Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Rushwa ya kisiasa KWA WABUNGE HIYOOO ina maana wakiongezewa posho watazidi kushiba na kulevywa na shibe hivyo kusinzia wakati wenzao serikali wakikatiza na mikataba feki hadi langoni halafu kwa best practice hiyo mikataba ya kifo kwa umma itaitwa nyaraka nyeti za serikali.
pumbaf!!

wabunge kumbukeni kuwa sisi ndio tunawalipa mishahara ila serilkali inasimamia tu na kumbukeni kuwa kuna watanzania wengi wamepoteza wake zao na watoto kabla na wakati wa kujifungua kwa kukosa huduma bora ambazo hawawezi kulipia. kuweni na huruma kidogo TUGAWANE UMASKINI basi
 
Baada ya hayo matamshi ya Pinda, ninahamu ya kujua manesi, polisi, walimu watamwambia nini. Watanywea au watamtolea uvivu?

Mimi nadhani kwa mujibu wa ccm Pinda yuko sahihi kabisa. Kama ccm ilivyo na wenyewe, pia nchi HII ina wenyewe! Hili liko wazi kuanzia mishahara, afya hata haki hata katika vyombo vya sheria. Unapojaribu kutafuta haki Tanzania, swali la msingi kujiuliza ni haki ya nani, ukishajua hilo, basi utakubaliana nami kuwa NCHI HII INA WENYEWE.

Tufanye nini kurudisha nchi mikononi mwa wananchi, ndio mawazo yetu na hoja zetu zielekezwe. Tusipochukua hatua kuwaelimisha watanzania wenzetu juu haki na nguvu waliyonayo, hali itaendelea hivihivi. Watu wansubiri kuthubutu, sijui ni lini?. ETI BORA ZIMWI LIKUJUWALO!
 
Kuna haja ya maandamano makubwa yakiongozwa na waalimu, manesi, madaktari na askari kupinga hili na kudai haki zao. Pinda alionekana kama msaada kwa wananchi lakini inaonyesha anakuwa mzigo sasa kwa kubariki ufisadi bungeni
 
Mimi sijawahi kusikia mtu yeyote yule ambaye anasema Mshahara wake una mtosha ni Dr. Slaa pekeyake ndio ametoa hiyo kauli. Kwa upande wangu naona kuwa Pinda ameibuka na hiyo kauli ili kumnyong'onyeza Dr Slaa.

Pinda huyu huyu ameondoa posho za Warsha, Semina etc kwa watumishi wa serikali kwa ajili ya kupunguza matumizi ya fedha za umma leo anaibuka na kutaka wabunge waongezwe mishahara, Mbona huyu Mzee anakurupuka.!!!
 
oh! my God - hivi wananchi kwanini tusikatae kuhudhuria mikutano yao - hao wanaotukandamiza? Watu wamesimama/or wamekaa - halafu unawaambia maneno ya kuwaumiza kama hayo ya KUONGEZA VIPATO AMBAVYO NI VIKUBWA TAYARI - wakati Watanzania wengine wanakula kwa shida, matibatu shida, elimu shida ukichanganya na MADKTARI WALI0 BUSY KUTIBU, WALIMU WANAOTEMBEA MILES KWA MIGUU KUFUTA SENTI KIDOGO WANAYOPEWA - waziri wetu mkuu ametuangusha sana - ANANIKUMBUSHA MIAKA YA KUAMBIWA TULE NYASI...... PINDA inabidi afikirie sana anapotoa kauli zake - asidhani WATZ ni wajinga - cha kusikitisha ni kuwa WATZ tumekuwa wapole mno - tunatiwa vidole vya macho ..... tumenyamaza - WHERE ARE MEN OF THIS COUNTRY?????? ITS HIGH TIME TO TAKE ACTION AND SPEAK OF OUR RIGHTS - WE ARE FED UP
 
Nataka kujua uwezo wa Pinda kifedha na maisha ya familia yake na ndugu zake alio waacha kule Chala, na sumbawanga, je Kwenye famila yake hana mwalimu, daktari au nesi. je hana mkulima, au mvuvi, mfugaji nk. inabidi tuwajue halafu twende tukawahoji nao watoe mchango wao kuhusu hali halisi ya maisha labda pinda atawaacha huu upuuzi.

Mkapa aliwahi kufukuza baadhi ya nduguze. kikwete najua ndugu zake kadhaa wanataabika kinoma, huku wakiomba yala. sasa hawa ndio viongozi wetu baada ya kutuibia wanasahau hata ndugu zao je sisi wasaka nyoka kweli watatukumbuka??????.

dawa hapa tuchapane bakora mpaka kieleweke. amani wanayo wao wenye uhakika wa kula milo mitatu sisi hata mlo mmoja tabu, tupo vitani long time na tulisha poteza vyote hivyo hakuna jipya tuanzishe moto kieleweke.
 
Pinda nae anataka apate cheap support kwa wabunge wenzake ambao wana uchu sana na wameweka tamaa mbele kuliko uzalendo.aruhusu basi na mashangingi yanunuliwe maana hakuna sababu kuzuia mashangingi then unawalipa wabunge 12m kwa mwezi......unaacha nini unafanya nini?Pinda unatuzingua.
 
nyie mnadhani walivyomtoa machozi siku ile ana hamu nao?
lazma awape mkate wao wa kila siku ili adumu ktk fikra zao.
 
Pinda sio tu kwamba haelewi bali hajui wala hafahamu. Tatizo hapa sio kwamba hiyo mishahara ya wabunge ni mikubwa bali ni mikubwa mno ukilinganisha na mishahara ya wafanyakazi wengine wa serikali. hasa madaktari, waalimu, polisi, jeshi, na watumishi wengine wengi serikalini.
Vile vile haina uwiano na mapato ya nchi na haizingatii maisha ya mtanzania wala pato halali la mtanzania. sasa kama mbunge hawezi kuishi kutokana na pato la nchi kweli ataweza kuwa na fikra za kuisaidia nchi yake. Hili ni tatizo la watu kugeuza siasa ndio ajira.

Pale wanapo fanya utafiti wa mishahara yabunge wakilinganisha na lile la uingereza nafikiri tunaona jinsi gani bunge limekuwa la kifisadi. bunge na wabunge wameamua kumfanyia mwananchi ufisadi kwenye kodi zake.
Ama kweli kila kitu chini ya jua ni ubatili mtupu.Ubatili ubatili mtu.

Sioni sababu gani , Polisi, wanajeshi, waalimu, madaktari,manesi,nk wasigome kudai nyongeza ya mishahara kwani wanayolipwa huwezi kuishi hata wiki moja. Waitishe migomo ya kitaifa kudai nao walipwe angalau robo ya mishahara ya wabunge wao na kuzingatia hali halisi ya maisha ya tanzania na bei na mifumoko yake.

Kinepi, hapo umeongea jambo la muhimu sana,
kwa kauli hii ya Pinda, ina bidi vyama vyote vya wafanyakazi, viitishe migomo kwa wafanyakazi wote wa serikali kulaani na kupinga unyonyaji huu, na pia kuwa tayari kubwaga manyanga, hao wabunge waje wawe madakitari walimu na wafanye kila kitu!

grrrrrrrrrrrrrrrrr inaudhi sana ebo!

Yaani badala aongelee mwalimu anashinda anahangaika na watoto mwezi mzima anaishia kupata laki moja, nesi anaokoa maisha ya raia anapata laki moja, anakuja na upuuzi eti wabunge mil 7 kwa mwezi hazitoshi? kwa lipi hasa hilo walifanayalo nyeti zaidi ya wengine??
 
Naona CiCiM wanajichimbia kaburi lao wenyewe.

Katika ripoti ya CAG, nafikiri nimesoma kuwa kuna mamilioni ya malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi na watumishi wa umma. Sidhani kati ya hayo malimbikizo, kuha hata shillingi moja ya wabunge.

They will pay the price.
 
Pinda nae anataka apate cheap support kwa wabunge wenzake ambao wana uchu sana na wameweka tamaa mbele kuliko uzalendo.aruhusu basi na mashangingi yanunuliwe maana hakuna sababu kuzuia mashangingi then unawalipa wabunge 12m kwa mwezi......unaacha nini unafanya nini?Pinda unatuzingua.

Pinda anajichanganya mwenyewe, wafanyakazi wengine wa serikali wanatakiwa wangunge mikanda, Wabunge mishahara haiwatoshi. PINDA vipi tena wewe si ndio ulikuwa unajiita mtoto wa mkulima?

Leo unatuambia Milioni 7 wanazozipata wabunge haziwatoshi kwa kukaa bungeni na wengi wao wakiwa wanasinzia. Kweli 2010 ndio hiyo kila mtu anatafuta staili yake ya kutoka.
 
Wapewe tu, mbona wenzao wa UK wanalipwa Pound 64,766/= kama Tsh 127,893,795.80 bila kodi na ukizingatia hili ni Bunge la kuigwa mfano na ni la Commonwealth. While now wanalipwa only Tsh 156,000,000/= hii ni pamoja na floating, sitting, enterteinment, takrima poshoz.

Summary of current rates with effect from 1 April 2008
Members' parliamentary salary £63,291 from 1 April
Allowances
Staffing Allowance Maximum of £100,205
Incidental Expenses Allowance (IEP) Maximum of £22,193
IT equipment (centrally provided) [worth circa £5,000]
Pension provision for Members' staff 10% of employee’s gross salary
London Supplement £2,916
Additional Costs Allowance Maximum of £24,006
Winding up Allowance Maximum of £40,799
Communications Allowance Maximum of £10,400
Car Mileage (per mile) 40p (for first 10,000 miles)
25p (after 10,000 miles)
Bicycle allowance (per mile) 20p
Motorcycle allowance 24p

Sasa mtaalam wa kujumlisha na kubadilisha fedha afanye totalization na comparison ya kile wanachopata pale B.... opps Mjengoni
This factsheet is available on the internet at:
Page could not be found | Houses of Parliament
ons_and_archives/factsheets.cfm
 
My take
Hivi ni kweli Pinda ni mtoto wa mkulima?
Ameacha kutetea mishahara ya watumishi wa ngazi za chini ambao maisha yao yamekuwa ya kukopa kopa na mshahara unaishia kulipa madeni ya mwezi uliopita..watumishi hawa ambao kwa kweli wanaishi maisha ya hali ya nchi sana kulingana na mishahara wanayo pata serikalini kama walimu,manesi,polisi na wengine neo.
Pinda umeshindwa kuwatetea hawa wanyonge umeamua kutetea ulaji wa tumbo lako,hivi haya mamilioni mnayo pewa kwa mwezi ukigawa utawalipa walimu wangapi kwa hiyo milioni 7? kwa mshahara wa 200,000/= naamini Pinda umepotoka na nina amini wewe sasa ni mtoto wa Bepari si mkulima tena.

Hakuna la ajabu alofanya Pinda. Unaweza kutegemea nini kutoka kwa Waziri Mkuu wa serikali ya MAFIOSO?
 
Kwa kazi gani wanayoifanya hao Wabunge mpaka mishahara yao haitoshi? Wanakutana kwa vikao vya Bunge kwa miezi isiyozidi minne na miezi mingine zaidi ya minane wanafanya uzururaji tu.

Namuunga mkono Dr Slaa kwamba mishahara na marupurupu ya Wabunge ni mikubwa mno na inastahili kupunguzwa kwa kiwango kikubwa na savings zipelekwe kwenye mishahara ya Walimu, polisi, madaktari na polisi.
 
Pinda sio tu kwamba haelewi bali hajui wala hafahamu. Tatizo hapa sio kwamba hiyo mishahara ya wabunge ni mikubwa bali ni mikubwa mno ukilinganisha na mishahara ya wafanyakazi wengine wa serikali. hasa madaktari, waalimu, polisi, jeshi, na watumishi wengine wengi serikalini.
Vile vile haina uwiano na mapato ya nchi na haizingatii maisha ya mtanzania wala pato halali la mtanzania. sasa kama mbunge hawezi kuishi kutokana na pato la nchi kweli ataweza kuwa na fikra za kuisaidia nchi yake. Hili ni tatizo la watu kugeuza siasa ndio ajira.

Pale wanapo fanya utafiti wa mishahara yabunge wakilinganisha na lile la uingereza nafikiri tunaona jinsi gani bunge limekuwa la kifisadi. bunge na wabunge wameamua kumfanyia mwananchi ufisadi kwenye kodi zake.
Ama kweli kila kitu chini ya jua ni ubatili mtupu.Ubatili ubatili mtu.

Sioni sababu gani , Polisi, wanajeshi, waalimu, madaktari,manesi,nk wasigome kudai nyongeza ya mishahara kwani wanayolipwa huwezi kuishi hata wiki moja. Waitishe migomo ya kitaifa kudai nao walipwe angalau robo ya mishahara ya wabunge wao na kuzingatia hali halisi ya maisha ya tanzania na bei na mifumoko yake.
Inamaanisha kazi ya siasa ni ya ufanisi zaidi na ya kuthaminiwa kuliko ya Professionals, haya yanaitwa matusi ya nguoni, na inasikitisha wasomi wa tanzania ni mabwege kama watu walio vijijini, kuanzia Ma-lecturer wa chuo kikuu ambao hutufundisha sisi, na ndio kioo cha jamii. Watu kama Akina Makamba ndio wanatuongozo na kutuibia, na sisi tunapiga makofi.
 
Pinda anajichanganya mwenyewe, wafanyakazi wengine wa serikali wanatakiwa wangunge mikanda, Wabunge mishahara haiwatoshi. PINDA vipi tena wewe si ndio ulikuwa unajiita mtoto wa mkulima??? Leo unatuambia Milioni 7 wanazozipata wabunge haziwatoshi kwa kukaa bungeni na wengi wao wakiwa wanasinzia. Kweli 2010 ndio hiyo kila mtu anatafuta staili yake ya kutoka.

Wewe unamzungumzia pinda Yupi? aliyesema ni mtoto wa mkulima ni yule pinda ambaye alikuwa bado hajaapishwa! baada ya kuapishwa siyo mtoto wa mkulima tena. Ni mwenzao na wao. Ni huyu huyu ambaye huwa anasema serikali haina pesa!!

PINDA, hebu angalau uvae viatu vya walimu, polisi,na wakulima wa jembe la mkono kule kijijini ulikotoka - yaani kodi wanayoporwa kwenye vijishahara/vijipato vyao vidogo namna hiyo ndiyo mjiongezee mishahara hivyo!
muwe na angalau chembe ya huruma kwa mwananchi
 
Wewe unamzungumzia pinda Yupi? aliyesema ni mtoto wa mkulima ni yule pinda ambaye alikuwa bado hajaapishwa! baada ya kuapishwa siyo mtoto wa mkulima tena. Ni mwenzao na wao. Ni huyu huyu ambaye huwa anasema serikali haina pesa!!

PINDA, hebu angalau uvae viatu vya walimu, polisi,na wakulima wa jembe la mkono kule kijijini ulikotoka - yaani kodi wanayoporwa kwenye vijishahara/vijipato vyao vidogo namna hiyo ndiyo mjiongezee mishahara hivyo!
muwe na angalau chembe ya huruma kwa mwananchi

Jibaba Bonge, nimekupata kumbe sasa hivi sio mkulima tena kama mimi na wengine wengi. Sasa hivi ni mwenzao na hana hata HURUMA bado anaona 7m ni ndogo. Pinda vipi tena mbona unafanya mambo ndivyo sivyo, kanusha kauli yako watanzania wataona uliteleza tu...!!!
 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Raisi -Mzigo

Waziri Mkuu - Mzigo

Wabunge - Viazi

Wanainchi - wapo wapo kila kitu wao kwao tambarare!

Unategemea nini?
 
Kwa kazi gani wanayoifanya hao Wabunge mpaka mishahara yao haitoshi? Wanakutana kwa vikao vya Bunge kwa miezi isiyozidi minne na miezi mingine zaidi ya minane wanafanya uzururaji tu. Namuunga mkono Dr Slaa kwamba mishahara na marupurupu ya Wabunge ni mikubwa mno na inastahili kupunguzwa kwa kiwango kikubwa na savings zipelekwe kwenye mishahara ya Walimu, polisi, madaktari na polisi.


Babu Ataka Kusema!

Nakushukuru for taking trouble kuwasemea Polisi na Walimu kwani over 98% yao hawana facility hii ya internet. Hapa jamii kuna wababe watakuuliza kwa nini unawasemea!!

The other side of it tujiulize pamoja na sheria za nchi hii kukataza migomo ya watumishi kama polisi. walimu na madaktari pamoja na watoa huduma wengine. Hebu tujiulize kwa nini hawagomi wakati wengi wao hiyo mishahara haitoshi kwa lolote!

Majibu kila mtu atakuwa na ya kwake!UTITIRI WA RUSHWA!!! Kila mbuzi anakula kulingana na urefu wa kamba yake period!!!

Ndio maana na serikali kwa kujua hilo wanafanya usanii na hii ni hatari. Wabunge wote wakapimwe akili including the president watuambie ni vipi Mbunge anapewa posho ya kikao cha siku moja ambayo inazidi mshahara wa polisi mwenye cheo cha chini!!! alafu anamwambia asidai mchango kwa hiace!

Kunatakiwa tuanze ukombozi upya ndio maana nchi ambazo watu hawajalogwa kama hapa tz kuna mapinduzi ya kila aina asubuhi na jioni siombei hilo lakini!!!!! Tusiendelee kumlaumu RA sisi wamatumbi tunakulana wenyewe!!!! HAINGII AKILINI KUMBEZA DR.SLAA that man is serious ooh!!70x Jakaya Mrisho Kikwete he is peredential material!!!

Pinda endelea kulia tu sijui hata kama kule kijijini Sumbawanga una hata vyumba viwili!!! NDIO maana JMK picked you kwani you are much much weaker than him!
 
Wapewe tu, mbona wenzao wa UK wanalipwa Pound 64,766/= kama Tsh 127,893,795.80 bila kodi na ukizingatia hili ni Bunge la kuigwa mfano na ni la Commonwealth.


Tanzania yetu hii! Huwezi kuacha kushangaa kila kukicha maana kila siku inaleta viroja vyake!
Ati wanajilinganisha na nchi zingine tena mpaka na Uingereza! Mbona ni kwenye mishahara ya wabunge tu? Kwanini si mishahara ya Waalimu, madaktari na wengineo? Mbona wasijilinganishe pia kwenye mambo mengine kama uwajibikaji, mifumo, taratibu, nyenzo,maadili ya uongozi,miundombinu na mengineyo?Mbona wasilinganishe jinsi wenzao wanavyofanya kazi na kuwajibika kwa wale waliowachagua kikamilifu?

Hilo tukio la jana tu la kulipuka mabomu na kuathiri wananchi, isingetosha mtu kuwajibika? Huku wamefanya nini zaidi ya kuunda BARAZA la kuchunguza ( siyo Tume tena ili wananchi waone ni kitu kipya) wakishachunguza ili iweje?
Sasa hivi mvua zinanyesha walioathirika na hayo mabomu na nyumba zao kubomoka, wanalala wapi, wanakula nini, wana uhakika gani na usalama wao na mali zao? WABUNGE WA ENEO HUSIKA SO FAR WAMESHAFANYA NINI?
Maswali ni mengi sana ila niachie hapo.
 
Back
Top Bottom