Mitandao ya simu inakata hela bila mtu kujiunga na huduma yoyote. Haya mambo wakati wa Hayati Magufuli hayakuwepo

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
1,424
4,731
Huo ndio ukweli. Kuna mambo ya ajabu sana yanaendelea kwa sasa hapa nchini.

Nadhani wahusika wanatamani watunyang'anye hata kidogo tulichonacho tubaki hatuna kitu.

Gharama za maisha zipo juu na bado mitandao ya simu inakata hela kwa kisingizio cha ulikopa au ulijiunga na huduma fulani wakati si kweli.

Huu ni uonevu! vodacom acheni utapeli
 
Juzi nimeweka salio la kawaida likakatwa vodacom hao. Nikawapigia simu huduma kwa wateja wakanambia nilijiunga sijui na huduma gani hata sizijui ndio kwanza nilizisikia siku hiyo. Nikamwambia aniondoe kwenyewe akasema sawa AISHANIONDOA tayari, nikamuuliza tena kama kaniondoa kwenye izo huduma kasema AISHANIONDO KABISA sitakatwa tena pesa za huduma.

Ajabu kesho yake nakatwa tena hela. Nakuta salio limepungua na ukiwatafuta jibu ni hilohilo la kujiunga na huduma zao ambazo hata hujawahi kuzisikia.
 
Hayo Mambo mm toka naanza kutumia simu miaka ya 2009 nikiwa form III yapo
Sio kweli. Labda kama wakati huo ulikuwa unajiunga mwenyewe na hizo huduma.

Sasa hivi yaani hata bila kujiunga wanakata tu. Wanatia hasira sana. Na wakati simu unaimiliki mwenyewe ukiwapigia wanadai inawezekana kuna mtu alikuunga bila wewe kujua!
Wanakera basi tu hakuna namna!
 
Juzi nimeweka salio la kawaida likakatwa vodacom hao. Nikawapigia simu huduma kwa wateja wakanambia nilijiunga sijui na huduma gani hata sizijui ndio kwanza nilizisikia siku hiyo...
Tutafute namna ya kuwashtaki. Uzuri mi nikiwapigia narecord maelezo yao. Hii nchi sasa hivi wanyonge hawana mtetezi! Nadhani watawala karibu wote ni wabia wa hiyo mitandao. Wakipewa 10% wanakaa pembeni wanakula kwa urefu wa kamba!
 
Juzi nimeweka salio la kawaida likakatwa vodacom hao. Nikawapigia simu huduma kwa wateja wakanambia nilijiunga sijui na huduma gani hata sizijui ndio kwanza nilizisikia siku hiyo. Nikamwambia aniondoe kwenyewe akasema sawa AISHANIONDOA tayari, nikamuuliza tena kama kaniondoa kwenye izo huduma kasema AISHANIONDO KABISA sitakatwa tena pesa za huduma.

Ajabu kesho yake nakatwa tena hela. Nakuta salio limepungua na ukiwatafuta jibu ni hilohilo la kujiunga na huduma zao ambazo hata hujawahi kuzisikia.
Haya makato niliyaona tigo, kumbe na voda yapo?
 
Tuchague serikali ya Chama kingine tutakomeshs matepeli wa makampuni ya simu.Wanawaunga wananchi bila rizaa Yao.Magu aliongoza nchi.
 
Huo ndio ukweli. Kuna mambo ya ajabu sana yanaendelea kwa sasa hapa nchini.

Nadhani wahusika wanatamani watunyang'anye hata kidogo tulichonacho tubaki hatuna kitu.

Gharama za maisha zipi juu na bado mitandao ya simu inakata hela kwa kisingizio cha ulikopa au ulijiunga ma huduma fulani wakati si kweli.

Huu ni uonevu! vodacom acheni utapeli
Siku zote unapokuwa na kiongozi dhaifu tegemea watu wenye nafasi za kumkanyaga aliye chini yao huwa wanajitawala
 
Huo ndio ukweli. Kuna mambo ya ajabu sana yanaendelea kwa sasa hapa nchini.

Nadhani wahusika wanatamani watunyang'anye hata kidogo tulichonacho tubaki hatuna kitu.

Gharama za maisha zipi juu na bado mitandao ya simu inakata hela kwa kisingizio cha ulikopa au ulijiunga ma huduma fulani wakati si kweli.

Huu ni uonevu! vodacom acheni utapeli
Juzi nimeweka salio la kawaida likakatwa vodacom hao. Nikawapigia simu huduma kwa wateja wakanambia nilijiunga sijui na huduma gani hata sizijui ndio kwanza nilizisikia siku hiyo. Nikamwambia aniondoe kwenyewe akasema sawa AISHANIONDOA tayari, nikamuuliza tena kama kaniondoa kwenye izo huduma kasema AISHANIONDO KABISA sitakatwa tena pesa za huduma.

Ajabu kesho yake nakatwa tena hela. Nakuta salio limepungua na ukiwatafuta jibu ni hilohilo la kujiunga na huduma zao ambazo hata hujawahi kuzisikia.
Tabia hii Halotel pia wanayo, Mara 4 Sasa naweka Salio la 1000, nikitaka kujiunga kifurushi naambiwa Salio halitoshi,ukiangalia,600 wamechukua , kwakweli utapeli huu sijui utakoma lini
 
Sasa si waseme tu tunawaibia na kuwadai service charges
 
Tabia hii Halotel pia wanayo, Mara 4 Sasa naweka Salio la 1000, nikitaka kujiunga kifurushi naambiwa Salio halitoshi,ukiangalia,600 wamechukua , kwakweli utapeli huu sijui utakoma lini
Binafsi hao halotel nilishaacha kabisa kutumia hiyo line ingawaje baada ya kuwalalamikia waliacha kukata.

Hawa vodacom mara nyingi huwa siweki salio nanunua kwa mpesa. Sasa jana wamenifanyia upuuzi niliweka muda wa maongezi nikakuta wamekata karibu elf 1. Nilipowagia wakadai eti nimejiunga na huduma ya muito kwa wanaokupigia!
How?, when?, where? Mara oh nilikopa nipige tafu! Me? When, how?

Yaani hapa nahitaji msaada wa kujua namna naweza kuwashtaki. Wanakera sana! Hela inatafutwa kwa shida jamani wenyewe wanaikwapua tu bila maridhiano!😲
 
Back
Top Bottom