Na kwa sababu hatujui, kutaka kujua kwa kuhoji habari za wosia unasemaje si baya. Kutojua dawa yake ni kujua.
mimi naweza kusema sisi hapa kumjadili marehemu kafanya au hakufanya nini tunatenda makosa zaidi.
Hapa tunachojadili wengine ni zaidi ya marehemu, ni some principles, ni individual's rights to their wishes even after they die, ni kutokurupuka na kuchanganya tamaduni kwa kesi za watu walioishi muda mrefu katika tamaduni tofauti.
Bongo utamaduni wetu unaweza kuwa ukisikia mtu anapiga kelele nje kwako nenda kamsaidie, wengine kwao utamaduni wao unaweza kuwa ukisikia mtu anapiga kelele nje kwako piga simu polisi/ security usijivije jukumu la kumsaidia. Kwa hiyo tamaduni mbili hizi zinapogongana, usipokuwa muangalifu unaweza kufikiri unasaidia kumbe ndiyo unazidi kuharibu mambo.
Anyway hapa kuna haki za wengi, mke pia anayo haki na watoto pia wanayo haki,
Nimeongelea haki za mke na watoto hapo juu, sina hakika kama umezisoma.
na kwa vile marehemu ametangulia tunaweza tukasema mwenye maamuzi makubwa kwa sasa ni mke wake,
Tunarudi kule kule kwenye migongano ya tamaduni. Wewe unatoka kwenye utamaduni unaosema mtu akifa hana uamuzi tena. Kuna watu wameandika precise prescription wakifa nini kifanyike, down to the suit they should be clothed in. Utasemaje "maamuzi makubwa sasa ni kwa mke" wakati hatujui kama kuna will na kama ipo inasemaje?
na kama mke wake kaamua ndugu watafutwe who are we to say otherwise ?
You are skirting the will entirely. Mke akienda tofauti na matakwa ya mume kuhusu nini kifanyike baada ya mume kufa itakuwaje hapo? Mke hafuati matakwa ya mume mara zote. A special case to stress that can be made for intercultural marriages, kwa nini tusitake kujua zaidi kwa kutafuta habari zingine?
Hata kama marehemu hakutaka ndugu zake watafutwe, Je mwanamke hana haki ya kuwatafuta wakwe zake ?
Napata mashaka kama unasoma/unaelewa nilichoandika. Nimeongelea haki za kuwatafuta "wakwe" zake, however funny that is, kwamba awatafute leo miaka karibu30 baadaye. Lakini let the man rest in peace first.
Privacy na rights za individual they are only valid in my opinion if they dont affect anyone else (emotional or otherwise), unless uniambie kwamba the significant other hana say kwenye maisha / maamuzi ya muhusika.
You are assuming kwamba napinga mke kujuana na upande wa ndugu, nimeeleza rights za watoto kujuana na ndugu zao wa upande mwingine (huyo mke kama miaka yote hii hajajuana na ndugu kwa sasa sipingi kujuana nao, lakini it's very awkward kwangu, if at all she chose that). So do not assume kwamba napinga mwanamke kujuana na ndugu, ila, under what circumstances? Mwanamme akiandika kwenye will yake hataki ndugu zake fulani na fulani waje kwenye mazishi yake kwa sababu ya beef lao la miaka 30 iliyopita, mwanamke ana haki ya kuita hao ndugu? Vipi kama mwanamme akisema hataki ndugu yake yeyote wa Tanzania kuja kwenye mazishi? Kuna sababu gani iliyomfanya huyu mume kukata mawasiliano kwa kipindi chote hicho? Mbona mnataka kui treat this outlier case kama mtu aliyefariki kijijini kwao amongst his people bila known peculiarities?
Pia jamii ya watu aliokuwa anaishi nao huku, kama hakuwaachia maamuzi ya kufanya iwapo atatangulia mbele ya Haki basi automatically wao ndio watajua cha kufanya, sababu ni wao ndio watahusika kuandaa mazishi yake as well as kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa (unless kama aliacha fungu la pesa na maelekezo ya kufanya siku akiondoka)
Jamii yenyewe ndio sisi, dunia ni kijiji siku hizi, acha kufikiria in parochial ways. Jamii forum yake si ndiyo hii Jamiiforums? Sasa unaongelea Jamii gani zaidi wakati ushaambiwa marehemu hata uanachama wa JF alikuwa nao?
By the way hapa ninatoa mifano tu kama hiki au kile kikitokea au mtu yoyote akikumbwa na issue kama hii simuongelei marehemu sababu sijui facts zozote
Which is precisely my point, to negate your point kwamba "mimi naweza kusema sisi hapa kumjadili marehemu kafanya au hakufanya nini tunatenda makosa zaidi". Kujadili hili suala ni kujifunza tunatakiwa kufanya nini kwa habari kama hizi.
Habari ambazo si muhali tukisikia hapo baadaye zinatokea tena, kwani wote ndiyo njia yetu hiyo, wnaolowea na kusahau kwao wengi.
Shauri zenu washashi. Mimi nimepiga simu na kuongea na nyumbani kwa kama masaa matatu hivi over the weekend.
Na kurudi bongo at least once every two years like House Elections.