Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,754
Ni wiki ya Mtandao wa Tigo Tanzania baada ya muajiriwa wake kitengo cha sheria kuwa mmoja wa mashahidi katika kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA.
Kampeni zimeanza kushika kasi kila kona kususia huduma za mtandao husika.
Hili lina madhara japo si makubwa. Mwaka jana Vodacom Tanzania ilipitia katika wakati mgumu kuhusiana na kutoa siri za wateja. Wateja wote ni wanasiasa wa upinzani wa chama cha CHADEMA. Kampeni ile ya kususia bidhaa na huduma za Vodacom Tanzania ilikuwa kubwa na mbaya, lakini yalipita japo jina lake lilichafuka kwa kaisi chake, ni zamu ya Tigo sasa.
Hizi kampeni za kususia bidhaa na huduma za mitandao husika haziwezi kufanikiwa kwa asilimia 100 lakini zinapeleka ujumbe kwa sauti ya juu kwa wahusika kwamba haya mambo si sawa na si sahihi hasa linapokuja hili la kulinda siri za wateja
Mimi siilaumu hii mitandao ya simu Tanzania. Ni sahihi kabisa kwa usalama wa nchi kuwa na nyoka na mapandikizi kila mahali.. Na hii sio Tanzania tuu bali ni popote pale ulimwenguni. Usalama wana watu wao kwenye sekta binafsi na za serikali pia. Wana nyoka wao kwenye makampuni makubwa na madogo. Kila mahali wapo na kiusalama sio kosa kabisa
Haya makampuni ya simu na sekta nyingine pia kuna wafanyakazi wanaajiriwa kwa vimemo ama kwa simu moja tuu.. Wengine huajiriwa kwa mlungula kabisa kuficha uhalisia na wengine huajiriwa kwa uwezo wao. Ni kati ya hao kuna nyoka na mapandikizi na kamwe huwezi kuwajua kwakuwa sifa moja ya usalama ni kuwa invisible kama huyu wetu hapa JF
Sasa kosa liko wapi? Kosa hili hapa
Kuna ombwe ama kasoro kubwa kwenye baadhi ya watendaji kwenye mamlaka zetu. Hasa linapokuja swala la kudili na wapinzani kwenye kaliba ya mashtaka na sheria za makosa ya jinai nk
Kama nilivyosema maswala yote ya usalama huwa ni invisible. Kwahiyo hata siku moja huwezi kumkuta mwanausalama wa taifa ngazi ya nyoka au pandikizi akisimama mahakamani na kutoa ushahidi. Kazi ya usalama ni kugundua na kuonesha tatizo lilipo.. Mamalaka za kisheria ndio hutafuta njia sahihi ya kudili nalo.
Kesi ya Mbowe imeonesha madhaifu mengi toka mamlaka zetu namna ya kuwatumia mashahidi vipenyo kama mashahidi visible hii ni hatari sana. Sana, na madhara yake ni mengi kama hilo la kujulikana kuwa kumbe kuna maafisa vipenyo huko na huko na kupelekea kuharibu biashara za wengine
Kitu kingine cha kushangaza ni hili la mashahidi wa ugaidi kuwa wazi na kujulikana na kila mtu. Kwa kanuni za kesi za kigaidi mashahidi hufichwa na ni ngumu mno kujulikana wazi wazi.
Tunapowatia ndimu machoni Tigo tusisayasahau na haya mengine mengi kwakuwa hata tunaokaa nao vijiweni mitaani, vijiweni mitandaoni huku wengine wakiwa ni wasiri wetu kati yao ni nyoka, mapandikizi na maafisa vipenyo