Haki na wajibu kwa watumishi wa Umma

A man with one idea

Senior Member
Jul 18, 2022
126
264
Haki na Wajibu wa Mtumishi wa Umma. Mtumishi wa Umma una wajibu wa kutumia elimu, ujuzi na bidii katika kutoa huduma bora kwa wananchi. Kadhalika una haki na stahiki mbalimbali unazopaswa kuzipata kutoka kwa mwajiri wako kama ifuatavyo:-

1. Kupewa Mkataba wa Kazi (Barua ya Ajira)
Mtumishi wa Umma una haki ya kupewa barua ya ajira inayoonesha jina lako, anuani yako, tarehe ya ajira, aina ya ajira, cheo, ngazi ya mshahara, kiwango cha mshahara na masharti mengine ya ajira yako [Rejea Kanuni D.32 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009]

2. Posho ya Kujikimu
Unapoajiriwa kwa mara ya kwanza unastahili kulipwa posho ya kujikimu ya siku 7 kwa ajili yako,. (Rejea Kanuni ya L. 6. Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2011). Aidha, unastahili kupata posho ya njiani kwa safari inayozidi masaa sita (6). Posho hii hulipwa kwa kiwango cha nusu ya posho ya kujikimu ya siku moja [Rejea Kanuni L. 2(3) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009]

3. Kuthibitishwa Kazini
Una haki ya kuthibitishwa kazini baada ya kipindi cha majaribio kisichozidi miezi kumi na mbili (12) chenye lengo la kupima tabia na utendaji wako wa kazi. Miezi mitatu (3) kabla ya muda wa majaribio kuisha, msimamizi wako wa kazi anapaswa kuamua kama:

Uthibitishwe kazini, au
Uongezewe muda wa majaribio, au Ajira yako isitishwe. Rejea Kanuni ya 14 (1) na (2) (a), (b) na (c) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003 na Kanuni D.40 na D.43 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009.

4. Likizo Maalum (Ruhusa)
Una haki ya kupewa ruhusa isiyozidi siku kumi na nne (14) kwa mwaka ili kushughulikia matatizo na masuala mbalimbali ambayo hayaepukiki kama vile msiba wa ndugu wa karibu ambao ni pamoja na baba, mama, mwenza na mtoto, kushiriki vikao vya vyama vya wafanyakazi, michezo, kuuguza, kufunga ndoa n.k. Iwapo utaomba ruhusa zaidi ya muda huo basi siku zitakazozidi siku kumi na nne (14) ni lazima zikatwe kutoka kwenye likizo yako ya mwaka.

Ni kosa kuomba ruhusa kufanya shughuli binafsi kama kulima, biashara, kufuga, kueneza dini au kufanya siasa kwani ni wizi wa muda wa serikali (Rejea Kanuni H.14 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009).

5. Likizo ya Mwaka
Baada ya kupita miezi nane (8) tangu ulipoajiriwa unastahili kwenda likizo ya mwaka ya siku ishirini na nane (28) ikijumuisha siku za Jumamosi na Jumapili na siku za sikukuu. Katika likizo hiyo, wewe, mwenza wako na watoto au wategemezi wasiozidi wanne mtakuwa na haki ya kulipwa nauli kwenda na kurudi kwenye makazi yako ya kudumu mara moja ndani ya kipindi cha miaka miwili cha mzunguko wako wa likizo [Rejea Kanuni H.1 (1), (2) na (3) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009 na Kanuni ya 97 (1) na (2) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003].

Iwapo mwajiri atazuia likizo yako ya mwaka utastahili kulipwa mshahara wa mwezi mmoja bila ya makato kama fidia [Rejea Kanuni ya 97(3) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003].

6. Likizo ya Uzazi kwa Mwanamke
Ikiwa wewe ni mwanamke unastahili likizo ya siku themanini na nne (84) au siku tisini na nane (98) (kama utajifungua watoto mapacha) ikiwa ni likizo ya uzazi mara moja ndani ya kipindi cha miaka mitatu.

Likizo hii haitaingiliana na likizo yako ya kawaida ya mwaka na iwapo ujauzito utaharibika au mtoto kufariki ndani ya miezi kumi na mbili (12) baada ya kujifungua, utastahili haki ya likizo ya uzazi katika ujauzito utakaofuata bila kujali masharti ya miaka mitatu [Rejea Kanuni H.12 (1-7) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009].

Aidha, kama utajifungua kabla ya kutimiza miaka mitatu baada ya kujifungua utastahili wiki 6 ambazo ni sawa na siku (42) siku hizi zitakakatwa/hazitakatwa katika likizo yako ijayo kulingana na mzunguko wako wa likizo.

7. Likizo ya Uzazi kwa Mwanaume
Ikiwa wewe ni mwanaume unastahili likizo ya uzazi ya anaglau siku tatu (3) mara moja ndani ya kipindi cha miaka mitatu (3) iwapo mke wako atakuwa amejifungua. Likizo hii inapaswa kuchukuliwa ndani ya siku 7 tangu mke wako alipojifungua na haitaingiliana na likizo ya mwaka [Rejea Kanuni ya H.13 (a) na (b) ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009].

8. Likizo Bila Malipo
Likizo hii hutolewa kwa muda usiozidi miaka mitatu (3) ili kukuwezesha kujiunga na mashirika ya umma, programu za kimataifa na mashirika ya kimataifa/ kitaifa yenye uhusiano na serikali. Ili kupata likizo hii ni sharti uwe umethibitishwa kazini na hauna mashauri ya kinidhamu.

Maombi ya likizo hii hupelekwa kwa Katibu Mkuu Utumishi kupitia kwa mwajiri wako. Aidha, hupaswi kulipwa mshahara, kupandishwa daraja na stahiki zako zote zitasimamishwa katika kipindi chote cha likizo hii [Rejea Kanuni ya 99 (1) na (2), ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003, na Kanuni H.19 (1) na (2) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009].

9. Likizo ya Ugonjwa
Likizo hii hutolewa kwa mtumishi mgonjwa baada ya kupata mapendekezo ya daktari yakithibitisha kwamba unapaswa kupumzika. Hutolewa kwa muda wa mwaka mmoja kwa utaratibu wa miezi sita (6) ya mwanzo, ambapo utapokea mshahara kamili na miezi sita ya mwisho utapokea nusu mshahara. Endapo hutakuwa umepona katika kipindi cha mwaka mmoja utastaafishwa kazi kwa ugonjwa [Rejea Kanuni ya 100 (1-2) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003].

10. Ruhusa ya Masomo
Ruhusa hii hutolewa baada ya mwajiriwa mpya kufanya kazi zaidi ya miaka miwili. Unaweza kuruhusiwa kwenda masomoni baada ya kuomba kuwekwa kwenye mpango wa mafunzo wa Taasisi.

Utaweza pia kuomba kugharamiwa na mwajiri au kujigharamia mwenyewe au kuomba ufadhili kupitia Bodi ya Mikopo n.k. Kwa kuwa nia ya masomo ni kukuendeleza kitaaluma, ni vema ukajiendeleza katika fani unayofanyia kazi (proffessional carrier development) [Rejea Kanuni ya G.7(1)(a-j) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009] kwa mujibu wa Mwongozo wa Uendeshaji wa Mafunzo kwa Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa. Wa mwaka 2008

11. Ruhusa Kwenda Nje ya Kituo cha Kazi
Huruhusiwi kutoka nje ya kituo chako cha kazi wakati wa saa za kazi bila ya ruhusa ya msimamizi wako. Pia, huruhusiwi kutoka nje ya kituo chako cha kazi kwenda nje ya mkoa wako bila ya ruhusa ya maandishi toka kwa mwajiri. Unapaswa kuomba ruhusa ya kwenda nje ya mkoa hata kama utasafiri siku za Jumamosi, Jumapili na siku za Sikukuu.

Pia, huruhusiwi kusafiri nje ya nchi bila ya kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi [Rejea Kanuni ya F.17(1-2) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009].

12. Likizo ya Kustaafu
Utakapokaribia kustaafu utastahili kupewa likizo ya siku ishirini na nane (28) ili kukuwezesha kujiandaa kabla hujastaafu (Rejea Kanuni ya 102 ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003).

13. Kupanda Madaraja ya Utumishi wa Umma
Kwa kuzingatia sifa za kimuundo, utendaji wa kazi, nidhamu kazini na uwepo wa bajeti ya mishahara mipya iliyotengwa na mwajiri, unastahili kupandishwa cheo (daraja) baada ya miaka mitatu

Tangu kuthibitishwa kazini au kila baada ya miaka mitatu (3) unapopanda kwa mara ya pili na kuendelea (Rejea Kanuni ya D.51 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009 na Waraka wa Katibu Mkuu Kumbukumbu CAC.45/257/01/E/83 wa tarehe 09 Septemba, 2013). Aidha, muda wa miaka mitatu (3) katika kupanda utategemea pia maagizo na maelekezo mbalimbali kutoka Ofisi ya Rais UTUMISHI katika kipindi cha utekelezaji wa IKAMA.

14. Matibabu
Unastahili kugharamiwa na mwajiri wako matibabu ambayo hayagharamiwi na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Unastahili kulipwa posho ya kujikimu na nauli kwenda kutibiwa nje ya kituo chako cha kazi, endapo utapewa rufaa na daktari [Rejea Kanuni 1 (1-2) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009]. Aidha, ukilazwa hustashili kulipwa posho ya kujikimu,.

15. Uhamisho
Unaweza kuhamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine na kustahili kulipwa malipo yafuatayo:

Posho ya kijikimu kwa siku 14 kwako, mwenza wako na nusu ya kiwango kwa watoto/wategemezi wako wasiozidi wanne.

Posho ya usumbufu kwa kiwango cha asilimia kumi (10%) ya mshahara wako wa mwaka mzima. Gharama ya kusafirisha mizigo kati ya tani 1.5 hadi tani 3 (kutegemea kiwango cha ngazi ya mshahara wa mtumishi)
Posho ya kujikimu ukilala njiani Nauli.

Endapo utaomba kuhama kwa sababu zako mwenyewe na umeishi zaidi ya miaka mtano (5) katika kituo chako cha kazi, au katika mazingira maalum mtumishi anapokaribia kustaafu na amefanya kazi nje ya Mkoa wake kwa muda wa miaka 10 mfululizo au zaidi, basi utastahili malipo husika kama mwajiri anao uwezo [Rejea Kanuni ya 107(1-5) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003 Kanuni J.4 na L.8 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009].

16. Fidia ya Kuumia au Kufa Ukiwa Kazini
Endapo utaumia au kufariki ukiwa kazini, utastahili kulipwa fidia kupitia Mfuko wa Fidia wa Watumishi (Rejea Kanuni ya 110 ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003).

17. Mikopo Mbalimbali
Una haki ya kukopa kwenye taasisi za kifedha/mikopo kwa makato ambayo kwa mwezi hayatazidi 2/3 ya mshahara wako. Hivyo basi, 1/3 ya mshahara wako ni lazima ibaki ili kukuwezesha kumudu maisha na kuondokana na mzigo wa madeni ili utekeleze majukumu yako ya kazi kwa ufanisi (Rejea Kanuni F.12 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009) ikisomwa pamoja na Ufafanuzi Kuhusu Utaratibu wa Kusiamamia Mikopo inayotolewa kwa Watumishi wa Umma na Serikali au Taasisi za Fedha,uliotolewa na Ofisi ya Rais Utumishi wa mwaka 2013.

18. Kushiriki Katika Shughuli za Vyama vya Wafanyakazi
Una haki ya kujiunga na kuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi kama vile TALGWU, TUGHE, CWT na CHAKAMWATA. Ni muhimu katika ushiriki huo, ukazingatia sheria na kujiepusha na migogoro na migomo isiyo ya kisheria (Rejea F.22 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009).

19. Posho ya Masaa ya Ziada
Iwapo utapata kibali cha kufanya kazi zaidi ya muda wa kawaida wa masaa ya kazi na umeajiriwa ukiwa mtumishi asiye wa zamu kama vile watumishi wa kada za afya, walinzi n.k., utastahili kulipwa posho ya masaa ya ziada kwa kiwango kilichowekwa na serikali (Rejea Kanuni ya L.21-22 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009).

20. Posho ya Kukaimu Madaraka
Iwapo utateuliwa kukaimu cheo cha madaraka kama vile Ukuu wa Idara au Ukurugenzi kwa zaidi mwezi mmoja (1) utastahili kulipwa posho ya kukaimu madaraka. Kiwango hicho ni tofauti ya mshahara wa cheo unachokaimu na mshahara wako wa cheo cha sasa (Rejea Kanuni ya L.15-18 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009) ikisomwa kwa pamoja na waraka wa Utumishi wa Umma Na.3,2018 Kuhusu Utaratibu wa Kukaimu Nafasi ya Uongozi. Pia, endapo mtumishi hajafika ngazi ya Afisa Mwandamizi atakaimishwa lakini hatastahili kulipwa posho ya madaraka na badala yake atakuwa katika kipindi cha kujifunza ‘Career Develeopment’

21. Posho ya Nyumba
Iwapo una haki ya kupewa nyumba kama vile mkurugenzi au mkuu wa idara na hujapewa nyumba wala kununua nyumba ya serikali, una haki ya kupewa posho ya nyumba kwa kiwango kilichowekwa na serikali kwa mwezi (Rejea Kanuni ya L.34 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009).

22. Posho ya Sare
Iwapo wewe ni mtumishi wa kada zinazostahili kulipwa posho ya sare kama vile madaktari, wauguzi, wanasheria, makatibu mahsusi, walinzi n.k, utastahili posho hiyo kila mwaka kwa kiwango kilichowekwa na serikali.(Rejea Kanuni ya L.37 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009).

23. Posho ya Mavazi
Iwapo utapata nafasi ya kwenda nje ya nchi kikazi au kimasomo unastahili kulipwa posho ya mavazi kwa kiwango kilichowekwa na serikali. Posho hiyo italipwa mara moja ndani ya miaka miwili ili kukuwezesha kununua mavazi maalumu yanayohitajika kwenye nchi unayokwenda (Rejea Kanuni ya L.20 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009).

24. Posho za Viongozi
kiIwa utateuliwa kushika nafasi ya uongozi katika taasisi kama vile ukuu wa idara, kitengo au ukurugenzi utastahili posho ya simu, umeme na samani kwa kuzingatia viwango vinavyotolewa na serikali kwa mwezi.

25. Kuacha Kazi
Una haki ya kuacha kazi kwa kutoa taarifa ya maandishi ya miezi 3 ya kusudio hilo au kutoa taarifa ya saa 24 ya kuacha kazi na kulipa mshahara wa mwezi husika (Rejea Kanuni ya F.49 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009).

Angalizo
Kwa kuzingatia Waraka wa Katibu Mkuu UTUMISHI Kumbukumbu Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010 iwapo utaacha kazi utapaswa kupata kibali cha kuajiriwa upya serikalini kama utaamua kuomba tena ajira serikalini.

26. Gharama za Mazishi
Ikitokea mtumishi amefariki au kufiwa na mwenza au mtoto wako, mwajiri atagharamia jeneza, uchimbaji wa kaburi, sanda, manukato na mapambo na usafiri kwenda kuzikwa eneo la makazi yako ya kudumu au eneo lingine lolote atakalochagua mtumishi mwenyewe (Rejea Kanuni ya Q.7(1-3) ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009).

27. Mtumishi wa Umma Kugombea Nyadhifa za Kisiasa
Unaruhusiwa kugombea nyadhifa za kisiasa kama udiwani, ubunge na urais. Hata hivyo utaratibu ni kama ifuatavyo:-

Ukigombea nafasi ya ubunge katika jimbo la uchaguzi, ubunge wa viti maalumu, ubunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, mara baada ya Tume ya Uchaguzi kukutangaza kuwa mgombea wa ubunge, utalazimika kuacha kazi na utalipwa mafao yako.

Ukigombea nafasi ya udiwani katika kata mara baada ya Tume ya uchaguzi kukutangaza kuwa mgombea wa udiwani, utalazimika kuacha kazi na utalipwa mafao yako.

Ukiteuliwa na waziri mwenye dhamana na TAMISEMI kuwa diwani, utakuwa na hiari ya kuchukua likizo bila malipo kwa kipindi chote utakachokuwa diwani, au kuacha kazi na utalipwa mafao yako kuanzia siku utakayoteuliwa kuwa diwani.

Ukigombea nafasi yoyote ya uongozi katika chama cha siasa utalazimika kuacha kazi na utalipwa mafao yako.
Ukiteuliwa na Rais kuwa mbunge, utakuwa na hiari ya kuchukua likizo bila malipo kwa kipindi chote utakachokuwa mbunge au kuacha kazi na utalipwa mafao yako kuanzia siku utakayoteuliwa kuwa mbunge.

Rejea Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na. 01, 2015 kuhusu utaratibu wa watumishi wa umma wanaogombea nyadhifa za kisiasa.

28. Makosa na Adhabu
Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, zimeainisha mamlaka za nidhamu kwa makundi mbalimbali ya watumishi wa umma, aina ya makossa na adhabu zake. Mamlaka za nidhamu katika utumishi wa umma ni kama ifuatavyo:

Rais ambaye ni mamlaka ya nidhamu ya Katibu Mkuu Kiongozi
Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ni mamlaka ya nidhamu ya watumishi wote wanaoteuliwa na Rais.

Katibu wa Bunge ambaye ni mamlaka ya nidhamu ya watumishi wanaofanya kazi Bungeni. Makatibu wakuu wa wizara ambao ni mamalaka za kinidhamu za watumishi wanaofanya kazi kwenye wizara mbalimbali
Katibu Tawala wa Mkoa ambaye ni mamalaka ya kinidhamu ya watumishi wanaofanya kazi katika sekretarieti za mikoa.

Waziri mwenye dhamana ya TAMISEMI ambaye ni mamlaka ya nidhamu ya Wakurugenzi wa serikali za mitaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka za serikali za mitaa ambaye ni mamlaka ya nidhamu ya wakuu wa Idara /vitengo /sehemu na watumishi wengine maafisa.

Katibu Kamisheni ya Huduma za Walimu ambaye ni mamlaka ya nidhamu ya walimu.

Wakuu wa Idara ambao ni mamlaka ya nidhamu ya watumishi wasio maafisa (Operational Service)

29. Makosa ya Kinidhamu
Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma zimeainisha makosa katika makundi mawili. Makundi hayo ni makosa madogo madogo na makosa makubwa.

Makosa madogo madogo yanajumuisha ni kutokuwepo kazini bila ruhusa (utoro wa kuanzia siku mbili zitarekodiwa kama kosa linalojitegemea), kuondoka kazini wakati wa saa za kazi, kuchelewa kazini, kushindwa kukamilisha kazi uliyopewa, uzembe kazini kusikosababisha athari kwa mali ya Mwajiri na kutotekeleza maagizo uliyopewa.

Ukitenda moja ya makosa haya adhabu yake inaweza kuwa ni kupewa onyo la maandishi, karipio, kuzuiliwa ongezeko la mshahara la mwaka (Rejea Kanuni za 43(1-2) ikisomwa kwa pamoja na Jedwali la Kwanza, Sehemu B) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003.

ii. Makosa Makubwa

Makosa makubwa yanajumuisha wizi, rushwa na matendo yanayofanya utumishi wa umma ukose hadhi yake. Pia, kutoheshimu mamlaka, utoro kazini wa kuanzia siku zinazozidi tano (5) na kuendelea, kutumia mali ya mwajiri kwa shughuli binafsi, kufanya kazi binafsi wakati wa kazi, na kushindwa kuripoti kituo kipya cha kazi. Aidha, kutoa siri za ofisi, kufanya kitendo tofauti na maslahi ya umma, ulevi kazini, uzembe mkubwa kazini, kufanya kosa lillilosababisha hasara kwa Mwajiri na kwenda kinyume na kanuni za maadili.

Ukitenda moja ya makosa haya adhabu zake ni pamoja na kufukuzwa kazi, kushushwa cheo na mshahara au kupunguziwa mshahara kwa 15% ya mshahara ghafi kwa muda wa miaka mitatu (3). Kipindi cha uchunguzi wa shauri la kinidhamu unaweza kusimamishwa kazi na kulipwa si chini ya nusu ya mshahara (Rejea Kanuni ya 42(1-2) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003. Kama ilivyorekebishwa mwaka 2019.
 
Uhamisho si jambo baya kwenye utumishi, ni kawaida mfanyakazi kuhamishwa kutoka kituo kimoja Kwenda kingine ili kuimarisha utendaji na kuleta ufanisi. Tatizo kubwa ni kuwa wafanyakazi tunahamishwa bila kulipwa stahiki zetu.

Mkuu wa Rasilimali aliyepo hapo anatulazimisha Kwenda kwenye vituo vipya bila kulipwa anasema kama huna hela za kuhama nenda kakope Benki au mahali popote ili mradi uende unakotakiwa Kwenda. Na anatishia kuwa usipokwenda utaona kitakachokukuta ikiwa ni Pamoja na kuhamishiwa TAMISEMI.

Inaonekana kuw TAMISEMI ndio sehemu ya kupeleka watu wasiotakiwa.
 
Tamisemi ndio jumba bovu ee, daah
 
Kaka nawezaje kupata softcopy za hizi kanuni??
 
Ahsante sana.

Summary ya standing orders imecapture almost everything.
 
Kupata Hii likizo ya ugonjwa na mastaili yake yote kipesa ni lazima uwe umeishathibitishwa kazini ? Au hata ukiwa hujathibitishwa bado utaipata tu iwapo ukiwa mgonjwa ?
 
Nilikuwa nina swali hapo kweny kuhamishwa kituo cha kazi.

Je wanaangalia yule aliyeamishwa ndani ya kada husika mfano mwalimu kutoka wilay moja kwenda nyingine au hata wale wanaoamishwa kutoka taasisi moja kwenda nyingine mfano umetoka TRA(Accountant) ukapelekwa TCRA( marketing and sales officer)ile ghafla labda uende kuziba pengo huko?

Sijaelewa huko hapo kabisa na kama ni uhamisho wa emergency?
 
Back
Top Bottom