TCRA itupieni macho kampuni ya Vodacom kwa kukata fedha za wateja kwa madai mteja kajiunga na huduma fulani wakati si kweli

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
TCRA, nawaomba muichunguze kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom kwa kukata fedha unaponunua muda wa maongezi kwa hoja kuwa mteja uliomba/ulijiunga na huduma fulani ambayo hutakiwa kulipia kwa kukatwa fedha mara tu unaponunua muda wa maongezi.

Mimi binafai ni mhanga wa hili jambo kwani nimeshakatwa fedha mara kadhaa na ukiwapigia huduma kwa wateja ukaongea na wahusika(mhudumu), unajibiwa kuwa umekatwa kiasi hicho kulipia huduma hii na ile wakati mtu hujawaji kujiunga na huduma hiyo.

Kinachotokea ni hiki: unaweka hela(airtime)kwenye simu yako ili ununue kifurushi lakini system inakugomea na ukicheki salio unakuta halijapungua.
Baada ya muda unaamua kuacha ukiamini labda ni tatizo la mtandao.Ukija kujaribu baadae inaendelea kugoma na ukiridi kucheki salio, unakuta wamekata kiasi fulani cha fedha (mfalno shilingi 40 au 99 kutegemea na huduma waliyokutoza kimagumashi).

Matokeo yake ni kwamba, kama uliweka airtime ya shilingi 1,000 ili ununue kifurushi cha shilingi 1000, hutaweza tena kupata huduma hiyo kwani salio linakuwa chini ya shilingi 1000, hivyo utalazimika kununua muda mwingine wa maongezi( kutiana hasara).

Ukiwapigia huduma kwa wateja kutaka ufafanuzi, wanakwambia tarehe fulani ulijiunga na huduma fulani na hiyo hela umekatwa kulipia huduma hiyo na wanakwambia sasa tumekutoa katika hiyo huduma.

Cha ajabu na cha kuudhi, tatizo linaisha kwa muda ila baadae linajirudia kwa tozo ile ile au tozo tofauti kwa maana ya kuunganishwa tena kimagumashi katika huduma ambayo hujaomba kujiunga.

Hivyo, tunawaomba TCRA mfuatilie jambo hili na muwachunguze hawa voda tujue hili linafanyika kwa makusudi au ni tatizo la system yao na ikibainika tatizo ni lao, basi warudishe fedha zetu pamoja na fidia kwani wanatuingiza gharama ambazo hazikuwa za lazima kwetu.

Naomba kama kuna mteja mwingine wa voda aliekutana na hii kero aweke hapa maelezo/ushuhuda wake na kama Vodacom wako humu nao watupe majibu/ufafanuzi.
 
Mwaka wa 18 sasa natumia Airtel 100%.
 
Wana mambo ya ovyo sana.Kuna yale yakuunganisha watu kwenye manyimbo ya kijinga hawajali mtu ana status gani kwenye jamii wenyewe nikuunganisha tu.unampigia mtu simu na heshima zake unakutana na lijimbo la ajabu ulikimuuliza nayeye anashangaa.
 
Na hizi huduma ndio wanazotoza watu fedha wakati mtu wala hukuomba kujiunga nazo.
 
Sina mazoea kutumia voda juzi Salio likaniishia la mtandao ninaotumia nikataka kuwasiliana kwa haraka nikanunua credit kupitia mpesa wakati huo nilisha agiza nitumiwe kifurushi kwenye mtandao ninaotumia, kabla sijajiunga na hii ya voda ili nitumie nikawa nimeshatumiwa credit kwenye huu mtandao mwingine sa Leo nikakumbuka kutumia hii ya voda ile najiunga naambiwa salio halitoshi eti nikope...kuwapigia wanadai nimejiunga na huduma sijui ya daktari na wamekata 400 nami sijawahi jiunga wajinga sana hawa voda.
 
Wana mambo ya ovyo sana.Kuna yale yakuunganisha watu kwenye manyimbo ya kijinga hawajali mtu ana status gani kwenye jamii wenyewe nikuunganisha tu.unampigia mtu simu na heshima zake unakutana na lijimbo la ajabu ulikimuuliza nayeye anashangaa.
Na vimeseji visivyo na kichwa wala miguu
 
Sina mazoea kutumia voda juzi Salio likaniishia la mtandao ninaotumia nikataka kuwasiliana kwa haraka nikanunua credit kupitia mpesa wakati huo nilisha agiza nitumiwe kifurushi kwenye mtandao ninaotumia, kabla sijajiunga na hii ya voda ili nitumie nikawa nimeshatumiwa credit kwenye huu mtandao mwingine sa Leo nikakumbuka kutumia hii ya voda ile najiunga naambiwa salio halitoshi eti nikope...kuwapigia wanadai nimejiunga na huduma sijui ya daktari na wamekata 400 nami sijawahi jiunga wajinga sana hawa voda.
Huu unaweza kuwa ni mradi wa watu na sio tatizo la system.
 
Hawa takataka ukiweka hela lazima wakukate ukiuliza wanajibu ' Uliomba Sukari ya Zuchu' Nina line ya Tigo hawa hawana njaa na visenti vidogo ukibakiza hata 100 hawaigusi VODA nusu saa kubwa lazima wapite nayo.
 
Back
Top Bottom