Mfalme Juha !

MFALME JUHA

Member
May 5, 2008
13
1
Nimekuwa msomaji makini wa JF kwa miezi kadhaa, nimesoma michango mingi ya wana forum anuai, hatimaye nami nimeamua kujiunga na JF rasmi naombasana mnipokee na mnipe ushirikiano wa kutosha isipokuwa tu kitu kimoja nitaomba mnivumilie sana kwa jina langu hilo kwani mi ni JUHA kweli kweli, nipo tayari kuuza utu wangu ajili ya 10% nipo tayari kufanya yafuatayo.

1. kuwekeza fedha kibao za kigeni nje ya nchi wakati dispensari za nchi yangu zikiwa zapigania mgao wa Apsrini

2. nipo tayari kumlinda yeyote katika viongozi mara wafanyapo makosa na sitokubali mtu yeyote anifuatefuate

3.nipo tayari kutoa ahadi nyingi kwa watu wangu hata kama hazitekelezeki

4.nipo tayari kukaribisha wazungu wote waliokimbia Zimbabwe wawekeze katika mashamba ya hapa Bongo hata kama baadae wananchi wangu watakosa sehemu za kilimo

5. nipo tayari kufukuza wafugaji wote wa Kimasai katika maeneo ili eneo hilo nipate muwekezaji kwani mara tu baada ya utawala wangu nataka nijenge hekalu zuri kuzidi lile la Lushoto

6.kwa kuwa kuna mgao kidogo kwenye mikata yote ya wawekezaji basi nitaendelea kubinafisisha maeneo yote kama vile Reli nk hata kama watu watalalamika sana sontojali

7. Wale wanaodai Barabara za mikoani wasinisumbue kama wanataka kuona Lami nawaruhusu waje Bongo kila mwisho wa mwezi yaani ya baada ya kupokea VIJImishahara vyao ambavyo kwa kweli havitoshi ila nifanyeje sasa.

8. Maana yangu kubwa ni kuwa ile Barabara yas kutoka Itigi hadi Kigoma kupitia Tabora haitawezekana kwani nimegundua wanyamwezi na waha hamna utaratibu wa kwenda sana kwenu hivyo Usafiri wa Reli unawatosha kabisa kwa kuzingatia wengi wenu husafiri kwavijisenti kiddogo muwapavyo ma Cleaner na hata ma TT

- Mwisho lakini si kwa umuhimu naomba Mode usiifute Thread hii ili wana JF waendelee kunipa ushirikiano wa mawazo kwa kuhakikisha kuwa naitafuna nchi hii hadi kieleweke.

NAOMBA USHAURI ZAIDI
MIMI MFALME JUHA
 
Mfalme Juha,

Mie nimekuelewa sana, tena sana. Karibu tunahitaji kupata upande mwingine wa shilingi.

Asante kwa tungo nzuri!

Karibu rasmi humu tuwatokomeze wenye mawazo kama hayo uliyoandika hapo juu!!!
 
Mfalme Juha,

Karibu sana........ujumbe wako wahusika wameupata.........next time tutakuita bingwa wa reverse
 
Imekaa vizuri sana hii japo naona Baba H kamponda sana in aonekana BabaH yu mbali sana na fasihi
 
Mfalme Juha

karibu , naona wamesha kupa shule ya kutosha kwa kukuvaa lakini nadhani una haki maana umeuliza umeomba na kusema wewe ni Juha.Unayotaka kuyalinda ukisha eleweshwa naaminiu utayaacha .So karibu na vumilia mkuu .Hapa ni baharini watu wanajitupa tu usikate tamaa .
 
Karibu jamvini Juha!
Ila umesahau kutaja umahiri na umakini wako wa kuyapandishia magari ya kifahari kodi ili uweze kupata mapesa mengi ya ku-spend unapotembelea nchi mbalimbali,na kulala ktk mahotel ya kifahari na majuha wenzio na Pia kupandisha bei ya umeme kila kukicha ili wananchi waendelee kutumia nuru ya Mwezina nyota usiku kutoka kwa Mungu maana umeme ni anasa ktk nchi hii
 
Yeah.......kila siku nasema, Upande wa pili wa shilingi. Tumuachie afikirie kama "wao" ili tukabiliane kwa HOJA.

Ni Fasihi nzuri sana.
 
Nimekuwa msomaji makini wa JF kwa miezi kadhaa, nimesoma michango mingi ya wana forum anuai, hatimaye nami nimeamua kujiunga na JF rasmi naombasana mnipokee na mnipe ushirikiano wa kutosha isipokuwa tu kitu kimoja nitaomba mnivumilie sana kwa jina langu hilo kwani mi ni JUHA kweli kweli, nipo tayari kuuza utu wangu ajili ya 10% nipo tayari kufanya yafuatayo
1. kuwekeza fedha kibao za kigeni nje ya nchi wakati dispensari za nchi yangu zikiwa zapigania mgao wa Apsrini
2. nipo tayari kumlinda yeyote katika viongozi mara wafanyapo makosa na sitokubali mtu yeyote anifuatefuate
3.nipo tayari kutoa ahadi nyingi kwa watu wangu hata kama hazitekelezeki
4.nipo tayari kukaribisha wazungu wote waliokimbia Zimbabwe wawekeze katika mashamba ya hapa Bongo hata kama baadae wananchi wangu watakosa sehemu za kilimo
5. nipo tayari kufukuza wafugaji wote wa Kimasai katika maeneo ili eneo hilo nipate muwekezaji kwani mara tu baada ya utawala wangu nataka nijenge hekalu zuri kuzidi lile la Lushoto
6.kwa kuwa kuna mgao kidogo kwenye mikata yote ya wawekezaji basi nitaendelea kubinafisisha maeneo yote kama vile Reli nk hata kama watu watalalamika sana sontojali
7. Wale wanaodai Barabara za mikoani wasinisumbue kama wanataka kuona Lami nawaruhusu waje Bongo kila mwisho wa mwezi yaani ya baada ya kupokea VIJImishahara vyao ambavyo kwa kweli havitoshi ila nifanyeje sasa
8. Maana yangu kubwa ni kuwa ile Barabara yas kutoka Itigi hadi Kigoma kupitia Tabora haitawezekana kwani nimegundua wanyamwezi na waha hamna utaratibu wa kwenda sana kwenu hivyo Usafiri wa Reli unawatosha kabisa kwa kuzingatia wengi wenu husafiri kwavijisenti kiddogo muwapavyo ma Cleaner na hata ma TT
- Mwisho lakini si kwa umuhimu naomba Mode usiifute Thread hii ili wana JF waendelee kunipa ushirikiano wa mawazo kwa kuhakikisha kuwa naitafuna nchi hii hadi kieleweke.
NAOMBA USHAURI ZAIDI
MIMI MFALME JUHA

imetulia karibu sana
 
Hii sio forum ya namna yako, nadhani umepotea njia mkuu, nenda darhot wire wanaweza kukukaribisha.
Tumia kidogo busara katika kufanya mambo yako, mambo uliyoyaandika hapo yanaonyesha na kubainisha wazi kuwa uwezo wako wa kuoanisha mambo na malengo ya forum hii uhuelewi, nadhani kuna document ya welcome, ningekushauri kuisoma hiyo ili uelewe ni nini kazi ya JF, na kama utaona hayo uliyoyaandika ni ya hapa, the Karibu sana kama sio ya hapa, sio lazima kupost hapa unaweza kutafuta Forum za aina yako mkuu
BABA H MSOME VIZURI MFALME JUHA NA POST YAKO KISHA ISOME KINYUME NYUME UTAMUELEWA
 
Karibu msanii sana Mfalme Juha,

Tunajua parody yako umemlenga nani.

Mfalme Juha ni Kikwete by any other name, leo kaona aibu kaja ku confess mwenyewe hapa.

A parody here and there and the pyramids were built, people, we can't be serious all the time.Tunahitaji wasanii wetu wawe na viwanja vya mazoezi pia, lol.
 
Yah ndio yuko hivyo mkuu wetu .

Aliyempinga kasahau sehemu muhimu ya mawasiliano ni kusikiliza ,fasihi iko wazi hii na fanani atambulika.
 
Nashukuru sana kwa wote mliochangia hoja yangu mbali na wale walioponda bado nafikiria sana juu ya kuzima midomo ya wote wanaolalamikia bei ndogo ya Tumbaku, Korosho,pamba,kahawa na mazao yote ya biashara njia ya kuziba midomo ya hao ni kuhakikisha kuwa katika misafara yangu yote ya Ughaibuni sikosi kuwa nao huko watapata posho nene ya utawala wangu. napenda tu kuwafahamisha kuwa katika utawala wangu kelele zote juu ya madini, mikataba ya reli n.k nina pasenti zangu sasa anaetaka niondoke kwenye himaya ya utawala halafu nianze kuomba lifti nani? acheni midomodomo acheni niitafune nchii bwana si nyinyi wenyewe ukifika wakati wa uchaguzi ndio mnao nipa kura za kumwaga endeleeni kuvumilia tu !
 
Hongera sana mfalme juha kwa fasihi nzuri ili mradi ujumbe ufike kwa walengwa yawezekana ujuha ukaomdoka
Hongera sana
 
Najua mtaendelea kunishangaa sana, prof Msolla kiasi kidogo alishindwa kwenye elimu ya juu na vijana walipiga kelele kidogo si vibaya sana akiendelea kutumikia wabongo wenzangu kwa nafasi hiyo ndogo niliompa swala la kelele kwangu si Ishu mwajua lazima watanzania tujenge moyo wa upendo na kuvumiliana bado naangalia uwezekano wa kuwarudisha Lowasa, Karamagi na bangu silo maana kidogo naona kazi za dorora kama ni makosa ni ajali za kisiasa tu na wale mnaojindaa kuning'oa kwenye utawala wangu hamtoweza maana Bwana VIJISENTI hatokubali niadhirike peke yangu na ndio maana nahakikisha hatosumbuliwa sana. yaani nimfae kwa jua ili aje anifae kwa mvua
MFALME JUHA
 
Nashukuru sana kwa wote mliochangia hoja yangu mbali na wale walioponda bado nafikiria sana juu ya kuzima midomo ya wote wanaolalamikia bei ndogo ya Tumbaku, Korosho,pamba,kahawa na mazao yote ya biashara njia ya kuziba midomo ya hao ni kuhakikisha kuwa katika misafara yangu yote ya Ughaibuni sikosi kuwa nao huko watapata posho nene ya utawala wangu. napenda tu kuwafahamisha kuwa katika utawala wangu kelele zote juu ya madini, mikataba ya reli n.k nina pasenti zangu sasa anaetaka niondoke kwenye himaya ya utawala halafu nianze kuomba lifti nani? acheni midomodomo acheni niitafune nchii bwana si nyinyi wenyewe ukifika wakati wa uchaguzi ndio mnao nipa kura za kumwaga endeleeni kuvumilia tu !hivi hiri richenkapa rina dharau namuna hiii, kumbe sio hadithi tu, adabu yako ndogo kweli kweli. Msalimie JK mwambie akufungulie mashitaka ya ufisadi
 
Najua mtaendelea kunishangaa sana, prof Msolla kiasi kidogo alishindwa kwenye elimu ya juu na vijana walipiga kelele kidogo si vibaya sana akiendelea kutumikia wabongo wenzangu kwa nafasi hiyo ndogo niliompa swala la kelele kwangu si Ishu mwajua lazima watanzania tujenge moyo wa upendo na kuvumiliana bado naangalia uwezekano wa kuwarudisha Lowasa, Karamagi na bangu silo maana kidogo naona kazi za dorora kama ni makosa ni ajali za kisiasa tu na wale mnaojindaa kuning'oa kwenye utawala wangu hamtoweza maana Bwana VIJISENTI hatokubali niadhirike peke yangu na ndio maana nahakikisha hatosumbuliwa sana. yaani nimfae kwa jua ili aje anifae kwa mvua
MFALME JUHAwe chenkapa, hapa unajibadirisha tukuone JK aahh, spin master!
 
Back
Top Bottom