, nilikuwa nabadilishana mawazo na mzungu mmoja raia wa Ujerumani kwenye N.G.O yake. Katamka maneno yaliyonistaajabisha.
Tumeongea mambo mengi lakini baadae tukaanza kuongelea siasa. Akasema kuna yule aliekuwa waziri mkuu anaitwa Lowasa, nimeona sasa mnampenda sana. Mimi nikamjibu inaonekana kuna Watanzania wanampenda awe Rais. Yule Mzungu akaniuliza, si yule aliejiuzuru kwa sababu ya Corruption?, nikamjibu ndie huyo. Akasema, wakati ule alionekana amekula Rushwa, sasa anataka kuwa Rais na watu wanamuunga mkono!, akaongezea kwa kusema how can you easily forget?, how can you easily change your mind?, yaani mnawezaje kuwa wasahaulifu namna hii, mnawezaje kubadili fikra zetu haraka hivi juu yake?, hapo mimi nikabaki na kigugumizi. Akaongeza, au Lowasa amewahi kuwaelezea uhusika wake na hizo corruption?, mimi nikamjibu hapana. Akasema tena, Or was he cleared by the court? yaani, je Mahakama iliona hana hatia?, nikamjibu kesi haijawahi kwenda Mahakamani. Akauliza, then which criteria do you use support him?, yaani mnatumia kigezo gani kumuunga Lowasa mkono? nikamjibu kwakweli sijui wananchi wanatumia kigezo gani.
Yule mzungu akasema, anyway, you are such amazing country, with this style it may take you so many years to change. Yaani ninyi ni nchi ya ajabu, kwa style hii itawachukua miaka mingi kupata mabadiliko.