Mishahara mipya Novemba 2017 kuna ongezeko?

Mishahara mipya Novemba 2017 kuna ongezeko?

Duu tuwekeze zaid...mana huku kuajiriwa huwezi kutoboa...kuajiriwa iwe kama kibarua tu
 
Wakuu kwema?Nadhani Leo 17 November,Payroll zimeshawafikia wakuu wa idara huko kwenye Halmashauri mbalimbali nchi nzma.

Itapendeza zaidi Maafisa Utumishi au Wakuu wa idara mkitujuza kuhusu Orodha za malipo ya Mishahara mipya kuanzia November hii kama Mkulu alivoahidi!Je kuna ongezeko?Na kama lipo Ningependa kufahamu scales zake zimekaaje kuanzia Madaraja ya chini mpaka juu.

Ahsanteni,nawasilisha!!
Kinachoendelea huku halimashauri ni kukusanya nyaraka za wale waliokua wamepandishwa madaraja lakini malipo hayakufanyika na wale waliokupandishwa na mishahara mipya kufutwa.
 
SCALE MPYA KWA WATUMISHI KUANZA KUTUMIKA NOV. 2017


1.TGS A1-746,000
2.TGS B1-894,000
3.TGS C1-982,500
4.TGS D1-1,139,000
5.TGS E1-1,219,000
6.TGS F1-1,405,000
7.TGS G1-1,670,000
8.TGS H1-1,884,000~ 2,665,000.

Hiyo ndiyo mishahara mipya ambayo waraka umetoka leo usiku huu.Inaanza kutumika
Novemba 2017.
*Kumbuka:mtumishi mwenye degree alietoka chuoni huwa anapokea mshahara grade: TGS D1*
Hivi ndivyo Dr.Shika alivyosikika akisema itapendeza mambo yakiwa hivyo hapa nchini,lakini hili jambo halipo kabisaaaa.
Kweli we unatafuta kiki!
 
Hapa mwendo ni kujilipua tu na crdb salary advance....haimalizi matatizo ila inasaidia kuyasogeza mbele.....loh!
Hivi Mkuu ukishatusua haya mapene ya Salary Advance huwa unarejesha mwenyewe au huwa wanakata wenyewe juu kwa juu mpunga ukiingia?! maana na hadi sasa ndio inayonipa heshima!
 
Watu wengi Hawajui tu tena Hawajui kwanini mkulu hawapendi watumishi.Watumishi wengi walishajitambua kitambo sana.Watumishi wachache waliokuwa wanakula keki ya nchi ndio walikuwa pro CCM.Mkulu analipiza kisasi kwa watumishi maana anajua wengi hawakumpa kura
He he he heee,sasa ndo watampa 2020???
 
Sasa mkuu mm nimeelewa kuwa ukikopa utalipa riba ya 5% ya pesa uliopewa. Hapo ulipokopa 95, 000/ asilimia tano ni 4,750/ na sio 5,000/. Kama wakikata 5, 000/ walipaswa wakupe 100, 000/. Na 5% ya 190,000/ ni 9,500/ sio 10,000/ utakayolipa.
Hujasoma masharti yao au? Riba inakatwa upfront....kwamaana hiyo ukichukua laki wanatoa kabisa riba yao.
 
Na ndiyo hiyo nyongeza, imeahi kutokea kwa Mkapa range kama hiyo and Mkapa was not friendly na wafanyakazi, quite hostile!
Dawa sio kuongeza mishahara, bali suluhu ni kuongezs uzalishaji nchini katika kila nyanja ili shillingi ipande thamani na vitu vishuke bei, tjen kutakua hakuna haja ya kuongeza mishahara baada ya bidhaa na huduma kushuka bei
 
SCALE MPYA KWA WATUMISHI KUANZA KUTUMIKA NOV. 2017


1.TGS A1-746,000
2.TGS B1-894,000
3.TGS C1-982,500
4.TGS D1-1,139,000
5.TGS E1-1,219,000
6.TGS F1-1,405,000
7.TGS G1-1,670,000
8.TGS H1-1,884,000~ 2,665,000.

Hiyo ndiyo mishahara mipya ambayo waraka umetoka leo usiku huu.Inaanza kutumika
Novemba 2017.
*Kumbuka:mtumishi mwenye degree alietoka chuoni huwa anapokea mshahara grade: TGS D1*
Hivi ndivyo Dr.Shika alivyosikika akisema itapendeza mambo yakiwa hivyo hapa nchini,lakini hili jambo halipo kabisaaaa.
Hapa naona unatwanga maji kwenye kinu.
Serikali hii ilipe hivyo viwango huku kauli mbiu yake ni kupunguza matumizi.

Chukulia hesabu ndogo tu kwamba hadi leo pamoja na kujinadi kwa mbwembwe zote kuna waajiliwa wapya hawajalipwa pesa yao ya kijikimu, pamoja na matamko mazito na ya kuogofya kutolewa na siri kali hii.

Leo ilipe hayo madaraja ya mshahara haipo, watu walishaambiwa km mshahara hautoshi wakalime.
 
Hivi Mkuu ukishatusua haya mapene ya Salary Advance huwa unarejesha mwenyewe au huwa wanakata wenyewe juu kwa juu mpunga ukiingia?! maana na hadi sasa ndio inayonipa heshima!
Unachekesha sana we jamaaa.....!

Ingekuwa ni kupeleka mbona wangejuta....

Wanakukata juu kwa juuu huko huko kama kodi vile!
 
Nimeitumia mara 2 hadi sasa sijaexperience hiko kitu....laba kwa vile hesabu kwenye uko wetu zililaaaniwa.

Ila mie maraa kwanza nilikopa lak nikapewa 95 elf. Siku ya salary nikalipa lak 1.

Mara ya pili nikachukua lak 2..nikapewa lak 190 elf...so keshokutwa nitalipa lak 2.

Mie hadi hapo naona sijaibiwa hata senti....nashukuru kwa aliyeleta hili wazo....maaana kimtaa mtaa hapa lak ilikuwa nalipa lak na 20....!
Uko sahihi kabisa, wako wazi na wala si wezi.
Wala si wezi hawa bali wanachofanya ni kuchukua ile 5% yao wakati unafanyiwa processing kabisa na wakati wa kulipa unalipa kile ulichokopa.
 
Back
Top Bottom