Uchaguzi 2020 Mgombea wa Urais wa Tanzania, Tundu Lissu afungiwa na NEC kufanya Kampeni siku 7

Robot la Matope

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
6,913
13,448
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemfungia kufanya kampeni Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu kwa siku saba kwa madai ya kukiuka maadili ya uchaguzi.

============

Leo tarehe 02 Oktoba 2020 kamati ya maadili ya Kitaifa imesikiliza malalamiko dhidi ya Mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Bwana Tundu Lissu.

Malalamiko yaliwasilishwa na Chama cha NRA na Chama cha Mapinduzi. Chama cha NRA walilalamikia kitendo cha mgombea wa kiti cha Rais kupitia CHADEMA kutoa maneno ya uchochezi yasiyothibitika. Ambapo akiwa mkoani Mara, alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. John Pombe Magufuli ameitisha kikao cha wasimamizi wa Uchaguzi nchi nzima ili kuhujumu uchaguzi. Pia imeelezwa kuwa alitoa maneno ya kichochezi na ya kudhalilisha kinyume na Maadili ya Uchaguzi akiwa mkoani Geita.

Barua ya kumtaka kujibu tuhuma hizo iliwasilishwa kwa Katibu mkuu wa CHADEMA kwa mujibu wa taratibu. Katibu Mkuu wa CHADEMA alijibu kuwa, malalamiko hayakihusu chama hivyo, mgombea na chama ni vitu viwili tofauti. Pamoja na kwamba Katibu mkuu wa CHADEMA alijibu barua ya malalamiko kuwa malalamiko apelekewe Tundu Lissu mwenyewe, kamati ya maadili imeridhika kuwa taarifa kuhusu malalamiko ya ukiukwaji na Maadili iliwasilishwa kwa mlalamikiwa kwa mujibu wa taratibu kwa kuzingatia masharti ya ibara ya 39 ya Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambapo bwana Tundu Lissu alidhaminiwa na CHADEMA kugombea kiti cha Rais. Hivyo, barua ya malalamiko kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu ni sahihi kabisa.

20201002_150556.jpg
20201002_150559.jpg
 
Wanaendelea kumpiga chura teke, na pia ili CCM ianguke, ni lazima mambo na matendo kama haya yatokee na yaendelee kutokea.

No wonder wale wengine wamejidai kusitisha wito wa kumuita Lissu kwani ingekuwa ni too much kwa hizi taasisi zote kumsghulikia mtu mmoja, hivyo wakaona watuzuge eti aendelee na kampeni kumbe wameshamzuia.

Lissu hata angeitikia huo wito, sidhani kama maamuzi yangekuwa tofauti na haya waliyoyatoa.

Waendelee tu kufumbia macho matendo ya Mgombea yule huku wakishughulikia wengine wakidhani ndio wanambeba kumbe wanammaliza kwa kumuongezea Lissu kura za huruma plus kura za hasira kutoka kwa watu wasiopenda doublestand na uonevu.

Kumfungia Lissu kufanya kampeni, ni kumfanyia kampeni kubwa zaidi tena isiyo na gharama yoyote kwake ( it is a blessing in disguise).

Wanaangamia kwa kukosa maarifa.

Tusubiri majibu/kauli ya Lissu.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom