GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
Huo hapo chini ni mche wa tunda la PASHENI. Inafahamika kuwa katika ukuaji wake, hutambaa juu ya miti au egemeo litakalokuwa jirani yake. Nilikuwa nasubiri ukue vya kutosha ndipo niuwekee egemeo. Lakini nimeshangaa kukuta umeshajisogeza kwenye fensi na kuendelea kukua kwa kuukwea.
Hakuna mtu aliyeuelekeza upande huo. Na kwa mazingira ya eneo hilo, nilitarajia ungekua kwa kuelekea upande wa Magharibi, badala ya Mashariki ambako ndiko kulipo na fensi.
Umewezaje kutambua kuwa egemeo lipo upande wa Mashariki na kuamua kuufuata bila usaidizi wa binadamu?
Je! Mimea ina akili?
Mimea ina macho au namna ya kuhisi?
Kuna tafiti za Kisayansi zilishawahi kufanyika kubaini kama mimea ina uwezo wa utambuzi?