Mjerumani amchambua Lowassa, awashangaa Watanzania

Mjerumani amchambua Lowassa, awashangaa Watanzania

Aise nimekushushia kofia mkuu, hakika huyu bwana wa ajabu kweli,karne ya 21 unatulete habari za mjerumani,hao hao ndo wamekuwa chanzo cha maisha ya mwafrika kuwa mabaya yeye
unamtukuza!! wakupima huyu!

Mkuu tunaangalia HOJA alizozungumza,hatuangalii kaongea Mjerumani,Msomali,Mmakonde nk.Jibuni hoja za huyo mzungu kwanza,ndipo tuangalie utaifa wake.Huyo fisadi mnayemshabikia kwa vi ujira uchwara mlivyopewa SI ndio anatibiwa huko anakotoka huyo mzungu
 
Wasira anaboa, anaongelea kuboresha kilimo wakati hadi sasa ameshindwa kuonyesha mfano, bei ya mazao haieleweki, hana jipya kabisaaa
 
Kwani Kikwete alikuwa na sifa gani na kawa raisi?
Wizara zote kavuruga na madili juu. Akaja kuwa raisi.
Tumlaumu nani?? Mchawi wetu nani? Viongozi? Nakataa
 
Mtoa mada eti anasema ana elmu ya chuo kikuu! halafu hajui kutofautisha kati ya mjeruman na mzungu,elimu....mzungu ni mtu hasa kutoka uingereza na maracphache u.s.a.kesho utakuja na hoja ya mchina kisa mweupe naye utamwita mzungu!

Hoja nyepesi sana hizo, jadili hoja za msingi
 
Ungempa mfano wa Blata wa fifa,mbona wazungu wenzake wamempa
urais wa fifa wakati alikuwa na kashfa ya Rushwa?

Binafsi naona wazungu wanamwogopa EL wanaikumbuka
story ya city water,na power solution net.Ambapo wenzao walifukuzwa na EL.

Kama alichokisema anamaanisha
mbona nchi zao ziko mstari wa mbele kusifia
ujinga eti nchi yetu uchumi unakua ilimradi wanazidi kupewa
sehemu muhimu kutunyonya,mpaka waliposhtuka wachina
wanaanza kugusa kwenye bakuri zao ndo wakagtuka na kutunyima misaada
kwa issue ya escrow,mbona hawakuwahi kufunga misaada kwa issue ya rich mond?

Natamani watz tujadili wenyewe kumkubali
au kumkataa EL na si shinikizo la wazungu
kwani wao wangependa mtu legelege wazidi kutunyonya
kwa kutusifia ujinga huku sisi tukichekelea kama mazuzu.

Kwa hiyo wewe ukisifiwa uchumi wako unakuwa (hata kama haukui) huwa unaona sifa na kujisikia umewini? Halafu kuhusu huyu fisadi wa FIFA, hujui kwamba kama sio waafrika kumpa support ungekuta ameondolewa siku nyingi? Ulaya na Marekani wamefanya kila njia atoke lakini waafrika (waliozoea uvivu, ufisadi na kuomba omba kiasi cha kushindwa kuendesha nchi bila misaada, huku wakijifanya eti waachiwe waamue mambo yao wenyewe) wakimkingia kifua?
 
Nimeipenda hii. Tujenge hoja kama huyu mwenzetu.

Maswali mazuri sana hayo ambayo hata mimi nimekuwa nikijiuliza kuhusu Lowassa na hawa weak minded supporters wake.
1)Lowassa si alishinikizwa na bunge kujiuzulu kutoka na kashfa ya ufisadi wa Richmond? Sasa mbona anagombea urais ina maana hana mshipa wa aibu?
2)Wanaomsapoti ina maana wameshasahau kwamba huyu bwana miaka kadhaa iliyopita alikumbwa na kashfa ya ufisadi?
3)Je,Lowassa alishawahi kusafishwa mahakama kwamba siyo fisadi?
4)Kama bado hajasafishwa na mahakama,je ni kwanini?Tena nakumbuka kipindi kile baada ya Dr Slaa kutangaza oridha ya aibu akina Lowassa walimtishia Dr Slaa kwamba watampeleka mahakamani kwa kuwachafua na Dr Slaa akawajibu kwamba watangulie tu huko mahakamani kwani atakutana nao huko huko,je kwanini sasa hawakwenda mahakamani kumshtaki Dr Slaa?
5)Nyinyi mashabiki wake mmepata wapi uhalali wa kumsafisha Lowassa kwamba ni msafi na anafaa kuwania ofisi kubwa hapa nchini?
 
Mahakama ndiyo njia sahihi, sio uchochoron, vyombo vya habari nk ambao kisheria hawawezi kuthibitisha validity ya kashifa ya fisadi Lowasa.

Hizi corrupt court zetu ndio unataka ziaminike kwa 100%?
 
Hawa wanae msapoti lowasa ni pro ukawa ili wapate hoja ya kuimaliza ccm kwa kashifa ya Richmond.
 
Mi naona huyo mzungu kaitukana serikali na vyombo vya kuzuia na
kupambana na rushwa kama vile takukuru,kwamba ni wasauhulifu,

kama EL alikula rushwa wangemshtaki,na kama
hawakumshtaki basi walisahau lile tukio na
kuendelea na mengine ya wanaoongwa mbuzi
na sh.10000/= maana ndo tunawaona mahakamani kila kukicha,
au walimkuta ni msafi wakasahau kuutangazia umma.
 
mimi sio mzungu, ni mtanzania, halisi,vizazi na vizazi. lakini siwezi kukubali kuona fisadi mla rushwa mwenye credibility mbovu kama Lowassa anaingia Ikulu. Tulikaa kimya 2005 hatukukemea watoa ahadi zisizoeleweka, tumeishi kwa kujutia miaka 10.

Watanzania wenye uwezo wa kuchambua baya na jema wana wajibu kwa watanzania wasio na uwezo huo kwa kuwaelmisha na kuwaambia upuuzi wa kuchagua viongozi wasiofaa kwa sababu tu ni mabingwa wakutoa pesa. Ndio maana nimetamka wazi, nitapayuka kadri niwezavyo kuwaonesha mapungufu ya huyu Lowassa.Kama CCM wakiamua kumpitisha na UKAWA kwa ujinga wao wakashindwa na fisadi kama huyu kwenye sanduku la kura. Iwe ni mwanzo na mwisho wa thread za maisha magumu humu JF, kwani tutakuwa tumejifanyia certification ya kuyamiliki maisha ya hovyo kwa miaka 10 ijayo na possibly mingine mingi sana.

Lowassa hana jipya kama kiongozi, ni mla rushwa, anakumbatia kila aina ya mafisadi, na mbaya zaidialifukuzwa yeye na kina mramba walioshtakiwa kwa kutuuzia umeme hewa.leo hii asijifanye msafi wakati hajasafishwa kokote.
 
CCM sintaiunga mkono ktk maisha yangu, sijawahi kuipigia kura katika kipindi cha pambio la maisha bora kwa kila Mtanzania na wala katika chorus hii ya safari ya matumaini sitawapa kura yangu.
 
Yani wewe jamaa sasa una tofauti gani na K ya kitimoto?
Au ngeliless? Mjerumani kwanza hajui kingereza yeye anaongea kijerumani kwa hio english yake ni ya kuunga unga.
Wewe anakuuliza maswali sio kwamba hujui ila unasema tu i dont know kuepuka kutoa maelezo.
-umesababisha watz waonekane viazi mbelw ya mzungu wako.
-ina maana hujui kuwa Obama na Mke wa Clinton walienda ubungo kufanya nini?
-hujui kuwa Lowasa alihusishwa indirect na ule mkataba ila waliohusika ni makatibu wakuu wa mawizara?
:ungemjibu hata kwa kiswahili basi badala ya kuongea neno moja tu i dont know i dont know!
Pole.

Kwa kweli akili za watanzania ni ngumu kuzielezea, kama ni hivyo naomba nikiri kwamba nafasi ya uwaziri mkuu Tz huwa ni pambo tu, yaani katibu au waziri wa wizara yeyote anaweza akafanya usenge wowote na PM akijua hana chakumfanya.
 
mimi sio mzungu, ni mtanzania, halisi,vizazi na vizazi. lakini siwezi kukubali kuona fisadi mla rushwa mwenye credibility mbovu kama Lowassa anaingia Ikulu. Tulikaa kimya 2005 hatukukemea watoa ahadi zisizoeleweka, tumeishi kwa kujutia miaka 10.

Watanzania wenye uwezo wa kuchambua baya na jema wana wajibu kwa watanzania wasio na uwezo huo kwa kuwaelmisha na kuwaambia upuuzi wa kuchagua viongozi wasiofaa kwa sababu tu ni mabingwa wakutoa pesa. Ndio maana nimetamka wazi, nitapayuka kadri niwezavyo kuwaonesha mapungufu ya huyu Lowassa.Kama CCM wakiamua kumpitisha na UKAWA kwa ujinga wao wakashindwa na fisadi kama huyu kwenye sanduku la kura. Iwe ni mwanzo na mwisho wa thread za maisha magumu humu JF, kwani tutakuwa tumejifanyia certification ya kuyamiliki maisha ya hovyo kwa miaka 10 ijayo na possibly mingine mingi sana.

Lowassa hana jipya kama kiongozi, ni mla rushwa, anakumbatia kila aina ya mafisadi, na mbaya zaidialifukuzwa yeye na kina mramba walioshtakiwa kwa kutuuzia umeme hewa.leo hii asijifanye msafi wakati hajasafishwa kokote.

KURA YAKO INA NGUVU SANA / JIANDIKISHE UPIGE KURA HAPO OCT 25/jr
 
Kwa hiyo wewe ukisifiwa uchumi wako unakuwa (hata kama haukui) huwa unaona sifa na kujisikia umewini? Halafu kuhusu huyu fisadi wa FIFA, hujui kwamba kama sio waafrika kumpa support ungekuta ameondolewa siku nyingi? Ulaya na Marekani wamefanya kila njia atoke lakini waafrika (waliozoea uvivu, ufisadi na kuomba omba kiasi cha kushindwa kuendesha nchi bila misaada, huku wakijifanya eti waachiwe waamue mambo yao wenyewe) wakimkingia kifua?
Mkuu ni nchi gani so far imetangaza kumsusia au kupinga matokea ya Blata kwa sababu amechaguliwa na waafrika
wakati hana vigezo au ni mla rushwa?
Mimi sipendi tabia ya kujidharau mbele ya watu weupe,hiyo ni infiriority complex.
Wazungu walimpa kura, kama una ushahidi ya kwamba hawakumpa bali alipewa na waafrika tu weka hapa mezani.

Nimesema hapo mwanzo kama tunamkataa EL,tumkatae sisi na siyo kuambiwa na weupe la kufanya.
wao wanaangalia maslahi yao,Wanataka mtu legelege wapige dili,na kwangu mimi
wanayempigia debe huyo ndo tumuogope kama ukoma.
Angalia Zimbabwe wanavyomchukia Mgabe,lkn kosa la Mgabe ni kuwapokonya
ardhi walowezi kuwapa wenyeji baaasi.
 
Katika hali ya kunishangaza, nilikuwa nabadilishana mawazo na mzungu mmoja raia wa Ujerumani kwenye N.G.O yake. Katamka maneno yaliyonistaajabisha.

Tumeongea mambo mengi lakini baadae tukaanza kuongelea siasa. Akasema kuna yule aliekuwa waziri mkuu anaitwa Lowasa, nimeona sasa mnampenda sana. Mimi nikamjibu inaonekana kuna Watanzania wanampenda awe Rais. Yule Mzungu akaniuliza, si yule aliejiuzuru kwa sababu ya Corruption?, nikamjibu ndie huyo. Akasema, wakati ule alionekana amekula Rushwa, sasa anataka kuwa Rais na watu wanamuunga mkono!, akaongezea kwa kusema how can you easily forget?, how can you easily change your mind?, yaani mnawezaje kuwa wasahaulifu namna hii, mnawezaje kubadili fikra zetu haraka hivi juu yake?, hapo mimi nikabaki na kigugumizi. Akaongeza, au Lowasa amewahi kuwaelezea uhusika wake na hizo corruption?, mimi nikamjibu hapana. Akasema tena, Or was he cleared by the court? yaani, je Mahakama iliona hana hatia?, nikamjibu kesi haijawahi kwenda Mahakamani. Akauliza, then which criteria do you use support him?, yaani mnatumia kigezo gani kumuunga Lowasa mkono? nikamjibu kwakweli sijui wananchi wanatumia kigezo gani.

Yule mzungu akasema, anyway, you are such amazing country, with this style it may take you so many years to change. Yaani ninyi ni nchi ya ajabu, kwa style hii itawachukua miaka mingi kupata mabadiliko.

Acha utumwa WA fikra , wazungu walishatuachia nchi yetu toka mwaka1961.
 
usimpende mtu kwa sababu ni kabila lako au mmetoka kijiji kimoja.mchaguwe kwa uwezo wake na uadilifu wake.btw angalia wassira anavyonenga hoja na kutushawishi watanzania tumchaguwe.ingawaje binafsi sitamchaguwa.
1. Sina kawaida ya kupenda kwanza, natumia rationality tu sio hisia wala insiprational speeches hizi za sasa haswa kwa mambo ya mustakabali wa Taifa. . . . .yaani ukimsikiliza jana na huyu wa leo ndio unashawishika kwa watu ambao wamekuwa kwa Govt kwa zaid ya miaka 30 uko makini kweli??!!!

2. Uwezo na uadilifu haupimwi kipindi cha kampeni mkuu. . . . . . amka sasa au lala daima
 
Kwa kweli akili za watanzania ni ngumu kuzielezea, kama ni hivyo naomba nikiri kwamba nafasi ya uwaziri mkuu Tz huwa ni pambo tu, yaani katibu au waziri wa wizara yeyote anaweza akafanya usenge wowote na PM akijua hana chakumfanya.
Usijitoe akili wewe.
Unakumbuka Pinda alivyolazimishwa na bunge amfukuze katibu wa nishati na madini alisemaje? Kumbuka vizuri pinda alichowajibu wabunge.
Serikali wewe iache tu kama ilivyo ndio maana madudu mengi sana
 
unaona sasa?
watanzania tunashida sana.
Kimsingi wewe mleta mada hujui unachokitaka na wala hujui unaish ili iwe nini?
ivi mtu kujisemea tu tayari ni credibility ......................

Hayo ni maswali ya msingi. Haijalishi yameulizwa na mzungu au mwafrika. Watanzania tunasahau haraka sana, tunaangalia sura na sio sera!
Maswali ya msingi, was he charged? Was he cleared? We are such myopic citizens!!!
 
Tatizo letu elim ni ndogo sana na wengi hawapo interested kufukunyua mambo. Ukienda mtaani ukimwambia mtu akupe maelezo kuhusu hizi kashfa usishangae mtu anakuambia tu Lowasa ni fisadi. Kivipi hajui kamezeshwa tu na media. Ndio wote watz tulivyo
 
Back
Top Bottom