Madela Wa- Madilu
JF-Expert Member
- Mar 24, 2007
- 3,062
- 731
Nadhani huu ni wasaa wa kuwekeza kwenye siasa.
Nagombea nikishindwa, najaribu tena.
Nagombea nikishindwa, najaribu tena.
Ni ngumu sasa mbunge anayepata 7m kwa mwezi kumtetea mwalimu wa primary anayepata 150,000!
waungwana ingekuwa vizuri tuanzishe blogg or website ya kuandika mishahara na mapato ya Watumishi wa umma eg Wabunge,Mawaziri,Diwani,na Raisi wale wote wanaoingia madarakani kwa kura za wananchi.
pili tuweke register ya wabunge wangapi wanaudhuria ktk vikao vya bunge,and how long do seat in bungeni
wataalam wa IT haya tuanze kazi
Namba 1
mimi niko tayari.
Ibrah,Dk Slaa anamsaka Spika Sitta na Kamati yake ya Maadili ya Bunge. Wenyewe huwa hawataki mambo yao ya maslahi yawekwe kwenye public.
Dk. Slaa, Je, unao uwezo wa kuhimili rungu la Spika na Kamati ya Maaadili? Asante kwa kutujuza na rungu likikushukia bado tuko upande wako; usijali songa mbele.
Nsaji Mpoki,PINDA SITISHA UHALIFU HUU
WAKATI NATAKA KWENDA KUPUMZIKA BAADA YA KAZI NZITO ZA LEO NAPATA HADITHI YA AJABU SANA KUTOKA KWA WATOA TAARIFA WA MKOA WA CHIFU MKWAWA KWAMBA KATIBU MKUU TAMISEMI NA MAAFISA WAKE 43 WAMEAMUA KUFANYA ZIARA YA WIKI MOJA KATIKA MKOA HUO KWA LENGO ETI LA KUKAGUA MIRADI. STAILI MPYA YA KULA PESA ZA UMMA KWA KUJITAFUTIA VISAFARI USHENZI ILIYOBUNIWA NA WIZARA ILIYO CHINI YA WAZIRI MKUU AMBAYE ANAONGOZA MAPAMBANO YA KUZUIA ULAJI KWA NJIA YA KONGAMANO NA SEMINA.NAAMBIWA, KAMA HAMUAMINI MAJJID AMBAYE YUKO KWENYE CHANZO ACHUNGUZE ATAAMBIWA, RATIBA YA KUZURURA ZURURA, KULAMBA BIA NA KUTAFUNA KUKU WA WANANCHI MASIKINI IMEPANGWA. WATAKULA KUKU NA KUNYWA BIA UBENA, UPANGWA NA UKINGA. HIVI KWELI FEDHA HII YA KUWALIPA POSHO MAAFISA WOTE HAWA INATOKA WAPI. FIKIRI WATU 43 X 80,000/= X SIKU 12 ZA SAFARI UNAPATA NINI. jAZA MWENYE ONGEZA GHARAMA ZA MAFUTA, UCHAKAVU WA MAGARI, GHARAMA ZA VILEO NA UCHAFUZI MWINGINE. KUMBUKENI NCHI HII NI MASKINI HAINA HATA KIWANDA KIMOJA CHA MAJEMBE YA MKONO NA UCHUMI WAKE UNAPORMOKA TULIDHANI KATIBU MKUU HUYO BASI ANGEMHESHIMU WAZIRI WAKE MKUU NA KUACHA HARAKA MPANGO WA KWENDA KULA FEDHA ZA UMMA BILA KUJUA TIJA YAKE ITAKUWA NINI. NINAWAOMBA WANAHARAKATI, MZEE SLAA NA WENGINE SJHIKIENI BANGO JAMBO HILI WAACHE KUUHADAA UMMA. FEDHA HII IPELEKWE HOSPITALI YA MWANANYAMALA AU KWENYE MATIBABU YA MTOTO ALIYEZALIWA BILA FUVU/AMBAYE UTOSI WAKE UKO NJE HUKO SINGIDA. NADHANI MLISIKIA DAKTARI WA MKOA ROBERT SALIM ALIVYOKATA TAMAA NA KUONYESHA KUSHINDWA NAMNA YA KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO. SASA HUYU MAMA ALIYEPEWA DHAMANA NA UMMA KUSIMAMIA TAWALA ZA MIKOA ANGELIONA HILO NA KUPELEKA FEDHA HIZO HUKO BADALA YA KWENDA KUZIMWAGA JALALANI. TUNAUA TAIFA LETU BURE KWA MAMBO AMBAYO SI LAZIMA TUYAFANYE.
Kuhani,Mkuu Dr. Slaa, heshima mbele.
Naomba kujua wewe mshahara/marupurupu/posho unayosema ni too much kwa wabunge, huwa unaifanyia nini?
Umewahi kuipokea ukala?
Nilikuwa napitia magazeti ya bongo mtandaoni kupitia blog ya mshikaji kennedytz.blogspot.com,nikakutana na gazeti la Rai la tarehe 26 mwezi huu ambalo linaripoti kuwa mshahara wa mbunge wetu pamoja na malupulupu yake yote unafikia Tsh.6,000,000kwa mwezi!?(hebu pitia na wewe uone na mchanganuo hasa wa posho anayopata mbunge wa Tanzania.
Sasa nikajaribu ku-Google nione jinsi gani watanzania tunaripoti habari zinazohusu maslahi ya waheshimiwa wetu,na kwa kweli sikupata matokeo mengi sana.Habari hii inakuwa kama either ni mpya masikioni wa Watanzania,au ni kwamba kwa kweli watanzaia hatujui hasa waheshimiwa wanapata kiasi gani kama mishahara yao.Sasa swali,je ni kwa sababu mishahara ya waheshimiwa haiwekwi wazi watanzania wajue au ni uzembe wa wanahabari wetu kutuhabarisha kuhusu swala hili?!
Nampongeza Mh.Slaa ambaye kwanza alitoka akatamka kiwango halisi cha mshahara anaopata mbunge,na pia kutaka kiwango hicho kipunguzwe kwani ni kikubwa mno na badala yake pesa hizo zitumike kufanyia shughuli nyingine za maendeleo,lakini sina uhakika how serious he is really kulisimamia hili,kwani kwa jinsi ninavyojua litakuwa ni swa la kelele za kisiasa tu.Je anaweza kulifikisha likajadiliwa bungeni kwenyewe?!
Pia kingine nilichoona ni kwamaba eti Mh. spika kapangishiwa nyumba,na unajua pango lake ni kiasi gani?!Analipiwa Tsh.9,000,000 kwa mwezi!!!!Sikiliza sasa kichekesho,ambacho kinakutoa machozi,eti nyumba ya zamani iliyokuwa inatumika kwa makazi ya Spika aliuziwa Spika aliyetoka,kwa hiyo Spika aliyekuja akawa hana nyumba ya kukaa YENYE MAHADHI YA KIUSPIKA WA BUNGE.Na habari hii imethibitishwa na katibu wa bunge Dr.Kashilila.so waliuza nyumba ya Spika wakijua kabisa kuwa anyemfuatia hatakuwa na makazi! na sasa wamenunua kiwanja kujenga makazi ya kudumu ya Spika..!Hivi kweli vichwa vyetu vinafanya kazi au ndo funza wanapiga mark-time vichwani mwetu!!Anyway wadau mtalijadili hili kwa jinsi mnavyoliona..
Lakini Tanzania cha mtoto,kwani Mbunge wa Watani wetu wa jadi Kenya anapata sawa na zaidi ya Tsh.12,000,000 kwa mwezi!!!!!
HIVI TUTAFIKA KWELI??????????
- Nyumba ya uwt ipo Dar mkuu, mbunge toka lini akakaa nyumba ya uwt? Wewe huoni kuwa ni mauza uza hayo, unaonekana kumjua vizuri sasa vipi hujui Dar anaishi wapi mkuu? Nyumba ipo Obey mkuu, unaijua nyumba aliyokuwa kiishi Mzee Mzena zamani kabla ya kuhamia Regent?
FMES!
Kuhani,
Ukiona yanaenea, ujue yameundwa. Wabunge wa Chadema, tunapozunguka kuelimisha watanzania unadhani tumetumia nini? Badala ya kula na familia zetu, na kwa hili sijisifu, na ukitaka tazama rasilimali ninazomiliki ndipo utoe kauli hiyo. Hakuna asiye jua Dr. Slaa, alipoingia Bungeni alikuwaje, na leo yukoje? Nadhani inatosheleza kwa hatua hii. kwa kifupi zinatumika kuwakomboa Watanzania.