TANZIA Mfanyabiashara Subhash Patel (mmiliki wa Hoteli za Sea Cliff na White Sands) afariki Dunia

maliyamungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
564
412
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Motisun Group ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa Mabilionea wachache nchini Tanzania na mfanyabiashara, Subhash Patel inadaiwa amefariki leo.

UPDATES:

MFANYABIASHARA maarufu wa Tanzania ambae ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Motisun Group, Subhash Patel amefariki dunia leo Desemba 15, 2020.

Miongoni mwa makampuni na bidhaa alizokuwa akimiliki Subhash Patel, ni kiboko Plastics, Kiboko Protected Sheets, MM Estates, White Sands Hotel, MMRDL, Neeklanth Cables, Pearlsun Hotel & Resorts, Sayona Drinks Ltd, Sea Cliff Hotel, Best Bite, Mamba Cement na nyingine nyingi.

=====

WAZIRI MKUU ATUMA SALAAM ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA SUBHASH PATEL

DAR ES SALAAM: DESEMBA 15, 2020

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ametuma salaam za rambirambi kutokana na kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Motisun Group, Subhash Patel, kilichotokea leo jijini Dar es Salaam.

“Hayati Shubash, ana mchango wake kwenye sekta ya viwanda, alikuwa rafiki wa wote, mcheshi, ametoa msaada kwa maskini na matajiri na hakuwa mbaguzi,”

“Ninatoa pole kwa wanafamilia, ndugu na wote walioguswa na msiba huu. Taifa limempoteza mmoja wa wazalendo wake. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Katika salamu alizozitoa Waziri Mkuu, amesema amehuzunishwa na kifo cha mfanyabiashara huyo maarufu nchini ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI) na mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Mmoja wa wanafamilia amesema, Bw. Patel amefia nyumbani kwake, Kisutu jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akiendelea na matibabu na anatarajiwa kuzikwa keshokutwa (Alhamisi, Desemba 17, 2020) kwenye makaburi ya Wahindu yaliyoko Kijitonyama, Dar es Salaam.

Screenshot_2020-12-15 DAR CRIME ALERTS (DCA) Facebook(1) www.diramakini.co.tz.png

Tanzania: Subhash Patel dies of MOTISON Group of Companies dies

1608003217898.png

Mfanyabiashara Subhash Patel enzi za uhai wake
Soma pia:

1) Subhash Patel ni nani ?!

2) Forbes: Top 10 Richest Men in Tanzania for October, 2018.

3) Subash Patel: Wafanyabiashara na wenye viwanda tunamuunga mkono Rais Magufuli anayetupeleka kwenye uchumi wa kati

4) Interview with CTI Chairman Mr. Subhash Patel on channel TV-E(TANZANIA)

5) Ugomvi wa mali wamsukuma bilionea kumkana mtoto wake. Ni ugomvi wa Ukurugenzi wa MOTISUN Group




 
Tunaamini ameweka mifumo mizuri ya kuendesha hizi mali isije kuwa kama Ngurdoto mara Sea Cliff iwe Hostel, itakua aibu sana.

Otherwise kifo ni fumbo gumu uwe tajiri au masikini, uwe na madaraka uwe nani siku yako yaja. Lazima utaondoka. Usisumbue watu na kunyanyasa watu, ishi vyema maana eneo letu la kuzikwa ni moja... udongoni.

RIP Subash.
 
Just to alert you that it has been observed a re- surgence of Covid -19 patients in Dar. Be alerted and ware of this development. The surge was caused by Diwali Festival (mid November).

Wahindi wengi sana kusafiri kurudi makwao. Nasikia walirudi TZ kwa wingi na baada ya festival ndio wagonjwa wengi (Wahindi) walilazwa Hindumandal; sasa kagonjwa kamekwenda kwa watu vifo ni vingi.
Diwali ilileta wave jipya la COVID. RIP Subash Patel.
 
Just to alert you that it has been observed a re- surgence of Covid -19 patients in Dar. Be alerted and ware of this development. The surge was caused by Diwali Festival (mid November). Wahindi wengi sana kusafiri kurudi makwao. Nasikia walirudi TZ kwa wingi na baada ya festival ndio wagonjwa wengi (Wahindi) walilazwa Hindumandal; sasa kagonjwa kamekwenda kwa watu Vifo ni vingi.
Huyo daktari atakae bainisha mgojwa amekufa kutokana na COVID, pole zake.
 
Back
Top Bottom