Mfumuko wa vijana wenye Elimu Ndogo Pesa Nyingi Tanzania ni mkubwa sana; wanaongea ujinga na kuweka mbele kujionyesha na kujisifia mafanikio yao

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
14,176
Reaction score
25,919
Tanzania hivi sasa tunakabiliwa kwa kiwango kikubwa sana cha vijana tunaowaita Elimu Ndogo Pesa Nyingi (Tuwaite EP kwa kifupi - Elimu Pesa), ambao utawatambua katika namna ya maongezi yao, kutamba kwao na kujionyesha kwao. Hata humu JF wapo wengi tu. Utaongea nae dakika tatu tu na kujua kwamba ana Range Rover, Premio, Toyota Crown, au BMW. Ndio magari yao.

Na mara nyingi utawakuta wanavojifanya kuweka maneno ya kiingereza wakati wa kuongea Kiswahili kwa maana ambayo ni broken ya juu sana. Unajiuliza hivi kwa nini asiongee Kiswahili tu lugha ya Taifa?

Mara nyingi wanajifanya wanajua sana mambo na wametembea sana duniani - wakati mara nyingi walikoenda ni Joburg South Afrika na wengine China. Mwingine utakuta anasimulia story za kupanda ndege utafikiri anapanda kila siku, kumbe kapanda mara moja!

Na tunaelewa kwamba hawa ni vijana ambao wameibukia kuwa na pesa kutokana na fursa zilizopo Tanzania, kama China au kuchimba madini. Lakini tunajua pia wengine ni madawa ya kulevya na utapeli tu wakitumiwa na viongozi mafisadi, na wengine ni wizi.

Sasa kama wewe unajitambua ni mmojawapo wa vijana wa Elimu Ndogo Pesa Nyingi, hebu acha tambo zako zinakera sana. Binafsi nawadharau sana vijana wa namna hii.
 
Tanzania hivi sasa tunakabiliwa kwa kiwango kikubwa sana cha vijana tunaowaita Elimu Ndogo Pesa Nyingi (Tuwaite EP kwa kifupi - Elimu Pesa), ambao utawatambua katika namna ya maongezi yao, kutamba kwao na kujionyesha kwao. Hata humu JF wapo wengi tu. Utaongea nae dakika tatu tu na kujua kwamba ana Range Rover, Premio, Toyota Crown, au BMW. Ndio magari yao.

Na mara nyingi utawakuta wanavojifanya kuweka maneno ya kiingereza wakati wa kuongea Kiswahili kwa maana ambayo ni broken ya juu sana. Unajiuliza hivi kwa nini asiongee Kiswahili tu lugha ya Taifa?

Mara nyingi wanajifanya wanajua sana mambo na wametembea sana duniani - wakati mara nyingi walikoenda ni Joburg South Afrika na wengine China.

Na tunaelewa kwamba hawa ni vijana ambao wameibukia kuwa na pesa kutokana na fursa zilizopo Tanzania, kama China au kuchimba madini. Lakini tunajua pia wengine ni madawa ya kulevya na utapeli tu wakitumiwa na viongozi mafisadi, na wengine ni wizi.

Sasa kama wewe unajitambua ni mmojawapo wa vijana wa Elimu Ndogo Pesa Nyingi, hebu acha tambo zako zinakera sana. Binafsi nawadharau sana vijana wa namna hii.
Naomba kujua kwanini wanakukera?
Unawadharau kwasababu wanakukera au wanakukera ndo maana unawadharau?
 
Hakuna mtu mwenye elimu ndogo anae miliki pesa , labda mtoa mada haujui maana ya elimu🤔
Mkuu nenda sehemu zenye machimbo ya madini huko ndio utakutana nao wengi. Au wale wanauza madawa.

Au hujaona watu wenye elimu duni wameenda kuchimba madini na kuibuka mabilionea? Ukiwa bilionea elimu duni inafutika?
 
Labd wana elimu ya madawa na namna ya kuchimba madini upate pesa🤔
 
Back
Top Bottom