Milioni 29 Zatolewa na Mbunge wa Viti Maalum Katavi Kuwainua Wanawake Kiuchumi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

MBUNGE MARTHA MARIKI ACHANGIA MILIONI 29 VIKUNDI VYA WANAWAKE KATA ZOTE ZA KATAVI ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki tarehe 03 Julai, 2023 ameanza ziara rasmi kutembelea Kata zote za Mkoa wa Katavi na kuzungumza na wananchi.

Katika ziara yake, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki ameanza kwa kuchangia Shilingi Milioni 29 kwa makundi ya akina Mama yaliyopo Kata zote za Mkoa wa Katavi ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mbunge Martha Mariki amekabidhi Kadi elfu mbili (2,000) za CCM kwa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwaajili ya kuwapa wanachama wapya wanaojiunga na Chama Cha Mapinduzi

Vilevile, Mhe. Martha Mariki, jana tarehe 03 Julai, 2023 ametembelea Bandari ya Karema iliyopo Kata ya Karema Wilaya ya Tanganyika alizungumza na wananchi na kusikiliza kero za wananchi wa Wilaya ya Tanganyika

Aidha, Mhe. Martha Mariki alihudhuria katika msiba wa aliyekuwa Balozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) shina namba 8 Tawi la Muweza Kata ya Karema na kuwapa mkono wa pole wafiwa, familia, Ndugu, jamaa na marafiki katika msiba huo.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Karema Wilaya ya Tanganyika, Mhe. Martha Mariki amewaomba wakinamama waliopatiwa fedha za kujikwamua kiuchumi kuzitumia kwa malengo mahususi ili mtaji ukue na kuongeza pato la familia, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla

Kwa upande wao, wananchi wa Wilaya ya Tanganyika wamemueleza changamoto mbalimbali Mbunge wao katika Kata ya Karema huku wakitoa maoni mbalimbali juu ya kuendelea kuinua uchumi wao.

Aidha, Mhe. Martha Mariki amewaahidi wananchi hao kuzifanyia kazi kero zilizopo huku akiwapongeza wananchi kwa ushirikiano wanaompa na kuwataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza uzalishaji mali na kukuza kipato.
WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.28(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-04 at 09.54.43.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-04 at 09.54.42(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.26.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.30(1).jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.28(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.28(2).jpeg
    139.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.29(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.29(1).jpeg
    161.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.29(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.29(1).jpeg
    161.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.28.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.28.jpeg
    147 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.28(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-04 at 08.41.28(1).jpeg
    109.6 KB · Views: 3
Back
Top Bottom