GE2025 Mgombea Urais, Coaster Kibonde: Nikishinda Urais, Rais Samia atabaki Ikulu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Makini Coaster Jimmy Kibonde amesema "nikishinda urais, Rais Samia atabaki Ikulu"

Na uwezi shinda chochote🚮🚮🚮

Yani uyu siyo mpinza ila nichawa kama wew unamuona ni bora kwanin anataka kugombea dhidi yake?

Hii tanzania kuna machawa kwenye kila sekta kila sehemu
 
Hivi vyama pandikizi ndivyo vinavyoharibu demokrasia hapa nchini, kwa kweli CCM ni adui wa haki kwa kila Mtanzania.
Halafu hao wapandikizi mbona wanakuwa kama wendawazimu!

Inakuwaje unashindwa hata kuzuga unaonyesha waziwazi kwamba wewe ni pandikizi?

Kumbe ni kweli ule msemo, kwamba '' Kunya waziwazi ndicho anachofanya mdwanzi''.
 
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia Makini, Coaster Jimmy Kibonde, amesema endapo atashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, atamwacha Rais wa sasa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndani ya serikali yake kwa nafasi maalumu ya kushughulikia diplomasia.

Kibonde, ambaye amezungumza kupitia kipindi cha Clouds360 cha Clouds TV, amesema amegundua Dkt. Samia ni mwanadiplomasia mahiri, hivyo atamkabidhi jukumu la kuongoza dawati maalumu litakalokuwa na idara tatu zinazoshughulika na masuala ya kisiasa, kiuchumi na ya kimataifa.

“Nimesema nikishinda urais, Mama Samia nitamwacha Ikulu. Nimegundua Mama Samia ni mwanadiplomasia mzuri mno. Kwenye diplomasia ya kisiasa, kiuchumi na mambo ya nje yuko vizuri. Kwa hiyo atakuwa mkuu wa dawati maalumu katika serikali yangu. Asiwe na presha, ajira nimeshamuahidi,” amesema Kibonde.
Yaani hawa ndiyo washindani wa Samia kwenye uchaguzi wa mwaka huu
 
Kwahiyo mama atazunguka TANZANIA nzima kupambana na cheyo?
Your browser is not able to display this video.
 
Haya yote ni ccm n machawa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…