Uchaguzi 2020 Mgombea wa Urais wa Tanzania, Tundu Lissu afungiwa na NEC kufanya Kampeni siku 7

Itakuwaje kama Lisu ataamua kuendelea na kampeni kwa kupuuza tishio la Tume? Nafikiri ifike mahali hawa watu wapime madhara yatakayotokea baada ya kukurupuka kumridhisha mtu mmoja.

Lissu anajua anachokifanya na wakiingia kichwakichwa wameuvuruga uchaguzi wote na kazi ya kuiweka nchi pamoja itawachukua muda.
 
ila jamani tuache ushabiki huyu jamaa anafanya siasa za ugomvi hata hivo mi naona wamemvumilia sana ...
analazimisha ugomvi yaani
Wewe nawe kama lipumbavu! Hivi umemsikia mwenyekiti wa kijani jana anawaambia watu msipomchagua Silinde sileti maji hapa! Huko siyo kuvunja maadili ya uchaguzi? Tume iache double standard za kijinga!
 
Wanaendelea kumpiga chura take!

No wonder Polisi wamejidai kusitisha wito wa kumuita Lissu kwani ingekuwa ni too much kwa hizi taasisi za serikali zote kumsghulikia mtu mmoja hivyo wakaona watuzuge eti aendelee na kampeni kumbe wameshamzuia..
Lissu atatoa majibu ya ujeuri na kejeri tu, hana jibu la maana na atafanya hayo kama mwendelezo wa mkakati wa kuleta fujo na uasi kama wanavyo elekezwa na Asmsterdam and his GANG wanaotaka kuendesha GANGSTER POLITICS hapa nchini ili kuleta fujo. Ila kitu cha uhakika ni kwamba kikiwaka hata huyo Lissu HATOKI! hILO AWE NA UHAKIKA NALO NA Amsterdam hatakuwepo kumsaidi. Hawaijui nchi hii!?
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemfungia kufanya kampeni Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu kwa siku saba kwa madai ya kukiuka maadili ya uchaguzi...
Haina shida Tundu Lissu apumzike akirudi apige spana mpaka jiwe liombe po. Wamemsaidia sana. Anastahili kupumzika
 
Mimi naona wanampa muda wa kuweka mambo sawa kuliko angekuwa kwenye kampeni anazunguka anakosa hata muda wa kuweka mipango sawa.
 
Hiyo zimbabwe chini ya zanupf wazimbabwe wanaishi Kama mashetani kuzimu na ndio CCM wanataka kutupeleka huko!
Haijalishi ipoje kikubwa Zimbabwe na Zanupf zipo mpaka sasa ila Tshvangirai hayupo.
Pamoja na Tshivangirai kupewa kichwa na mabeberu lakini alipigwa spana
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemfungia kufanya kampeni Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu kwa siku saba kwa madai ya kukiuka maadili ya uchaguzi...
NEC haijafungua malalamiko juu ya Lisu ni NRA na vyama vingine vya siasa Sasa mpaka hapo tuiache NEC iendelee na majukumu mengine ya kufanikisha uchaguzi mkuu Lissu akapambane na kamati ya maadili kwa sababu yeye mwenyewe alisaini na kutoa tamko la kuheshimu hayo maadili Sasa ameamua kuzivunja makusudi hapo asisukumie lawama NEC akapambane na hali yake tuone Kama Robert Amsterdam atamsaidia
 
  • Thanks
Reactions: RMC
*Wito wa dharura, Mkutano na Waandishi wa Habari*

Chief, habari za muda huu?

Naomba kukutaarifu kuwa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Tundu Lissu, atazungumza na vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa, nyumbani kwake, *Tegeta (Azania) jijini Dar es Salaam leo Ijumaa, Oktoba 2, 2020, *saa 10.30, jioni*, kuhusu jambo la dharura na muhimu katika kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazoendelea nchini.

Tunatanguliza shukrani na samahani kwa wito huu wa dharura sana. Asante sana.

*Tumaini Makene*
*Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano*
*Chadema*
 
Wanaendelea kumpiga chura take!

No wonder Polisi wamejidai kusitisha wito wa kumuita Lissu kwani ingekuwa ni too much kwa hizi taasisi za serikali zote kumsghulikia mtu mmoja hivyo wakaona watuzuge eti aendelee na kampeni kumbe wameshamzuia...
Kauli ya kuropoka. Hasa sawa
 
Back
Top Bottom