TANZIA Mfanyabiashara Emilian Woiso afariki dunia

Mzee alikua ni master kabisa...walienda walioenda na hakucheka na mtu! Ila mwishoni aliokoka kweli na trakea ikawa kanisa badala ya baa...woiso wa Wop ni kijana mdogo sana...sidhani hata kama 44 anafika...ila kwa umri wa woiso kulikua hamna namna ya namna ya kutafuta hela kipindi chao...hela ilikua haipatikani instagram ilibidi uichukue kwa watu!
Huyo jamaa alikuwa hatari bin danger.

Nakumbuka kisa almanusura atupitie.
Ni miaka zaidi ya 20 iliyopita.

Tumeenda zetu Morogoro kumchukua mdogo wetu marehemu aliyefariki kwa ajali.
Tuko na gari Prado mpyaaa ndo kwanza zimeanza kutoka.
Tulioenda kuchukua maiti na tunarudi Dar , mmoja wa tuliokuwa nao alimtambua Leshesya baada ya kusimama sehemu fulani.
Ilikuwa jioni na kagiza kanaingia.

Huyooo Lesheya akatuambia nyie msiagize, msiagize kabisa chakula, mimi nitawaletea chakula, nyie ndugu zangu.
Tulikataa, lakini haikupita dk 5 tayari akaleta sahani nne za chips mayai!

Ambacho huyu Lesheya hakujua ni kwamba kati ya tulikuwa katika msafara alikuwemo ndugu ambaye ni kachero mbaya sana, na alitupa ishara tusikiguse chakula kile.

Baadaye tusiomfahamu yule kachero akatuambia, tatizo ni hilo gari, tungekula tu takrima ya huyo Lesheya, aidha tungekufa au kusinzia na kunyang'anywa hilo gari.

RIP Lesheya.
 
Jf ni balaa watu wanaubuyu balaa yani mzee marehemu amedadavuliwa kama wachambuzi wa soka wanavyo lichambua soka.
Kiufupi ukisoma komenti karibia zote zinaonesha marehemu alikuwa mtu hatari.
Kinachonifurahisha ni kwamba humu kuna memba amesoma na kila marehemu. Yani koment rip classmate hatakama marehemu alikuwa na miezi miwili utaikuta.
 
JF ni zaidi ya Sosho media
 
Back
Top Bottom