Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,418
114,398
Kuna mtu anayejua mshahara wa raisi wa Tanzania ni kiasi gani?

Kuna mtu kaniambia ni $200,000 na kitu kwa mwaka...sikuamini lakini akanihakikishia kuwa taarifa zake ni za uhakika.

Bado ninasita kuamini ingawaje sina taarifa zozote na sijawahi kuona mahala popote pale kuhusu mshahara wa rais.

Na mshahara wa makamu wa raisi..?
Waziri mkuu..?
Spika wa bunge..?
Mkuu wa majeshi ya ulinzi, polisi,magereza..?
Jaji mkuu..?

Kama kuna mtu anayejua...ni wapi tunaweza kupata taarifa hizi?
 
Hiyo nayo ni siri kubwa Watanzania hatustahili kuijua!!! Tunajua mshahara wa Rais wa Marekani lakini hatujui mshahara wa Rais wetu!

Bill clinton ndiye alikwa Rais wa mwisho wa Marekani kupokea mshahara wa $200,000 kwa mwaka alipomaliza awamu yake ya miaka minane mwaka 2000. Kuanzia 2001 mshahara wa Rais wa marekani uliongezwa na kufikia $400,000 kwa mwaka.

Kama kumbu kumbu zangi ni nzuri walidai wameoungeza maradufu kwa sababu ni miaka mingi imepita tangu nyongeza ya mwisho na pia gharama za maisha zimepanda sana. Lakini tukirudi kwa Rais wetu hatuujui mshahara wake!!! Mwe hii ni sirikali!!!
 
Niliona hapa, kama sikosei kwenye topic moja kuhusu mkapa, mdau moja alisema mshahara wa rais ni $12,000 kwa mwezi.

Kama nimekosea naomba nirekebishwe

Nadhani ilikuwa ni mshahara wa Gavana wa BOT ni $ 12,000 kwa mwezi, Rais mshahara wake ni tax free kwa hiyo anauchota kama ulivyo.
Kuna mchangiaji mmoja alisema mawaziri wetu wanalipwa $ 1,100 kwa mwezi http://jamboforums.com/showpost.php?p=40900&postcount=20
 
Hivi mishahara na marupurupu ya viongozi wa juu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inajulikana? Viongozi hawa ni Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na Spika.

Nauliza kwa sababu nadhani mishahara wa marais nyingine inakuwa wazi. Kwetu ikoje?
 
Mwaka jana Mbeki aliongezewa kutoka Rand 1.18 milioni hadi rand 1.27 milioni ingawa Tume ya Moseneke ilipendekezwa alipwe rand 1.89 milioni.

Rais Kibaki alikataa nyongeza ya 186% ambayo inasemekana ingemtoa kutoka US$ 10,000 kwa mwezi hadi US$ 27,600 na marupurupu ya US$ 18,600. Sisi wa kwetu analipwa ngapi? Na nani anayeamua kiasi gani anastahili?
 
Bwana hata mie ningependa kujua ila inaonekana ni siri kubwa sana,nachojua tu ni kwamba wanalipwa toka kwenye mfuko mkuu ambao hauko subject to debate by parliament,sasa sijui ndio kusema Rais huwa anajiuamulia au vipi.manaake huu mfuko mkuu unaoitwa consolidated fund sijui hata ni nani huwa anaushikilia
 
Heshima Mbele Wakuu,

Jana katika kikao cha wabunge kilichofanyika pale DIIC na kuhudhuliwa na baadhi ya wabunge,waliomba kuongezewa Posho na Mishahara,.

Spika wa bunge ak.a Mzee wa kukanususha 'Vilowassa' alitoa hoja kwa wabunge kwamba waongezee pesa katika bajeti ya bunge ili wao wapate maslahi zaidi,hoja hiyo iliungwa na Mhe. Masilingi na zitto ,ila zitto alissisitiza hilo liambatane na kurudishwa kwa pesa za EPA ili zifanye kazi ya kuendeleza Maendeleo ya Wananchi.

mhe. Massilingi alienda mbali zaidi na kusema inabidi posho iboreshwe ili wasifanye shughuli zingine na wawatumikie wananchi.

Je wakuu mnaona ni haki na bora kwa hawa waheshimiwa waongezee Mishahara??Je posho yao Haitoshi??

Kuna haja ya kuwa na wagombea ambao wanaojitosheleza kama Ndesamburo ili wawatumikie wananchi..sasa nimeanza kuyakumbuka maneno ya Ndesa Pesa wakati akichangia mjadala wa suala la RDC katika kiako nkilichopita cha bunge.

Wabunge wanastaili kuongezewa mishahara zaidi ya wafanyakazi wa Serikali.

Namnukuu Mzelohalisi hapa:

JF,

Mshahara na marupupupu ni milioni 7 kwa mwezi! Bado vikao vya kamati na maslahi mengine!

Kwa mwaka Mbunge hupata Shilingi milioni 84!

Na akimaliza mda wa miaka mitano hupata milioni 30 kama kifuta jasho!

Mwal Msingi hulipwa 150,000 kwa mwezi na kwa mwaka hupata 1,800,000! Hebu angalia tofauti ni shilingi 82,800,000 kwa mwaka!!!

Uwiii !!!!! Jamani hii tofauti kwa nchi maskini ni kubwa mno!!!

Ndo maana rushwa ktk uchaguzi haitaisha!

Hivi Jaji Mkuu, Spika, Raisi na PM kuna mtu ana data wanalipwa kiasi gani tz?

Source: Slaa akiongea Hedaru Bunge mradi wa ulaji

Pia hapa:

Breakdown............

Bei ya Mafuta katika vituo vya mafuta ni kati ya shilingi 1,200 kwa jiji la Dar es Salaam na shiling 1,500 kwa mji wa Musoma, Mbunge amekuwa akipata lita moja ya mafuta kwa shilingi 2,500 ikiwa ni shilingi elfu moja juu zaidi kwa gharama ya Musoma ambayo ni mji wenye bei ya juu ya mafuta aina ya petroli.

Kama hiyo haitoshi, Mbunge mmoja anapatiwa Lita 1,000 za mafuta kila mwezi ambapo kiasi hicho ni sawa na Sh 2,500,000. Licha ya fedha hizo, kila Mbunge sasa anapewa asilimia 40 ya fedha hizo kwa ajili ya matengenezo ya magari yao, kiasi ambacho ni sawa na Sh 1,000,000.

Kiasi hicho cha fedha ni mbali na Sh 765,000 kwa ajili ya matumizi ya ofisi yake kwa mwezi, na pia anapatiwa mshahara wa dereva kiasi cha Sh 100,000 kila mwezi.

Malipo haya hayaisihii hapo, bali mbunge sasa anapata Sh 300,000 kama posho kwa ajili ya dereva wake kila mwezi kwa ajili ya kutembelea jimbo. Kwa maana hiyo dereva wa Mbunge anapaswa kulipwa Sh 400,000 kila mwezi kutoka kwa Mbunge.

Mbunge pia anapewa kiasi cha Sh 45,000 kila siku kwa muda wa siku 10, ambapo anapaswa kutumia fedha hizo kutembelea jimbo kila mwezi. Kwa ajili ya kazi hii jumla anapewa Sh 450,000 kila mwezi kwa ajili ya kutembeelea jimbo.

Mshahara wa mbunge nao umeogezeka sasa kutoka Sh 1,200,000Sh 1,800,000. Jumla kwa mwezi Mbunge anapata Sh 6,915,000 kutoka serikalini.

Magari hayo wanayoendesha wabunge kila miaka mitano huwa wanakopesha Sh 40,000,000 kwa ajili ya kununua gari analotumia kwa muda wote wa miaka mitano anayokuwa bungeni.

Hata hivyo, wabunge wanapata mafao zaidi ya hayo kwani kwa muda wanaokuwa bungeni hupata posho za vikao kwa wastani wa Sh 100,000 kila siku na hiyo haiesabiki katika sehemu ya malipo yaliyotajwa hapo juu.

Bunge linalipa $ 7,000 kila mwezi kwa ajili ya nyumba anayoishi Spika wa Bunge, Samwel Sita. Nyumba ipo Masaki. Nyumba iliyokuwapo awali, ilinunuliwa na Spika wa Bunge aliyemaliza muda wake, Pius Msekwa.

note:Villowassa=vimada=kashfa
 
These wabunge must understand the issue is not about pay rise; it is about increasing productivity. Kuongeza mishahara bila tija, ni chanzo cha mfumuko wa bei katika uchumi.

Every time, these wabunge will demand more and more pay rise as purchasing power falls since there is no TIJA. And if the government is not careful enough, this is a recipe for disaster--inflation spiral. TIJA,TIJA,TIJA ndio mbadala. Kuongeza mishahara isiyoendana na TIJA ni sawa na kubandika plasta juu ya donda ndugu.
 
Back
Top Bottom