Mirathi ya Kobe Bryant yazua gumzo USA, utajiri wote wagawanywa kwa mke na watoto huku wazazi wakiishi kimaskini

Ni wajibu wa kisheria na maadili wazazi kulea na kutunza watoto wanaowazaa, sio wajibu wa watoto kutunza waliowazaa, ni hisani tu. Ndio maana mzazi anaweza kupelekwa mahakamani akaamriwa na mahakama kisheria kutoa matunzo ya mtoto ila mtoto hawezi kupelekwa mahakamani akaamriwa kutoa matunzo ya wazazi au ndugu.
Hivi umesoma vizuri comment yake au unakurupuka.
 
Nishaanza kuzeeka na siogopi hilo.
Ndivyo dunia ilivyo.
Usiweke matumaini sana kwa wanao utakufa kihoro.
Nawapenda wanangu so nahitaji pia upendo kutoka kwao.
Nikisema upendo simaanishi upendo wa kiuchumi.
Maisha yangu nimeshayazoea, sihitaji ndege wala gari uzeeni. Kwakifupi nshazeeka sina hayo matumizi nahitaji upendo tu
Hilo neno ni pana sana. Utajifanya unampenda mtu ambaye analala njaa wakati wewe unasaza?
 
kobe aliwatenga wazee wake toka enzi za uhai wake
kuna mshikaji wake mmoja wa Lakers aliwalipia wazazi wake ticket vip wakacheki game kobe hakumsamehe mwamba kwa hilo na L. A Lakers walimuuza mwamba msimu ulivyoisha kwa influence ya kobe kiufupi hayati alikua na nongwa kuu
 
Grudges , grudges, grudges.............she hold those for a loooooong time .

Ila sheria za kiislamu tamu sana kwa sababu kwenye mirathi hadi wazazi wapo pia mfano mume anaweza rithiwa na mke wake, watoto wake , wazazi wake na kuna muda hadi ndugu baadhi upande wa mume wanarithi na kwa mke vivyo hivyo.

Na kuwatunza wazazi wawili ni jukumu la lazima la mtoto as long as upo hai na kushindwa kufanya hivyo ni madhambi makubwa mno.
Lakini watoto wa njee wa mwanamke amna kurithi mali ya Mme ambae sio baba yao
 
Kobe Bryant alikuwa Mkatoliki kama sikosei.

Kwa Wakatoliki, kuna amri ya Mungu inayosema " Waheshimu wazazi wako upate miaka mingi na heri duniani".

Mtoto anayekuwa na kiburi na dharau Kwa wazazi mara nyingi haishii vizuri...!
Mkuu usichanganye mambo.
Kuheshimu mzazi na kumrithisha mzazi ni vitu viwili tofauti.
Tunapaswa kuheshimu wazazi ila sio kurithisha wazazi.
Tunarithisha watoto, wazazi tunawapa only upendo
 
Kutunza wazazi ni hisani tu, sio wajibu.
Wazazi wanatakiwa watafute pesa zao wawaachie watoto wao urithi.
Ni kweli kusaidia wazazi inaweza kuwa hisani lakini je si vyema kusaidia wazazi waliokulea?

Wazazi wanapambana lakini pengine wanaweza wasifanikiwe sana kiuchumi pamoja na jitihada. Je, si vyema kumsaidia mama au baba mwenye uhitaji?

Kobe alikuwa mtu poa sana sifahamu hii inekuwa vipi tena hii.
 
mirathi.

Aya tulizozirejea (4:11-12) zimetaja kwa uwazi na kwa ukamilifu watu wenye kurithi na mafungu yanayorithiwa. Wenye kurithi kwa wanaume ni kumi na tano (15). Watu hao ni:

1. Mtoto mwanamume

2. Mtoto mwanamume wa mtoto mwanamume (mjukuu)

3. Baba

4. Baba wa kwa baba

5. Ndugu mwanamume wa kwa baba na mama

6. Ndugu mwanamume wa kwa baba tu

7. Ndugu mwanamume wa kwa mama tu.

8. Mtoto mwanamume wa kwa ndugu mwanamume wa kwa baba na mama

9. Mtoto mwanamume wa ndugu mwanamume wa kwa baba tu

10. Ami (baba ndogo) wa kwa baba na mama (ndugu yake baba).

11. Ami wa kwa baba tu

12. Mtoto mwanamume wa Ami wa kwa baba na mama

13. Kijana mwanamume wa ami wa kwa baba

14. Mume

15. Bwana mwenye kumwacha mtumwa huru.

Wenye kurithi katika wanawake ni kumi (10) wafuatao:

1. Binti (mtoto mwanamke)

2. Binti wa mtoto mwanamume (mjukuu)

3. Mama

4. Dada wa kwa baba na mama

5. Dada wa kwa baba

6. Dada wa kwa mama

7. Bibi mzaa baba

8. Bibi mzaa mama

9. mke

10. Bibi mwenye kuacha mtumwa huru.
 
mirathi.

Aya tulizozirejea (4:11-12) zimetaja kwa uwazi na kwa ukamilifu watu wenye kurithi na mafungu yanayorithiwa. Wenye kurithi kwa wanaume ni kumi na tano (15). Watu hao ni:

1. Mtoto mwanamume

2. Mtoto mwanamume wa mtoto mwanamume (mjukuu)

3. Baba

4. Baba wa kwa baba

5. Ndugu mwanamume wa kwa baba na mama

6. Ndugu mwanamume wa kwa baba tu

7. Ndugu mwanamume wa kwa mama tu.

8. Mtoto mwanamume wa kwa ndugu mwanamume wa kwa baba na mama

9. Mtoto mwanamume wa ndugu mwanamume wa kwa baba tu

10. Ami (baba ndogo) wa kwa baba na mama (ndugu yake baba).

11. Ami wa kwa baba tu

12. Mtoto mwanamume wa Ami wa kwa baba na mama

13. Kijana mwanamume wa ami wa kwa baba

14. Mume

15. Bwana mwenye kumwacha mtumwa huru.

Wenye kurithi katika wanawake ni kumi (10) wafuatao:

1. Binti (mtoto mwanamke)

2. Binti wa mtoto mwanamume (mjukuu)

3. Mama

4. Dada wa kwa baba na mama

5. Dada wa kwa baba

6. Dada wa kwa mama

7. Bibi mzaa baba

8. Bibi mzaa mama

9. mke

10. Bibi mwenye kuacha mtumwa huru.
Hii inafaa zaidi Uarabuni labda na kwa Wahindi ambako mali huwa zinatafutwa zaidi na kumilikiwa kifamilia, kiukoo au kijamii. Mtu aliyezitafuta pesa zake mwenyewe huwezi kumpangia mlolongo wote huo, yeye mwenyewe kwa utashi wake ndiye ataamua anagawaje urithi wake.
 
Wamarekani wanamlaumu Kobe Kobe ana makosa ya kutowapa wazazi wake maisha hakuandika wosia kabla hajafa hivyo ni kama alichagua kutojumuisha wazazi wake katika wosia wake hivyo mali zote zimeenda kwa mke wake.

Ukweli wamarekani wana utamaduni wa ajabu sana, how can a person be worth Trillions of Money and his parents are broke? This life is not fair.

Kobe Bryants parents are broke. His dad was forced to auction off the ring Kobe gave him in the year 2000 ili apate hela ya ku survive huku mkewe na Kobe kapewa mirathi ya dola milioni 600 ambazo kobe kaacha bank.


Nyie ndio hamuelewi maisha.

Mzazi ana wajibu wa kulea mtoto, mtoto hana wajibu wa kulea mzazi. Ikitokea mtoto kalea mzazi, vizuri. Ikitokea mtoto kajikita zaidi kulea watoto wake wazazi kawaacha, hiyo pia ni haki yake. Mzazi hatakiwi kumuacha mtoto, hususan akiwa mdogo, lakini mtoto ana uhuru wa kuwa karibu na mzazi au kujiengua aende na maisha yake.

Na urithi ni jambo la hiyari. Kobe Bryant angeweza kumpa mke wake pasu la mali na kugawa mali zake kwa watoto masikini.

Hakulazimika hata kuwaachia watoto wake urithi. Angeweza kusema nyie watoto siwaamini, nikiwapa mali mtazitapanya, nazigawa kwa watoto yatima ambao watazitumia vizuri, ni haki yake. Mali yake, yeye bdiye anaamua itumike vipi. Ukitaka kumpa baba yake Kobe mali, tafuta zako.

Licha ya hayo, urithi ni kwa watoto. Wazazi wanarithisha watoto.

Baba yake Kobe Bryant, Joseph Bryany, alikuwa mchezaji wa basketball wa NBA (Philadelphia, San Diego, Houston) na kimataifa. Yeye ndiye kamrithisha Kobe kucheza basketball. Baba Kobe kacheza mpaka Italy na France, Kobe kakulia Italy mpaka Kitaliano alikuwa anaongea. Sasa baba yake Kobe kashindwaje kujipanga miaka yote hiyo aliyocheza basketball NBA, Italy na France?

Mnajuaje uhusiano wa Kobe na baba yake ulikuwaje? Mnajuaje kama walikuwa na beef?

Kwa nini mnataka kuwafanya watoto kuwa ni mafao ya uzeeni?

Hizi tabia za watoto kutumiwa na wazazi kama mafao ya uzeeni ni ushamba, umasikini na ujinga. Tunaona watoto wengine wanakufa kabla ya wazazi wao, sasa ukitegemea mtoto atakufaa uzeeni, halafu akafariki kabla yako, hapo utafanyaje uzeeni?

Proved
 
Sheria za Kiislam ni sheria za jamii ya kizamani sana, mtu ukichuma mali zako hupaswi kupangiwa matumizi yake.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
HA HA HA uislamu maana yake ni kujisalimisha kwa ALLAH[ the almighty] Mola wa vyote vilivyomo , sasa yeye ndo kaweka hesabu za hivyo na ikiwa wewe ni muislamu utafuata ima kwa kupenda au kutopenda IKIWA WEWE NI MUISLAMU.

KWENDA KINYUME NA HAPO NI KUJITAFUTIA MADHAMBI BURE BURE TU.
 
HA HA HA uislamu maana yake ni kujisalimisha kwa ALLAH[ the almighty] Mola wa vyote vilivyomo , sasa yeye ndo kaweka hesabu za hivyo na ikiwa wewe ni muislamu utafuata ima kwa kupenda au kutopenda IKIWA WEWE NI MUISLAMU.

KWENDA KINYUME NA HAPO NI KUJITAFUTIA MADHAMBI BURE BURE TU.
Hapa kwenye issue ya Kobe sheria za Marekani hususan jimbo alilokaa Kobe ziko relevant kuliko sheria za Kiislamu.

Kwa sababu Kobe Bryant hakuwa Muislamu.

Msitake kulazinisha sheria za Uislamu hata pale ambapo hazihusiki.
 
Nyie si ndo mliwasapoti big shark na Jack chan kwamba watoto wao watafute zao, sasa shida nn hapo.
Tusipende kushadadia mambo ya watu. Kila mtu na njia yake kupata kukosa mipango ya maanani. Mbona kikongwe wa wakojako alilamba mabilioni.
 
Hapa kwenye issue ya Kobe sheria za Marekani hususan jimbo alilokaa Kobe ziko relevant kuliko sheria za Kiislamu.

Kwa sababu Kobe Bryant hakuwa Muislamu.

Msitake kulazinisha sheria za Uislamu hata pale ambapo hazihusiki.
Hakuna sheria duniani inaoishinda sheria za uislam
 
Back
Top Bottom