Akili ni nini?

NDUKI

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
3,423
2,414
Neno AKILI ni neno ambalo limezoeleka na linatumika sana karibia kila mtu analitumia neno hili lakini unaweza ukamuuliza mtu na akashindwa kukujibu au akajibu anavyojua yeye juu ya neno hili, AKILI ; ilimradi kila mtu ana mtazamo na tafsiri yake juu ya neno AKILI.

Neno hili asili yake limetokana na Lugha ya Kiarabu na ndipo likaja kwenye Lugha yetu ya asili ya Kiswahili, limeanza kutumika tangu karne ya 7 takriban ni miaka zaidi ya 1200 kabla ya kuzaliwa Lugha ya Kiswahili. Na mfano wa matumizi ya neno hili AKILI lilishatumiwa na MTUME MUHAMMAD (S.A.W) aliposema kuwa ; MAKTASABAL MAR-U, MITHLA A'QILI akiwa na maana kuwa HAJACHUMA AU HAJAPATA MWANADAMU KITU KILICHOKUWA BORA MFANO WA AKILI. Kwa kauli hiyo tunaweza kuona kuwa neno hili kumbe limeanza kutumika miaka mingi sana iliyopita kabla halijaja kwenye Lugha yetu ya Kiswahili. Na kwa kauli hiyo pia tunaweza kuona kuwa kumbe kati ya vitu vyote ambavyo mwanadamu atafanikiwa kuvipata katika MAISHA yake hakuna kilicho bora kati ya hivyo kuushinda ubora wa AKILI, hata awe na mali vipi kama hana AKILI basi ni KAZI BURE TU na hata WASWAHILI wakafikia hatua ya kusema kuwa "BORA UKOSE MALI UPATE AKILI.

Kuna kauli nyingine pia inasema; AT-TAJIRIBATU MIRA-ATUL A'QILI ikiwa na maana kuwa; MAJARIBIO NDIO KIOO CHA AKILI kwenye kauli hiyo kuna neno MIRA-ATUL ikiwa imetumika kama KIOO, ila acha nisiende huko turudi humu humu kwa kutazama kauli hii ya MTUME MUHAMMAD (S.A.W) inayosema kuwa; AL AQILUN NUURUN FIL QALBI ikiwa na maana kuwa AKILI NI NURU INAYOPATIKANA NDANI YA MOYO.

Lengo la kuzungumza kauli hizo ni kutaka ujue kwanza thamani ya neno AKILI na pia ujue ASILI ya neno lenyewe limetokea wapi.

Tukiangalia kwa upande wa pili nikimaanisha katika Lugha ya Kiingereza neno AKILI limeitwa INTELLIGENCE na neno hili pia limeazimwa au limetokana na Lugha ya Kifaransa na pia limetokea moja kwa moja kwenye Lugha ya Kilatini. Hiyo ndio asili na maana halisi ya neno hili ambapo katika Lugha ya Kiswahili asili yake imetokana na Lugha ya Kiarabu na katika Lugha ya Kiingereza imetokana na Lugha ya Kifaransa na Kilatini

AKILI NI NINI?

Katika Mtazamo wa Kisayansi
Charles Spearman.

Kwa mtazamo wa KISAYANSI tuanze kwa kumuangalia huyu mtu anayejulikana kwa jina la Charles Edward Spearman

Charles-Spearman1.jpg


Katika historia, huyu ni mmoja kati ya watu wa kwanza kabisa kufanya utafiti juu ya masuala ya AKILI na katika moja ya tafiti zake ni aliyoifanya mwaka 1904 Charles E. Spearman | British psychologist na kufikia kusema kuwa ; AKILI INATENGENEZWA NA VITU VIKUBWA VIWILI AMBAVYO NI GENERAL INTELLECTUAL SKILLS NA SPECIFIC COGNITIVE SKILLS ambapo kwa wanaosoma SAIKOLOJIA watakuwa wananipata vizuri katika hili, hapa nazungumzia G-FACTOR NA S-FACTOR hizi kwa pamoja zilijulikana kama Two-factor theory of intelligence - Wikipedia.

General Intellectual Skills hapa nazungumzia ule ujuzi wa moja kwa moja nikimaanisha GENERAL yani ni ujuzi ambao mtu anaupata na kumuwezesha kufanya kitu fulani na Specific Cognitive Skills ni utambuzi unaomuonesha au unaomuwezesha mtu kufanya kitu fulani. Yani ni ujuzi unaomuwezesha mtu kufanya kitu fulani pamoja na ujuzi unaomuonesha au kumuwezesha mtu kufanya jambo fulani i.e yani alifanye vipi jambo hilo kwa ufasaha zaidi. General Intellectual Skills ni ujuzi ambao lazma uambatane na UFAHAMU kuwa jambo hili ukitaka kulifanya ulifanye vipi, hiyo ni kwa mujibu wa Bwana Charles Spearman.

Kwa hiyo basi, kutokana na utafiti wa Bwana huyu juu ya AKILI tunaweza kuona kuwa AKILI kwa ujumla inatengenezwa na UTAMBUZI/UELEWA/UFAHAMU na pia UJUZI aidha wa kuzaliwa nao au wa kujifunza pahala, hivi vitu kwa ujumla vinatengeneza au kujumuisha kuwa mtu fulani ana AKILI. Lakini pia aliongeza kitu kimoja na kusema kuwa hata KUONA pia hujumuisha mtu kuonekana ana AKILI, ambapo utafiti huu ulikuja kupingwa na wanasayansi wengi sana kuwa KUONA sio moja ya sababu ifanyayo mtu aonekane kuwa ana AKILI. Kwa hiyo kwa mujibu wa Bwana Charles Spearman alibainisha kuwa vitu hivi ndivyo vinavyojumuisha AKILI ambavyo ni UFAHAMU/UELEWA, UTAMBUZI pamoja na UJUZI/KUJUA, hivi kwa pamoja ndivyo hujumuisha AKILI kwa mujibu wa Bwana Charles Spearman.

Katika utafiti mwengine uliofanywa na mtu mmoja anayejulikana kwa jina la L. L. Thurstone.

images

slide_10.jpg


Huyu nae katika utafiti wake alikuja kuthibitisha kuwa kuna vitu au mambo 7 ndio hujumuisha mtu kuwa na AKILI kwa ujumla, katika vitu hivyo alisema kuwa kuna ;-

1.) Verbal Comprehension, - Wechsler Adult Intelligence Scale - Wikipedia | Verbal comprehension « General Psychology - huu ni uwezo wa kufahamu maneno yanayotamkwa na kuzungumzwa pia kufahamu mitazamo na mawazo tofauti tofauti.

2.) Spatial relation - Spatial relation - Wikipedia - huu ni uwezo wa kutambua kitu, ability to visualize and manipulate different patterns and forms in space, ni uwezo wa kuangalia kitu kinachokuja baadae, yani kufahamu kitu kitakachokuja baadae hapa simaanishi KUTABIRI au KUPIGA RAMLI, LAA, ila namaanisha kuwa fikra ya mtu kuweza ku-focus kwamba "HIKI NNACHOFANYA MATOKEO YAKE BAADAE YATAKUWA NI NINI?" Hiko pia ni moja kati ya vitu vinavyojumuisha kuwa mtu fulani ana AKILI.

Lakini sasa kwa mtazamo wa huyu bwana, yee anasema ili mtu ukubalike kuwa una AKILI ni lazma uwe na hivyo vitu 7 ambavyo amevifanyia utafiti wake na mwisho kuja na majibu yake. Na kitu cha 3 kati ya hivyo ni ;-

3.) Perceptual Speed - Perceptual speed « General Psychology - huu ni uwezo wa kufahamu na kutambua kitu kwa kasi au kwa haraka zaidi na kwa USAHIHI pia, ni moja kati ya vitu vinavyomjumuisha mtu kuwa ana AKILI.

4.) Word Fluency - Thurstone Word Fluency Test - Wikipedia - huu ni uwezo wa kutumia maneno kwa haraka na kwa mpangilio unaoeleweka au kwa ufasaha zaidi.

5.) Memory Memory - Wikipedia - huu ni uwezo wa kutunza kumbukumbu au kukumbuka vitu kwa haraka zaidi. Na katika memory au kumbukumbu kuna aina 2 za KUMBUKUMBU hapa nikimaanisha kuwa kuna Short Term Memory na Long Term Memory, sasa hapa kinachozungumziwa ni mtu anatakiwa kuwa na Long Term Memory au KUMBUKUMBU ya muda mrefu. Tuchukulie kwa mfano jambo limetokea nusu saa au hata masaa mawili nyuma halafu ghafla tu ikawa umesahau na wala hukumbuki kabisa, basi wewe itakuwa una matatizo ya AKILI kwa njia moja au nyingine, kwa hiyo moja ya vitu vinavyojumuisha AKILI ni kuwa na KUMBUKUMBU nikimaanisha (L.T.M).

6.) Inductive Reasoning - Inductive reasoning - Wikipedia - huu ni uwezo wa kuhoji na kuelezea, kwa mfano ; jambo hili asili yake nini, linatokana na nini, liko vipi na litakuaje baada ya hapa, hapa ikijumuisha uthibitisho au evidence wa jambo lenyewe kukiwa na ukweli ndani yake mwishowe kupelekea kupata jawabu lililo sahihi kabisa. Hii ni moja ya vitu vijumuishavyo mtu kuwa na AKILI.

7.) Numerical Ability - Thurstone « General Psychology - huu ni uwezo wa kutumia namba au hesabu kwa kifupi ni kutatua matatizo kwa haraka kwa kutumia namba au hesabu, hii ni moja ya sababu ya mtu kuonekana kuwa ana AKILI pia. Kwa hiyo tumeweza kuona kupitia huyu Bwana L. L. Thurstone na Charles Spearman kuwa, ili mtu aweze kuonekana kuwa ana AKILI yatakiwa awe sawa katika thoughts, understanding, reasoning, communicating, learning and planning. AKILI ni uwezo wa KUFIKIRI, KUELEWA/KUFAHAMU/KUTAMBUA/KUJUA, KUWASILIANA, KUHOJI, KUJIFUNZA NA KUPANGA. Hivyo ni kwa mujibu wa upande wa KISAYANSI lakini pia kuna mtazamo wa KIDINI kuhusiana na AKILI pia, ambao hautofautiani sana na wa KISAYANSI lakini katika mtazamo wa KIDINI kuna NYONGEZA au ZIADA.

Katika Mtazamo wa Kidini
Kama tulivyokwisha kuona hapo juu ASILI ya neno hili AKILI katika Lugha ya Kiswahili tumeazima kutoka kwenye Lugha ya Kiarabu, lakini pia kwenye hiyo hiyo Lugha ya Kiarabu hili neno pia limeazimwa kutoka pahala, neno AQLU au HABL tafsiri yake ni KAMBA kwa KIARABU, neno hili limetumika kuwa ni kamba ya kumfungia Ngamia ili asiweze kwenda mahala ambapo mmiliki wake hataki, katika kitabu kinachoitwa ADAABU DUNIA WA DIYN mtunzi akiwa ni IMAM ABUU HASSAN ALI IBN MUHAMMAD BIN HABIB AL BASWAARIYYU katika ukurasa wa 15 wa kitabu chake hicho anasema ;- "SUMMIYA BIDHAALIKA TASHBIYHAM BI AQLI NAARQA" - imeitwa hivyo AKILI kwa kufananishwa na kamba ya Ngamia, akiwa na maana gani?, anaendelea kusema mtunzi kuwa "LIANNAL AQLA YAMNA'UL-INSAANA MINAL IKHDAAMY A'LAA SHAHAWAATIHY IDHAA QABUHAT" amesema imeitwa hivyo kwa nini "kwa sababu AKILI inamzuia MWANAADAMU kufika kwenye matamanio yake ya nafsi pindi yale matamanio yake yanapoharibika au matamanio yake yanapokuwa mabaya". Naweza nikawa nimekuacha hapo kidogo ila nnachomaanisha ni kuwa, MWANAADAMU ana matamanio ya aina 2, huwa ANATAMANI au kwa kifupi huwa na TAMAA, sasa TAMAA zipo za aina 2 zipo TAMAA NZURI na TAMAA MBAYA.

TAMAA MBAYA kwa kawaida humpeleka MWANAADAMU SEHEMU MBAYA na TAMAA NZURI kwa kawaida humpeleka MWANAADAMU SEHEMU NZURI, sasa TAMAA zako zinapokuwa MBAYA na zikakutuma PABAYA lazma zitakupeleka PABAYA na hapo ndipo AKILI inapotumika na kama TAMAA zako zinapokuwa ni NZURI na zikakutuma kufanya yaliyo MAZURI basi lazma zitakupeleka PAZURI ; kama tulivyosema kuwa AKILI ni KAMBA ya kukuzuia wewe kufika kwenye matamanio yako ya NAFSI pindi pale MATAMANIO yako YANAPOHARIBIKA au yanapokuwa ni MABAYA sasa hapo AKILI ndipo inapotumika. Anaendelea kusema IMAAM kuwa ; "KAMAY YAMNAUL I'QAALUN NAAQATA MINA SHURUUDI IDHAA NAFARAT" anasema "kama vile mfano wa kamba zinazofungia Ngamia zinapomzuia Ngamia asiende anapopataka au kutoroka pindi anapokuwa amechachamaa au amekasirika basi huo ndio mfano wa AKILI inapotakiwa KUMZUIA mtu asiayaendee MATAMANIO MABAYA coz mwishowe yatampeleka PABAYA tu, huo ni kwa MTAZAMO WA KIISLAM. Kwa hiyo, hapo ndipo lilipoazimwa neno AKILI na likatumika mithili ya KAMBA INAYOMZUIA MWANADAMU ASIYAENDEE MABAYA au MAOVU.

Kama tulivyoona kupitia wanasayansi kuwa wamebainisha mambo takriban 7 ili mtu kuweza kuambiwa kuwa ana AKILI lakini katika UISLAM imekusanya mambo takriban 6 ili kumthibitisha mtu kuwa ana AKILI na katika mambo hayo 6 yamebebwa na MAMBO MAKUBWA 3 ambayo ni ;- BUSARA, HEKIMA na UTAMBUZI

1.) BUSARA - maana yake ni kufikiri sana jambo kabla ya kulitenda. Kufkiri au Fikra ni nini pia?, haya pia ni maneno ya KIARABU kwa hiyo hata kutafsiri kwake tukitumia Kiswahili inaweza isieleweke vyema. Neno FIKRA pia limeazimwa kwenye Lugha ya Kiarabu likijulikana kama KALIMATUL MAQLUUHU ikimaanisha kuwa neno hili limegeuzwa kutokana na neno FIRKU. FIRKU maana yake ni nini?, mama yake ni kama KUTAFUTA kitu kwa undani zaidi au kuchakura chakura kama afanyavyo kuku anavyotafuta chakula kwenye uchafu ili kimfae aweze kula. Kuna kauli moja inasema AL FIKR MAQLUUBU A'NIL FIRK LAAKINI

STA'AMAL FIKR WAHUWA FIRKUL UUMUUR WABAH THURAA TWALABA LIL USUUL ILAA HAQIYQATIHAA
maana yake ni kwamba "FIKRA AU KUFKIRI NI KULE KUYACHAMBUA CHAMBUA MAMBO NA KUPEKUA PEKUA KWA LENGO LA KUFIKA KWENYE HAKIKA YAKE" hiyo ndio FIKRA au KUFKIRI. Hivyo basi, tunaposema BUSARA ni KUFIKIRI KABLA YA KUTENDA maana yake ni kwamba ni kulichambua chambua jambo mpaka ulifahamu vizuri sana, baada ya kulifahamu ndio unatenda hiyo ndio, inaitwa BUSARA. Na katika neno BUSARA tuangalie mfano mmoja hapa unaohusiana na BUSARA hapa tutamuangalia ADUI mmoja wa MTUME MUHAMMAD (S.A.W) aliyejulikana kwa jina la UBAIYYA BIN KHALAF aliuchukua mfupa na kuufanya kuwa ni moja kati ya hoja ya kumpinga MTUME na kumwambia iweje MUNGU wako aweze kufufua huu mfupa hali ya kuwa umeshaoza kiasi hiki, binadam akifa ndio ameshakufa wala hakuna kufufuliwa tena. Kwa kauli hii ya huyu ADUI ukitazama utaona wazi kuwa hapa alichokikosa ni BUSARA kwa sababu angekuwa na BUSARA angeweza KUFKIRI kuwa huu mfupa kabla ya kuwa mfupa ulikuwa ni kitu gani mpaka ukaja kuwa mfupa?, akaweza kufkiri ya mbele bila ya kufkiri ya nyuma kuwa kabla ya kuwa mfupa ulikuwa kitu gani mpaka baadae MUNGU wako aweze kufufua huu mfupa na uje kuwa tena BINADAM?, huku ni kukosa BUSARA yani kulichambua chambua jambo au kulifikiria kwanza kabla ya kulitenda. Sasa basi, kama tulivyoona kwenye mtazamo wa KISAYANSI kuwa hii inajulikana kama INDUCTIVE REASONING.

Kule kufikiri kitu kwa umakini au kukijua kitu kwa umakini au kwa undani kabla ya kuamua kukisema au kukitenda, kwa hiyo alishindwa kujua kwanza mfupa ni nini, umetokana na nini na asili yake pia ni nini mpaka ukaja kuwa mfupa. Mfano mwengine ulio wazi ni kuwa, unaweza kukuta mtu mzima na heshima zake na pengine ana ELIMU kubwa tu akijisaidia mbele za watu au hata barabarani, huyu ni wazi kuwa amekosa HEKIMA NA BUSARA kwa sababu angekuwa na BUSARA ingemtuma AFIKIRI lile analolifanya kabla hajalitenda, ila kwa kuwa kakosa BUSARA that's why akashindwa KIFIKIRI. Katika hiyo mifano unaweza kuona kuwa kuna tofauti kubwa ya mtu kuwa na ELIMU na kuwa na AKILI coz mtu anaweza kuwa na ELIMU lakini ikawa hana AKILI. Ila pia anaweza kuwa na AKILI lakini asiwe na AKILI NYINGI japokuwa amesoma mpaka Chuo Kikuu. Na hii mifano ipo mpaka kwenye maisha yetu ya kila siku kuwa, utakuta mtu amesoma na ana ELIMU kubwa sana lakini mambo anayoyafanya ni kama mtoto au zaidi ya mtoto, hii inaonesha kuwa huyu mtu ana ELIMU kubwa lakini hana BUSARA wala hana AKILI ya kutosha coz AKILI SIO ELIMU NA ELIMU SIO AKILI coz wapo watu hawajasoma lakini mambo wanayoyafanya ni MAKUBWA kuliko mtu amabaye amesoma. Huyu tunaweza kumuita kuwa ni Street Smart. Unaweza kujiuliza swali kama tulivyoona hapo nyuma kuwa moja ya vitu vinavyofanya mtu awe na AKILI NI KUMBUKUMBU sasa iweje mtu awe na ELIMU halaf asiwe na AKILI wakati amesoma na alikuwa na uwezo wa KUTAMBUA, KUELEWA, KUPANGA, KUFAHAMU, KUHOJI, KUKUMBUKA etc sasa iweje asiwe na AKILI, ndio mana kwenye UISLAM tunasema kuwa mtu kuwa na AKILI inamlazimu kuwa na BUSARA, HEKIMA NA UTAMBUZI vikijumuisha mambo 6 ndani yake. Mtu anaweza akawa na A+ masomo yake yote lakini ukamleta kwenye maisha yetu halisi ya kila siku akashindwa kuishi hata na jirani yake, akashindwa kupanga wala kupambanua mambo yake mpaka awaone watu wampe ushauri n.k, sasa huyu alikuwa na KUMBUKUMBU ya kukumbuka vile alivyofundishwa darasani tu lakini kakosa HEKIMA, BUSARA au UTAMBUZI wa KUTAMBUA mambo kadha wa kadha. Kwa hiyo, mtu kama huyu tunaweza kusema kuwa kilichomsaidia sana kupata ELIMU ni MEMORY aliyonayo, sasa kwa MEMORY peke yake haitoshi kupelekea kuona eti mtu ana AKILI mpaka awe na haya mambo 3 ambayo ni BUSARA, HEKIMA NA UTAMBUZI.

Kwa mfano mwengine ni kuwa, mtu anaweza akawa amesoma na akapata A+ mitihani yake yote lakini kumbe alichokijibu kwenye mitihani alikuwa amekariri tu, lakini kumbe hata alichokijibu hakijui ni kitu gani wala maana yake ni nini, kwa kifupi kuna KUKARIRI NA KUELEWA kile ulichokisoma, sasa hivi ni vitu viwili tofauti kabisa. Ambapo huyu akipata cheti ambacho ni kizuri watu watasema huyu jamaa ana ELIMU na ana AKILI lakini kiukweli ni kuwa anaweza kuwa na hiko cheti lakini ikawa HANA AKILI.

Sasa basi, katika UISLAM hii BUSARA, HEKIMA NA UTAMBUZI ndio sawa na yale yaliyosemwa na Bwana Thurstone na Spearman ambapo Thurstone hii BUSARA yeye ameiita ni INDUCTIVE REASONING kwamba ni ule uwezo wa KUFIKIRI jambo, kabla lilikuwaje, sasa likoje na baadae litakuwaje. Na mtu mwenye BUSARA anakuwa na mambo makubwa 6 katika KUTENDA KWAKE na KUSEMA KWAKE kwa MTAZAMO WA KIISLAM. Kwanza kabisa mtu mwenye BUSARA huwa ANAJITAMBUA yeye ni nani, tukiangalia kwenye kusema kwake huwa ;-

1.) Anajitambua yeye ni nani.
2.) Kile anachokisema pia ni anasema na nani?
3.) Anasema nini au kitu gani anachokisema?
4.) Anasema wapi?
5.) Anasema wakati gani?
6.) Kwa dhumuni gani au kwa lengo gani anasema?


Hiyo ni BUSARA ya mtu mwenye AKILI pale anapotaka KUSEMA ni kuwa imekusanya vitu hivyo 6. Sasa tuangalie mfano wa mtu ambaye amekosa BUSARA pia, kwa mfano tuchukulie wewe ni KIONGOZI WA DINI kwa mfano, ukaingia kwenye NYUMBA YA IBADA na kuchukua kipaza sauti na kuanza kusema "NDUGU WANANCHI, NINATOA AMRI KESHO MITARO YOTE IZIBWE, NA ASIYEZIBA ATAKIONA CHA MTEMA KUNI", hapo unajua kilichokosekana kwa huyu KIONGOZI WA DINI ni nini...?. NI BUSARA. Kitu kikubwa alichoshindwa kukifahamu huyu anayetoa AMRI kashindwa kujitambua kuwa YEYE NI NANI, ANASEMA NINI, ANASEMA NA NANI, ANASEMA WAPI, WAKATI GANI NA KWA DHUMUNI GANI pia. Ameshindwa kujitambua kuwa yeye ni KIONGOZI WA DINI na wala sio KIONGOZI WA SERIKALI YA MTAA, kwa mfano, hapo atawaamrisha watu watakaokuwa WAISLAM na wasio WAISLAM ambapo watakuwepo wanaomtii na pia tangazo lile litawagusa hata wasioswali kabisa MSIKITINI pale, sasa reaction ya hawa watu huwezi kujua watapokea vipi tangazo hilo, kwa hiyo hapa kilichokosekana ni INDUCTIVE REASONING au BUSARA yani kashindwa KUFIKIRI KABLA YA KUTENDA. Na jambo la pili katika MTAZAMO WA KIDINI ili mtu aweze kuthibitishwa kuwa ana AKILI anatakiwa kuwa na ;-

2.) HEKIMA - huu ni uwezo wa mtu kuliweka jambo mahala pake, yani kuweka jambo au kauli mahala panapostahili. Tuchukulie kwa mfano mtu kapika chakula kizuri kabisa chenye kunukia na ladha tamu juu yake kwa ajili ya mgeni wake, halaf baada ya hapo akamkaribisha mgeni chakula hiko kisha akakiweka kwenye gauni au nguo yenye thamani kweli kweli, au kwenye kiti cha gharama ya hali ya juu, au hata kwenye kiatu ambacho ni cha dhahabu pengine, akiwa na lengo la kutaka kumfurahisha mgeni wake, lengo lake linaweza kuwa ni zuri sana kuwa anataka mgeni wake afurahi kwa kuwa kawekewa chakula kwenye kitu cha thamani ya hali ya juu, lakini kile anachokifanya anajua kitaleta matokeo gani au mgeni wake atakitafsiri vipi, je atapendezewa nacho kitendo hiko?, je ile furaha anayotaka mgeni wake aipate ataipata kwa kumuandalia chakula kwenye kiatu, gauni au kiti ambacho kina gharama ya hali ya juu kupita kiasi, kwa jibu moja au jingine tunaona wazi kuwa hata kama ungekuwa ni wewe usingefurahishwa na kitendo hiki hata kidogo japo kuwa usingeweza kusema ila usingependezewa moyoni kwa jambo hilo, hapa tunaweza kuona kuwa kilichokosekana hapa kwa huyu mtu ni HEKIMA yani KUSHINDWA KUWEKA JAMBO MAHALA PAKE. Kwa sababu chakula hakiwekwi kwenye kiti au gauni au kiatu hata kama kiatu hiko au gauni hilo au kiti hiko kitakuwa kina gharama kubwa kiasi gani, hata kama kitakuwa na gharama kubwa kuliko sahani ya plastiki huwezi kuweka chakula ndani ya kiatu, huku ni kukosa HEKIMA. Sasa basi, mtu mwenye AKILI anakuwa na HEKIMA yani anakuwa na uwezo wa kuliweka jambo mahala pake kwa ufasaha zaidi. Jambo lingine ambalo ni la 3 katika MTAZAMO WA KIDINI lenye kupelekea kuthibitisha kuwa mtu fulani ana AKILI ni mtu kuwa na ;-

3.) UTAMBUZI - ambapo kwenye SAYANSI jambo hili wamesema kuwa mtu awe na PERCEPTUAL SPEED kwa sababu watu wanatofautiana katika kutambua mambo, mwengine hutambua kwa haraka, mwengine kwa kawaida tu, mwengine huchelewa zaidi na mwengine hata kutambua kwake ni kugumu kabisa, kwa hiyo huwa tunatofautiana katika KUTAMBUA NA KUJITAMBUA na tupo tofauti tofauti kwenye suala zima la Perceptual Speed. Sasa katika mtazamo wa KIDINI mtu ambaye ana AKILI ni yule mwenye uwezo mkubwa wa KUFIKIRI wapi ametoka, yuko wapi, anaelekea wapi, kwa nini yupo hapo alipo na kwa lengo gani yupo hapo na pia je ANATAMBUA nafasi yake akiwa yeye kama MWANADAMU ni ipi...?. Ndio mana ikaelezwa kuwa AKILI NI KAMBA MAALUM AMBAYO INAMFUNGA MTU ASITOKE KATIKA MIPAKA ALIYOWEKEWA NA MUNGU WAKE KATIKA KUYAENDEA MABAYA na ndio mana MTUME MUHAMMAD (S.A.W) aliwahi kumwambia SWAHABA wake kuwa "ZIDISHA AKILI YAKO UTAZIDI KUWA KARIBU SANA NA MUNGU WAKO" huyu SWAHABA akamuuliza MTUME "VIPI NITAZIDISHA AKILI YANGU...?" MTUME akamwambia "JIEPUSHE NA ALIYOYAKATAZA MUNGU WAKO NA UTEKELEZE YALE ANAYOYATAKA MUNGU WAKO UTAKUWA NI MWENYE AKILI". Kwa hiyo basi, tunaweza kuona kwenye mtazamo wa KIDINI neno AKILI lipo katika WIGO au MIPAKA MAALUM ikiwa na maana kuwa huwezi kuitwa mwenye AKILI ikiwa umetoka kwenye MIPAKA hiyo na hii pia ipo hata kwenye ULIMWENGU wa kawaida au katika MAISHA yetu ya kawaida ipo hivyo kwamba kuna MIPAKA MAALUM ambayo mtu akiivuka kwa matendo yake au kauli zake basi huonekana wazi kuwa HANA AKILI.

Na pia kwenye UISLAM AKILI imewahi kuitwa NUHAA ambapo maana yake ni KATAZO na pia imewahi kuitwa HIJR ambapo maana yake ni KIZUIZI inatakiwa KUMKATAZA AU KUMZUIA mtu kuyaendea au kuyafanya baadhi ya mambo flani yatayopelekea kuonekana kuwa hana AKILI. Kama ilivyoonekana kwa Ngamia kuwa neno AKILI ni KAMBA iliyomfunga Ngamia asiende kule ambapo mmiliki wake hataki aende na ndio hivyo hivyo kwetu sisi wanadamu pia AKILI ni kama KAMBA ambayo tumefungwa nayo na BWANA MUNGU WETU ambaye hataki sisi twende kwenye mambo ambayo yeye hayataki na kututaka kuyaendea tu yale mambo ambayo anataka tuyaendee ambayo ni MAMBO MAZURI na kuacha yaliyo MABAYA. Na kamba aliyotufunga nayo ni vitabu vyake na makatazo yaliyomo ndani ya vitabu hivyo kwamba hatutakiwi kutenda yaliyokatazwa katika vitabu vyake ambavyo ndio KAMBA iliyotumika kutufunga WANADAMU, na kama ukivuka au kufanya yale ambayo ameyakataza MUNGU[/COLOR] basi wewe utakuwa ni mmoja kati ya watu ambao watakuwa wameikata KAMBA hiyo kwa hiyo utakuwa hauna KAMBA nikimaanisha kuwa utakuwa HAUNA AKILI. Chukulia unapomwambia mtu kuwa "HUNA AKILI WEWE" mwengine atakasirika mwengine atachukulia kawaida tu lakini hapa itategemea na uelewa wa mtu kwa vile jinsi alivyoelewa. Lakini pia, AKILI inaweza ikaongezeka na pia inaweza ikapungua itategemea na mtu binafsi atakavyoishughulisha AKILI yake. Kwa mfano, unaweza kuskia mtu akisema "AISEE, YULE JAMAA ANA AKILI SANA AISEE" au ukasikia mtu akisema "JAMAA HAJATULIZA TU AKILI YAKE NDIO MANA AKASHINDWA". AKILI imegawanyika katika sehemu KUU 2 ambapo kuna "AKILI YA KUZALIWA NAYO" na "AKILI YA KUSOMA AU KUJIFUNZA BAADHI YA MAMBO" kupitia sehemu tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na darasani au mtaani tu kwenye maisha yetu ya kila siku tunayoishi.


Katika kuongeza AKILI kwenye MTAZAMO WA KIDINI imetakiwa kwa MWANADAMU kutembea sehemu nyingi tofauti ili kuweza kuona mambo mengi mengi tofauti, katika MTAZAMO WA KIDINI inasemekana, kufanya hivyo kunakuwa ni SABABU ya kuongezeka kwa AKILI ya mtu kwa sababu mtu ataweza kuona mambo mengi yakiwemo mambo ya kale pamoja na uumbaji wa MUNGU hivyo itapelekea mtu kuongezeka kwa AKILI yake na ndio mana utaskia watu wakisema "UNAPOTEMBEA SEHEMU NYINGI UNAFUNGUA AU UNAPANUA (UNAONGEZA) AKILI YAKO". Hebu tuangalie pale MWENYEZI MUNGU aliposema ndani ya KITABU CHAKE kwa kutaja vitu alivyoviumba vikiwamo MIMEA, MVUA NA WANYAMA, pale mtu anapotazama vitu hivi kama MVUA ikawa ni sababu ya MIMEA kuota na yeye akapata CHAKULA cha kumfanya aweze kuishi, hapa kuna MAZINGATIO MAKUBWA sana kwa watu wenye AKILI, anasema MUNGU kwenye KITABU CHAKE ya kuwa ; "KULENI HIYO MIMEA NA MCHUNGE WANYAMA WENU, HAKIKA KATIKA HAYO KUNA DALILI ZA WAZI ZA KUKUFAHAMISHA UTUKUFU NA UWEZO WA MWENYEZI MUNGU KWA WATU WENYE AKILI." [QURAN 20:54]

Na pia tulisema AKILI imeitwa NUHAA tuangalie kwenye kitabu chake hiko hiko pale MUNGU alipowatuma watu wafanye UTALII kwa kuzunguka sehemu tofauti tofauti za DUNIA, hapa ndipo lilipotumika neno NUHAA=AKILI, Kwa nini watu wametakiwa wafanye UTALII, hii yote ni kwa sababu au kwa lengo la kuongeza AKILI na KUMJUA MUNGU WAO VYEMA, ambapo imeshauriwa UTALII huo ufanywe kwenye vitu ambavyo ni vya ZAMANI au MABAKI YA VITU VYA ZAMANI au MAMBO YA KALE SANA kwa sababu kufanya hivyo utaweza kujifunza na kuyaelewa na kunaongeza AKILI YA MTU. Unaweza ukaskia kuwa, kuna watu wengine bwana MUNGU amemjaalia AKILI NYINGI SANA sasa hapa kuna tofauti kidogo, sio kwamba AKILI mtu anapendelewa na MUNGU, LAA. Ila ifahamike tu kuwa AKILI imegawanyika katika sehemu 2 ambayo ni ; kuna AQLIL GHARIZIYYU na AQLIL MUTTASAB hii AQLIL GHARIZIYYU ni ile AKILI YA ASILI (YA KUZALIWA NAYO) ambayo kila mtu amewekewa na MUNGU ili tu ule MUONGOZO aliopewa na MUNGU aweze kuufuata kwa kutumia AQLIL GHARIZIYYU au AKILI YA ASILI na ndio mana MWENYEZI MUNGU anazungumzia katika moja ya malalamiko ya WATU WA MOTONI ambayo watayatoa watalalamika wakisema kuwa ; [colo=red]"LAU KUNNAA NASMA'U AU NA'AQILU MAA KUNNAA FIY ASW-HAABIS SA'IYR, FA'ATARAFUU BIDHANBIHIM FASUHQAN LI ASW-HAABIS SA'IYR - LAU TUNGEKUWA NI WENYE KUSKIA NA WENYE AKILI BASI TUSINGEKUWA SISI NI WATU WA MOTONI, NA WATAYAKUBALI MADHAMBI YAO NA KUJIUNGA KATIKA KUNDI LA WATU WA MOTONI"
[QURAN 67:10-11]

images

images


Hapo tunaweza kuona wazi kuwa hao wanaolalamika walishindwa kutumia AKILI zao kuishi katika ile KAMBA aliyotufunga nayo BWANA MUNGU WETU na kupelekea kuyafuata MATAMANIO MABAYA mwishowe yakawapeleka MOTONI kutokana na yale aliyoyakataza MUNGU wao, wao wakayatenda.

Tuchukulie mfano mwengine wa wasomi ili kuweza kuona je, kusoma sana ndio kuwa na AKILI, hapa tuwaangalie watu ambao wapo mavyuoni kwa mfano, na tuwaangalie zaidi dada zetu au wanawake kwa ujumla ambao wamesoma mpaka wamefika Chuo Kikuu kwa matendo wanayoyafanya je, ni sahihi ukilinganisha na ile ELIMU waliyo nayo halafu tujiulize je, vinafanana?, au je, mtu huyo unaweza ukasema kuwa ana AKILI? Kwa mfano, utakuta msomi kama huyu amevaa kiguo ambacho kwanza kinambana sana na pili kiguo chenyewe ni kifupi mno kiasi kwamba hata akitembea tu inampasa kuwa anakivuta vuta kukishusha chini kwa sababu kiguo chenyewe kinapanda juu, lakini hakuna aliyemlazimisha kukivaa kiguo hicho amekivaa kwa hiari yake na anajua wazi kuwa kiguo hicho anapovaa anapata tabu sana anapopita mbele za watu, lakini kwa makusudi akaamua kukivaa bila ya kujali tabu atakazopata njiani na wala aibu atakayopata anapopishana na watu mpaka kupelekea kupata tabu ya kukivuta vuta kishuke chini wakati kiguo chenyewe kinapanda juu, sasa huyu alichokikosa ni INDUCTIVE REASONING ambayo ni BUSARA it means HAKUFIKIRI KABLA YA KUVAA, lakini angefikiri kwamba "AAH, NAWEZA NIKAKUTANA NA WATU AMBAO NAWAHESHIMU SANA" au anaweza kukutana na watu kadha wa kadha, basi wala asingefanya hicho alichokifanya ila yote ni kwa sababu tu ya kushindwa KUFIKIRI that's why akashindwa kupambanua mambo na kushindwa kuliweka jambo mahala pake, kwa kifupi kakosa HEKIMA mtu kama huyu, sasa kwa tafsiri ya haraka haraka hapa tunaweza kusema kuwa huyu ni msomi ndio na ana ELIMU kweli lakini AKILI HANA.

Hebu turudi kwenye ile AYA inayozungumzia UTALII na kututaka watu tufanye UTALII kwa lengo la KUONGEZA AKILI ZETU na KUMJUA MUNGU WETU VYEMA, AYA hii inasema kuwa ; AFALAM YAHDI LAHUM KAM AHLAKNAA QABLAHUM MINAL QURUUNI YAMSHUUNA FIY MASAAKINIHIM, INNA FIY DHAALIKA LA AYAATIN LIULIN NUHAA - HIVI, HAWAKUPATA HABARI HAWA (WATU WA MOTONI) WAKATI WAPO DUNIANI YA KUWA NI WANGAPI TULIOWAANGAMIZA KABLA YAO KATIKA KARNE ZILIZOPITA, WAKATEMBELEA MAKAZI YAO HAO WATU WALIOPITA ILI KUJIONEA, HAKIKA KATIKA HAYO ZIPO DALILI ZA WAZI ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU KWA WATU AMBAO WANA AKILI" [QURAN 20:128].
KAxKA0wNYAcL-_Zb_c1Aen1D2PAlfnenNz69Ugax466XfLVlbaPyw_WCdwqXrCo8w-46biqQ7Bgt3WKTHuPDMylSO9oxeNoSiP3OLmFCSVbSshUZ_dnPckF7mYToNNuCx3IxaQ=w341-h432-nc

Hapo tunaweza kuona neno NUHAA lilivyotumika kama AKILI na pia tumeona ni jinsi gani MUNGU anataka tujifunze kupitia matukio au sehemu mbalimbali zilizopita au za kale ili tuweze kuongeza AKILI zetu na KUMJUA YEYE zaidi na zaidi. Na pia, kuna neno jingine ambalo ni HIJR tulisema pia kuwa ni AKILI, hili tunaweza kuliona pale MUNGU aliposema kuwa ; "HAL FIY DHAALIKA QASAMUN LIDHIY HIJR - YANI KATIKA HAYO KUNA KIAPO KWA MWENYE AKILI [QURAN 89:5].
Aj-CSky65mJi5Em4QxaMrLFXizdj8r3BusWlsJqMXjxKffc9DfjgjvmKDXP3yfQgJLTXUzS-axHtfyKm1ppvI71h-r5vHgfJ-TQVd6Bk8482xf4hZAjO6OTiCGXB8i_V9G1PzQ=w384-h384-nc

images


Hivyo basi, katika MTAZAMO wa KIDINI ili mtu aonekane kuwa ana AKILI inabidi ajumuishe hayo mambo ma 3 ambayo ni BUSARA, HEKIMA NA UTAMBUZI. Kuwa na MAARIFA ni sehemu ndogo sana ya AKILI kwa sababu MAARIFA anaweza kuwa nayo yoyote yule kwa sababu ni ujuzi wa kufanya kitu fulani, mtu anaweza kuwa ni mgonjwa wa AKILI lakini akatumiwa kutengeneza hata RADIO au TV, sasa hayo ndio MAARIFA ambayo huwa ni sehemu ndogo sana ya AKILI, anaweza hata akatumwa jambo na akaleta, haya ndio tunaita kuwa ni MAARIFA, mfano mzuri ni kama Mbwa ambapo anaweza kuwa na ujuzi wa kufanya jambo fulani, huwezi kusema eti Mbwa ana AKILI, huyu Mbwa atakuwa ana maarifa tu ambapo MAARIFA ni ujuzi mdogo sana wa kuweza kufanya jambo fulani, ambapo kwenye suala la mgonjwa wa AKILI au CHIZI ndipo mtu unapoweza kuskia mtu akiitwa CHIZI MAARIFA, hapa ndipo lilipopatikana hili jina, ni kwamba mtu ana uwezo au ujuzi tu wa kufanya jambo fulani hii tunasema kuwa huyu mtu ana MAARIFA lakini hana AKILI.

Katika Lugha nyingine hii Verbal Comprehension tunaweza tukaiita kuwa ni TAMEEZ yani no uwezo wa kupambanua jambo, sasa TAMEEZ ni uwezo ambao hata mnyama anaweza kuwa nao, tuchukulie mfano labda kwa mnyama kama SIMBA unaweza kusema ana AKILI au HANA? Tumeamua kumuangalia SIMBA kwa mfano, pale anapowinda na kuona kundi la wanyama, anaamua kwanza kuwatisha lakini lengo lake linajulikana ni lipi, sasa anapowatisha na kuona kuwa hawajashtuka anaamua kuingia katikati ya kundi au kuwazunguka kwa kasi, basi yule atakayeamua kukimbia peke yake ndio huyo huyo atakayemkimbiza na kumkamata, sasa unaweza ukasema hii aliyotumia hapa ni AKILI au ni nini?

Ile sio AKILI isipokuwa kuna kitu kinachoitwa ILHAAMUL AS-LIYYA ni ujuzi wa kiasili ambao MUNGU anauweka kwa viumbe wake ili kuweza kuyatawala mazingira yao. Licha ya huyo Simba au Mbwa lakini pia kuna wanyama wengi tu ambao wanafundishwa kufanya mambo tofauti tofauti na hili huwa tunaona hata kwenye circus maonesho ya wanyama tofauti tofauti wakifanya vitu mbalimbali, sasa unaweza ukasema hawa wanyama wana AKILI? Ukitaka kujua kama wana AKILI au hawana watazame kwenye suala la BUSARA, HEKIMA na UTAMBUZI ndio utajua kuwa wana AKILI au LAA kwa mfano, hao hao wanyama ambao wamefundishwa kufanya mambo fulani ukiwapelekea vitu au mambo ambayo hawajafundishwa, unafkiri watayafanya kwa usahihi kama wanavyofanya hayo mengine waliyofundishwa...?. Utaona wazi kuwa jibu utakalopata litakuwa ni HAPANA hawataweza kuyafanya kwa USAHIHI tofauti na vile walivyofundishwa. Kwa hivyo basi, katika mtazamo wa KIDINI au KIISLAM utaweza kuona kuwa mwenye AKILI ni yule anayeishi katika MIPAKA aliyowekewa ya kuwa, hili akilifanya atakuwa ni MWENYE AKILI na hili akilifanya atakuwa SI MWENYE AKILI. Na hili suala pia lipo hata kwenye maisha halisi ya kawaida tunayoishi pia ni hivyo hivyo kuna mambo ukiyafanya utaonekana kuwa ni una AKILI na kuna mambo ukiyafanya pia utaonekana kuwa hauna AKILI hata kidogo.

Mfano wa haya tunayojadili katika kupata mtazamo wa kuona kuwa AKILI ni nini kupitia BUSARA, HEKIMA na UTAMBUZI tunaweza kuona kuwa kuna mtu anaweza kuwa na UTAMBUZI MDOGO yani kutambua kwake ni kudogo sana, sio kwamba HANA AKILI hapana anayo ila ana sehemu kidogo tu katika suala zima la AKILI, ndio mana kumkuta mtu ambaye hana AKILI kabisa haiwezekani, itakuwa tu ana UTAMBUZI mdogo lakini sio kwamba hana kabisa AKILI, lazma atakuwa ana sehemu japo kidogo tu katika AKILI aidha atakuwa na KUMBUKUMBU ambapo ukiwa nayo hiyo wala huhesabiki saaana eti kuwa una AKILI kwa sababu, kuwa na KUMBUKUMBU tu ikawa huna BUSARA, HEKIMA wala UTAMBUZI kwa kifupi haisaidii kitu na haipelekei kuonekana eti una AKILI, kwa maana hata Paka pia ana KUMBUKUMBU nzuri sana, katika kulithibitisha hili kwa Paka hata ukimchukua ukaenda kumtupa utakapomtupa basi juwa wazi kuwa ATARUDI TU, sasa hiyo ndio inaitwa ILHAAMUL AS-LIYYA ni ujuzi wa kujua au ni uwezo ambao ni wa ASILI MUNGU ameamua kuuweka kwa viumbe wake ili waweze kuishi katika mazingira yao vyema kabisa.

Naweza kusema kuwa mada ya AKILI ni mada ngumu sana halaf pia ni PANA SANA, lakini kwa ujumla wake ni kuwa, kwenye hii sehemu ya KUMBUKUMBU katika UISLAM wanaitambua pia ambapo huku kwengine wanaiita kuwa ni MEMORY ambapo katika UISLAM tunaambiwa kuwa mtu kama hana KUMBUKUMBU nzuri basi habari zake tunaambiwa sio sahihi. Kwa sababu mtu hawezi kukupa HABARI wakati KUMBUKUMBU yake sio nzuri kisha akawa anakupa habari za nyuma tofauti tofauti, hili suala katika UISLAM wala haikubaliki na tunasema kuwa "MTU AMBAYE HANA KUMBUKUMBU ILO NZURI BASI HABARI ZAKE SIO SAHIHI".

Hapa tunazungumzia kuhusiana na MEMORY ya mtu na ndio mana utaona kwa mfano ulio halisi kwa mtoto mdogo unapomkataza kitu asishike au asifanye jambo fulani, lakini utakuta baada ya muda mfupi tu anaweza akarudia jambo lile lile ambalo umemkataza asilifanye, yote hii ni kwa sababu MEMORY yake au utunzaji wake wa KUMBUKUMBU ni mdogo sana kiasi kwamba wanasahau kwa kipindi kifupi mno, lakini pia tuangalie mfano mwengine kupitia hawa hawa watoto, kwa kuwa AKILI zao bado haziko sawa sawa basi utunzaji wao wa KUMBUKUMBU huwa ni mdogo sana na hili utaweza kuthibitisha pindi tu pale wanapogombana, huwa haichukui muda mrefu utaona wameshasahau ugomvi wao, wanarudi kama awali na kuendelea kucheza pamoja kama vile hakijatokea kitu chochote kile kati yao.

Sasa basi, kutokana na maelezo yooote hayo uliyosoma nikikuuliza AKILI NI NINI utaweza kunipa jibu gani?, au hii AKILI hii inakaa sehemu gani katika mwili wa BINADAM utaweza kunipa jibu gani? Katika SAYANSI unaweza ukasema hii AKILI hii ikoje ikoje labda umbo lake, au ina muonekano gani labda, au ina rangi gani pengine, labda unaweza ukaishika au laa, katika mtazamo wa KISAYANSI hiko kitu hakijulikani kuwa kikoje au kinafananaje hasa mtu anaposema AKILI, katika SAYANSI kuna kitu kinaitwa EXPERIMENT na OBSERVATION watu hufanya UTAFITI NA MAJARIBIO mwishowe huibuka na majibu kamili, lakini mpaka leo bado haijajulikana kuwa hii AKILI hasa ni kitu gani umbo lake ni lipi au ikoje na inafananaje pia, sio kitu kama vile moyo au ubongo au nini, ila KISAYANSI wameweza tu kujua kuwa AKILI inakaa wapi, katika SAYANSI ya zamani imeweza kujua tu kuwa AKILI ni inakaa kwenye ubongo peke yake.

Na kuna nadharia moja katika SAYANSI inajulikana kama - P-FIT, P-FIT, P-FIT inasemaje hii theory, inasema kuwa AKILI zetu huwa zinategemea kazi mbalimbali za ubongo na sehemu mbalimbali za ubongo ambazo zinapatana, sasa basi, kwa kauli hii ya WANASAYANSI tunaweza kuona kuwa wanaafikiana kwamba AKILI inakaa kwenye ubongo, lakini swali ni kwamba je, unaweza ukaichukua, ukaishika, ukaiona? Hapa ndipo SAYANSI inapojifunga yenyewe kuwa, kile ambacho SAYANSI haikijui isiseme kwamba hakipo, kwa sababu hapa SAYANSI inakubali kitu ambacho HAKIPO lakini KIPO, kwa sababu AKILI si haionekani na wala hauwezi kuishika lakini bado SAYANSI inaamini kuwa ipo na kuna kitu kinachoitwa AKILI lakini sasa kwa nini isiamini kwamba kuna MUNGU?. Kwa sababu huwezi kumuona, huwezi kumuhisi, wala kumthibitisha ila uwepo wake unaweza kuujua tu kutokana na matokeo fulani kama ilivyo kwa AKILI kwamba, unajua mtu fulani ana AKILI au HANA kutokana na matokeo ya MATENDO au KAULI zake, sasa kwa nini wasiamini juu ya uwepo wa MUNGU kutokana na matokeo yote yaliyopo ULIMWENGUNI.?. Sio kila ambacho hakionekaniki HAKIPO, kwa sababu hata kwenye SAYANSI kuna mambo mengi ambayo hayaonekaniki lakini wanasema yapo na wanayapa mpaka majina, chukulia mfano kitu kama VITAMIN au PROTEIN na wanasema kabisa kuwa eti kwenye maziwa kuna Protein waliwahi kuiona...?. Ukiwaambia waitoe hiyo Protein watuoneshe wataweza kufanya hivyo, ila kwa sababu tu kuna dalili ya kitu fulani ndio husema kuwa eti kwenye Maziwa Protein ila ukiwaambia hebu tutoleeni hiyo Protein tuishike na tuione sidhani kama wataweza kufanya hivyo lakini wanaamini kuwa ipo ila hawaamini kabisa katika uwepo wa MUNGU wakati matokeo au dalili zake zipo wazi kila sehemu atakayokuwepo BINADAMU katika MBINGU NA NCHI.

Lakini katika UISLAM hii inayofahamika kwa jina la AKILI, ni kweli UISLAM unakubali kuwa ipo lakini kiuhalisia huwezi kuiona ila ina maelezo yake kama alivyosema MTUME MUHAMMAD (S.A.W} anasema kuwa "AKILI ni NURU inayopatikana ndani ya moyo wa MWANADAMU. Na ndio mana kwa mtazamo wa KIISLAM tunasema kuwa akili hupatikana sehemu au maeneo mawili, nikimaanisha kuwa kuna UBONGO na pia kuna MOYO. Tuanze kuangalia kwanza MOYO kwa nini tunasema AKILI hupatikana ndani ya MOYO, hii pia bado ina utata kwa WANASAYANSI kwa sababu hii ni SAYANSI ya hivi karibuni tu tofauti na vile ambavyo wamevifanyia utafiti miaka mingi iliyopita ambapo QURAN ilishayaelezea mambo hayo then wao wakaja nyuma na kufanya utafiti wao na kisha wakaja na majibu yao, ila kuhusu hii ya kuwa AKILI kupatikana kwenye MOYO bado inawaletea UTATA kidogo na hawajaafikiana kisawa sawa juu ya hili WANASAYANSI kwa sababu ni utafiti wa juzi tu si wa miaka mingi. Na hii dhana ya kusema kuwa AKILI hupatikana ndani ya MOYO ni kutokana na AYA inayopatikana ndani ya QURAN Sura ya 22 aya ya 46 inasema kuwa ; "HIVI WATU KWA NINI WASITEMBEE KWENYE MAENEO MBALIMBALI YA ARDHI (WAFANYE UTALII NA KUJIFUNZA) ILI KUTEMBEA HUKO WAWEZE KUWA NA MIOYO AMBAYO INAELEWA (NA KUWAFAHAMISHA MAMBO) hapa tunaona wazi kuwa neno kuelewa au kufahamu limetumika ambapo kitu kinachotumika KUELEWA AU KUFAHAM MAMBO (FAHAM) ni inaeleweka neno FAHAM au KUELEWA ni jambo ambalo linahusiana na AKILI", sasa basi kwa kauli hiyo unaweza kuona kuwa ni jinsi gani MOYO ulivyohusishwa na AKILI kwa njia moja au nyingine, hata katika SAYANSI lipo hili japo wamelifanyia utafiti baada ya QURAN kulithibitisha tangu karne nyingi zilizopita, wao wakaja na majibu kuhusu AKILI kuhusishwa na MOYO na wakasema kuwa inajulikana kama HEART INTELLIGENCE pitia hapa kujua zaidi - What is Heart Intelligence? - Gabriel Gonsalves
Heart-Intelligence-Education.001.png

Katika mtazamo wa KIDINI tuangalie tena ndani ya QURAN kuna AYA nyingine katika Surah ya 7 aya ya 179 inasema kuwa ; "WANA MIOYO LAKINI NYOYO LAKINI HAWAELEWI (WALA HAWAFAHAMU) KUPITIA MIOYO HIYO, WANA MASKIO LAKINI HAWASIKII NA WANA MACHO LAKINI HAWAONI, BASI HAO NI KAMA WANYAMA, LAKINI WAO WAMEPOTEA ZAIDI KULIKO WANYAMA" [Q 7:179]

images


Sasa basi, hizi hoja ambazo zinaongelea kuhusu HEART INTELLIGENCE kwenye SAYANSI ni hoja za juzi tu yani ni miaka ya hivi karibuni tu ndio wameweza kubainisha kuhusu HEART INTELLIGENCE wakati QURAN ilishazungumzia hiki kitu karne nyingi tu zilizopita. Kwa mfano, tumuangalie huyu Daktari anaitwa Dr. Anne Hilty
cColpGFFpP4-V_mVPgVQOTrk-fdMXyEfbZVDU61GYsebpGmXUh9ln7eRIaL8sqhWTk1VjI6eqn8Bavz2PC0Lnoa7DeAvLm8UxpTijkzmUYA=w242-h288-nc


Katika moja ya tafiti zake amewahi kusema kuwa "WANASAYANSI WAMEGUNDUA KUWA, NISHATI INAYOTOLEWA NA NGUVU YA MOYO INATUSAIDIA SANA KATIKA MAISHA KULIKO WATU WANAVYOWEZA KUFIKIRIA" kwenye hili kuna maelezo mengi tu na hata huyu MWANASAIKOLOJIA maarufu ameweza kubainisha hilo kuhusu HEART INTELLIGENCE.
hearts-brain1.jpg

images


Sio akili peke yake ndio inaweza kufikiri ila hata moyo pia una uwezo wa kufikiri.
images

intuition-card-intelligence.jpg


Hapo ndipo unapoweza kuona tofauti ya SAYANSI na DINI ni kuwa ; kwenye SAYANSI bado kuna vitu vingi ambavyo HAWAVIJUI au vinavyotakiwa kusomwa au kufanyiwa UTAFITI mara kwa mara ambapo kwenye DINI kuna vitu vingi tayari vimeshaongelewa ambavyo SAYANSI inakuja kupata UTHIBITISHO wake miaka mingi baadae. Unaweza kupitia hapa chini kwa maelezo zaidi kuhusiana na HEART INTELLIGENCE
What is Heart Intelligence? - Gabriel Gonsalves

Ila pia katika kuthibitisha uwepo wa AKILI ndani ya ubongo QURAN ilishalieleza suala hilo karne nyingi sana ndani ya Surah ya 96 Aya ya 15-16 kuwa ;
images

8562a4401770dbfa08597d4ad2226516.jpg


Unaweza kuona hapo juu kuwa QURAN imeongelea ubongo wa mbele wa MWANADAMU kuwa unahusika na kazi gani, moja ya kazi zake ni kutengeneza UONGO. Sasa haya mambo yalishaongelewa KARNE NYINGI sana nyuma na QURAN ambapo hata SAYANSI ilikuwa bado haijavijua hivi vitu.
lying.png

DHbt53ZonR5z0FOgY6Z4vlYzZBpFaVIdZZ5jQrPLkhOuZT_8rKnctvwmS9fWBBxJZHrB8JYNj40mVzrA9OHlHRD37tpyp2hwQ_IB=w443-h332-nc


Well, katika maelezo yooote hayo uliyosoma hapo juu nikikuuliza swali kuwa, mbona kuna familia nyingine karibia familia nzima utaskia wanasema karibia wote wana AKILI kutokana na mtazamo wao, pia utakuta kuna familia nyingine karibia wote wana matatizo ya ugonjwa wa AKILI sasa je, kuna suala zima la kurithishana kuhusiana na masuala ya AKILI au inakuaje...?. Suala la Genetical Inheritance lipo ila pia hili lipo katika mtazamo tofauti pia.

Kwa kifupi AKILI ni Lugha ya jumla ambayo inakusanya vitu vingi ndani yake ambapo mtu akiwa navyo au akivifanya ataonekana kuwa ana AKILI na asipokuwa au asipovifanya akafanya tofauti ataonekana kuwa hana AKILI. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa AKILI ni matokeo ya kile anachokifanya mtu mwishowe yale matokeo yanayopatikana ndio huweza kujua AKILI ya mtu husika. Hii ikijumuisha vile vitendo unavyovitenda, kauli unazoongea, matatizo unavyoyasuluhisha, vile unavyoishi katika kupata suluhisho ya matatizo yako na jamii inayokuzunguka kwa ujumla ikawaletea faida au madhara. Lakini pia, katika mtazamo wa KIDINI yapo maelezo yanayohusiana na AKILI kupitia BIBLIA NA DINI YA KIKRISTO ambapo kwa sababu ya urefu wa mada na maelezo yaliyomo nimeona niandae mada kamili peke yake. Lakini pia, nimeona nianze na hii then ikija hiyo utaweza kuelewa zaidi kufuatia mlolongo na mpangilio ulivyo ikiwa ni kutokana na ASILI ya neno lenyewe AKILI limetokana na Lugha ya Kiarabu na ndio mana nikasema niichambue kupitia mtazamo huo kwanza then nikileta uchambuzi wa utazidi kufunguka zaidi na zaidi japokuwa mpaka hapo utakuwa umeshaelewa kuwa AKILI NI NINI.

Sent using Jamii Forums mobile app[/color]
 
Mkuu nimepata mambo mawili matatu, ila next time usiegemee kwenye dini moja tu, ingependeza zaidi kama tungepata uelewa wa hiyo mada kwenye context ya dini nyingine pia kama vile wakristu wanasemaje, mabudha wanasemaaje, scientologist and atheist wanasemaje. Hii ingeifanya story yako kuwa more comprehensive,but its good thread.
 
Mkuu nimepata mambo mawili matatu, ila next time usiegemee kwenye dini moja tu, ingependeza zaidi kama tungepata uelewa wa hiyo mada kwenye context ya dini nyingine pia kama vile wakristu wanasemaje, mabudha wanasemaaje, scientologist and atheist wanasemaje. Hii ingeifanya story yako kuwa more comprehensive,but its good thread.
Nashkuru sana kiongozi wangu unachosema ni kweli kabisa, hiko ulichokibainisha kipo kwenye hatua za kati katika kuandaa na itakapokuwa tayari tu ntaiweka hapa jamvini kiongozi.

Nimeona nitangulize hii nikiwa na maana, ili ntakapoleta katika mtazamo mwengine iwe rahisi zaidi kueleweka hata kwa watu wasioelewa itawasaidia kuelewa zaidi kiongozi.

Nashkuru sana kuwa tuko pamoja mkuu. Thanks.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante NDUKI kwa kurejea... Hili neno AKILI lilishawahi kuzua mjadala mkubwa sana hapa jamvini

Jr
Asante kiongozi nimerudi nyumbani HOGT nilipotea kidogo jukwaani majukumu yanabana kiasi.

Well, unachosema mkuu nakubaliana nawe kabisa kwa asilimia zaidi ya 100 kuwa hili neno wengi sana huwa linawachanganya na hata wengine kushindwa kujielewa kuwa wana AKILI au hawana yote ni kwa sababu tu, ya utata wa neno lenyewe ; AKILI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom