Michael Augustine Lukindo

Michael Augustine Lukindo

JC Freak

Member
Joined
Dec 4, 2013
Posts
57
Reaction score
31
Habari jamani.

Ninaandika ujumbe huu kwa kuomba msaada. Mtanzania mwenzetu amefariki in Madison Wisconsin-USA, wanatafutwa ndugu zake. Ni mtu wa Tanga Michael Agustine Lukindo.

Alikuja USA miaka mingi iliyopita, inasemekana zaidi ya mika thelathini. Ameacha mke (African American) na watoto wanne, mkubwa alizaliwa 1989 familia yake haijui ndugu za Michael. Mazishi yatafanyika Jumamosi, ila mwili utachomwa.

Kama unafununu au kujua lolote kuhusiana na ndugu yetu huyu unijulishe. Lengo nikuweza kuwafahamisha ndugu zake nyumbani Tanzania.

Asante kwa ushirikiano wako.
 
Habari jamani. Ninaandika ujumbe huu kwa kuomba msaada. Mtanzania mwenzetu amefariki in Madison Wisconsin-USA, wanatafutwa ndugu zake. Ni mtu wa Tanga Michael Agustine Lukindo. Alikuja USA miaka mingi iliyopita, inasemekana zaidi ya mika thelathini. Ameacha mke (African American) na watoto wanne, mkubwa alizaliwa 1989 familia yake haijui ndugu za Michael. Mazishi yatafanyika Jumamosi, ila mwili utachomwa. Kama unafununu au kujua lolote kuhusiana na ndugu yetu huyu unijulishe. Lengo nikuweza kuwafahamisha ndugu zake nyumbani Tanzania. Asante kwa ushirikiano wako.

daaa mgosi wa kaya huyo jamani lakin ndio hvyo ukimyA na kutokutoa taarifa kwa ndugu madhara yake ndio hayo.
 
Acha achomwe kama baniani.
Nyie mkifika huko hata mungu hamumjui.Maana inaonekana hataKanisani alikuwa ahudhurii.
Maana mie najua makanisa mengi ya huko waumini wake wanafahamika na ni rahisi kuzikw Kiimani.
Anachomwa hapa na Mungu anamsubir,atajua Faid ya kula bta na kumsaha Mungu.

Na Mbaya zaidi,watu wanaona kwamba wakifika huko hakuna kufa,na hata kusaidia ndugu zake angalau hata mmoja kumtoa kwa kumpeleka huko,kwa mika yote 30 aliyokaa huko eti hana ndugu.Nyambaafffffff huko ulipo
.Na kizazi chake ndio kimepotea kabisaa.Maana hao watoto ni wa mama.

Na nyie mnashindwa hata na baadhi ya makabila yana umoja wao katika mikoa ya hapa Bongo.Nyie mmekaa tu huko hata umoja wenu wa wa Tanzania hamna,mana lazima mngejua ndugu zake.

Wakati anakula maisha hakuwatafute,huo mzoga ndio ndugu watafutwe,mitoto mikubwa hiyo hata kwa baba yao haipajui.

Waambie kwa miaka hiyo 30 na huku ndugu zake wote wameishakufa.

Halafu naomba kesho kabla hajachomwa nenda kamfunue Umzabe kibao kimoja kwanza cha adabu.
 
Huyu hakuwahi kujiandikisha kwenye daftari. Trust me, nimelipitia tena daftari na jina lake halipo kabisa.

Kuna wabongo wengine wakishafika huko kujichanganya mwiko na mawasiliano na bongo zero.
Kuna mmoja nilikutana nae ni mtu mzima sana na aliondoka bongo in 1958. Aliniambia hata kwao kasahau wala hakuna anaemjua.
 
Mkuu,at least mngekuwa mnajua anatokea Tanga sehemu gani kwa sababu hilo jina la Lukindo wapo weeengi wa koo tofauti,wazigua,wabondei.sasa huyo katokea Tanga ipi?
 
Kuna mmoja mchagga yuko Adelaide keshakuwa mzee kbs hata sijui kama ndugu zake wanataarifa nae. Anapiga lager na kuishi kisela mtu mzee kbs, hatari sana!

Majina ya akina Lukindo wako wwngi huenda atapatikana nduguye, poleni sana




Sent from Nokla using Jf app
 
mkuu msiishie kum pm jamaa mcoment pia maanaake tunataka kupata undani wa hili swala. vp alikuwa member jf?
 
Acha achomwe kama baniani.
Nyie mkifika huko hata mungu hamumjui.Maana inaonekana hataKanisani alikuwa ahudhurii.
Maana mie najua makanisa mengi ya huko waumini wake wanafahamika na ni rahisi kuzikw Kiimani.
Anachomwa hapa na Mungu anamsubir,atajua Faid ya kula bta na kumsaha Mungu.
Mkuu huko nje wanachoma sio sababu ya Imani, pia sababu ya gharama na sehemu za kuzika hakuna, burial places zinakuwa na gharama kwahio hata ukiwa mkristu unajikuta unachomwa na ndugu kuchukua majivu for remembrance.

Hata huku tunavyouza nchi yetu na population inavyoongezeka maybe a 1000 years from now kutakuwa hakuna alternative bali kuchomwa moto.

By the way sio busara kuanza kumsema vibaya mtu aliyetangulia mbele ya haki...

RIP Mtanzania mwenzetu.
 
May all beings attain enlightenment.

Mnajua kama alitaka ndugu zake wajulishwe au mna assume assume tu kibongobongo?

Mtu kakaa kiwanja mvua thelathini, pengine alichotaka ni ndugu zake wasijulishwe.

May all beings attain enlightenment.
 
May all beings attain enlightenment.

Mnajua kama alitaka ndugu zake wajulishwe au mna assume assume tu kibongobongo?

Mtu kakaa kiwanja mvua thelathini, pengine alichotaka ni ndugu zake wasijulishwe.

. May all beings attain enlightenment.
You are absolutely right, mkuu.
I'm pretty sure he had left a will behind and his wishes have been carried out as he wanted (cremation)
 
Akiwa mzima hajataka kuwasiliana na ndugu zake, kafa mnamtafutia ndugu, kisa nini?
Huyo mke wake asiwatafute hawa jamaa maana watamletea mila zetu nyeusi afe kwa stress.
 
Mkuu kuna tangazo limekuja hapa foreign affairs kutafuta ndugu toka kwa mkewe ni serious watanzania wa mbele wanatia aibu

Ndivyo alivyotaka hivyo mwenyewe?

Watu wengine wanagombana na familia zao wanajitia nchi za watu mahsusi ili kukata link zozote na ndugu zao, angalieni msije kuwa mnafikiri mnasaidia kumbe mna violate wishes za marehemu.

Aliacha will? Kama ipo inasemaje? Kama haipo sababu zinazomfanya huyu mkewe awatafute ndugu zake ni nini?

Kuna hela ya life insurance anataka kuwagawaia? Kuna majivu ya marehemu anataka kuwagawia? Anataka wanawe wajuane na ndugu wengine wa Tanzania?

Mtu kakaa miaka thelarhini hana habari na ndugu zake Tanzania, leo kafariki rationale ya kutafuta ndugu ni nini?
 
Ndivyo alivyotaka hivyo mwenyewe?

Watu wengine wanagombana na familia zao wanajitia nchi za watu mahsusi ili kukata link zozote na ndugu zao, angalieni msije kuwa mnafikiri mnasaidia kumbe mna violate wishes za marehemu.

Aliacha will? Kama ipo inasemaje? Kama haipo sababu zinazomfanya huyu mkewe awatafute ndugu zake ni nini?

Kuna hela ya life insurance anataka kuwagawaia? Kuna majivu ya marehemu anataka kuwagawia? Anataka wanawe wajuane na ndugu wengine wa Tanzania?

Mtu kakaa miaka thelarhini hana habari na ndugu zake Tanzania, leo kafariki rationale ya kutafuta ndugu ni nini?
Labda anataka kuwapatia sehemu ya majivu baada ya cremation
 
Silly.............

Kama hujaweza kueleza what is silly and how is it silly, wewe ndiye unakuwa silly zaidi.

Mimi nataka uchunguzi tu, msije kutafuta ndugu wakati jamaa alikuwa hataki ndugu watafutwe kwa sababu ndugu wanaweza kutaka habari za kumrithi mke na kugombea mali, kitu ambacho kitamsumbua mke wake.
 
Labda anataka kuwapatia sehemu ya majivu baada ya cremation

Marehemu mwenyewe alitakaje?

Mke anaweza kuwa anataka kuwapa ndugu majivu ya mtu ambaye hakutaka hilo.

Na huko nyumbani unaweza kuambiwa hawakubali kwa sababu habari nzima ya kumchoma mtu moto kimila ni laana.

Ndiyo maana nauliza kuna will?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom